20. Asiyeamini ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu?

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale wote walio na uelewa wa uongo wa maneno ya Mungu ni makafiri. Hawana maarifa yoyote halisi, sembuse kimo chochote halisi; wao ni watu wenye kujigamba bila ya uhalisi. Hiyo ni, wale wote wanaoishi nje ya dutu ya maneno ya Mungu ni makafiri. Wale wanaoonekana kuwa makafiri na wanadamu ni wanyama mbele za Mungu, na wale wanaoonekana kuwa makafiri na Mungu ni wale ambao hawana maneno ya Mungu kama maisha yao. Kwa hiyo, wale ambao hawana uhalisi wa maneno ya Mungu nao wanashindwa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ni makafiri.

Umetoholewa kutoka katika “Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ni Kuwa na Uhalisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kunao baadhi ya watu ambao imani yao haijawahi kutambuliwa katika moyo wa Mungu. Kwa maneno mengine, Mungu hatambui kwamba watu hawa ni wafuasi Wake, kwa sababu Mungu haisifu imani yao. Kwa watu hawa, haijalishi wamemfuata Mungu kwa miaka mingapi, mawazo na mitazamo yao haijawahi kubadilika. Wao ni kama wasioamini, wanatii kanuni na njia ambayo wasioamini wanafanya mambo yao, kutii sheria zao za kusalia na imani. Hawakuwahi kukubali neno la Mungu kama maisha yao, hawakuwahi kusadiki kwamba neno la Mungu ni ukweli, hawakuwahi kunuia kukubali wokovu wa Mungu, na hawakuwahi kutambua Mungu kama Mungu wao. Wanachukulia kusadiki Mungu kuwa uraibu fulani wa wanagenzi, wakishughulikia Mungu kama riziki ya kiroho, hivyo basi hawafikirii kwamba ipo thamani ya kujaribu na kuelewa tabia ya Mungu, au kiini halisi cha Mungu. Unaweza kusema kwamba kila kitu kinacholingana na Mungu wa kweli hakihusiani kwa vyovyote vile na watu hawa. Hawana hamu yoyote, na hawawezi kusumbuliwa kutilia maanani. Hii ni kwa sababu ndani kabisa ya mioyo yao kunayo sauti ya nguvu ambayo siku zote inawaambia: Mungu haonekani na hagusiki, na Mungu hayupo. Wanasadiki kwamba kujaribu kumwelewa Mungu wa aina hii hakutastahili jitihada zao; itakuwa sawa na wao kujidanganya. Wanamtambua Mungu kwa maneno tu, na hawachukui msimamo wowote halisi. Pia hawafanyi chochote katika hali ya kimatendo, wakifikiri kwamba wao ni werevu sana. Mungu anachukulia vipi watu kama hawa? Anawachukulia kuwa wasioamini. Baadhi ya watu huuliza: “Je, wasioamini wanaweza kulisoma neno la Mungu? Je, wanaweza kutekeleza wajibu wao? Je, wanaweza kuyasema maneno haya: ‘Nitaishi kwa ajili ya Mungu’?” Kile ambacho binadamu huona mara nyingi ni maonyesho ya juujuu tu ya watu, na wala si kiini chao halisi. Ilhali Mungu haangalii maonyesho haya ya juujuu; Yeye huona tu kiini chao halisi cha ndani. Hivyo basi, Mungu anao mwelekeo wa aina hii, ufafanuzi wa aina hii, kwa watu kama hawa.

Umetoholewa kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa wanaitwa wanaotafuta mamlaka. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.

Unachopendezwa nacho sio unyenyekevu wa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Hupendi maarifa au kupendeza kwa Kristo, bali unapenda wale watukutu wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea wao, sifa zao, hadhi zao, na ushawishi wao. Ilhali unazidi kuchukua mtazamo ambapo unaona kazi ya Kristo kuwa ngumu sana kukubali na huko tayari kuikubali. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa hukuwa na chaguo jingine. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wenu, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.

Kwa vyovyote vile, Ninasema kuwa wote wale wasioenzi ukweli ni wasioamini na waasi wa ukweli. Watu kama hawa hawatawahi kuipokea idhini ya Kristo.

Umetoholewa kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ikiwa, katika imani yao katika Mungu, watu mara nyingi hawaishi mbele ya Mungu, hawamchi Mungu mioyoni mwao, na hivyo hawawezi kuepukana na uovu. Mambo haya yanahusiana. Ikiwa moyo wako huishi mara nyingi mbele za Mungu, utazuiwa, na utamcha Mungu katika mambo mengi. Hutavuka mipaka, au kufanya chochote kilicho kiovu. Hutafanya kile kinachochukiwa na Mungu, wala hutasema maneno ambayo hayana maana. Ukikubali uchunguzi wa Mungu, na kukubali nidhamu ya Mungu, utaepuka kufanya mambo mengi maovu—na hivyo utapukana na uovu, siyo? Ikiwa, katika imani yako katika Mungu, wewe mara nyingi huishi katika hali tatanishi, bila kujua kama Mungu yupo moyoni mwako, bila kujua unachotaka kufanya moyoni mwako, na kama huwezi kuwa na amani mbele ya Mungu, na humwombi Mungu au kutafuta ukweli jambo linapokutendekea, ikiwa mara kwa mara wewe hutenda kulingana na mapenzi yako, huishi kulingana na tabia yako ya shetani na kufichua tabia yako ya kiburi, na ikiwa hukubali uchunguzi wa Mungu au nidhamu ya Mungu, na humtii Mungu, basi mioyo ya watu kama hawa daima itaishi mbele ya Shetani na kutawaliwa na Shetani na tabia zao potovu. Kwa hivyo watu kama hao hawana uchaji hata kidogo wa Mungu. Hawana uwezo kabisa wa kuepukana na uovu, na hata kama hawafanyi mambo maovu, kila kitu wanachofikiri bado ni kiovu, na hakihusiani na ukweli na kinakwenda kinyume cha ukweli. Kwa hivyo je, watu kama hawa kimsingi hawana uhusiano na Mungu? Ingawa wanatawaliwa na Mungu, hawajawahi kuripoti mbele ya Mungu, hawajawahi kumchukulia Mungu kama Mungu, hawajawahi kumchukulia Mungu kama Muumba anayewatawala, hawajawahi kukiri kwamba Mungu ni Mungu wao na Bwana wao, na hawajawahi kufikiria kumwabudu Mungu kwa mioyo yao. Watu kama hawa hawaelewi maana ya kumcha Mungu, na wanafikiri kuwa ni haki yao kutenda uovu, wakisema: “Nitafanya kile ninachotaka. Nitashughulikia mambo yangu mwenyewe, sio shauri ya mtu mwingine yeyote.” Wanafikiri kuwa ni haki yao kutenda uovu, na wao huchukulia imani katika Mungu kama aina ya maneno yanayorudiwarudiwa, kama aina ya utaratibu. Je, hii haiwafanyi wao kuwa wasiomwamini Mungu? Wao ni watu wasiomwamini Mungu!

Umetoholewa kutoka katika “Ukiiishi mbele ya Mungu Kila Wakati tu Ndio Unaweza Kuitembea Njia ya Wokovu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Kila mtu ndani ya familia ya Mungu anamwamini Mungu. Hata hivyo, kuna aina moja ya mtu ambaye, ingawa anadai kuwa anamwamini Mungu, ndani ya moyo wake ana shaka juu ya kuwepo kwa Mungu, kuhusu ukweli kwamba Mungu aliumba yote yaliyomo, juu ya Mungu kutawala vyote ambavyo vipo, kuhusu kupata mwili kwa Mungu, kuhusu neno la Mungu na juu ya ukweli. Kipengele kimoja ni kwamba hawezi kuthibitisha ikiwa mambo haya ni ya kweli au la. Kipengele kingine ni kwamba bado anatilia shaka, akiamini mambo haya kuwa yasiyowezekana. Anaamini nini moyoni mwake? Anaamini katika vitu vyote vilivyopo katika ulimwengu wa mwili. Anaamini kila kitu ambacho macho yake yanaweza kuona, na anaamini kila kitu ambacho mikono yake inaweza kugusa. Yeye huwa na mtazamo wa shaka kuhusiana na kitu chochote ambacho macho yake hayawezi kuona, hadi pale ambapo hata hakitambui. Mtu wa aina hii humwamini Mungu kwa maneno tu, lakini kwa kweli, yeye ni kafiri tu. Nimesikia kuwa ndani ya dini ya magharibi, asilimia 25 ya wachungaji, yaani kimsingi mchungaji mmoja kati ya kila wachungaji 4, hawaamini kwamba mimba ya Bwana Yesu ilipatikana kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, na wanahodhi shaka fulani juu ya Biblia. Kati ya wachungaji wa magharibi, kuna wengi kiasi hiki ambao hawaamini. Hasa inapofikia kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu, wao hupinga hata zaidi. Wanaamini kwamba Mungu yupo mbinguni pekee na kwamba Mungu hatawahi kufanya kazi miongoni mwa wanadamu. Kwa sababu hiyo, yeyote asemaye kuwa Mungu amekuja atashutumiwa na wachungaji wengi wa magharibi kama waasi wa dini. Je, si waweza kusema kuwa hawa watu ni makafiri? Wao ni makafiri. Makafiri hawaamini kazi ya Roho Mtakatifu. Wao husema, “Hili ni jambo lililofikiriwa na mwanadamu. Moyo wa mwanadamu unaweza kutiwa msukumo kwa muda mfupi na wakati mwingine unaweza kunurishwa. Lakini hii haihusiani na kazi ya Roho Mtakatifu.” Hawaamini kazi ya Roho Mtakatifu. Pia, hawaamini kwamba maneno ya Mungu hunenwa na Mungu. Wao husema, “Maneno haya yalinenwa na mwanadamu. Ni nani ambaye amemwona Mungu akiyanena maneno haya? Mungu aliwezaje kusema mambo haya? Haya yalinenwa na mwanadamu.” Wote wasioamini katika kupata mwili kwa Mungu au kazi ya Roho Mtakatifu, na hata hawaamini kwamba maneno ya Mungu huonyeshwa na Mungu au Roho wa Mungu, ni makafiri. Bila kujali wanasema imani yao katika Mwenyezi Mungu ni ya kweli vipi, wao ni makafiri. Kafiri si mtu anayedai kuwa hamwamini Mungu. Yeye husema kuwa anamwamini Mungu kwa kinywa chake, lakini moyo wake hauamini. Hivi ndivyo inavyomaanisha kuwa kafiri, na pia inaweza kusemekana kwamba yeye ni ayari.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kutambua Watu wa Aina Zote” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha III

Kiini cha Mafarisayo ni unafiki. Wanaamini katika Mungu lakini hawapendi ukweli au kutafuta maisha. Wanamwamini tu katika Mungu asiye dhahiri juu mbinguni na mawazo yao wenyewe na dhana zao, lakini hawamwamini au kumkubali Kristo mwenye mwili. Kusema kweli, wote ni wasioamini. Kumwamini kwao Mungu ni kuifanyia utafiti teolojia na kuchukulia imani kwa Mungu kama aina ya maarifa ya kufanya utafiti. Riziki yao inategemea kuifanyia utafiti Biblia na teolojia. Katika mioyo yao, Biblia ni riziki yao. Wanafikiri jinsi walivyo bora zaidi katika kueleza ujuzi wa kibiblia na nadharia ya kiteolojia, ndivyo kutakuwa na watu zaidi ambao wanawaabudu na ndivyo wanavyoweza kusimama juu zaidi na kuwa imara zaidi kwenye jukwaa, na ndivyo hadhi zao zitakavyokuwa imara zaidi. Ni hasa kwa sababu Mafarisayo ni watu ambao wanaishi tu kwa ajili ya hadhi zao na riziki yao, na ni watu ambao wamechoshwa na kudharau ukweli, kwamba wakati Bwana Yesu alikuwa mwili na kuja kufanya kazi, walishikilia kwa utundu mawazo yao na dhana zao na ujuzi wa kibiblia kwa ajili ya kulinda hadhi zao na riziki yao, kufanya kila kitu ili kupinga na kumshutumu Bwana Yesu na kumpinga Mungu. …

Katika dini, watu wote wanaamini katika Mungu chini ya udhibiti wa Mafarisayo, wakiwafuata kikamilifu na kuwasikiliza. Kama wao, wanajifunza Biblia tu na teolojia, wakiwa makini tu kuelewa ujuzi wa kibiblia na nadharia ya kiteolojia, na kamwe kutolenga kutafuta ukweli au kutenda maneno ya Bwana. Kama Mafarisayo, wanaamini tu katika Mungu asiye dhahiri mbinguni, lakini hawaamini katika Kristo mwenye mwili wa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu. Haijalishi jinsi ukweli ulioonyeshwa na Mwenyezi Mungu ulivyo na mamlaka na nguvu, bado wanaendelea kushikilia dhana na mawazo yao kwa ukaidi, na kufuata wachungaji na wazee katika kumpinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu. Ni wazi kuwa, watu kama hao ni aina sawa na Mafarisayo, na wanatembea njia ya kumpinga Mungu ya Mafarisayo! Hata kama watu kama hao hawawafuati Mafarisayo, bado ni aina moja ya watu kama Mafarisayo na pia ni vizazi vya Mafarisayo kwa sababu asili yao na kiini ni sawa. Wao ni wasioamini ambao wanajiamini tu wenyewe lakini hawapendi ukweli! Wao ni wapinga Kristo ambao hudharau ukweli na kupinga Kristo!

Umetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Iliyotangulia: 19. Unafiki ni nini?

Inayofuata: 21. Kumfuata Mungu ni nini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

3. Kumfafanua Mungu mmoja wa kweli kama Mungu wa utatu ni kumkana na kumkufuru Mungu

Mwanadamu anaamini kwamba Yehova ndiye Baba ya Yesu, ila hili halijakiriwa na Yesu ambaye alisema: “Hatukubainishwa kamwe kama Baba na Mwana; Mimi na Baba aliye Mbinguni ni kitu kimoja. Baba yu ndani Yangu Nami ni ndani Yake; wanadamu wanapomwona Mwana, wanamwona Baba.” Baada ya yote kusemwa, iwe Baba au Mwana, Wao ni Roho mmoja, Hawajagawanywa kuwa nafsi tofautitofauti. Mara tu wanadamu wanapojaribu kueleza, mambo hutatizwa na wazo la nafsi tofauti, na vilevile na uhusiano kati ya Baba, Mwana na Roho. Mwanadamu akizungumzia nafsi tofauti, je, hili halimfanyi Mungu kuwa kitu? Mwanadamu hata zaidi huziorodhesha nafsi hizi kama nafsi ya kwanza, ya pili, na ya tatu; haya yote ni mawazo ya mwanadamu yasiyofaa kurejelewa, hayana uhalisi kabisa!

2. Kwa nini Mungu hubariki tu kanisa ambalo huikubali na kuitii kazi Yake? Kwa nini Yeye huyalaani mashirika ya kidini?

Dhihirisho la wazi zaidi wa kazi ya Roho Mtakatifu ni kwa kuyakumbatia ya sasa, sio kushikilia ya zamani. Wale ambao hawajiendelezi na kazi ya leo, na wale ambao wametengwa na utendaji wa leo, ni wale wanaopinga na hawaikubali kazi ya Roho Mtakatifu. Watu kama hao wanaipinga kazi ya Mungu ya sasa. Ijapokuwa wanashikilia nuru ya zamani, hili halimaanishi kwamba inaweza kukanwa kwamba hawajui kazi ya Roho Mtakatifu. … Walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu daima hudhani wako sahihi, lakini kwa hakika, kazi ya Mungu ndani yao ilisita zamani na kazi ya Roho Mtakatifu haimo ndani yao. Kazi ya Mungu imeshahamishiwa kwa kundi jingine la watu, kundi ambalo kwalo Anapania kukamilishia kazi Yake mpya. Kwani walio katika dini hawawezi kuikubali kazi mpya ya Mungu, na kushikilia tu kazi kongwe za zamani, hivyo Mungu amewaacha watu hawa na anafanya kazi Yake mpya kwa watu wanaoikubali kazi hii mpya. Hawa ni watu wanaoshiriki katika kazi Yake mpya, na usimamizi Wake utatimilika kwa njia hii tu.

2. Kupata Mwili Ni Nini? Ni Nini Kiini cha Kupata Mwili?

Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki