31. Wanawali wenye hekima ni nini? Wanawali wapumbavu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Zamani, watu wengine wamefanya utabiri kuhusu “mabikira watano wenye busara, mabikira watano wapumbavu”; ingawa utabiri huo si sahihi, si wenye makosa kabisa, kwa hiyo Naweza kuwapa ninyi maelezo fulani. Mabikira watano wenye busara na mabikira watano wapumbavu hakika hawawakilishi idadi ya watu, wala hawawakilishi watu wa aina moja mtawalia. Mabikira watano wenye busara wanamaanisha idadi ya watu, mabikira watano wapumbavu wanawakilisha watu wa aina moja, lakini hakuna kati ya hivi viwili vinarejelea wazaliwa wa kwanza, na badala yake vinawakilisha uumbaji. Hii ndiyo maana wameulizwa waandae mafuta katika siku za mwisho. (Uumbaji hauna sifa Yangu; kama wanataka kufanya wale wenye busara wanahitaji kuandaa mafuta, na hivyo wanahitaji kujitayarisha na maneno Yangu.) Mabikira watano wenye busara wanawakilisha wana Wangu na watu Wangu kati ya wanadamu ambao Niliumba. Kuwaita[a] “mabikira” ni kwa sababu ingawa wamezaliwa duniani, bado wanapatwa na Mimi; mtu anaweza kusema kwamba wamekuwa watakatifu, kwa hivyo wanaitwa “mabikira.” “Watano” liliotajwa awali linawakilisha idadi ya wana Wangu na watu Wangu ambao Nimewajaalia. “Mabikira watano wapumbavu” linarejelea watendaji huduma. Wananifanyia huduma bila kuweka kiwango kidogo zaidi cha umuhimu kwa maisha, wakifuatilia mambo ya nje pekee (kwa sababu hawana sifa Yangu, bila kujali kile wanachokifanya ni jambo la nje), na hawawezi kuwa wasaidizi Wangu wenye uwezo, kwa hiyo wanaitwa “mabikira wapumbavu.” “Watano” lililotajwa awali linamwakilisha Shetani, na wao kuitwa

“mabikira” kunamaanisha kwamba wameshindwa na Mimi na wanaweza kunifanyia huduma, lakini mtu wa aina hii si mtakatifu, kwa hivyo wanaitwa watendaji huduma.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 116” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Leo, wale wote ambao hufuata maneno ya sasa ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno ya leo ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. … “Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu. Kuwa na ufahamu wa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu si jambo rahisi, lakini kama watu wana nia ya kutii kazi ya Mungu kwa kudhamiria na kuitafuta kazi ya Mungu, basi watakuwa na nafasi ya kumwona Mungu, na watakuwa na nafasi ya kupata uongozi mpya zaidi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao hupinga kazi ya Mungu kwa kudhamiria hawawezi kupata nuru ya Roho mtakatifu au uongozi wa Mungu. Hivyo, kama watu wanaweza kupokea kazi ya karibuni zaidi ya Mungu au la hutegemea neema ya Mungu, hutegemea ukimbizaji wao, na hutegemea makusudi yao.

Wale wote ambao huweza kutii matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Haijalishi vile walikuwa, au vile Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kazi ndani yao—wale ambao wamepata kazi ya karibuni zaidi ni waliobarikiwa zaidi, na wale ambao hawawezi kufuata kazi ya karibuni zaidi huondoshwa. Mungu anataka wale wanaoweza kukubali nuru mpya, na Anataka wale ambao hukubali na kujua kazi Yake ya karibuni zaidi. Kwa nini husemwa kwamba lazima uwe mwanamwali safi? Mwanamwali safi anaweza kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu na kuelewa mambo mapya, na zaidi ya hayo, kuweza kuweka kando dhana za zamani, na kutii kazi ya Mungu leo.

Umetoholewa kutoka katika “Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa.

Umetoholewa kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Malengo ya kuonekana kwa Mungu, bila vizuizi vya nchi yoyote, ni kumruhusu Akamilishe kazi ya mpango Wake. Kwa mfano, Mungu alipopata mwili kule Uyahudi, lengo Lake lilikuwa kutimiza kazi ya msalaba na kuwakomboa wanadamu wote. Na bado Wayahudi waliamini kuwa Mungu asingeweza kulifanya hili, na wakafikiri kuwa Mungu asingeweza kuwa mwili na kuchukua umbo la Bwana Yesu. “Kutowezekana” kwao kukawa msingi wa kumshutumu na kumpinga Mungu na hatimaye ikawa kuangamizwa kwa Israeli. Leo hii, watu wengi wamefanya kosa lile lile. Wanatangaza kuonekana kwa Mungu ambako kumekaribia, na vilevile kukushutumu kuonekana huku; “kutowezekana” kwao kwa mara nyingine kunabana kuonekana kwa Mungu katika mipaka ya dhana zao. Na kwa hivyo Nimeona watu wengi wakicheka na kuanguka baada ya kuyasikia maneno ya Mungu. Kicheko hiki kinatofautianaje na shutuma na kukufuru kwa Wayahudi? Hamna moyo wa dhati katika kukabiliana na ukweli, sembuse kutamani ukweli. Nyinyi huchunguza tu kama vipofu na kusubiri kwa utepetevu. Mtajifaidi na nini kwa kutafiti na kusubiri kwa njia hii? Je, mnaweza kupata uongozi binafsi wa Mungu? Kama huwezi kuyang’amua matamshi ya Mungu, umehitimu vipi kushuhudia kuonekana kwa Mungu? Mahali ambapo Mungu anajitokeza, kuna maonyesho ya kweli, na kuna sauti ya Mungu. Ni wale tu wanaoukubali ukweli ndio watakaoisikia sauti ya Mungu, na ni hao tu waliowezeshwa kushuhudia kuonekana kwa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Wale “wanawali wenye hekima” ni wale ambao wanaweza kuijua sauti ya Mungu na kuitambua sauti ya “bwana harusi” na hivyo wanaweza kumkubali na kumtii Kristo, na hapokukaribishakukaribisha kurudi kwa Bwana na kuhudhuria karamu ya harusi ya Mwanakondoo. Kwa sababu “wanawali wapumbavu” hawaijui sauti ya “bwana harusi” na hawawezi kuitambua sauti ya Mungu, wanamkataa Kristo na kuendelea kumtamani sana Mungu asiye yakini mpaka wanapoachwa na kuondolewa na Mungu. Tunaweza kuona kwamba katika imani yetu, ni vigumu sana kumkubali Kristo bila imani ya kweli. Wale ambao wanakataa kumkubali Kristo wataikosa “sherehe ya harusi ya Mpendwa” na hawawezi kukubaliwa tena na Bwana nyumbani katika ufalme wa mbinguni na hawawezi kuingia katika sehemu ambayo Mungu amemwandalia mwanadamu. Hivyo, ikiwa watu wanaweza kumpokea Kristo wa siku za mwisho na kuitii kazi Yake ni sababu muhimu ya kuamua iwapo watu watafanikiwa au kutofanikiwa katika imani yao kwa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Bwana Yesu alitabiri katika Biblia kwamba wakati wa kurudi Kwake kutakuwa na aina mbili za watu—Aliwatumia mabikira wenye busara na mabikira wapumbavu kama mfano kwa waumini wote wa Enzi ya Neema: Wote wanaosikia sauti ya Mungu na wanaweza kuikubali na kuitii ni mabikira wenye busara; wote wasioweza kusikia sauti ya Mungu, wanaosikiliza lakini hawaamini na bado wanaikana, ni mabikira wapumbavu. Je, mabikira wapumbavu wanaweza kunyakuliwa? La, hawawezi. Kwa hiyo hawa mabikira wapumbavu na wenye busara wanaweza kufichuliwa vipi? Wanafichuliwa kupitia neno la Mungu, na kupitia mitazamo yao baada ya wao kusoma maneno ya Mungu katika siku za mwisho—Neno laonekana katika Mwili. Baada ya waumini wengine kuyasoma, wanasema, “Maneno ya kina kweli—maneno haya yana ukweli.” Baada ya wao kuyasoma tena kwa makini, wanasema, “Maneno haya hayawezi kuwa yametoka kwa mtu wa kawaida; yanaonekana kuwa yametoka kwa Mungu.” Kisha wanaangalia kwa makini tena na kusema, “Hii ni sauti ya Mungu; haiwezekani kwamba maneno haya yalitoka kwa mwanadamu!” Mtu huyu amebarikiwa; yeye ni bikira mwenye busara. Kuhusu mabikira wapumbavu, wengine ni wachungaji, wengine ni wazee, wengine ni wahubiri, na wengine ni waumini waliokanganywa wanaotaka tu kula hadi washibe. Mtazamo wao ni upi baada ya kusoma neno la Mungu? “Hmmm, maneno haya hayakubaliani na fikira na mawazo yangu, sikubaliani.” Na baada ya kuyasoma kwa makini tena, wanasema: “Baadhi ya maneno haya yanaonekana kuwa ya maana, lakini hilo haliwezekani; hii haiwezi kuwa kazi ya Mungu.” Kwa hiyo kwa mara nyingine tena, halikubaliani na fikira na mawazo yao. Mwishowe, kadiri wanavyolisoma, ndivyo linavyokubaliana na fikira zao kwa kiwango kidogo zaidi. Wanasema: “Hili silo neno la Mungu—siwezi kulikubali. Huyu ni bandia, Kristo wa uongo anayejaribu kuwadanganya watu. Siwezi kuliamini!” Huyu ni mtu wa aina gani? Huyu ni Mfarisayo, bikira mpumbavu. Wale ambao ni mabikira wenye busara na wale ambao ni mabikira wapumbavu wanafichuliwa na neno la Mungu. Ni neno la Mungu katika siku za mwisho linalowaainisha na kuwagawa katika makundi yao, na kisha Mungu ataanza kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu.

Umetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha, Juzuu ya 133

Mabikira wenye busara wataisikiza sauti ya Bwana, hasa kwa sababu ni wale wanauopenda na kuutafuta ukweli. Wanatamani kuonekana kwa Mungu; hii ndiyo maana wanaweza kutafuta na kuchunguza kuja kwa Bwana, na ndiyo maana wanaweza kuitambua sauti ya Bwana. Kwa kuwa mabikira wapumbavu hawaupendi ukweli, hawatafuti au kuchunguza kuja kwa Bwana, wakijua tu kushikilia sheria kwa ukaidi. Wengine wao wanasisitiza kwamba hawatamkubali au kumchunguza Bwana yeyote Asiyekuja juu ya wingu. Wengine wanatii utawala wa hila wa wachungaji na wazee wa dunia ya dini kikamilifu. Chochote ambacho wachungaji na wazee wanasema, watasikiza na kufuata. Wanamwamini Bwana kwa jina, lakini kwa kweli, wanafuata na kuwatii wachungaji na wazee hawa. hawaichunguzi njia ya kweli kwa ajili yao wenyewe na hawawezi kuitambua sauti ya Bwana. Wengine hata ni wapumbavu zaidi. Kwa kuwa kuna Makristo wa uongo wanaoonekana katika siku za mwisho, hawamtafuti au kumchunguza Kristo wa kweli na hata wanaweza kumkana na kumshutumu. Je, huku si kukata pua ili uunge wajihi? Hili pia ni dhihirisho la bikira mpumbavu.

Umetoholewa kutoka katika Majibu kwa Maswali ya Tamthilia

Tanbihi:

a. Maandiko ya awali hayana neno “Kuwaita.”

b. Maandiko ya awali hayana maneno “wao kuitwa.”

Iliyotangulia: 30. Kwa nini Mungu hawaokoi wale wanaofanyiwa kazi na pepo wabaya na wale waliopagawa?

Inayofuata: 32. Ni thawabu ipi inayopewa wanawali wenye hekima? Wanawali wapumbavu wataanguka katika maafa?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

5. Tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.

4. Sura ya tatizo la mtu asiyejua umuhimu wa jina la Mungu na asiyelikubali jina jipya la Mungu ni ipi?

Katika kila kipindi cha wakati, Mungu ataanza kazi mpya, na katika kila kipindi, patakuwepo na mwanzo mpya kwa mwanadamu. Laiti mwanadamu ashikilie tu ukweli kwamba “Yehova ni Mungu” na “Yesu ni Kristo,” ambao ni ukweli unaozingatiwa katika enzi moja tu, basi mwanadamu hatawahi kwenda sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, na daima hataweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Bila kujali jinsi Mungu anavyofanya, mwanadamu anafaa kufuata bila shaka lolote, na afuate kwa ukaribu. Kwa jinsi hii basi itakuwaje mwanadamu aondolewe na Roho Mtakatifu? Bila kujali kile anachofanya Mungu, kama mwanadamu ana uhakika ni kazi ya Roho Mtakatifu, na kushirikiana katika kazi ya Roho Mtakatifu bila mashaka yoyote, na kujaribu kufikia mahitaji ya Mungu, basi ataadhibiwaje? Kazi ya Mungu kamwe haijasimama, hatua Zake hazijakwama na kabla kukamilisha kazi Yake ya usimamizi, siku zote Mungu amekuwa mwenye kazi nyingi, na kamwe hajasimama.

2. Ni nini tofauti muhimu kati ya kuokolewa na wokovu?

Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki