Wimbo wa Injili | Kristo wa Siku za Mwisho Hufichua Siri ya Mpango wa Mungu wa Usimamizi (Music Video)
18/04/2020
Na kuhusu maono ya kazi katika mpango wote wa usimamizi wa miaka elfu sita,
hakuna anayeweza kupata ufahamu au kuelewa.
Maono kama hayo yamebaki kuwa mafumbo kila wakati.
Haijalishi mwanadamu ana maarifa makubwa ya Biblia vipi,
yanabaki tu kuwa maneno na si kitu zaidi,
kwani mwanadamu haelewi kiini cha Biblia.
Kazi hii ya miaka elfu sita
ni ya fumbo zaidi kuliko unabii wote wa manabii.
Ni fumbo kuu zaidi tangu uumbaji,
na hakuna nabii wa awali ambaye
amewahi kuweza kulielewa,
kwani fumbo hili hufumbuliwa tu katika enzi ya mwisho.
Mwanadamu anaposoma Biblia, anaweza kupokea baadhi ya ukweli,
kueleza baadhi ya maneno ama kuchunguza vifungu maarufu na nukuu,
lakini hatawahi kuwa na uwezo wa kunasua maana iliyoko katika maneno hayo,
kwani yote aonayo mwanadamu ni maneno yaliyokufa pekee,
sio matendo ya kazi ya Yehova na Yesu,
na mwanadamu hawezi kufumbua mafumbo ya kazi ya aina hiyo.
Kwa hivyo, fumbo la mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita ni fumbo kuu,
iliyofichwa zaidi
na isiyoshawishika kwa mwanadamu.
Hakuna anayeweza kuelewa moja kwa moja mapenzi ya Mungu, ama,
Yeye Mwenyewe Aeleze na kumfungulia mwanadamu,
vinginevyo, yatabaki kuwa mafumbo milele kwa mwanadamu
na kubaki mafumbo yaliyofungwa milele.
Usiwajali wale walio katika ulimwengu wa kidini;
kama hamngeambiwa leo,
pia nyinyi hamngeweza kuelewa.
Kazi hii ya miaka elfu sita ni
ya fumbo zaidi kuliko unabii wote wa manabii.
Ni fumbo kuu zaidi tangu uumbaji,
na hakuna nabii wa awali ambaye
amewahi kuweza kulielewa,
kwani fumbo hili hufumbuliwa tu katika enzi ya mwisho.
kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya
Ikiwa una matatizo au maswali yoyote katika imani yako, tafadhali wasiliana nasi wakati wowote.
Aina Nyingine za Video