Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

204 Natamani Kusimama Tena

1

Utajiri na sifa ni kama pingu zinazoufunga moyo wangu.

Nanyenyekea mno, yote kwa ajili ya mafanikio.

Kuangaliwa mara moja, sauti moja ya kutoridhika kutoka kwa mwingine, huufanya moyo wangu kupigapiga.

Mimi kila mara hutafuta nafasi yangu katika umati, nikihofia kupuuzwa na wengine.

Moyo wangu unamilikiwa na malengo na tamaa ya kupita kiasi, sielewi thamani ya kufuatilia ukweli.

Uhasi mwingi sana, mafanikio mengi ya kazi, yote kwa ajili ya hadhi, sifa, na utajiri.

Katika kazi yangu na kuhubiri, najiona kuwa wa juu na kuringa; naacha vitu, na kulipa gharama, lakini hiyo, pia, ni kubadilishana na Mungu.

Mimi ni mbinafsi na mwenye aibu, sina kabisa ubinadamu, mwasi sana, ningewezaje kutodharauliwa na Mungu?

2

Ninapopambana katikati ya giza, roho yangu ni tupu sana.

Bila uwepo wa Mungu, mimi ni kama mfu anayetembea, aliyelemewa na mateso na uchungu.

Kila neno la Mungu ni ukweli; najidharau kwa kutoyathamini sana na kuyahifadhi.

Leo, baada ya kuonja kutokiukwa kwa tabia ya Mungu, nasujudu ardhini, nikiwa nimejawa na majuto.

Ee Mungu! Natamani majilio ya hukumu Yako, kama jangwa lenye kiu ya mvua.

Natamani kuishi katikati ya hukumu Yako na kuadibu Kwako, nisiishi tena kwa ajili ya Shetani.

Nadharau jinsi nilivyo dhaifu, jinsi nilivyomruhusu Shetani anikandamize.

Ee Mungu! Nakuomba Uwe na huruma, Uniruhusu nipokee hukumu na utakaso Wako.

3

Maneno ya Mungu ni kama upanga mkali, yanachoma roho yangu.

Ni sasa tu ndipo naona jinsi nilivyopotoshwa sana na Shetani, kwamba nimepoteza ubinadamu na urazini wangu.

Mimi ni vumbi, mdogo na duni; Mungu alinipa uzima, na Yeye ni mwenye huruma na hunihangaikia.

Bila kuzingatia mapenzi ya Mungu, mimi ni mdeni Wake mkubwa; kwa kweli sistahili kufurahia upendo wa Mungu.

Ee Mungu! Kumwokoa mwanadamu Umekuwa mwili kwa unyenyekevu, Ukivumilia fedheha miongoni mwa wanadamu.

Ulifanya kazi kwa bidii kwa ajili ya mwanadamu; upendo mwingi sana upo ndani ya maneno Yako.

Ninapojua wema na uzuri Wako, najidharau hata Zaidi.

Leo, ingawa nimeanguka, nataka kusimama tena, kujitoa kabisa kufuatilia ukweli na kuanza upya.

Iliyotangulia:Neno la Mungu ni Nuru

Inayofuata:Sitaacha Majuto Moyoni Mwangu

Maudhui Yanayohusiana