41. Matendo maovu ni yapi? Maonyesho ya matendo maovu ni yapi?

Maneno Husika ya Mungu:

Ni kiwango kipi ambacho kulingana nacho matendo ya mtu yanaonwa kuwa mema au mabaya? Inategemea na iwapo katika fikira, maonyesho, na matendo yako, una ushuhuda wa kutia ukweli katika vitendo na wa kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli au la. Ikiwa huna uhalisi huu au huishi kwa kudhihirisha hili, basi bila shaka wewe ni mtenda maovu.

Kimetoholewa kutoka katika “Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Ukiishi daima kulingana na mwili, daima kuridhisha tamaa zako mwenyewe za binafsi, basi mtu kama huyo hana uhalisi wa ukweli. Hii ni alama ya mtu ambaye anamwaibisha Mungu. Unasema, “Sijafanya chochote; nimemwaibisha Mungu vipi?” Katika mawazo na fikira zako, katika nia, malengo na sababu za matendo yako, na katika matokeo ya yale ambayo umeyafanya—katika kila njia unamridhisha Shetani, ukiwa kichekesho chake, na kumwacha ajue jambo litakalokuathiri. Huna ushuhuda unaopaswa kuwa nao kama Mkristo hata kidogo. Unafedhehesha jina la Mungu katika mambo yote na huna ushuhuda wa kweli. Je, Mungu atakumbuka mambo ambayo umeyafanya? Mwishowe, Mungu atakuwa na uamuzi upi kuhusu matendo yako na wajibu ambao umetimiza? Je, hakupaswi kuwa na matokeo ya hayo, aina fulani ya maelezo? Katika Biblia, Bwana Yesu anasema, “Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, je, hatujatabiri kupitia jina Lako? na kutoa mapepo kupitia jina Lako? na kutenda miujiza mingi kupitia jina Lako? Na hapo ndipo Nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni Kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.” Kwa nini Bwana Yesu alisema hili? Kwa nini wale wanaowaponya wagonjwa na kuwatoa mapepo katika jina la Bwana, ambao wanasafiri kuhubiri katika jina la Bwana, wanageuka kuwa watenda maovu? Hawa watenda maovu ni nani? Je, ni wale wasiomwamini Mungu? Wote wanamwamini Mungu na kumfuata Mungu. Pia wanatelekeza vitu kwa ajili ya Mungu, kujitumia kwa ajili ya Mungu, na kutimiza wajibu wao. Hata hivyo, katika kutimiza wajibu wao wanakosa moyo na ushuhuda, kwa hiyo imekuwa kutenda maovu. Hii ndiyo maana Bwana Yesu anasema, “Tokeni Kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.”

Kimetoholewa kutoka katika “Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Unaviona vitendo hivi vyote vya Mungu sasa, ilhali ungali unapinga na unakuwa mwasi na hutaki kunyenyekea; unayahifadhi mambo mengi ndani yako na unafanya utakacho; unafuata ashiki zako, na kile upendacho—huu ni uasi; huu ni upingaji. Imani katika Mungu ambayo inatekelezwa kwa ajili ya mwili, kwa ajili ya ashiki za mtu, na kwa ajili ya kile anachopenda mtu, kwa ajili ya ulimwengu, na kwa ajili ya Shetani ni chafu; ni upinzani na uasi. Kunazo aina zote tofauti za imani sasa: Baadhi hutafuta hifadhi dhidi ya janga, na wengine hutafuta kupokea baraka, huku baadhi wakitamani kuelewa mafumbo na bado wengine hujaribu kupata pesa. Hiyo yote ni mifumo ya upinzani; hiyo yote ni kukufuru! Kusema kwamba mtu anapinga au anaasi—huku si kwa mujibu wa mambo haya? Watu wengi sasa hivi wanalalamika, wanatamka manung’uniko au kutoa hukumu. Haya yote ni mambo yanayofanywa na waovu; wao ni binadamu wapinzani na waasi; watu kama hao wamemilikiwa na kujawa na Shetani.

Kimetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale miongoni mwa ndugu ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani, na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi sio tu kwamba hawatashindwa kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomwasi Mungu. Wakati ambapo mtu anayeamini Mungu hamtii Mungu ama kumcha Mungu lakini badala yake anamwasi, basi hii ndiyo aibu kuu zaidi kwa muumini. Ikiwa usemi na mwenendo wa muumini daima havina mpango na bila kizuizi kama asiyeamini, basi huyu muumini ni mwovu zaidi kumpiku asiyeamini; yeye ni ibilisi halisi. Wale walio kanisani ambao wanaeneza matamshi yao yenye sumu, wale miongoni mwa ndugu ambao wanasambaza uvumi, kuchochea utengano na kufanya magenge wanapaswa kufukuzwa kutoka kanisani. Lakini watu hawa wamezuiwa kwa kuwa sasa ni enzi tofauti ya kazi ya Mungu, kwa sababu wamehukumiwa kuwa vyombo vya kuondolewa. Wale waliopotoshwa na Shetani wote wana tabia iliyopotoka. Hata hivyo, baadhi ya watu wana tabia potovu tu, huku kuna wengine walio tofauti: Si tu kwamba wana tabia potovu za kishetani, lakini asili zao pia ni mbovu kupita kiasi. Si tu kwamba maneno yao na vitendo vyao vinafichua tabia zao potovu za kishetani; watu hawa, aidha ndio Shetani wa kweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kila moja ya kanisa lina watu wanaolivuruga kanisa, watu wanaokatiza kazi ya Mungu. Watu hawa wote ni Shetani wanaojifanya katika familia ya Mungu. Watu kama hawa ni waigizaji wazuri: wanakuja mbele Yangu na uchaji mkubwa, wakiinama na kuchakura, wakiishi kama mbwa koko, wakijitolea “yote” waliyo nayo ili kufanikisha malengo yao wenyewe—lakini mbele ya kina ndugu, anaonyesha sura yake mbaya. Anapomwona mtu akiutenda ukweli anamshambulia na kumtenga; anapomwona mtu wa kutisha kumpiku yeye mwenyewe, anamsifu mno na kujipendekeza kwake, wakitenda kama viongozi wa kiimla kanisani. Inaweza kusemwa kuwa mengi ya makanisa yana aina hii ya “nyoka mwovu wa ndani,” aina hii ya “mbwa wa kupakata” kati yao. Wanatembea kwa siri kwa pamoja, wakikonyezana na kuashiriana, na hakuna hata mmoja wao anayetenda ukweli. Yeyote aliye na sumu zaidi ndiye “ibilisi mkuu,” na yeyote aliye na hadhi ya juu zaidi huwaongoza, akipeperusha bendera yao juu zaidi. Watu hawa wanakuwa huru na kufanya wanachotaka kanisani, wakieneza ubaya wao, wakiachilia kifo, wakifanya watakavyo, wakisema wanachopenda, bila anayethubutu kuwakomesha, wakijawa na tabia za kishetani. Punde tu wanapoanza kusababisha usumbufu, hewa ya kifo inaingia ndani ya kanisa. … Iwapo kanisa lina waonevu kadhaa wa hapo, na wanafuatwa na “nzi wadogo” wasio na ufahamu kabisa, na ikiwa washiriki wa kanisa, hata baada ya kuona ukweli, bado hawawezi kukataa vifungo na kuchezewa na hawa waonevu—basi hawa wajinga wataondolewa mwishoni. Ingawa nzi hawa wadogo wanaweza kuwa hawajafanya lolote baya, wao ni wenye hila hata zaidi, wadanganyifu hata zaidi na wenye kukwepa hata zaidi na kila mtu aliye namna hii ataondolewa. Hakuna yeyote atakayeachwa!

Kimetoholewa kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Udanganyifu wenu, kiburi chenu, tamaa yenu, tamaa yenu yenye fujo, usaliti wenu, kuasi—lipi kati ya haya linaweza kujificha kutoka kwa macho Yangu? Ninyi mnanitendea hobela hobela, mnanidanganya Mimi, mnanitusi, mnanibembeleza, mnanilazimisha na kupata sadaka kutoka Kwangu kwa nguvu—ni jinsi gani tabia ya kudhuru kama hii itaepuka ghadhabu Yangu? Udhalimu wenu ni thibitisho la uadui wako Kwangu, na ni thibitisho la uwiano wenu na Mimi. Kila mmoja wenu anaamini mwenyewe akilingana na Mimi, lakini ikiwa ni hivyo, basi ni kwa nani ushahidi huu dhahiri unatumika? Mnaamini wenyewe kwamba mnao ukweli wa juu sana na uaminifu Kwangu. Mnafikiri kwamba nyinyi ni wema sana, wenye huruma sana, na mmetoa sana Kwangu. Mnafikiri kwamba mmefanya vya kutosha kwa ajili Yangu. Bado hamjawahi kulinganisha imani hizi dhidi ya tabia zenu wenyewe? Nasema mmejaa mengi ya kiburi, tamaa nyingi, wingi wa uzembe; hila mnayotumia kunidanganya ni janja sana, na mna mengi ya nia ya kudharau na mbinu ya kudharau. Uaminifu wenu pia ni mdogo, bidii yenu pia ni ndogo, na dhamiri yako hata haipo zaidi. Kuna mabaya mengi sana katika nyoyo zenu, na hakuna mtu anayeepuka kuathiriwa na hila yenu, hata Mimi mwenyewe. Mnanifungia nje kwa ajili ya watoto wenu, au waume wenu, au kwa ajili ya hifadhi zenu wenyewe. Badala ya kunijali, mnajali familia zenu, watoto wenu, hali yenu, maisha yenu ya baadaye, na kujitosheleza wenyewe. Ni lini mmewahi kuniwaza Mimi mnapozungumza au kutenda? Wakati hali ya hewa ni baridi, mawazo yenu hurejea kwa watoto wenu, waume wenu, wake wenu, au wazazi wenu. Wakati hali ya hewa ni ya joto, hata Siwezi kupata nafasi katika mawazo yenu pia. Unapotekeleza wajibu wako, wewe huwaza tu kuhusu maslahi yako mwenyewe, ya usalama wako mwenyewe binafsi, ya watu wa familia yako. Ni nini umewahi kufanya kwa ajili Yangu? Ni lini umeweza kuwaza kunihusu Mimi? Ni lini umewahi kujitoa mwenyewe, kwa gharama yoyote, kwa ajili Yangu na kazi Yangu? Uko wapi ushahidi wa uwiano wako na Mimi? Uko wapi ukweli wa uaminifu wako kwa ajili Yangu? Uko wapi ukweli wa utiifu wako Kwangu? Ni lini mujibu wako hujakuwa kwa sababu ya kupokea baraka Zangu? Mnanilaghai na kunidanganya Mimi, mnacheza na ukweli na kuficha kuwepo kwa kweli, na kuisaliti dutu ya ukweli, na mnajiweka wenyewe kwa uadui kama huu na Mimi. Basi, ni nini kinawangoja katika siku za usoni? Ninyi mnatafuta tu uwiano na Mungu asiye yakini, na kutafuta tu imani zisizo yakini ilhali ninyi hulingani na Kristo. Si uovu wenu utapata adhabu kama ile wanayostahili waovu?

Kimetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kufanya tendo mbaya, lakini katika ushirika wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kwa uaminifu, au kutii neno la Kristo; basi, Ninasema kwamba wewe ndiye mtu mwovu zaidi na mwenye nia mbaya zaidi duniani. Unaweza kuwa mkunjufu na mwaminifu mno kwa jamaa zako, marafiki, mke (au mume), wanao na mabinti, na wazazi, na kamwe huwatumii wengine vibaya, lakini kama huwezi kulingana na kupatana na Kristo, basi hata ukitumia vitu vyako vyote kuwasaidia majirani zako au kulinda vizuri baba yako, mama, na wanakaya, Ningesema kwamba wewe bado ni mwovu, na zaidi ya hayo aliyejaa hila za ujanja. Usifikiri, kwamba wewe unalingana na Kristo kwa sababu tu unapatana na wengine au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unafikiri kwamba nia yako ya huruma inaweza kupata baraka kutoka Mbinguni kwa ujanja? Je, unafikiri kwamba matendo machache mema yanaweza kubadilishwa na utii wako?

Kimetoholewa kutoka katika “Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu.

Kimetoholewa kutoka katika “Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote, mkitafuta mahali pa amani na mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani? Ninyi, minyoo wadogo wenye uvundo mnaiba sadaka kutoka kwa madhabahu ya Mimi, Yehova; kwa kufanya hivyo, mnaweza kuokoa majina yenu yaliyoharibika, yenye kasoro kuwa wateule wa Israeli? Ninyi ni mafukara wasio na haya!

Kimetoholewa kutoka katika “Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Je, maonyesho ya kutenda kila aina za matendo maovu ni yapi? Onyesho la kwanza hutokea katika nyumba ya Mungu mtu anapomhukumu Mungu na kuihukumu kazi ya Mungu. Linahusisha kuwa na mawazo kumhusu Mungu na mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu mara kwa mara. Watu wengine hata huhodhi uadui, wakieneza uhasi na mawazo juu ya Mungu kila mahali, wakieneza uvumi kumhusu Mungu na mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu ili kuwadanganya watu wa Mungu walioteuliwa na kuvuruga kazi ya nyumba ya Mungu. Haya ndiyo maovu makubwa zaidi. Haya ndiyo mambo yanayovuruga na kuharibu kuingia katika maisha kwa watu wa Mungu walioteuliwa na kazi ya nyumba ya Mungu zaidi. Hii ndiyo sababu haya ndiyo maovu makubwa zaidi. Wale wote wanaoweza kufanya aina hizi za matendo maovu ni wale ambao hutenda kila aina za matendo maovu. Onyesho la pili ni kwamba baadhi ya viongozi katika nyumba ya Mungu si wenye kufikiri kuhusu mapenzi ya Mungu na hawafanyi kazi muhimu ambayo Mungu huwaaminia kufanya. Badala yake, wao hufanya kazi ili kujishuhudia na kuhifadhi hadhi zao. Wao hutayarisha nafasi za uongozi katika ngazi zote katika nyumba ya Mungu kwa ajili ya wasaidizi wao na wenzao wa kuaminika. Mtu wa aina hii pia ni mtu ambaye hufanya kila aina za matendo maovu. Hawafanyi mipango kwa ajili ya wale wanaofuatilia ukweli kwa kweli na ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu; badala yake, wao huwaweka wenzake, wasaidizi wa kuaminiwa, na wanaojipendekeza katika nyadhifa muhimu za kazi. Je, si huku ni kuweka vikwazo na ugumu kwenye njia ya kuingia katika maisha kwa watu wa Mungu walioteuliwa? Kwa hiyo, watu kama hao pia ndio ambao hufanya kila aina za matendo maovu. Nyumba ya Mungu huwainua na kuwaruhusu wawe viongozi, lakini wao hujishuhudia, hujionyesha na hawashuhudii kabisa kwa Mungu au kwa vyote ambavyo Mungu anavyo na Alicho. Hawawasiliani kuhusu ukweli wa neno la Mungu na hawawaongozi watu kuingia katika ukweli. Wao kila mara hufanya kazi ili kuhifadhi hadhi zao wenyewe, wao daima huzungumza kwa ajili ya hadhi na sifa yao wenyewe, wao huhifadhi hadhi zao wenyewe miongoni mwa watu wa Mungu walioteuliwa na huhifadhi hadhi zao katika moyo wa uongozi. Mtu wa aina hii ni mpinga Kristo. Watu ambao ni wapinga Kristo ni wale ambao hutenda kila aina za matendo maovu. Onyesho la tatu ni kwamba mtu hutimiza wajibu wake bila upendo wowote kwa Mungu, daima akitenda ovyovoyo, na kufuata mwili wake na upendeleo wake binafsi anapoyafanya mambo. Matokeo ni kwamba yeye husababisha shida nyingi kwa kazi ya nyumba ya Mungu na husababisha nyumba ya Mungu kupata hasara kubwa za kifedha. Mtu wa aina hii ni mtu anayefanya kila aina za matendo maovu. Onyesho la nne ni kwamba wale wote ambao hawafuatilii ukweli lakini huwakatiza wengine kufuatilia ukweli, ambao daima hueneza uhasi, na ambao daima hueneza maoni ya uongo ya makafiri au watu wa dini ili kuwasumbua watu wa Mungu walioteuliwa pia ni watu wanaofanya aina zote za matendo maovu.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Matendo Thelathini Maovu ya Kukatiza na Kuvuruga Kazi ya Mungu na Kumpinga Mungu Moja kwa Moja:

1. Kukosa kulenga kabisa kutekeleza wajibu wako kanisani lakini badala yake kushiriki katika mizozo yenye wivu na mashindano ya hadhi yanayosababisha fujo katika maisha ya kanisa ni tendo ovu.

2. Kueneza utesi, kuunda magenge na kusababisha vurugu zinazoishia kwa utengano kanisani na kuvuruga kazi ya kanisa kwa uzito ni tendo ovu.

3. Kutopenda ukweli, kutenda utundu na kuunda mgogoro mara kwa mara, kuchochea utesi kati ya watu, na kuvuruga maisha ya kanisa ni tendo ovu.

4. Kusema uongo, kulaghai na kuwadanganya watu, kugeuza ukweli mara kwa mara na kuchanganya mema na mabaya ili kuchochea vurugu ni tendo ovu.

5. Kueneza uongo na uzushi kuwapotosha watu ili wasiweze kufuatilia ukweli, wakose njia, na kujihusisha na Shetani na roho wabaya ni tendo ovu.

6. Kueneza uhasi na kifo, kueneza mawazo kila mahali ili kuwadanganya watu, kuvuruga maisha ya kanisa, na kuwasababisha watu wawe katili na kujitenga na Mungu ni tendo ovu.

7. Ikiwa unajua wazi kwamba huna uhalisi wa ukweli, kwamba huna ubinadamu mzuri na bado kwa kushikilia unashindana kwa ajili ya nafasi za uongozi, hivyo kusababisha vurugu, hili ni tendo ovu.

8. Kutenda kwa namna moja mbele ya watu na namna nyingine nyuma yao, kujifanya unakubaliana huku ukitenda kwa upinzani, kuwadanganya wale walio juu na pia chini yako, na kutumia mbinu nafiki kuwadanganya wengine ni tendo ovu.

9. Kutoweza kushiriki kuhusu ukweli kutatua shida, daima kushambulia udhaifu wa wengine ili kuwaadhibu, na kuwakemea wengine kwa njia inayowashusha hadhi ni tendo ovu.

10. Kusisitiza dhambi za viongozi na wafanyakazi, kutowatendea vizuri na kuathiri kazi yao ya kawaida ni tendo ovu.

11. Katikati ya kuchukuliwa hatua kali kwa viongozi wa uongo na wafanyakazi, kuwapangia mabaya, kujaribu kuwaangamiza bila kuwapa fursa ya kutubu, na kuibua hofu kubwa ni tendo ovu.

12. Kuwa kiongozi au mfanyakazi asiyewajibika na kutulia tu wakati waovu wanavuruga kanisa, na kukosa kulinda kazi ya kanisa ni tendo ovu.

13. Kutotekeleza wajibu wako kwa mujibu wa mipango ya kazi ili kutatua shida za kiutendaji na kuwaruhusu waovu kuvuruga kanisa ni tendo ovu.

14. Kukiuka mipango ya kazi kwa uzito na kufanya vitu kwa njia yako mwenyewe, kusisitiza kupinga ukweli hadi mwisho kabisa, kuwadhuru watu wateule wa Mungu ni tendo ovu.

15. Ikiwa viongozi na wafanyakazi hawatendi ukweli lakini wanacharuka na hawakubali usimamizi na ukosoaji wa watu wa Mungu wateule, hili ni tendo ovu.

16. Viongozi na wafanyakazi wakitenda kama wapendavyo na kuwachagua na kuwatumia wale ambao hawana uhalisi wa ukweli na hawawezi kutekeleza kazi ya utendaji, kusababisha athari mbaya sana, hili ni tendo ovu.

17. Daima kumaliza wajibu wako kwa kubahatisha bila matokeo hata kidogo, kufanya madhara zaidi badala ya mema na kuathiri kazi ya kanisa kwa uzito ni tendo ovu.

18. Sio tu kutotenda ukweli wewe binafsi, lakini pia kuwashambulia wengine na kuwazuia kufanya wajibu wao na kuandaa matendo mema ni tendo ovu.

19. Kukataa kukubali kushughulikiwa na kupogolewa, kutokuwa mtiifu hata kidogo, kuvuruga kanisa kwa kutenda kama dikteta na kufanya chochote unachotaka bila kuzuiwa ni tendo ovu.

20. Daima kujikuza na kujishuhudia, kutoa ushuhuda wa uongo, na kujionyesha ili kupata upendo wa wengine kunaainishwa kama kuwadanganya watu na ni tendo ovu.

21. Daima kuwasiliana na kushirikiana na watu wabaya na waovu, daima kuzungumzia maslahi yao na kuvuruga kazi ya kanisa ni tendo ovu.

22. Kushirikiana na waovu katika kuchochea shida bila kufikiria, kuvuruga kazi ya kanisa na kuathiri maisha ya kanisa, na kutotubu hadi mwisho kabisa ni tendo ovu.

23. Daima kuhodhi tamaa za makuu na kutafuta hadhi, mara nyingi kueneza mawazo ili kuwadanganya wengine na kung’ang’ania mamlaka kupitia mbinu mbalimbali ni tendo ovu.

24. Kutumia hila ovu kueneza injili, kufedhehesha jina la Mungu, kuwa na athari mbaya sana na kuchochea karaha ya wengine ni tendo ovu.

25. Kutowatunza wale waliopatwa kupitia uinjilisti, kutowajibika kabisa na kuathiri kazi ya injili kwa uzito ni tendo ovu.

26. Kuiba sadaka, kufurahia anasa kwa ulafi, kutofanya kazi ya kiutendaji na kuzuia kazi ya kanisa kwa uzito ni tendo ovu.

27. Kubadhiri sadaka na mifuko ya msaada ya kanisa, kutumia pesa za nyumba ya Mungu bila maadili, kuwa mfisadi na mpotovu na mwenye athari mbaya sana ni tendo ovu.

28. Kutowajibika katika kulinda sadaka za nyumba ya Mungu, kuwakabidhi viongozi wa uongo, wapinga Kristo na joka kubwa jekundu sadaka ni tendo ovu.

29. Kusaliti kanisa, kuwasaliti ndugu, hata kumtolea Shetani huduma, na kufuatia na kufuatilia viongozi na wafanyakazi ni tendo ovu.

30. Kuwa mwasherati na mwovu kwa uthabiti, kushiriki katika uzinzi wa jinsia tofauti au shughuli ya usenge, kuvuruga maisha ya kanisa na kuwa na athari mbaya sana ni tendo ovu.

Kimetoholewa kutoka katika Mipango ya Kazi

Iliyotangulia: 40. Matendo mema ni nini? Maonyesho ya matendo mema ni yapi?

Inayofuata: 42. Mungu huwaokoa watu gani? Yeye huwaondosha watu gani?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

2. Tofauti kati ya maneno ya watu wanaotumiwa na Mungu yanayokubaliana na ukweli na maneno ya Mungu Mwenyewe

Ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha.

4. Kwa nini atashindwa kupata uzima wa milele akiitetea na kuiabudu Biblia

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki