Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX
Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III) (Sehemu ya Kwanza)
Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya hii. Ni mada gani? (Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote.) Inaonekana yale mambo na mada niliyoyazungumzia yaliwachia kila mtu wazo dhahiri. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao. Kwa kweli, kile ambacho Mungu anafanya si tu kuandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu wala si tu kuandaa riziki yao ya kila siku, bali ni kuandaa vipengele mbalimbali vya kazi kubwa ya ajabu na ya lazima kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa watu na kwa ajili ya maisha ya binadamu. Haya yote ni matendo ya Mungu. Matendo haya yanayofanywa na Mungu hayakomei tu kwenye maandalizi Yake ya mazingira kwa ajili ya watu kuendelea kuishi na riziki zao za kila siku—yana mawanda mapana zaidi kuliko hayo. Licha ya aina mbili hizi za kazi, pia Anaandaa mazingira mengi na hali kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo ni lazima kwa ajili ya maisha ya mwanadamu. Hii ni mada nyingine ambayo tutaijadili leo. Pia inahusiana na matendo ya Mungu; vinginevyo, kuizungumzia hapa isingekuwa na maana. Ikiwa watu wanataka kumjua Mungu lakini wana maana ya moja kwa moja ya “Mungu,” ya neno hilo, au ya vipengele vyote vya kile Mungu anacho na alicho, huo sio uelewa wa kweli. Sasa, njia kwa ajili ya maarifa ya Mungu ni ipi? Ni kumjua Yeye, kujua kila kipengele Chake kupitia matendo Yake. Kwa hiyo, kinachofuata tunapaswa kushiriki kuhusu matendo ya Mungu pale alipoumba vitu vyote.
Tangu Mungu alipoviumba, kulingana na sheria ambazo Aliziamua, vitu vyote vimekuwa vikitenda kazi na vimekuwa vikiendelea kukua kwa kawaida. Chini ya uangalizi Wake, chini ya kanuni Yake, vitu vyote vimekuwa vikiendelea kwa kawaida sambamba na kuendelea kuishi kwa binadamu. Hakuna kitu hata kimoja kinaweza kubadilisha sheria hizi, na hakuna hata kitu kimoja kinachoweza kuziharibu sheria hizi. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu ndipo viumbe vyote vinaweza kuongezeka, na kwa sababu ya kanuni na usimamizi Wake ndipo vitu vyote vinaweza kuendelea kuishi. Hii ni kusema kwamba chini ya kanuni ya Mungu, viumbe vyote vinakuwepo, vinastawi, vinatoweka, na kuzaliwa upya kwa namna ya mpangilio. Msimu wa machipuo unapowadia, mvua ya manyunyu huleta hisia hiyo ya machipuo na kuipatia nchi unyevunyevu. Ardhi huanza kuyeyuka, majani huota na kujipenyeza juu ya udongo na miti taratibu hubadilika kuwa ya kijani. Viumbe hai hivi vyote vinaleta uzima mpya katika dunia. Hii ndiyo picha ya viumbe vyote kuwepo na kustawi. Wanyama wa kila aina pia hutoka matunduni mwao ili kupata uvuguvugu wa msimu wa machipuo na kuanza mwaka mpya. Viumbe vyote vinaota jua kwenye joto wakati wa kiangazi na kufurahia uvuguvugu unaoletwa na msimu huu. Vinakua haraka; miti, nyasi, na aina zote za mimea inakua haraka sana, kisha inachanua na kuzaa matunda. Viumbe vyote vinakuwa vimetingwa sana wakati wa kiangazi, binadamu wakiwemo. Katika msimu wa majani kupukutika, mvua inaleta utulivu wa msimu wa majani kupukutika, na aina zote za viumbe hai vinaanza kupitia uzoefu wa msimu wa kiangazi. Viumbe vyote vinazaa matunda, na binadamu pia wanaanza kuvuna aina zote za vitu kwa sababu ya msimu wa majani kupukutika kuzalisha viumbe vyote hivi, ili kuandaa chakula kwa ajili ya msimu wa baridi. Katika msimu wa baridi viumbe vyote taratibu vinaanza kupumzika katika ubaridi, kuwa kimya, na watu pia wanachukua pumziko wakati wa msimu huu. Mabadiliko haya kutoka msimu wa machipuo kwenda msimu wa kiangazi kwenda msimu wa mapukutiko na kwenda msimu wa baridi—mabadiliko haya yote yanatokea kulingana na sheria zilizoanzishwa na Mungu. Anawaongoza viumbe na binadamu kwa kutumia sheria hizi na Ameanzisha maisha yenye utajiri na ya kupendeza kwa ajili ya mwanadamu, Akiandaa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo yana halijoto tofautitofauti na misimu tofautitofauti. Chini ya mazingira haya yaliyopangiliwa kwa ajili ya kuendelea kuishi, binadamu wanaweza kuendelea kuishi na kuongezeka kwa namna ya mpangilio. Binadamu hawawezi kuzibadilisha sheria hizi, na hakuna mtu hata mmoja au kiumbe ambacho kinaweza kuzivunja. Haijalishi ni mabadiliko makubwa kiasi gani yanatokea duniani, sheria hizi zinaendelea kuwepo na zipo kwa sababu Mungu yupo. Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Kwa aina hii ya mpangilio, mazingira makubwa, maisha ya watu yanaendelea ndani ya sheria na kanuni hizi. Sheria hizi ziliendeleza kizazi baada ya kizazi cha watu na kizazi baada ya kizazi cha watu wameendelea kuishi ndani ya sheria hizi. Watu wamefurahia viumbe na mazingira haya ya mpangilio kwa ajili ya kuendelea kuishi yaliyoumbwa na Mungu kwa ajili ya kizazi baada ya kizazi cha binadamu. Ingawa watu wanahisi kwamba aina hii ya sheria ni za kiasili, ingawa wanazipuuza kabisa sheria hizo, na ingawa hawawezi kuhisi kuwa Mungu ndiye anaweka utaratibu wa sheria hizi, kwamba Mungu anatawala sheria hizi, haijalishi, Mungu siku zote anajihusisha katika kazi hii isiyobadilika. Kusudi lake katika kazi hii isiyobadilika ni kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na ili binadamu waweze kuendelea.
Mungu Huweka Mipaka kwa ajili ya Vitu Vyote ili Kuwalea Binadamu Wote
Leo nitazungumzia mada ya jinsi aina hizi za kanuni ambazo Mungu amezileta kwa viumbe wote hulea wanadamu wote. Hii ni mada kubwa, kwa hiyo tunaweza kuigawanya katika sehemu kadhaa na kuzijadili moja baada ya nyingine ili ziweze kufafanuliwa vizuri kwenu. Kwa njia hii itakuwa rahisi kwenu kupata maana na taratibu mnaweza kuielewa.
Kwanza, Mungu alipoviumba vitu vyote, Aliweka mipaka kwa ajili ya milima, tambarare, majangwa, vilima, mito, na maziwa. Duniani kuna milima, tambarare, majangwa, vilima, vilevile vyanzo mbalimbali vya maji. Je, hayo si mandhari tofautitofauti? Mungu aliweka mipaka kati ya mandhari haya yote tofautitofauti. Tunapozungumza juu ya kuweka mipaka, ina maana kwamba milima ina mipaka yake, tambarare zina mipaka yake, majangwa yana mawanda fulani, na vilima vina eneo mahususi. Pia kuna kiwango mahususi cha vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa. Yaani, Mungu alipoumba vitu vyote aligawanya kila kitu vizuri kabisa. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha mlima ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Mungu ameshajua nusu kipenyo cha tambarare ni kilometa ngapi, mawanda yake ni mapana kiasi gani. Alipokuwa anaumba viumbe vyote pia Aliamua mawanda ya jangwa, vilevile mawanda ya vilima na uwiano wao, na vile vilivyopakana navyo—pia Aliamua yote haya. Aliamua mawanda ya mito na maziwa Alipokuwa anaviumba—vyote vina mipaka yao. Kwa hiyo ina maana gani tunaposema “mipaka”? Tulizungumza tu kuhusu ambavyo utawala wa Mungu kwa vitu vyote unavyoanzisha sheria kwa viumbe vyote. Yaani, mawanda na mipaka ya milima havitaongezeka au kupungua kwa sababu ya mzunguko wa dunia au muda kupita. Hii haibadiliki: Hii “isiyobadilika” ni kanuni ya Mungu. Kwa maeneo ya tambarare, mawanda yao, kile kilichopakana nayo, hii imewekwa na Mungu. Yana mipaka, na tuta haliwezi kutokea tu bila mpangilio, katikati ya tambarare. Tambarare haiwezi tu kubadilika na kuwa mlima—hii haitatokea. Sheria na mipaka tuliyoizungumzia inarejelea hili. Kwa jangwa, hatutataja wajibu wa jangwa au mandhari nyingineyo au eneo la kijiografia hapa, ni mipaka yake tu. Chini ya kanuni ya Mungu mawanda ya jangwa nayo pia hayatapanuka. Hii ni kwa sababu Mungu amelipatia sheria yake, mawanda yake. Eneo lake ni kubwa kiasi gani na wajibu wake ni upi, kile kilichopakana nalo, na lipo mahali gani—hii imeshawekwa na Mungu tayari. Halitazidisha mawanda yake, kuhamisha sehemu yake, na halitaongeza eneo lake kiholela tu. Ingawa mtiririko wa maji kama vile mito na maziwa yote yapo katika mpangilio na mwendelezo, hayajawahi kwenda nje ya mawanda yao au kwenda zaidi ya mipaka yao. Yote yanafuata mwelekeo mmoja kwa namna ya mpangilio, yakitiririka kuelekea mwelekeo yanaopaswa kwenda. Kwa hiyo chini ya sheria ya kanuni ya Mungu, hakuna mto au ziwa ambalo litakauka kiholela tu, au kubadilisha mwelekeo au kiwango cha kutiririka kwake kiholela tu kwa sababu ya mzunguko wa dunia au kupita kwa muda. Hii yote ipo ndani ya maarifa ya Mungu. Hiyo ni sawa na kusema, viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu katikati ya binadamu vina sehemu zao, maeneo yao, na mawanda yao yasiyobadilika. Yaani, Mungu alipoviumba viumbe vyote, mipaka yao ilianzishwa na hii haiwezi kugeuzwa kiholela tu, kufanywa upya au kubadilishwa. “Kiholela” inamaanisha nini? Ina maana kwamba havitahama, kupanuka, au kubadilisha umbo lao asilia bila mpangilio kwa sababu ya hali ya hewa, halijoto, au kasi ya mzunguko wa dunia. Kwa mfano, mlima una kimo fulani, kitako chake ni cha eneo fulani, una mwinuko fulani, na una kiasi fulani cha uoto. Hii yote imepangwa na kukokotolewa na Mungu na kimo au eneo lake halitabadilika kiholela. Kwa tambarare, idadi kubwa ya binadamu wanaishi katika tambarare, na hakuna mabadiliko ya hali ya hewa yatakayoathiri maeneo yao au thamani ya uwepo wao. Sio hata kile ambacho kimejumuishwa katika mandhari haya na mazingira ya kijiografia ambayo yaliumbwa na Mungu yatabadilika kiholela. Kwa mfano, vipengele vya jangwa ni vipi, ni aina gani ya madini yaliyopo chini ya ardhi, yanajumuisha mchanga kiasi gani na rangi ya mchanga, upana wake—haya hayatabadilika kiholela. Kwa nini hayatabadilika kiholela? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu na usimamizi Wake. Ndani ya mandhari haya yote tofautitofauti na mazingira ya kijiografia yaliyoumbwa na Mungu, Anasimamia kila kitu kwa njia iliyopangwa na kwa mpangilio. Kwa hiyo mazingira haya yote ya kijiografia bado yapo kwa miaka elfu kadhaa, makumi elfu ya miaka baada ya kuwa yameumbwa na Mungu. Bado yanatimiza kila wajibu wao. Ingawa wakati wa vipindi fulani volkano hulipuka, wakati wa vipindi fulani matetemeko ya ardhi hutokea, na kuna mabadiliko makubwa ya ardhi, hakika Mungu hataruhusu aina yoyote ya mandhari kupoteza kazi yake ya asili. Ni kwa sababu tu ya usimamizi huu unaofanywa na Mungu, utawala Wake na udhibiti wa sheria hizi, kwamba yote haya—yote haya yanayofurahiwa na binadamu na kuonwa na binadamu—yanaweza kuendelea kuishi duniani kwa njia ya mpangilio. Sasa kwa nini Mungu anasimamia mandhari yote haya yaliyopo duniani kwa njia hii? Kusudi ni ili viumbe hai vinavyoendelea kuishi katika mazingira mbalimbali ya kijiografia yote yatakuwa na mazingira imara, na kwamba wataweza kuendelea kuishi na kuongezeka katika mazingira hayo imara. Viumbe vyote hivi—vile vinavyotembea na vile ambavyo havitembei, vile ambavyo vinaweza kupumua na vile ambavyo haviwezi—vinaunda mazingira ya tofauti kabisa kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi. Ni aina hii tu ya mazingira ndiyo inaweza kulea kizazi baada ya kizazi cha binadamu, na ni aina hii tu ya mazingira inaweza kuruhusu binadamu kuendelea kuishi kwa amani, kizazi baada ya kizazi.
Yale nimetoka kuzungumzia ni mada kubwa mno kwa hivyo inaonekana geni sana kwenu, lakini mnaweza kuelewa, sivyo? Yaani, sheria za Mungu katika utawala wake wa vitu vyote ni muhimu sana—muhimu sana! Je, masharti ya awali ni yapi kwa viumbe vyote kukua ndani ya sheria hizi? Ni kwa sababu ya kanuni ya Mungu. Ni kwa sababu ya kanuni Yake ndipo viumbe vyote vinafanya kazi zao ndani ya kanuni Yake. Kwa mfano, milima inalea misitu, halafu misitu inalea na kuwalinda ndege mbalimbali na wanyama wanaoishi ndani yake. Tambarare ni jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya binadamu kupanda mazao vilevile kwa ajili ya ndege na wanyama mbalimbali. Zinaruhusu idadi kubwa ya binadamu kuishi katika ardhi tambarare na kutoa hali isiyo na taabu katika maisha ya binadamu. Na tambarare pia zinajumuisha ukanda wa mbuga—malundo ya ukanda wa mbuga. Ukanda wa mbuga ni uoto wa nchi. Unalinda ardhi na kuwalea ng’ombe, kondoo na farasi wanaoishi katika ukanda wa mbuga. Jangwa pia linafanya kazi yake. Sio sehemu kwa ajili ya binadamu kuishi; jukumu lake ni kufanya hali ya hewa ya unyevunyevu kuwa kavu. Kutiririka kwa mito na maziwa kunaleta hali isiyo ya usumbufu kwa ajili ya watu kunywa maji na kwa mahitaji ya viumbe vyote. Vyovyote vile yanavyotiririka, watu watakuwa na maji kwa ajili ya kunywa. Hii ni mipaka iliyochorwa na Mungu kwa ajili ya mandhari mbalimbali.
Kwa sababu ya mipaka hii ambayo Mungu ameichora, mandhari mbalimbali yamezalisha mazingira tofautitofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, na mazingira haya kwa ajili ya kuendelea kuishi yamekuwa na hali isiyokuwa na usumbufu kwa ajili ya aina tofautitofauti ya ndege na wanyama na vilevile kuleta nafasi kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kutokana na hili, mipaka kwa mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa viumbe hai mbalimbali imeendelezwa. Hiki ndicho tutakachokwenda kuzungumzia baadaye. Hoja ya pili: Kwanza kabisa ni aina gani ya mazingira ambamo ndege na wanyama na wadudu wanaishi? Je, wanaishi katika misitu na vijisitu? (Ndiyo.) Haya ndiyo makazi yao. Kwa hivyo, kando na kuanzisha mipaka kwa ajili ya mazingira mbalimbali ya kijiografia, Mungu pia Aliweka mipaka kwa ajili ya ndege na wanyama, samaki, wadudu mbalimbali, na mimea yote. Pia alianzisha sheria. Kwa sababu ya tofauti za mazingira mbalimbali ya kijiografia na kwa sababu ya uwepo wa mazingira tofauti ya kijiografia, aina tofautitofauti za ndege na wanyama, samaki, wadudu, na mimea vina mazingira tofauti kwa ajili ya kuendelea kuishi. Ndege na wanyama na wadudu wanaishi miongoni mwa mimea, samaki wanaishi majini, na mimea inakua kwenye nchi kavu. Nchi kavu inajumuisha nini? Maeneo mbalimbali kama vile milima, tambarare, na vilima. Kwa hiyo, pindi ndege na wanyama wana makazi yao yasiyobadilika, hawatazungukazunguka mahali popote tu. Makazi yao ni misitu na milima. Ikiwa, siku moja makazi yao yataharibiwa, wangefanya nini? (Wangezungukazunguka mahali pote.) Mpangilio huu utakuwa machafuko. Mara tu mpangilio huo unapokuwa machafuko, madhara yake ni yapi? Wa kwanza kuumizwa ni akina nani? (Binadamu.) Ni binadamu. Ndani ya sheria na mipaka hii ambayo Mungu ameianzisha, je, mmewahi kuona tukio lolote la ajabu? Kwa mfano, tembo wakizungukazunguka tu jangwani kwa kawaida. Mmewahi kuona tukio hilo? Kama ingekuwa hivyo, lingekuwa ni tukio la ajabu sana, kwa sababu tembo wanaishi msituni, na ni mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliwaandalia. Wana mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi na wana makazi yao yasiyobadilika, sasa kwa nini watangetange? Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kuona simba au duma wakizungukazunguka baharini? Hakuna, siyo? Makazi ya simba na duma ni msituni na kwenye milima. Je, kuna mtu yeyote ambaye amewahi kumwona nyangumi au papa kutoka baharini wakitembea jangwani? Hakuna ambaye ameona hayo, siyo? Nyangumi na papa makazi yao ni baharini. Katika mazingira ya kuishi ya binadamu, je, kuna watu ambao wanaishi pamoja na dubu wa kahawia? Je, kuna watu ambao siku zote wamezungukwa na tausi au ndege wengineo, ndani au nje ya makazi yao? Je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaona tai au bata bukini wa mwituni wakicheza na tumbili? (Hakuna.) Haya yatakuwa ni matukio ya pekee sana. Sababu Ninazungumza juu ya vitu hivi ambavyo ni matukio ya pekee machoni mwenu ni kuwafanya muelewe kwamba vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu—haijalishi kama vimewekwa katika sehemu moja au vinapumua—vyote vina sheria zao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Zamani kabla Mungu hajaumba viumbe hai hivi Alikuwa ameviandalia makazi yao, mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai hivi vilikuwa na mazingira yao yasiyobadilika kwa ajili ya kuendelea kuishi, chakula chao, makazi yao yasiyobadilika, sehemu zao zisizobadilika zinazowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi, maeneo yenye halijoto inayowafaa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa njia hiyo wasingezungukazunguka au kuhafifisha hali ya mwanadamu kuendelea kuishi au kuathiri maisha yao. Hivi ndivyo Mungu anavyosimamia viumbe vyote. Ni kumwandalia binadamu mazingira mazuri kabisa kwa ajili ya kuendelea kuishi. Viumbe hai chini ya viumbe vyote kila kimoja kina chakula kinachokimu maisha ndani ya mazingira yao wenyewe kwa ajili ya kuendelea kuishi. Kwa chakula hicho, vinajifunga katika mazingira yao ya asili kwa ajili ya kuendelea kuishi. Katika aina hiyo ya mazingira bado vinaendelea kuishi, kuzaliana, na kuendelea kulingana na sheria za Mungu alizozianzisha kwa ajili yao. Kwa sababu ya aina hizi za sheria, kwa sababu ya majaaliwa ya Mungu, viumbe vyote vinaingiliana na binadamu kwa upatanifu, na binadamu na viumbe vyote vinategemeana.
Mungu aliviumba viumbe vyote na akaanzisha mipaka kwa ajili yao na miongoni mwao akalea aina zote za viumbe hai. Wakati Alikuwa akilea aina zote za viumbe hai, pia Aliandaa mbinu tofauti kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi, hivyo unaweza kuona kwamba binadamu hawana njia moja tu kwa ajili ya kuendelea kuishi. Pia hawana aina moja tu ya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi. Hapo kabla tulizungumza juu ya Mungu kuandaa aina mbalimbali za chakula na vyanzo vya maji kwa ajili ya binadamu, kitu ambacho ni muhimu sana kufanya uhai wa binadamu katika mwili kuendelea. Hata hivyo, miongoni mwa binadamu huyu, sio watu wote wanaishi kwa kula nafaka. Watu wana mbinu tofautitofauti za kuendelea kuishi kwa sababu ya tofauti za mazingira ya kijiografia na mandhari. Mbinu hizi za kuendelea kuishi zote zimeandaliwa na Mungu. Hivyo si binadamu wote wanajihusisha na kilimo. Yaani, si watu wote wanapata chakula chao kwa kulima mazao. Hii ni hoja ya tatu ambayo tutakwenda kuizungumzia. Mipaka imetengenezwa kutokana na mitindo mbalimbali ya maisha ya binadamu. Kwa hiyo ni aina nyingine ipi ya mtindo wa maisha ambayo binadamu wanayo? Ni vyanzo gani vingine vya vyakula ambavyo binadamu wanavyo? Kuna aina za msingi kadhaa:
Ya kwanza ni mtindo wa maisha wa uwindaji. Kila mmoja anajua kuhusu hilo, siyo? Watu wanaoishi kwa kuwinda wanakula nini? (Windo.) Wanakula ndege na wanyama wa mwituni. “Windo” ni neno la kisasa. Wawindaji hawaoni kwamba ni mchezo, wanaona kama chakula, kama riziki yao ya kila siku. Kwa mfano, wangepata paa. Wanapopata paa huyu ni sawa tu na mkulima kupata mazao kutoka ardhini. Mkulima hupata mazao kutoka ardhini, na anapoona mazao yake anakuwa na furaha na anahisi amani. Familia haitakuwa na njaa ya mazao ya kula. Moyo wake una amani na anahisi kuridhika. Na mwindaji pia anahisi amani na kuridhika akiangalia kile ambacho amekamata kwa sababu hana haja ya kuwa na wasiwasi tena kuhusu chakula. Kuna kitu cha kula kwa ajili ya mlo unaofuata, hakuna haja ya kuwa na njaa. Huyu ni mtu ambaye anawinda kwa ajili ya kuishi. Ni mazingira ya aina gani wanayoishi? Wengi wa wale ambao hutegemea uwindaji wanaishi katika misitu ya milima; hawalimi au kupanda mazao. Sio rahisi kupata ardhi inayolimika hapo, kwa hiyo wanaishi kwa kutegemea viumbe hai mbalimbali, aina mbalimbali za mawindo. Hii ni aina ya kwanza ya mtindo wa maisha ambao ni tofauti na ule wa watu wa kawaida.
Aina ya pili ni mtindo wa maisha wa ufugaji. Wale ambao wanafuga kwa ajili ya kuishi hawalimi, sasa wanafanya nini? Ikiwa yeyote miongoni mwenu hapa ni mtu wa Mongolia, mnaweza kuzungumza kidogo kuhusu mtindo wenu wa maisha ya kuhamahama. (Kwa sehemu kubwa, tunafuga ng’ombe na kondoo kwa ajili ya kuishi, hatulimi, na msimu wa baridi tunawachinja na kuwala mifugo wetu. Chakula chetu kinatokana haswa na nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, na tunakunywa chai ya maziwa. Ingawa wafugaji wanatingwa misimu yote minne, lakini wanakula vizuri. Hawapungukiwi na maziwa, bidhaa za maziwa, au nyama.) Chakula cha msingi cha watu wa Mongolia ni kula nyama ya ng’ombe na nyama ya kondoo, kunywa maziwa ya kondoo na ng’ombe, na wanaendesha madume ya ng’ombe na farasi uwandani na upepo kwenye nywele zao, jua usoni pao. Hawana msongo wa mawazo juu ya maisha ya kisasa. Siku nzima wanaona tu upana wa wingu la bluu na tambarare za majani. Wengi wa watu wanaofuga mifugo kwa ajili ya kuishi wanaishi kwenye uwanda wa mbuga na wanaweza kuendelea na mtindo wao wa maisha ya kuhamahama kwa kizazi baada ya kizazi. Ingawa maisha katika uwanda wa mbuga ni ya upweke kidogo, pia ni maisha ya furaha. Si mtindo mbaya wa maisha!
Aina ya tatu ni mtindo wa maisha ya uvuvi. Kuna sehemu ndogo ya binadamu wanaoishi pembezoni mwa bahari au kwenye visiwa vidogo. Wamezungukwa na maji, wakikabiliana na bahari. Na kuna wengine wanaoishi kwenye mashua. Watu hawa hufanya uvuvi kwa ajili ya kuishi. Ni nini chanzo cha chakula kwa wale wanaofanya uvuvi kwa ajili ya kuishi? Ni aina zote za samaki, vyakula vya baharini, na mazao ya baharini, siyo? Wakati Hong Kong ilikuwa ni kijiji kidogo tu cha uvuvi, watu ambao waliishi pale waliweza kuvua kwa ajili ya kuishi. Hawakulima—walikwenda kuvua kila siku. Chakula chao cha msingi kilikuwa ni aina mbalimbali za samaki, na vyakula vya baharini. Mara chache waliweza kubadilishana vitu hivi na mchele, unga, na mahitaji ya kila siku. Huu ni mtindo tofauti wa maisha wa watu wanaoishi karibu na maji. Wale wanaoishi karibu na maji wanayategemea kwa ajili ya chakula chao, na uvuvi ni riziki yao. Ni chanzo cha riziki yao vilevile chanzo chao cha chakula.
Licha ya wale ambao hulima kwa ajili ya kuishi, kimsingi kuna aina tatu tofauti za mtindo wa maisha zilizotajwa hapo juu. Licha ya wale ambao wanaishi kwa kutegemea ufugaji, uvuvi, na kuwinda, idadi kubwa ya watu hulima kwa ajili ya chakula. Na watu wanaolima kwa ajili ya kuishi wanahitaji nini? Wanahitaji udongo. Wao wanategemea kupanda mazao kwa vizazi na kupata chakula chao kutoka ardhini. Haijalishi wanapanda mbogamboga, matunda au nafaka, wote wanapata mahitaji yao ya kila siku kutoka ardhini.
Masharti ya msingi kwa mitindo tofauti ya maisha ya binadamu ni yapi? Je, hayahitaji utunzaji wa msingi wa mazingira yao kwa ajili ya kuendelea kuishi? Hii ni sawa na kusema, ikiwa wawindaji wangepoteza misitu ya milima au ndege na wanyama, basi wasingekuwa tena na riziki yao. Hivyo ikiwa watu ambao wanategemea uwindaji wangepoteza milima ya misitu na wasiwe tena na ndege na wanyama, wasingekuwa tena na chanzo cha riziki yao, basi mwelekeo wa aina hiyo ya mbari ungechukua na mahali watu wa aina hii wangeelekea ni kiwango kisichojulikana, na wangeweza pia tu kutoweka. Na wale ambao wanafuga kwa ajili ya riziki yao hutegemea nini? Kile ambacho kweli wanakitegemea si mifugo yao, lakini ni mazingira ambayo mifugo wao wanaendelea kuishi—uwanda wa mbuga. Kama kusingekuwa na uwanda wa mbuga, wangelishia wapi mifugo wao? Kondoo na ng’ombe wangekula nini? Bila mifugo, watu wanaohamahama wangekuwa na riziki gani? Wasingekuwa na riziki. Bila chanzo cha riziki yao, watu hawa wangekwenda wapi? Kuendelea kuishi kungekuwa vigumu sana; wasingekuwa na maisha ya baadaye. Bila vyanzo vya maji, mito na maziwa yangekauka. Je, samaki hao wote wanaotegemea maji kwa ajili ya maisha yao wangeendelea kuwepo? Samaki hao wasingeendelea kuishi. Je, watu hao ambao wanategemea maji na samaki kwa ajili ya riziki yao wangeendelea kuishi? Ikiwa hawakuwa na chakula, ikiwa hawakuwa na chanzo cha riziki zao, watu hao wasingeweza kuendelea kuishi. Yaani, kama kuna tatizo na riziki zao au kuendelea kwao kuishi, jamii hizo zisingeendelea kuwepo. Zisingeweza kuendelea kuishi, na zingeweza kupotea, kufutiliwa mbali kutoka duniani. Na ikiwa wale ambao wanalima kwa ajili ya riziki yao wangepoteza ardhi yao, kama hawangeweza kupanda vitu, na kupata vyakula vyao kutoka kwa mimea mbalimbali, matokeo yake yangekuwa nini? Bila chakula, je, watu wasingekufa kwa njaa? Ikiwa watu wangekufa kwa njaa, je, aina hiyo ya watu isingefutiliwa mbali? Kwa hiyo hili ni kusudi la Mungu katika kudumisha mazingira mbalimbali. Mungu ana kusudi moja tu katika kudumisha mazingira mbalimbali na mifumo ya ikolojia, kudumisha viumbe hai tofautitofauti ndani ya kila mazingira—ni kulea aina zote za watu, kuwalea watu pamoja na maisha katika mazingira ya kijiografia tofautitofauti.
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?