Swali la 32: Mafarisayo mara kwa mara waliielezaBiblia kinaganaga kwa watu katika masinagogi, wakionekana kuwa wacha Mungu na wenye huruma, na kwa dhahiri hawakuonekana kufanya kitu chochote kinyume cha sheria. Kwa nini Mafarisayo walilaaniwa na Bwana Yesu? Unafiki wao ulidhihirishwaje? Kwa nini husemekana kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hutembea njia sawa na Mafarisayo wanafiki?

Jibu:

Watu wanaoamini katika Bwana wanajua kwamba Bwana Yesu kweli aliwachukia Mafarisayo na aliwalaani na kutamka dhiki saba juu yao. Hii ina maana sana katika kuruhusu waumini katika Bwana kutambua Mafarisayo wanafiki, kujitenga na utumwa na udhibiti wao na kupata wokovu wa Mungu. Hata hivyo, ni aibu. Waumini wengi hawawezi kutambua kiini cha unafiki wa Mafarisayo. Hata hawaelewi ni kwa nini Bwana Yesu aliwachukia na kuwalaani Mafarisayo sana. Leo tutazugumza kidogo kuhusu matatizo haya. Mafarisayo mara nyingi waliwafafanulia wengine Biblia katika sinagogi. Mara nyingi waliomba mbele ya wengine na kutumia sheria ya Biblia kuwalaani watu. Kwa waangalizi wa nje, walionekana kama waliofuata Biblia kwa staha sana. Kama ni hivyo, basi kwa nini Bwana aliwachukia na kuwalaani sana? Sababu kuu ni kwamba walijali tu kuhusu kufanya sherehe za dini na kufuata sheria; walifafanua tu kanuni na mafundisho katika Bibilia na kamwe hawakuwasiliana kwa karibu mapenzi ya Mungu na mtu yeyote, wala hawakulenga kutenda maneno ya Mungu au kutii amri za Mungu. Kwa kweli, walipuuza amri za Mungu. Kila kitu walichofanya kilikuwa kabisa upinzani kwa mapenzi na mahitaji ya Mungu. Hicho ndicho kiini cha unafiki wa Mafarisayo. Hiyo ndiyo sababu muhimu ya Bwana Yesu kuwachukia na kuwalaani. Bwana Yesu alisema vivyo hivyo wakati ambapo aliwafunua, “Kwa nini nyinyi pia mnavunja amri ya Mungu kwa utamaduni wenu? Kwani Mungu aliamuru, Akisema, Mwonyeshe babako na mamako heshima: na, Yule anayemlaani baba au mama yake, na afe hicho kifo. Lakini mnasema, Yeyote ambaye atamwambia baba au mama yake, ni zawadi, chochote ambacho ungefaidi kupitia mimi; Na asimwonyeshe baba yake au mama yake heshima, atakuwa huru. Hivyo hamjaibatilisha amri ya Mungu kwa utamaduni wenu. Nyinyi wanafiki, Isaya alitabiri vyema kuwahusu, akisema, Watu hawa wananikaribia kwa vinywa vyao, na wananiheshimu kwa midomo yao; lakini moyo wao uko mbali nami. Lakini wananiabudu bure, wakifunza mafundisho ya dini ambayo ni amri za wanadamu” (Mathayo 15:3-9). Sasa kwa kuwa Bwana Yesu amewafunua Mafarisayo, tunaweza kuona waziwazi kwamba ingawa Mafarisayo mara nyingi waliwafafanulia wengine Biblia katika sinagogi, Hawakumcha au kumtukuza Mungu katu. Hawakufuata amri za Mungu, na hata walibadilisha amri za Mungu na desturi za wanadamu; walisahau kuhusu amri za Mungu. Walikuwa wanampinga Mungu hadharani. Je, si huu ni ushahidi tosha wa jinsi ambavyo Mafarisayo walimtumikia Mungu ilhali pia walimpinga? Wangewezaje kuepuka kupata laana na chuki ya Mungu? Amri za Mungu zilisema waziwazi, “Usiue. … Usitoe ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yako” (Kutoka 20:13, 16). Lakini Mafarisayo walipuuza amri za Mungu. Walitoa ushahidi wa uongo hadharani na kuwalaani na kuwaua manabii na watu wenye haki waliotumwa na Mungu; walimpinga Mungu moja kwa moja. Kwa hivyo, Bwana Yesu aliwashutumu na kuwalaani Mafarisayo, Akisema, “Ninyi nyoka, nyinyi kizazi cha nyoka, mnawezaje kuepuka laana ya jahanamu? Hivyo, tazama, natuma kwenu manabii, na wanadamu wenye busara, na waandishi: na mtauwa na kusulubisha baadhi yao; na mtawacharaza baadhi yao katika masinagogi yenu, na kuwatesa kutoka mji mmoja hadi mji mwingine: Ili damu yote yenye haki iliyomwagika duniani iweze kuwa juu yenu” (Mathayo 23:33-35). Mafarisayo walimpinga Mungu mno na kuwaua manabii na watu wenye haki Aliowatuma. Walijaribu kuharibu kazi ya Mungu na kuzuia utekelezwaji wa mapenzi Yake. Walighadhabisha sana tabia ya Mungu. Wangewezaje kutolaaniwa na Yeye? Kila kitu ambacho Mafarisayo walifanya kilikuwa ukweli, siyo? Je, hatuwezi kuona kiini na tabia yenye unafiki ya Mafarisayo?

Mafarisayo walionekana wenye staha kutoka nje, lakini kiini chao kilikuwa cha kudhuru sirini na cha hila; walikuwa hasa wenye ujuzi katika kujifanya na kuwadanganya wengine. Kama Bwana Yesu hangeyafichua matendo yao yote maovu, yakiwa ni pamoja na usaliti na utelekezwaji wa amri za Mungu, tusingeweza kuona asili ya unafiki wa Mafarisayo. Sasa tuangalie tena mfichuo na hukumu ya Bwana Yesu ya Mafarisayo. “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, ninyi wanafiki! kwani mnatoa fungu la kumi la mnanaa na bizari na jira, na mmeacha mambo muhimu zaidi ya sheria, hukumu, fadhili, na imani: mlipaswa kuyafanya haya, na sio kutolifanya lingine. Nyinyi viongozi vipofu, mnaochunguza sana visubi, na kumeza ngamia” (Mathayo 23:23-24). “Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, nyinyi wanafiki! Kwani nyinyi ni kama makaburi yaliyopakwa rangi nyeupe, ambayo kwa nje yanaonekana mazuri sana, lakini ndani yake mna mifupa ya wafu, na yenye uchafu wote. Hata hivyo ninyi pia mnaonekana wenye haki kwa wanadamu, lakini ndani yenu mmejaa unafiki na dhambi” (Mathayo 23:27-28). Mafarisayo walijifanya kuwa wenye staha sana mbele ya wengine. Waliomba kwa makusudi katika sinagogi na pembeni mwa mitaa. Walipofunga, walikuwa na onyesho la huzuni katika nyuso zao kwa makusudi. Waliandika maandiko kwenye shada za nguo zao. Walihakikisha kwamba watu wengine waliwaona wakifanya hivyo. Walihakikisha hawakusahau kulipa fungu la kumi la nanaa, jira na bizari. Hata walifuata amri nyingi za kihistoria kama vile, “Usile isipokuwa kama umenawa mikono kabisa” nk. Mafarisayo shughulikia maelezo mengi madogo vizuri sana. Hata hivyo, hawakutii matakwa ya Mungu ya sheria, yaani kumpenda Mungu, kuwapenda wengine, kuwa mwenye haki, mwenye huruma, na mwaminifu. Hawakutii amri za Mungu wakati wote. Walizungumza tu kuhusu maarifa ya kibiblia na nadharia ya kiteolojia. Walifanya tu sherehe za dini na kutii sheria. Huu ndio upeo wa unafiki wao na jinsi walivyowadanganya wengine. Tabia zao zinatuonyesha waziwazi kwamba kila kitu ambacho Mafarisayo walifanya kilikuwa sehemu ya jaribio lao la kuwadanganya na kuwazuia wengine. Walitafuta kujiimarisha wenyewe hivyo wangeabudiwa. Walijishughulisha tu na kusimamia na kuimarisha vyeo vyao na riziki. Walisafiri kwenye njia ya uongo ya unafiki na upinzani kwa Mungu. Hiyo ndiyo sababu kuwa upinzani wao kwa Mungu ulimfanya Mungu kuwalaani.

Mafarisayo hawaupendi ukweli. Kamwe hawakutia maanani kutenda maneno ya Mungu au kutii amri za Mungu. Walilenga tu kufanya sherehe za dini na kutembea kwenye njia ya upinzani kwa Mungu. Kwa hiyo, Bwana Yesu alipokuja kufanya kazi na kuhubiri, asili yao ya kishetani ya unafiki na uadui dhidi ya Mungu ilifunuliwa kikamilifu na Mungu. Mafarisayo walijua vizuri sana kwamba maneno ya Bwana Yesu yalikuwa na mamlaka na nguvu. Licha ya wao kutotafuta kiini na chanzo cha maneno na kazi ya Bwana Yesu, pia walimshambulia na kumkashifu Bwana Yesu kwa nia mbaya; walisema Bwana Yesu alikuwa akiwatoa pepo kwa kutumia mkuu wa pepo; walipachika kazi ya Bwana Yesu, iliyojawa na mamlaka Mungu na nguvu, jina la wazimu. Walifanya dhambi ya kukufuru dhidi ya Roho Mtakatifu na wakakosea sana tabia ya Mungu. Walikosea tabia ya Mungu. Mafarisayo hawakumkufuru na kumlaani Bwana Yesu tu wenyewe, lakini pia waliwachochea na kuwalaghai waumini ili wampinge na kumlaani Bwana Yesu. Waliwafanya waaminifu kupoteza wokovu wa Bwana na kugeuka kuwa vitu vya mazishi na waathiriwa wao. Kwa hivyo, wakati ambapo Bwana Yesu aliwashutumu na kuwalaani, Alisema, “Lakini ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnafunga ufalme wa mbinguni wasiingie wanadamu: kwani ninyi hamwingii wenyewe, wala hamkubali wanaoingia ndani waingie” (Mathayo 23:13). “Ole wenu nyinyi, waandishi na Mafarisayo, mlio wanafiki! Kwa maana mnazingira bahari na ardhi kwa ajili ya kumfanya mtu kubadili imani, na anapobadili, mnamfanya awe mwana wa kuzimu mara dufu zaidi kuwaliko” (Mathayo 23:15). Kwa hivyo, tunaweza kuona kwamba Mafarisayo walikuwa wanafiki ambao walimpinga na kumkufuru Mungu, wapinga Kristo waliosimama kama adui kwa Mungu. Walikuwa kundi lenye uovu ambalo liliteketeza nafsi za watu na kuwavuta hadi Jehanamu. Kwa hivyo, Bwana Yesu aliwalaanu Mafarisayo kwa “dhiki saba” kutokana na tabia yao ya mbovu. Hii inaonyesha kikamilifu utakatifu wa Mungu na tabia ya Mungu ya haki ambayo haiwezi kukosewa.

Sasa tumepata utambuzi kiasi kuhusiana na asili ya Mafarisayo yenye unafiki. Sasa hebu tuangalie wachungaji na wazee wa kanisa wa kisasa. Wao hufafanua tu maarifa ya kibiblia na nadharia ya kiteolojia. Wao hufanya tu sherehe za dini na kufuata amri. Huwa hawatendi maneno ya Mungu katu, wala hawatekelezi amri Zake. Wao ni sawa na Mafarisayo, wakitembea kwenye njia ambapo wanamtumikia lakini pia kumpinga Mungu. Bwana Yesu alisema, “Yesu akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako mzima, na roho yako nzima, na akili yako nzima. Hii ni amri ya kwanza na kubwa. Na ya pili ni kama hiyo, Mpende jirani yako kama unavyojipenda” (Mathayo 22:37-39). Wampendao Mungu wanapaswa kutenda maneno Yake na lazima wayazingatie mapenzi Yake. Wanapaswa kuwajibika kwa ajili ya maisha ya ndugu zao. Sasa wachungaji na wazee wa kanisa wanakabiliana na makanisa yenye ukiwa na imani ya waumini na upendo unapunguka. Hawaongozi waumini kutafuta ukweli na kutafuta kanisa ambalo lina kazi ya Roho Mtakatifu. Badala yake, wao huwadhibiti waumini kwa karibu. Hasa Mwenyezi Mungu anapokuja kuonyesha ukweli na kuwapa watu uzima, wanaukataa; hawauchunguzi au kukubali. Wanaendelea kupinga na kuulaani huku wakiwazuia waumini kutafuta njia ya kweli. Hawaruhusu waumini kuwasiliana na watu kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu, wala kuwaruhusu kusoma wa maneno ya Mwenyezi Mungu. Wao hulaani au kushambulia ndugu zetu ambao hueneza injili ya ufalme Wake. Wanaweza hata kuwaita polisi na kuwafanya wakamatwe. Si wanafanya maovu na kumpinga Mungu na kila kitu wanachofanya? Kuna tofauti gani katika ya wanachofanya na jinsi Mafarisayo walimpinga na kumshutumu Bwana Yesu? Ili kulinda vyeo vyao na riziki, wachungaji na wazee wa kanisa huwazuia waumini kukubali wokovu wa Mungu katika siku za mwisho. Je si wanawavuta watu hadi kuzimu? Je, si wao ni watumishi waovu ambao Bwana Yesu alizungumzia? Je, si wao ni Mafarisayo wa kisasa? Je, bado tunaweza kutambua hili?

Wachungaji na wazee wa kanisa bila shaka si waumini wa kweli au watumishi wa Mungu. Wao daima husaliti maneno ya Bwana, hutelekeza amri Zake na kumchukulia kama adui yao. Inapofikia kuhusu ni watu wa aina gani wanaoweza kuingia katika ufalme wa mbinguni, Bwana Yesu alisema kwamba ni wale tu wanaofanya mapenzi ya Baba wa Mbinguni wataruhusiwa kuingia katika ufalme Wake. Hata hivyo, wachungaji na wazee wa kanisa husema kwamba kwa kuwa watu wamethibitishwa kuwa halali na imani na wameokolewa kwa neema wataingia katika ufalme wa Mbinguni. Je, si wanayasaliti maneno ya Bwana na kuzungumza kwa kumpinga moja kwa moja? Bwana Yesu alihitaji kwamba “Lakini acheni maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; La, la” (Mathayo 5:37). Hata hivyo, wachungaji na wazee wa kanisa hueneza uongo, hulaani na kumkufuru Mwenyezi Mungu. Wanatoa ushahidi wa uongo na kukashifu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Bwana Yesu alisema waziwazi, “Yeye ambaye humpokea yeyote nimtumaye hunipokea Mimi” (Yohana 13:20). Wachungaji na wazee wa kanisa hawaruhusu waumini kupokea ndugu ambao hueneza injili ya ufalme. Yeyote anayewapokea hutupwa nje ya Kanisa. Bwana Yesu anahitaji watu kuwa wanawali wenye busara, kusikiliza sauti ya Bwana arusi na kwenda kumlaki. Hata hivyo, kila wachungaji na wazee wa kanisa wanaposikia mtu akishuhuda kwa kurudi kwa Bwana Yesu. Wao huhukumu na kuulaani bila kamwe kuuchunguza. Kweli sijui ni sentensi gani ya maneno ya Bwana ambayo wachungaji na wazee wa kanisa wanatenda. Kama wachungaji na wazee wa kanisa kweli waliamini katika Mungu, kama walikuwa angalau kidogo wacha Mungu kabisa, hawangeeneza aina hizi za uongo, wala wasingeshutumu na kupinga Mwenyezi Mungu mno. Hii ni kweli. Wachungaji na wazee wa kanisa ni Mafarisayo wa kisasa. Hii ni sahihi kabisa!

Kimetoholewa Kutoka Katika Majibu ya Mswada wa Filamu

Hapo zamani, Mafarisayo Wayahudi mara nyingi walieleza Maandiko na kuwaombea waumini katika masinagogi. Je, hawakuonekana kuwa wacha Mungu mbele ya watu pia? Basi kwa nini Bwana Yesu aliwafunua na kuwalaani Mafarisayo, akisema ole wao Mafarisayo wanafiki? Je, Bwana Yesu anaweza kuwa Aliwakosea? Je, watu hawaamini kwamba neno la Bwana Yesu ni ukweli? Je, watu bado wanashuku kuwa Bwana Yesu alifanya jambo baya? Kutofautisha kama wachungaji na wazee ni Mafarisayo wanafiki na wapinga Kristo au la hakuwezi kufanywa kwa kuangalia tu jinsi wanavyowatendea watu vizuri kwa nje. Jambo la msingi ni kuangalia jinsi wanavyomtendea Bwana na ukweli. Kwa nje wanaweza kuwa na upendo kwa waumini, lakini wana upendo kwa Bwana? Ikiwa wana upendo kabisa kwa watu lakini wamejawa na uchovu na chuki kwa Bwana na kweli, na kumhukumu na kumshutumu Kristo wa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu, basi wao si Mafarisayo wanafiki? Je, sio wapinga Kristo? Wanaonekana kuhubiri na kufanya kazi kwa bidii nje, lakini ikiwa ni kwa ajili ya kuvikwa taji na kuzawadiwa, basi hii inamaanisha kwamba ni watiifu na waaminifu kwa Bwana? Ili kutofautisha kama mtu ni mnafiki, zaidi unapaswa kuangalia ndani ya mioyo yao na kuona malengo yao. Hilo ndilo jambo muhimu zaidi kuhusu kutofautisha. Ni baada ya mawasiliano kama hayo tu ndiyo ninaelewa! Mungu huchunguza mioyo ya watu. Hivyo ili kuona kama mtu kweli anampenda na anamtii Bwana, jambo kuu ni kuangalia kama anafanya na kuzingatia neno Lake na kuzingatia amri Zake, na zaidi angalia kama wanamtukuza Bwana Yesu na kushuhudia Bwana Yesu, na ikiwa wanafuata mapenzi ya Mungu. Tunaona kwamba Mafarisayo mara nyingi walieleza Maandiko kwa watu katika masinagogi, walishikilia sheria za Biblia kwa kila kitu, na pia walikuwa na upendo kwa watu. Lakini kwa kweli, kila kitu walichofanya hakikuwa kutenda neno la Mungu au kuzingatia amri za Mungu, lakini ilifanyika kuonekana na watu. Kama Alivyosema Bwana Yesu alipowafunua: “Lakini vitendo vyao vyote huvitenda ili vionekane na watu: hupanua visanduku vyao vya maandishi, na hutanua mapindo ya nguo zao” (Mathayo 23:5). Wao hata walisimama kwa makusudi katika masinagogi na kwenye pembe za mitaani ili kushiriki katika sala ndefu. Wakati wa kufunga wao kwa makusudi walifanya nyuso zao kuangalia huzuni sana, ili watu waweze kujua kuwa walikuwa wanafunga. Walifanya hata kwa makusudi matendo mema mitaani ili watu wote waweze kuona. Hata waliendelea kushikilia mila ya kale na mila ya kidini kama vile “usile kama hujaosha mikono kwa uangalifu.” Kuwadanganya watu kuwasaidia na kuwaabudu, Mafarisayo kuendelea kufanya mambo madogo yaonekane kuwa makubwa ili wajifiche, na waliwaongoza watu tu kushiriki katika ibada za kidini, kuimba na kusifu, au kushikilia mila kadhaa za mababu, lakini hawakuwaongoza watu kutenda neno la Mungu, kushikilia amri za Mungu, na kuingia katika uhakika wa ukweli. Aidha, hawakuwaongoza watu kutenda ukweli na kumtii na kumwabudu Mungu. Yote waliyofanya yalikuwa kutumia vitendo vingine vya nje ili kuwachanganya na kuwadanganya waumini! Wakati Bwana Yesu alikuja kuhubiri na kufanya kazi, kwa ajili ya kulinda hadhi zao na riziki zao, Mafarisayo hawa ambao walijifanya kuwa wacha Mungu kwa hakika waliacha sheria na amri za Mungu waziwazi chini ya kisingizio cha “kulinda Biblia.” Walibuni uvumi, walitoa ushahidi wa uongo, na wakamhukumu kwa ukali na kumsingizia Bwana Yesu, wakifanya yote waliyoweza kuwazuia waumini wasimfuate Bwana Yesu. Mwishowe, hata walishirikiana na wale walio mamlakani kumtundika Bwana Yesu msalabani! Hivyo, unafiki wa Mafarisayo na kuchukia kwao kwa ukweli kulifunuliwa kabisa. Kiini chao cha upinga Kristo hivyo kilifunuliwa kabisa. Hii inaonyesha kwamba kiini cha Mafarisayo kilikuwa na unafiki, kidanganyifu, cha uongo na kiuovu. Wote walikuwa wachungaji wa uongo ambao waliacha njia ya Mungu, waliwadanganya watu na waliwafungia watu! Waliwadanganya na kuwafunga waumini, wakiudhibiti ulimwengu wa kidini kumpinga Mungu, wakikataa kwa ukali, kumshutumu na kumchukia Kristo mwenye mwili. Hii inatosha kuthibitisha kuwa walikuwa wapinga Kristo ambao walitaka kuimarisha utawala wao wenyewe wa kujitegemea!

Sasa tunaona wazi maneno mbalimbali ya unafiki wa Mafarisayo, tunapowafananisha na wachungaji wa kidini na wazee wa leo, je, hatutambua kwamba wao ni kama Mafarisayo? na wote ni watu ambao hawatendi neno la Bwana au kuzingatia amri za Bwana, na zaidi ya hayo si watu wanaomwinua Bwana na kumshuhudia Bwana? Wao ni watu tu ambao wanaamini kwa upofu katika Biblia, kuabudu Biblia, na kuinua Biblia. Wanashikilia tu ibada mbalimbali za dini, kama vile kuhudhuria huduma za mara kwa mara, kesha za asubuhi, kuvunja mkate, kushiriki katika Sakramenti Takatifu, na kadhalika. Wao huwa makini na kuzungumza na watu juu ya kuwa wanyenyekevu, wenye subira, wacha Mungu na wenye upendo, lakini hawampendi Mungu mioyoni mwao, na zaidi ya hayo hawamtii Mungu na hawana moyo unaomwogopa Mungu. Kazi yao na mahubiri yanalenga tu kuendelea na kueleza ujuzi wa Biblia na nadharia ya kiteolojia. Lakini linapokuja suala la jinsi ya kutenda na kujifunza neno la Bwana, jinsi ya kuzingatia amri za Bwana na jinsi ya kueneza na kulishuhudia neno la Bwana, jinsi watu wanapaswa kufuata mapenzi ya Baba wa mbinguni, jinsi ya kumpenda Mungu kweli, kumtii Mungu, na kumwabudu Mungu, na mambo haya yote ambayo Bwana Yesu anahitaji kwa wanadamu, hawatafuti, wala kuchunguza, na wala hawajui nia za Bwana, na hata hivyo usiwaongoza watu kufanya mazoezi au kuzingatia. Kusudi lao wanazunguka kila mahali wakihubiri ujuzi wa Biblia na nadharia ya kiteolojia ni kujionyesha wenyewe, kujijenga wenyewe, na kuwafanya watu kuwatazamaia na kuwaabudu yao. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu alipokuja kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho, hawa wachungaji na wazee, kwa ajili ya kufikia mamlaka ya kudumu katika ulimwengu wa kidini, na kwa tamaa yao kuu ya kuwadhibiti waumini na kujenga ufalme wao wenyewe wa kujitegemea, ilikiuka wazi wazi neno la Bwana Yesu, kubuni uvumi, kuhukumu, kushambulia na kumkufuru Mwenyezi Mungu, kufanya vyovyote ili kuwazuia waumini kutokana na kuchunguza njia ya kweli. Kwa mfano, Bwana Yesu aliwafundisha watu kuwa wanawali wenye busara: Mtu anaposikia mtu akisema “Tazama, anakuja bwana arusi,” anapaswa kwenda kumpokea. Lakini baada ya wachungaji na wazee kusikia habari ya kuja kwa pili kwa Bwana Yesu, wao badala yake walifanya yote waliyoweza kufunga kanisa na kuwazuia waumini wasitafute na kuchunguza njia ya kweli! Bwana Yesu alitufundisha “Mpende jirani yako kama unavyojipend.” Na bado, waliwachochea waumini kukashifu na kuwapiga ndugu ambao wanashuhudia kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Bwana Yesu alimwambia mwanadamu asiseme uongo, asishuhudie uongo, lakini wachungaji na wazee walibuni uongo wa kila aina kumtukana Mwenyezi Mungu, na hata kuungana na CCP ya kishetani kupinga, kushutumu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho na kulipaka tope Kanisa la Mwenyezi Mungu. Kutoka kwa hili tunaweza kuona kwamba kile ambacho wachungaji wa kidini na wazee wamesema na kufanya kabisa kinakiuka mafundisho ya Bwana. Wao ni kama Mafarisayo wanafiki. Wao ni watu wote ambao huongoza bila kufikiria, kumpinga Mungu, na kuwadanganya watu.

Niruhusu nisome kifungu cha neno la Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Wale wote ambao hawatafuti utii kwa Mungu kwa imani yao wanampinga Mungu. Mungu anaomba kwamba watu watafute ukweli, kwamba wawe na kiu ya neno la Mungu, na wanakula na kunywa maneno ya Mungu, na kuyaweka katika matendo, ili waweze kupata utii kwa Mungu. Kama motisha zako ni hizo kweli, basi Mungu atakuinua juu hakika, na hakika Atakuwa mwenye neema kwako. Hakuna anayeweza kutilia shaka hili, na hakuna anayeweza kulibadilisha. Ikiwa motisha zako sio kwa ajili ya utii kwa Mungu, na una malengo mengine, basi yote ambayo unasema na kufanya—maombi yako mbele ya Mungu, na hata kila tendo lako—litakuwa linampinga Mungu. Unaweza kuwa unaongea kwa upole na mwenye tabia ya upole, kila tendo lako na yale unayoyaonyesha yanaweza kuonekana ni sahihi, unaweza kuonekana kuwa mtu anayetii, lakini linapofikia suala la motisha zako na mitazamo yako juu ya imani kwa Mungu, kila kitu unachofanya kipo kinyume cha Mungu, na ni uovu. Watu wanaoonekana watii kama kondoo, lakini mioyo yao inahifadhi nia mbovu, ni mbwa mwitu katika ngozi ya kondoo, wanamkosea Mungu moja kwa moja, na Mungu hatamwacha hata mmoja. Roho Mtakatifu atamfichua kila mmoja wao, ili wote waweze kuona kwamba kila mmoja wa hao ambao ni wanafiki hakika watachukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Usiwe na shaka: Mungu atamshughulikia na kumkomesha kila mmoja” (“Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Wachungaji wa kidini na wazee huonekana nje kuwa wanyenyekevu, wenye subira na upendo, lakini mioyoni mwao wamejaa uongo, udanganyifu na uovu. Chini ya kisingizio cha “kulinda njia ya kweli, kulinda kundi,” wao hupinga wazi na kumhukumu Mwenyezi Mungu na kupanga kuwadhibiti waumini ili kufikia lengo la mamlaka ya kudumu katika ulimwengu wa kidini na kuanzisha utawala wao wenyewe wa kujitegemea. Mafarisayo hawa wanafiki wanaowachukia ukweli na kumchukia Mungu ni hasa kikundi cha wapinzani wasumbufu wa Mungu waliowekwa wazi na kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Kwa hiyo, wote ambao kweli wanamwamini Mungu wanapaswa kujifunza jinsi ya kutofautisha asili yao ya unafiki na asili ya kishetani, na ya upinga Kristo. Usidanganyifu, usichanganywe, kufungiwa na kudhibitiwa nao tena. Unapaswa kutafuta na kuchunguza njia ya kweli na kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, na kurudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu!

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Iliyotangulia: Swali la 31: Unashuhudia kuwa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Neno Laonekana katika Mwili ni maneno ya Mungu Mwenyewe, lakini tunaamini kuwa ni maneno ya mtu aliyepatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, Kile ningependa kufuatilia ni, ni nini hasa tofauti kati ya maneno yanayoonyeshwa na Mungu mwenye mwili na maneno yaliyosemwa na mtu ambaye amepatiwa nuru na Roho Mtakatifu?

Inayofuata: Swali la 33: Wakati huo, wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, Mafarisayo Wayahudi walimkana na kumhukumu Yeye vikali na kumtundika msalabani. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anapokuja kufanya kazi Yake, wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa pia wanamkana Yeye vikali na kumhukumu Yeye, wakimtundika Mungu msalabani tena. Kwa nini Mafarisayo Wayahudi na wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa huuchukia ukweli hivyo na kumpinga vikali Kristo kwa njia hii? Ni nini hasa kiini chao cha asili?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

4. Iwapo wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote kweli wamewekwa na Mungu, na iwapo kuwatii wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa ni kumtii na kumfuata Mungu?

Ingekuwa vyema kwa wale watu wanaosema kuwa wanamfuata Mungu kufungua macho yao watazame vizuri waone ni nani wanayemwamini hasa: Je, ni Mungu unayemwamini hakika, ama Shetani? Ikiwa unajua kuwa unayemwamini si Mungu ila sanamu zako mwenyewe, basi ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Ikiwa hakika hujui unayemwamini ni nani, basi, pia, ni vyema kabisa usiseme kuwa wewe ni muumini. Kusema hivi kutakuwa kukufuru! Hakuna anayekushurutisha umwamini Mungu. Msiseme kuwa mnaniamini Mimi, kwa kuwa Niliyasikia maneno hayo hapo kale wala Sitamani kuyasikia tena, kwa kuwa mnachoamini ni sanamu zilizo katika mioyo yenu na nyoka waovu wa ndani walio miongoni mwenu. Wale wanaotikisa vichwa vyao wanaposikia ukweli, wanaotabasamu sana wanaposikia mazungumzo ya kifo ni watoto wa Shetani, na wote ni vyombo vya kuondolewa.

6. Sababu ya kusemwa kuwa kupata mwili kuwili kwa Mungu hukamilisha umuhimu wa kupata mwili

Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki