44. Watu wa Mungu ni nini? Watendaji huduma ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

“Mabikira watano wenye busara” wanawakilisha wana Wangu na watu Wangu kati ya wanadamu Niliowaumba. Wanaitwa “mabikira” kwa sababu wanapatwa na Mimi, licha ya wao kuzaliwa duniani; mtu anaweza kuwaita watakatifu, kwa hivyo wanaitwa “mabikira.” “Watano” liliotajwa awali linawakilisha idadi ya wana Wangu na watu Wangu ambao Nimewajaalia. “Mabikira watano wapumbavu” linarejelea watendaji huduma, kwa kuwa wananifanyia huduma bila kushikilia hata umuhimu mdogo kwa maisha, wakifuatilia tu mambo ya nje (kwa sababu hawana sifa Yangu, bila kujali kile wanachokifanya, hicho ni kitu cha nje), na hawawezi kuwa wasaidizi Wangu wenye uwezo, kwa hiyo wanaitwa “mabikira wapumbavu.” “Watano” lililotajwa awali linamwakilisha Shetani, na ukweli kwamba wanaitwa “mabikira” kunamaanisha wameshindwa na Mimi na wanaweza kunifanyia Mimi huduma—lakini watu kama hao sio watakatifu, kwa hivyo wanaitwa watendaji huduma.

Kimetoholewa kutoka katika “Sura ya 116” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Hilo likiwa hivyo, kutakuwa na njia mpya: Wale wanaolisoma neno Langu na kulikubali kama uzima wao kabisa ndio watu wa ufalme Wangu. Kwa vile wako katika ufalme Wangu, wao ni watu Wangu katika ufalme. Kwa sababu wanaongozwa na maneno Yangu, ingawa wanatajwa kama watu Wangu, jina hili si la chini ya kuitwa “wana” Wangu. Baada ya kufanywa kuwa watu wa Mungu, wote ni lazima wawe waaminifu katika ufalme Wangu na kutimiza majukumu yao, na wale wanaokosea amri Zangu za usimamizi lazima wapate adhabu Yangu. Hili ni onyo Langu kwa wote.

Kimetoholewa kutoka katika “Sura ya 1” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Ni watu walio watulivu tu mbele ya Mungu ndio wanaotilia maanani maisha, wanaotilia maanani ushirika katika roho, walio na kiu ya maneno ya Mungu, na wanaofuatilia ukweli. Wale wote wasiotilia maanani kutulia mbele ya Mungu, wasiofanya mazoezi ya kuwa watulivu mbele ya Mungu ni watu ovyo ambao wamejifunga kabisa kwa dunia, wasio na uzima; hata wakisema wanaamini katika Mungu wanaunga mkono kwa maneno matupu tu. Wale ambao Mungu hukamilisha na kufanya kamili hatimaye ni watu wanaoweza kuwa watulivu mbele ya Mungu. Kwa hivyo, watu walio watulivu mbele ya Mungu ni watu walioneemeshwa na baraka nyingi. Watu ambao mchana hutumia muda mchache kula na kunywa maneno ya Mungu, ambao wameshughulika kabisa na mambo ya nje, na hawatilii maanani kuingia katika uzima wote ni wanafiki wasiokuwa na matarajio ya kuendelea katika siku za usoni. Ni wale wanaoweza kutulia mbele ya Mungu na kushiriki kwa uhalisi na Mungu ndio watu wa Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Sasa hivi watu wengi (kumaanisha watu wote isipokuwa wazaliwa wa kwanza) wako katika hali hii. Nasema mambo haya kwa wazi sana na watu hawa hawana mjibizo mdogo na bado wanajali kuhusu raha zao za kimwili—wanakula na kisha kulala; wanalala na kisha wanakula, na hawatafakari maneno Yangu. Hata kama wamechangamshwa, itakuwa kwa muda tu, na baadaye watabaki vile vile walivyokuwa, wasibadilike kabisa, kana kwamba hawakunisikiza hata kidogo. Hawa ndio mfano hasa wa binadamu wasiojali wajibu ambao hawana mizigo—wasio na kazi dhahiri kabisa. Baadaye, Nitawatelekeza mmoja mmoja. Msijali! Nitawarudisha mmoja mmoja kwenye shimo lisilo na mwisho. Roho Mtakatifu hajawahi kuwashughulikia watu kama hawa, na kila kitu waanachokifanya kinatokana na uwezo walioupokea. Ninapozungumza kuhusu hizi nyezo, Namaanisha kwamba huyu ni mtu asiye na uzima, ambaye ni mtendaji huduma Wangu. Simtaki yeyote kati yao na Nitawaondoa (lakini sasa hivi bado ana manufaa kiasi).

Kimetoholewa kutoka katika “Sura ya 102” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Na ni ipi nafasi ya watendaji huduma? Kuwahudumia wateule wa Mungu. Kwa ujumla, kazi yao ni kuihudumia kazi ya Mungu, kushirikiana na kazi ya Mungu, na kushirikiana na ukamilisho wa Mungu wa wateule Wake. … Kitambulisho cha mtendaji huduma ni mtendaji huduma, lakini kwa Mungu, ni miongoni mwa vitu vyote Alivyoumba—tofauti ni kwamba tu nafasi yao ni ile ya watendaji huduma. Kama mmoja wa viumbe wa Mungu, kuna tofauti kati ya watendaji huduma na wateule wa Mungu? Kwa hakika, hakuna. Kwa mazungumzo ya kawaida, kuna tofauti, katika kiini kuna tofauti, kwa kurejelea nafasi wanazoshika kuna tofauti, ila Mungu hawabagui hawa watu. Hivyo ni kwa nini hawa watu wanatambuliwa kama watendaji huduma? Unapaswa kuelewa hili. Watendaji huduma wanatokana na wasioamini. Kutaja wasioamini kunatuambia kuwa maisha yao ya awali ni mabaya: Wote ni wakana Mungu, katika maisha yao ya nyuma walikuwa wakana Mungu, hawakumwamini Mungu, na walikuwa mahasimu wa Mungu, wa ukweli, na vitu vizuri. Hawakumwamini Mungu, hawakuamini kuwa kuna Mungu, hivi wana uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu? Ni haki kusema kwamba, kwa kiwango kikubwa, hawana. Sawa tu na wanyama wasivyo na uwezo wa kuelewa maneno ya mwanadamu, watendaji huduma hawaelewi Mungu anasema nini, Anahitaji nini, kwa nini Ana mahitaji kama hayo—hawaelewi, hivi vitu havieleweki kwao, wanabaki bila nuru. Na kwa sababu hii, watu hawa hawana uhai tuliouzungumzia. Je, bila uhai, watu wanaweza kuelewa ukweli? Je, wana ukweli? Je, wana uzoefu na ufahamu wa maneno ya Mungu? (La.) Hizo ndizo asili za watendaji huduma. Lakini kwa kuwa Mungu anawafanya hawa watu watendaji huduma, bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo; Hawadharau, na Hawachukulii kwa uzembe. Japo hawaelewi maneno yake, na hawana uhai, bado Mungu ni mwema kwao, na bado kuna viwango Anavyohitaji wawe navyo. Mmevizungumzia hivi viwango hivi karibuni: Kuwa mwaminifu kwa Mungu, na kufanya Asemacho. Katika huduma yako ni lazima uhudumu unapohitajika, na ni lazima uhudumu hadi mwisho. Ikiwa unaweza kuwa mtendaji huduma mwaminifu, unaweza kuhudumu hadi mwisho, na unaweza kutimiza agizo uliloaminiwa na Mungu kikamilifu, basi utaishi maisha ya thamani, na utaweza kubaki. Ukitia bidii kidogo, ukijaribu kwa nguvu, ukiongeza maradufu jitihada zako za kumjua Mungu, ukiweza kuongea kidogo kuhusu ufahamu wa Mungu, ukiweza kumshuhudia Mungu, na zaidi, ukielewa kitu kuhusu mapenzi ya Mungu, ukiweza kushirikiana katika kazi ya Mungu, na ukiyazingatia kidogo mapenzi ya Mungu, basi wewe, mtendaji huduma, utapata bahati. Na hili litakuwa badiliko gani katika bahati? Hutaweza kubaki tu. Kutegemea tabia yako na malengo na juhudi zako binafsi, Mungu atakufanya mmoja wa wateule. Hii itakuwa bahati yako. Kwa watendaji huduma, ni nini kizuri kuhusu hili? Ni kwamba unaweza kuwa mmoja wa wateule wa Mungu. … Je, hiyo ni habari njema? Ndiyo, na ni habari njema. Inamaanisha, watendaji huduma wanaweza kufinyangwa. Si kwamba kwa mtendaji huduma, Mungu akimpangia awali kuhudumu, daima atahudumu; si lazima iwe hivyo. Kutegemea tabia yake binafsi, Mungu atamtendea tofauti, na kumjibu tofauti.

Kimetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Watu wa Mungu ni nini? Wote ambao ni watu wa Mungu ni wale ambao wataweza kubaki na kuendelea kuishi katika Enzi ya Ufalme. Wao ni wale ambao wamepitia kazi ya Mungu na kupata ukweli; ni watu wenye maisha mapya. Watu wa Mungu wana maarifa ya kweli kumhusu Mungu, wanaweza kutenda ukweli, na mwishoni baada ya kupitia majaribio, usafishaji, mateso, na maafa mengi, wamefanywa kuwa wakamilifu. Wao ni wale ambao hukamilishwa kupitia kupata uzoefu wa kazi ya Mungu. Wote ambao ni watu wa Mungu wana sifa tatu. Moja, wana moyo wa kumcha Mungu—hili ndilo jambo kuu. Pili, wana ubinadamu mzuri kiasi, wana sifa nzuri, na watu wengi wanawapenda. Tatu, wao hufanya kazi yao kwa kujitolea. Mtu yeyote ambaye ana sifa hizi tatu ni mmoja wa watu wa Mungu. Kwa watu wa Mungu, haijalishi jinsi ubora wao wa tabia ulivyo wa juu; wao angalau wana ubora wa wastani wa tabia na wanaweza kuelewa ukweli wa kawaida, lakini jambo kuu ni kwamba wana mioyo ya uchaji na ubinadamu mzuri. Bila kujali wanapowekwa au ni wajibu gani unaowaomba waufanye, wao ni wa kuaminika kabisa. Wao hawatendi kwa namna moja mbele yako lakini vingine kisirisiri; wao si wanafiki, na hawakubaliani hadharani lakini kupinga sirini. Wao ni waaminifu na wa kutegemewa kiasi; wao huvutia imani ndani ya wengine. Watu wote kama hawa wana ubinadamu mzuri kiasi na wanaaminika kabisa; wao ni watu wa Mungu katika Enzi ya Ufalme.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Watendaji huduma hawajapata ukweli kama maisha yao kabisa; wanamfanyia Mungu pekee huduma. Wana mioyo miaminifu kwa Mungu na pia imani, na wana ubinadamu mzuri kiasi, lakini hawapendi ukweli sana. Wanategemea shauku yao katika kujitumia kwa ajili ya Mungu na wako tayari kupitia mateso yoyote. Watafuata hadi mwisho kabisa na kutowahi kuondoka kutoka kwa Mungu. Hii ndiyo maana watu ambao ni watendaji huduma waaminifu watasalia. … Mbona inasemwa kwamba wao ni watendaji huduma? Ni kwa sababu hawafuatilii ukweli. Wale wanaofuatilia ukweli pia wana wakati ambapo upotovu wao unafichuliwa na nyakati ambazo wanashindwa, lakini punde wanapopogolewa na kushughulikiwa, wanapitia kushindwa na vipingamizi, au kufukuzwa kutoka kwa nyumba ya Mungu, wanatambua: “Yeye asiye na ukweli ni wa kusikitisha sana, yeye ategemeaye raghba hawezi kusimama imara! Kama mtu hawezi kutenda ukweli, kama mtu haelewi ukweli, basi mtu hatawahi kuweza kufanya wajibu wake hadi kufikia kiwango kilichowekwa. Je, huyu si mtendaji huduma? Siwezi kuwa mtendaji huduma—lazima nifuatilie ukweli na kujitahidi kukamilisha wajibu wangu hadi kufikia kiwango kilichowekwa ili kuufariji moyo wa Mungu, na kulipiza upendo wa Mungu.” Anazinduka na kuanza kufuatilia ukweli, na mwishowe hakika anapata ukweli kiasi, hakika anaanza kuwa na moyo unaomcha Mungu. Kwa hiyo, je, watu kama hawa bado ni watendaji huduma? Wao ni watu wa Mungu kwa sababu wana ukweli kiasi na wana mioyo inayomcha Mungu, mioyo inayompenda Mungu. Mara wanapokuwa wasiotii na wanaopinga wanatambua hilo na kutubu kwa Mungu, na kisha kubadilika; mtu wa aina hii ni yule ambaye amepata ukweli kama maisha yake mwenyewe.

Je, kuna tofauti kubwa kati ya watu wa Mungu na watendaji huduma? Ingawa si kubwa sana au wazi sana, hakika wao ni tofauti kimsingi. Watendaji huduma wanamwogopa Mungu kidogo, wakisema tu kama ni sana: “Usimkosee Mungu! Ukimkosea Mungu utaadhibiwa!” Je, kitu kidogo kama hicho kinaweza kufikiriwa uchaji wa kweli kwa Mungu? Wale wenye moyo ambao unamcha Mungu kwa kweli hawafikirii iwapo watamkosea Mungu au la tu, lakini pia wanafikiria iwapo wanaenda kinyume na maneno ya Mungu au la, iwapo kufanya kitu fulani ni kutomtii Mungu, iwapo kinaweza kuumiza moyo wa Mungu, na jinsi wanavyoweza kumridhisha Mungu. Wanafikiria vipengele hivi vyote, huku ni kuwa na moyo unaomcha Mungu. Yeye aliye na moyo unaomcha Mungu, huku akitenda ukweli, anaweza angalau kujitenga na maovu na kuepuka kufanya mambo yanayompinga Mungu; anaweza kupita kiwango hiki cha msingi. Huku kunaitwa kuwa na moyo unaomcha Mungu. Kuna tofauti kati ya moyo unaomcha Mungu na kuwa na moyo unaomwogopa Mungu kidogo. Mtu aliye na moyo unaomcha Mungu hakika anaelewa ukweli kiasi na anaweza kuweka maneno kiasi ya Mungu katika vitendo, basi mtu huyu hakika ana uzima; yeye aliye na ukweli kama uzima wake ni wa watu wa Mungu. Watendaji huduma hawana ukweli kama uzima wao, hawapendi ukweli, na yote waliyo nayo ni imani katika Mungu. Aidha, angalau wana raghba na ubinadamu wa wastani; wako tayari kujitumia kwa ajili ya Mungu. Haijalishi kiasi cha shida zilizo nyumbani, haijalishi wanakabiliwa na hali na majaribu yapi, wanashikilia katika kumfanyia Mungu huduma kiasi na ni waaminifu hadi mwisho kabisa bila kurudi nyuma. Hawa ni watu ambao watasalia, watendaji huduma waaminifu. Watendaji huduma wengine hawahudumu hadi mwisho; punde wanaposikia hawatapata baraka, wanaacha kutoa huduma. Watendaji huduma wengine ambao hawawezi kutoa huduma vizuri, hawaruhusu mtu yeyote awashughulikie. Punde mtu anapowashughulikia, wanasema, “Sitafanya huduma tena, naenda nyumbani.” Watendaji huduma wengine, wanapokabiliwa na hali nzito, kwa mfano, kukamatwa, wanakuwa waoga na kurudi nyuma. Katika mkondo wa huduma yao, wengine bado wana wasiwasi kuhusu maisha ya familia yao: “Je, familia yangu itaishi vipi? Lazima nirudi na kuchuma fedha kiasi, lazima niwatunze mume (au mke) na watoto vizuri.” Wanaangalia nyuma wakianza kazi, wakiwa hawana uaminifu wowote kwa Mungu. Watendaji huduma wa aina hii hawajafikia kiwango kilichowekwa, na hivyo wote wataondoshwa.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Zamani, kulikuwa na watu wengi ambao hawakuwa na ufahamu wa watu wa Mungu. Hata hiyo, watu wa Mungu ni nini? Je, si kweli kwamba sisi ambao tumemkubali Mwenyezi Mungu ni watu Wake? Sio unapokubali jina la Mwenyezi Mungu ndipo unakuwa mmoja wa watu Wake. Kwa ajili ya hilo, kuna mchakato wa kukamilishwa, ambao una kigezo. Kigezo hiki ni kipi? Ni kwa wewe kuwa umetekeleza wajibu wako kufikia kiwango kilichowekwa, na ni hapo tu ndipo unakuwa mmoja wa watu wa Mungu; wale ambao hawajafikia kigezo hiki katika wajibu wao si watu wa Mungu. Wao si watu wa Mungu. Kusema kwa usahihi, wao ni watendaji huduma—hivi ndivyo wanavyoitwa katika kipindi hiki cha utendaji. Wale ambao bado hawajapata ukweli wanaitwa watendaji huduma. Wakati mtu amepata ukweli na anaweza kushughulikia masuala kwa mujibu wa kanuni, inamaanisha kwamba amepata uzima. Ni wale tu walio na ukweli kama uzima wao ndio watu wa Mungu kwa kweli.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Iliyotangulia: 43. Mungu hutegemeza nini uamuzi Wake wa mwisho wa mtu?

Inayofuata: 45. Ahadi za Mungu kwa wale ambao wameokolewa na kukamilishwa ni zipi?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

1. Kufuata mapenzi ya Mungu ni nini na iwapo kufuata mapenzi ya Mungu ni kuhubiri na kumfanyia Bwana kazi tu

Ninaamua hatima ya kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu.

2. Sababu ya ulimwengu wa kidini daima kumkana, kumkataa na kumhukumu Kristo

Jinsi inavyovutia! Kwa nini kupata mwili kwa Mungu daima kumekataliwa na kushutumiwa na watu? Kwa nini watu hawawi na ufahamu wowote wa kupata mwili kwa Mungu kamwe? Inawezekana kuwa Mungu amekuja wakati mbaya? Inawezekana kuwa Mungu amekuja mahali pabaya? Inawezekana kwamba hili hutokea kwa sababu Mungu ametenda peke yake, bila “sahihi” ya mwanadamu? Inawezekana ni kwa sababu Mungu alifanya maamuzi Yake Mwenyewe bila ruhusa ya mwanadamu? …

3. Jina la Mungu linaweza kubadilika, lakini asili Yake haibadiliki kamwe

Kuna wale ambao wanasema kuwa Mungu habadiliki. Hiyo ni sahihi, lakini inaashiria mabadiliko ya tabia ya Mungu na pia kiini chake. Mabadiliko ya jina lake na kazi hayathibitishi ya kuwa kiini chake kimebadilika; kwa maneno mengine, Mungu siku zote Atakuwa Mungu, na hii kamwe haitabadilika. Iwapo utasema kuwa kazi ya Mungu daima inabaki vile vile, basi Angekuwa na uwezo wa kumaliza mpango wake wa usimamizi wa miaka elfu sita?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki