29. Kupagawa ni nini? Kupagawa hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:

Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. … Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, “Mimi ni Mungu!” Lakini mwishowe, hufichuliwa, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. … Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!

Kimetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Watu waliopagawa na mashetani ni wale ambao wameingiliwa na kudhibitiwa na pepo wabaya. Onyesho kuu ni kuwa na maradhi ya saikolojia, au kutokuwa na akili timamu nyakati nyingine, kupoteza kabisa mantiki ya kawaida. Wanamwamini Mungu lakini hawawezi kukubali ukweli na wanaweza tu kuvuruga. Hii ndiyo maana, ingawa wanamwamini Mungu, hawawezi kuokolewa na lazima waondolewe. Wengi wa watu ambao wamepagawa na pepo wabaya ni vikaragosi wa Shetani na huvuruga kazi ya Mungu. Kuna maonyesho kumi makuu kama yafuatayo:

1. Wale wote wanaojifanya kuwa Mungu au Kristo wamepagawa na pepo wabaya.

2. Wale wote wanaojifanya kuwa na roho za malaika wamepagawa na pepo wabaya.

3. Wale wote wanaojifanya kuwa Mungu mwingine mwenye mwili wamepagawa na pepo wabaya.

4. Wale wote wanaosema kwamba maneno ya Mungu ni yao wenyewe au ambao wanawafanya wengine wachukulie maneno yao kama maneno ya Mungu wamepagawa na pepo wabaya.

5. Wale wote wanaojifanya kutumiwa na Roho Mtakatifu ili kuwafanya wengine wawafuate na kuwatii wamepagawa na pepo wabaya.

6. Wale wote wanaozungumza kwa ndimi mara nyingi, wanaofafanua ndimi na wanaweza kuona kila aina za maono ya miujiza, au ambao mara nyingi wanaonyesha dhambi za wengine wamepagawa na pepo wabaya.

7. Wale wote ambao mara nyingi husikia sauti za mwujiza za pepo au milio ya pepo au ambao mara nyingi huona mazimwi, na wale wote ambao kwa dhahiri ni wenye akili punguani wamepagawa na pepo wabaya.

8. Wale wote ambao wamepoteza fikira ya kawaida ya binadamu, wanaozungumza kwa maneno yenye kichaa mara kwa mara, wanaojizungumzia mara nyingi, wanaozungumza upuuzi au wanaosema mara nyingi kwamba Mungu amewaagiza na kwamba Roho Mtakatifu amewagusa pia wamepagawa na pepo wabaya.

9. Wale wote ambao wana matukio ya tabia isiyo ya kawaida, wanaotenda kipuuzi, ambao wakati mwingine ni wajinga, na hawawezi kuzungumza na wengine kwa kawaida ni watu ambao wamepagawa na pepo wabaya. Wale wote ambao wanaainishwa kama wasenge ni aina ya watu ambao wamepagawa na mashetani na ni miongoni mwa wale ambao wataondolewa.

10. Watu wengine kwa desturi ni wa kawaida kabisa lakini, kwa kipindi cha miezi kadhaa au mwaka mmoja au miaka miwili, huenda wakachokozwa na kukuza ugonjwa wa akili. Wakati wa ugonjwa huo wako sawa tu na wale ambao wamepagawa na roho wabaya. Ingawa watu hawa ni wa kawaida wakati mwingine, pia wanaainishwa kama waliopagawa na mashetani. (Ikiwa mtu ana ugonjwa wa akili miaka mingi kabla lakini amekuwa sawa kwa miaka mingi baadaye, anaweza kuelewa na kukubali ukweli kama imani yake, na kupitia mabadiliko kiasi, hawezi kuainishwa kama aliyepagawa na pepo wabaya.)

Mtu ambaye amepagawa na mashetani amemilikiwa na kudhibitiwa kikamilifu na Shetani, ni wa Shetani, na amelaaniwa.

Kimetoholewa kutoka katika Mipango ya Kazi

Kuna aina mbili tu za hali ambapo roho waovu humdanganya mwanadamu: Moja ni kazi isiyo ya kawaida ya roho waovu, na nyingine ni roho waovu waliopata mwili tena kama binadamu. Wale wanaopinga Mungu na ukweli kama vile pepo ambaye ni joka kuu jekundu pia ni roho waovu; wao ni wenye kudhuru kwa siri zaidi, wenye nia mbaya zaidi. Baadhi ya roho waovu hutawala miili ya watu wakati fulani katika maisha yao; roho wengine waovu ni kupata mwili tena kwa pepo. Ingawa kwa nje hakuna kazi isiyo ya kawaida ya roho waovu na huwezi kuona dalili yoyote ya umiliki na pepo, wao hupinga ukweli kwa mhemko; wao humkataa na kumpinga Mungu kwa hasira. Pepo waliopata mwili tena si wa mwujiza, bali ni wa kawaida. Hata hivyo, ni dhahiri shahiri kuwa wao ni adui wa ukweli. Joka kubwa jekundu ni la kundi la pepo waliopata mwili tena, na wanasiasa wote na wakuu wa nchi wanaompinga Mungu pia ni pepo waliozaliwa tena. Kusema kwamba wale tu ambao wana kazi ya roho waovu wamepagawa na pepo na wao wenyewe ni pepo waovu hakukubaliani na uhalisi. Baadhi ya roho waovu hujificha ndani zaidi na huwezi kuwatambua; wao ni wa kundi la pepo waliopata mwili tena.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Iliyotangulia: 28. Kuna tofauti zipi kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya pepo wabaya?

Inayofuata: 30. Kwa nini Mungu hawaokoi wale wanaofanyiwa kazi na pepo wabaya na wale waliopagawa?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

3. Waumini lazima waweze kutambua wachungaji wa uwongo na wapinga Kristo ili kwamba kuiacha dini na kurudi kwa Mungu

Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki