Swali la 40: Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, huonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ya kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, na bado Yeye hukabiliwa na uasi mkali na uchukuliwaji wa hatua kali wa ukatili wa ulimwengu wa kidini na serikali ya Kikomunisti ya China. Serikali ya CCP hata huhamasisha vyombo vyake vyote vya habari na majeshi kumshutumu Kristo, kukufuru dhidi Yake, kumtia mbaroni na kumwangamiza. Wakati Bwana Yesu alizaliwa, Mfalme Herode alisikia kuwa “Mfalme wa Israeli” alikuwa amezaliwa na akaamrisha watoto wote wa kiume wauawe Bethlehemu na wa chini ya umri wa miaka miwili; ingekuwa afadhali kwake kuwaua watoto elfu kumi kuliko kumwacha Kristo aishi. Mungu amekuwa mwili ili kuwaokoa wanadamu, hivyo kwa nini ulimwengu wa kidini na serikali kana Mungu hushutumu na kukufuru dhidi ya kuonekana na kazi ya Mungu? Kwa nini wanaipinda nguvu ya nchi yote na kutumia jitihada zote kumtundika Kristo msalabani? Kwa nini wanadamu ni waovu sana, na kwa nini wanamchukia Mungu hivyo na kujiweka dhidi Yake?

Jibu:

Swali hili kweli ni muhimu sana na ni wachache sana katika binadamu wote ndio wanaweza kuelewa hili kabisa! Kwa nini binadamu wanamwasi Mungu kwa kichaa imekuwa vichwa vya habari, na tanzia ya kihistoria ya Kristo mwenye mwili kusulubiwa msalabani inajirudia tena; je, huu si ukweli? Hebu tusome vifungu vingine la Maandiko, Bwana Yesu alisema, “Na hii ndiyo shutuma, ya kwamba mwanga umekuja duniani, na wanadamu walipenda kiza badala ya mwanga, kwa kuwa vitendo vyao vilikuwa viovu. Kwa kuwa kila mtu afanyaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwa mwanga, vitendo vyake visije vikashutumiwa” (Yohana 3:19-20), “Ikiwa dunia ikiwachukia, ninyi mnajua ya kwamba ilinichukia mimi kabla iwachukie ninyi” (Yohana 15:18), “Hiki ni kizazi kibaya” (Luka 11:29). Biblia inasema, “Ulimwengu mzima uko ndani ya maovu” (1 Yohana 5:19). Hatukuelewa hasa tuliposoma maneno haya katika Biblia awali. Ni tunapoona tu kwamba kupata mwili kuwili kwa Mungu kumepitia shutuma ya pamoja, kuwindwa na ukandamizaji wa serikali za kumkana Mungu na dunia ya kidini, hata hivyo, ndipo tunaelewa kwamba maneno haya ndani ya Biblia hakika ni ya kweli. Matendo ya binadamu na mtazamo wanaochukua katika kumtendea Kristo unatosha kuthibitisha kwamba dunia nzima iko chini ya Shetani kabisa na katika mamlaka yake. Siku hizi, wengi wetu tunaweza kuona wazi kwamba wengi wa wachungaji na wazee wa dunia ya kidini ni watu wanaoasi, kumshutumu na kumkataa Kristo, na kwamba dunia ya kidini tangu kitambo imekuja chini ya udhibiti wa hawa Mafarisayo wanafiki na wapinga Kristo. Kwa hivyo, Mungu mwenye mwili anapoonekana na kufanya kazi, wachungaji na wazee katika dunia ya kidini ndio wa kwanza kuinuka na kumshutumu na kumkataa—hili haliepukiki. Serikali ya CCP ni mamlaka ya kishetani ambayo inachukia ukweli zaidi na kumpinga Mungu, na kila wakati imekuwa ikiwakamata na kuwatesa Wakristo. Kristo wa siku za mwisho Alipokuja kuonekana na kufanya kazi Yake nchini China, serikali ya CCP kwa ufidhuli na ukatili ilijaribu kumwinda, kumkamata na kumwondoa Kristo, ikisababisha mawimbi katika dunia nzima. Huu ukweli ulitimiza kabisa unabii wa Bwana Yesu: “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24-25). Mungu amepata mwili mara mbili miongoni mwa wanadamu kuzungumza na kufanya kazi, kukomboa binadamu na kuwaokoa binadamu, nyakati zote mbili akiteseka shutuma, kufuru, kuwindwa na ukandamizaji wa pamoja uliotekelezwa na viongozi wa kidini na chama kinachotawala; ukweli huu unatosha kuthibitisha kwamba dunia hii ni yenye giza sana na ovu na kwamba binadamu wamepotoshwa sana kwa kina! Binadamu wamepotoshwa na kuharibiwa kufikia kiasi kwamba wamechoshwa kabisa na ukweli, wanauchukia ukweli, wanaenzi uovu na wanajiweka katika upinzani na Mungu, kuwa wa aina moja na Shetani na kuwa watoto wa Shetani, wasiweze kabisa kuvumilia kuwepo kwa Mungu. Udhihirisho na kazi ya Mungu mwenye mwili lazima hata hivyo bila kuzuilika upitie mateso na kuachwa. Na kuhusu kwa nini binadamu wanampinga Mungu, Mwenyezi Mungu amefunua kipengele hiki cha ukweli, na tutaelewa kuhusu hili baada ya kusoma vifungu kadhaa vya maneno ya Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu anasema, “Mwanadamu ameendelea kwa makumi ya maelfu ya miaka ya historia mpaka kufikia alipo leo. Hata hivyo, mwanadamu wa uumbaji Wangu wa asili kwa muda mrefu uliopita amezama katika upotovu. Tayari amecha kuwa kile Ninachotaka, kwa hivyo wanadamu, Ninavyowaona, hawastahili tena jina la uanadamu. Badala yake wao ni uchafu wa wanadamu, ambao Shetani amewateka nyara, maiti zilizooza zinazotembea ambamo Shetani huishi na huvalia. Watu hawaamini hata kidogo kuwepo Kwangu, wala hawakaribishi kuja Kwangu” (“Maana ya Kuwa Mtu Halisi” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi” (“Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Mwanadamu si kitu kingine ila ni adui Yangu. Mwanadamu ni yule mwovu anayenipinga na kuniasi. Mwanadamu si mwingine ila kizazi cha yule mwovu aliyelaaniwa na Mimi. Mwanadamu si mwingine ila ukoo wa malaika mkuu ambaye alinisaliti Mimi. Mwanadamu si mwingine ila mrithi wa shetani ambaye, akiwa amekataliwa kwa dharau na Mimi kitambo, amekuwa adui Wangu asiyeweza kupatanishwa tangu wakati huo” (“Maana ya Kuwa Mtu Halisi” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Shetani huwapotosha watu kwa kupitia masomo na ushawishi wa serikali za kitaifa na walio mashuhuri na wakuu. Upuuzi wao umekuwa uzima wa mwanadamu na asili. ‘Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa’ ni msemo wa kishetani unaojulikana sana ambao umeingizwa ndani ya kila mtu na umekuwa maisha ya watu. Kuna maneno mengine ya falsafa ya kuishi ambayo pia ni kama haya. Shetani hutumia utamaduni mzuri wa kila taifa kuwaelimisha watu, akisababisha wanadamu kuanguka ndani na kumezwa na lindi kuu lisilo na mipaka la uharibifu, na mwishowe watu wanaangamizwa na Mungu kwa sababu wanamtumikia Shetani na kumpinga Mungu” (“Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo).

Kwa sababu ya kuzaliwa katika nchi ya uchafu vile, mwanadamu ameangamizwa kabisa na jamii, amekuwa akishawishiwa na maadili ya kikabaila, na amefundisha katika ‘taasisi za elimu ya juu.’ Fikra zilizo nyuma kimaendeleo, maadili potovu, mtazamo mbaya juu ya maisha, falsafa za kudharauliwa za kuishi, uwepo usio na thamani, na hali potovu za maisha na desturi—mambo yote haya yameuingilia moyo wa mwanadamu, na kudhoofisha na kushambuliwa dhamiri yake pakubwa. Matokeo yake, mwanadamu kamwe yuko mbali kutoka kwa Mungu, na kila mara anampinga” (“Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa imani kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalia kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha. … Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu” (“Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Hakuna anayetafuta nyayo za Mungu kwa vitendo au kuonekana Anakoonyesha, na hakuna aliye na hiari ya kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani, yule mwovu, ili kurekebishwa kufuatana na dunia hii na kanuni za kuwepo ambazo watu waovu hufuata. Wakati huu, moyo na roho za mwanadamu hutolewa ushuru kwa shetani na kuwa riziki ya Shetani. Hata zaidi, moyo wa binadamu na roho yake zimekuwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na uwanja wake wa kuchezea unaofaa. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni za kuwa binadamu, na wa thamani na maana ya kuwepo kwa binadamu. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu, na yeye huacha kumtafuta na kumsikiza Mungu. Wakati upitavyo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu na yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu kisha huanza kupinga sheria na amri za Mungu na moyo na roho zake hufishwa…. Mungu humpoteza mwanadamu ambaye Alimuumba mwanzoni, na mwanadamu hupoteza mzizi wa mwanzo wake: Hii ndiyo huzuni ya hii jamii ya wanadamu” (“Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanakimbia kila mahali, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi,[1] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida.[2] Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu bila hisia yoyote, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, wanaenda kinyume na dhamiri yote, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! … Kwa nini uweke kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini utumie mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini utumie nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini usimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini umsumbue Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? Wema upo wapi miongoni mwa wanadamu? Ukarimu upo wapi miongoni mwa wanadamu? Kwa nini usababishe matamanio makubwa kiasi hicho kwa Mungu? Kwa nini umfanye Mungu kuita tena na tena? Kwa nini umlazimishe Mungu kuwa na wasiwasi kwa sababu ya Mwana Wake mpendwa? Katika jamii hii ya giza, kwa nini mbwa wao walinzi wasimruhusu Mungu kuja bila kizuizi na kuzunguka dunia ambayo Aliiumba?” (“Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Mwenyezi Mungu amezungumza kwa urefu kuhusu chanzo na hali ya sasa ya upotovu wa binadamu. Tunaposoma maneno ya Mwenyezi Mungu, tunapata ufahamu fulani kuhusu masuala kama vile kwa nini kuna giza nyingi na uovu duniani, kwa nini binadamu wanampinga Mungu bila akili, na ukweli na kiini cha upotovu wa binadamu ni nini, sivyo? Uovu na giza la nyakati hizi yanathibitisha kwamba upotovu wa binadamu mikononi mwa Shetani ni mwingi kwelikweli, hivyo ni watu wangapi miongoni mwa binadamu wapo ambao wana kiu ya kuonekana kwa Mungu na kukaribisha kuja Kwake? Wapo wangapi ambao hupenda kusikia neno la Mungu na kukubali ukweli? Wapo wangapi ambao huchunguza na kutafuta kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Wengi wa watu hawapuzilii tu mambo haya; kinyume na hili, wao husikiliza tu uvumi na uongo wa serikali ya kishetani ya CCP na hufanya kazi pamoja na nguvu za kishetani kupinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu. Huu ni ukweli ambao kila mmoja anaelewa wazi. Hata ingawa kuna watu wengi wenye imani kwa Mungu, wapo wangapi ambao wanaweza kuukubali ukweli, watafute ukweli, na kumtii Mungu kwa kweli? Tukikumbuka wakati ambao Bwana Yesu alionekana kufanya kazi Yake, watu wote wa Uyahudi waliwafuata wakuu wa makuhani, waandishi, na Mafarisayo kumpinga na kumshutumu Bwana Yesu. Katika siku za mwisho kwa vile Mwenyezi Mungu ameonekana kufanya kazi Yake, wengi wa wachungaji na wazee katika dunia ya kidini sasa wanampinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu; wanaenda mpaka kwa kiwango cha kuwazuia kuingia katika makanisa yao na kutowaruhusu waumini kuchunguza njia ya kweli. Hii inatosha kuonyesha kwamba dunia hii wakati huu imejaa giza na uovu. Binadamu wamechoshwa na ukweli, wanauchukia ukweli, na wamemtelekeza Mungu na kuchagua kumpinga. Chanzo cha giza hili na uovu wa dunia ni udhibiti wa Shetani juu ya binadamu na kwamba dunia nzima iko chini ya miliki ya mwovu. Kwa miaka elfu kadhaa iliyopita, Shetani ametumia ukana Mungu, nadharia ya mabadiliko, na uyakinifu na vile vile mafunzo mengine na uongo kuwadanganya na kuwapotosha binadamu. Hili limemsababisha binadamu kuabudu na kuweka imani ya upofu katika uongo kadhaa na udanganyifu wa wafalme wa ibilisi na “watu wakuu,” ambao wamesema mambo kama: “Hakuna Mungu wala Mwokozi”; “Mwanadamu anaweza kupigana dhidi ya mbingu na dunia na kuushinda ulimwengu”; “Majaliwa ya mja yako mikononi mwake”; “Kila mtu ajijali na asiye na lake aelekee jiwe”; “Wale wenye akili wanawatawala wale wenye nguvu”; “Pesa ni muhimu sana;” “Kama vile akili ndogo haimfanyi mtu kuwa muungwana, mtu kamili hawi bila sumu,” na kadhalika. Binadamu amendanganywa na kupotoshwa na haya mafundisho maovu na uongo, ambayo yamewafanya kuwa na kaburi, wadanganyifu, wenye ubinafsi, tamaa na waovu; hakuna mwanadamu anayezungumzia ubinadamu na uadilifu, hakuna mwanadamu anayezungumzia dhamiri na mantiki, na hakuna mwanadamu anayeweza kuzungumzia kuwa mwaminifu. Katika utafutaji wa sifa, umashuhuri na heshima, wanadamu wanapigana kama mbwa na wanakula njama na kudanganyana; hata wanauwana. Kwa maslahi tofauti tofauti, mataifa yanapigana na mataifa mengine katika migogoro isiyoisha. Je, haya sio matokeo ya upotovu wa wanadamu na Shetani? Ukweli huu unaonyesha kwamba binadamu wamepotoshwa kabisa na Shetani na kwamba binadamu wamekuwa wa namna sawa na Shetani, ukoo wa Shetani. Binadamu wamekuwa nguvu ya uovu ambao wanasimama katika uadui dhidi ya Mungu. Kwa sababu hii, Mungu alipokuwa mwili mara mbili kuzungumza na kufanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu, binadamu wapotovu walipinga, wakashutumu, na wakamwacha Mungu mara zote mbili, hata kwenda kwa kiwango cha kumsulubisha. Huu ni baadhi ya ukweli kwa nini binadamu anampinga Mungu.

Ukandamizaji wa wazimu wa CCP na mashambulizi dhidi ya Umeme wa Mashariki yamesababisha vurugu katika ulimwengu mzima. Watu wengi hawana utambuzi kuhusu ni kwa nini wanampinga na kumkataa Mungu kwa wayowayo. Ni kwa sababu hasa Mwenyezi Mungu mwenye mwili amenena ukweli mwingi katika Neno Laonekana katika Mwili na ni kitabu hiki ndicho kimetikisa kila kundi la kidini. Wengi ambao wanamwamini Bwana wamesikia matamshi ya Mwenyezi Mungu na kuyathibitisha kama sauti ya Mungu na kazi Yake wamemgeukia. Idadi inayoongezeka bila kukoma ya wale ambao wanatangaza na kuwa na ushuhuda kwa Mwenyezi Mungu imesababisha CCP kiwe na wasiwasi. CCP kimekata idadi isiyohesabika ya wale ambao wamekuwa na ushuhuda kwa Mungu katika kueneza injili kwao, na kimechua ngawira ya nakala nyingi za Neno Laonekana katika Mwili. Wanakichunguza kitabu hiki siku baada ya siku, na wanahisi zaidi jinsi kilivyo cha kuogofya. Kina uwezo wa kushinda yote. Haijalishi jinsi CCP kinavyojaribu kukashifu, kumhukumu na kumwaibisha Mwenyezi Mungu, hawawezi kuthubutu kufanya Neno Laonekana katika Mwili kijulikane kwa umma. Hawataji hata kidogo kile ambacho Mwenyezi Mungu ametamka. Kwa nini wanabaki kimya sana kama jibu kwa Neno Laonekana katika Mwili? Wanahofu kwamba dunia nzima itaona kwamba Mungu amejidhihirisha Mwenyewe akifanya kazi Yake Mashariki, kwamba Mwokozi wa binadamu Ameonekana Mashariki, na hapo kuna matumaini ya binadamu. Kwa nini CCP kinaogopa binadamu akisoma Neno Laonekana katika Mwili? Kwa sababu kitabu hiki ni sauti ya Mungu, ni matamshi ya ukweli, na ni mwanga wa kweli ambao umeonekana Mashariki! CCP ni mamlaka ya Shetani ambaye ndiye mwovu kuliko wote na anayechukia ukweli zaidi. Kinaogopa zaidi ya yote kwamba ukweli utakuja katika dunia ya binadamu, kwamba binadamu atakubali ukweli, kwamba Mungu atachukua mamlaka kama Mfalme kutawala ulimwengu wa mwanadamu, na kwamba ufalme wa Kristo utaonekana duniani. Kwa hiyo, CCP kwa wazimu kinafuatilia na kumsumbua Kristo, na hutumia mitandao ya vyombo vya habari kwa propaganda kusingizia kwa utukutu, kushitaki na kulidharau Kanisa la Mwenyezi Mungu. Hawajizuii hata kuhamasisha polisi wa taifa wenye silaha kukandamiza sana, kukamata na kuwatesa wateule wa Mungu. Bila mahali pa kujificha, wateule Wake wamelazimika kwenda uhamishoni kwa sababu ya mateso ya CCP, na serikali ya China chini ya CCP imenyoosha mkono wake mbaya katika kila nchi ughaibuni na kwa kutumia njia za kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia inashinikiza baadhi yao kuwafanya wale Wakristo waliokimbilia ughaibuni warudi Uchina ili iwaumize na kuwatesa. Hata la kuchukiza zaidi ni kwamba CCP pia huwakamata na kuwatesa jamaa za Wakristo hao ambao wamekwenda ughaibuni na huwachukulia kama mateka ambao inawatumia kutishia Kanisa la Mwenyezi Mungu. Inawalazimisha kuchukua pasipoti zao kwenda ughaibuni na kulivuruga Kanisa la Mwenyezi Mungu katika kila nchi, na hujaribu kupitia njia za kidiplomasia kulisingizia na kukashifu Kanisa la Mwenyezi Mungu, ili kupotosha kwa uvumi, kuendesha maoni ya umma na kulidharau. CCP inachochea serikali pamoja na watu wa nchi nyingine kupinga na kulikataa Kanisa la Mwenyezi Mungu, na kuwarejesha wanachama wa Kanisa walio ughaibuni; lengo lake ovu ni kufanikiwa katika kuzuia, kuwekea mipaka na kukandamiza kuenea kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu na kazi yake ya injili ughaibuni. Je, hamwezi kusema kuwa CCP ni ibilisi Shetani ambaye huchukia ukweli na kumchukia Mungu? CCP kina ustadi katika unyanyasaji wa ukatili wa watu na uteketezaji wa roho; ni pepo ambalo hula watu bila kutema mifupa yao. Sasa ninyi nyote mnaona hapa taswira ya kweli ya kwa nini serikali ya China chini ya CCP kwa wazimu inamkataa na kumshtaki Mwenyezi Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Tanbihi:

1. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo ibilisi hutumia huwadhuru watu.

2. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo ibilisi hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.

Iliyotangulia: Swali la 39: Kwa miaka elfu mbili, dunia nzima ya kidini imeamini kwamba Mungu ni Utatu, na Utatu ni nadharia bora zaidi ya mafundisho yote ya Kikristo. Hivyo, tafsiri ya “Utatu” inashikilia kweli? Utatu una uwepo kweli? Kwa nini unasema kwamba Utatu ni uwongo mkuu mno wa ulimwengu wa kidini?

Inayofuata: Swali la 41: Tumeona mazungumzo mengi kwa mtandao na serikali ya Kikomunisti ya Kichina na ulimwengu wa kidini wakilisingizia, kulikashifu, kulishambulia na kulitahayarisha Kanisa la Mwenyezi Mungu (kama vile “tukio la 5.28” huko Zhaoyuan, jimbo la Shandong). Tunajua pia kuwa CCP ni bora mno kwa kudanganya na kunena uongo na kupinda ukweli ili kuwahadaa watu, na vilevile kuwa bora sana katika kuyakashifu, kuyashambulia na kuyahukumu yale mataifa ambayo ina chuki kwayo, hivyo neno lolote ambalo CCP husema ni lazima lisiaminiwe kabisa. Lakini mambo mengi yanayosemwa na wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa ni sawa na yale ambayo CCP huyasema, hivyo ni jinsi gani tunafaa kutambua maneno ya kashfa, ya kutahayarisha yanayotoka kwa CCP na ulimwengu wa kidini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

2. Tofauti kati ya kazi ya Mungu mwenye mwili na kazi ya Roho

Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu atasikia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili.

1. Makusudi ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki