Wimbo wa Kikristo | Azimio Linalohitajika ili Kufuatilia Ukweli

17/03/2020

Je, wengi wenu sasa wana azimio la kuelewa ukweli,

kupata ukweli na kukamilishwa mwishowe?

Lazima ufikie hatua ambapo

azimio lako halibadiliki bila kujali ni mazingira gani unayoyakabili;

huku tu ndiko kuwa mwaminifu,

na huo ndio upendo halisi wa ukweli na shauku halisi ya kuwa aina hii ya mtu.

Itakuwa bure kujikunyata wakati hoja fulani ndogo

au shida inapotokea, au kuwa hasi,

kusononeka na kuacha azimio lako mwenyewe wakati unapokabiliwa na shida ndogo.

Unahitaji kuwa na nguvu ya mtu anayechagua kuhatarisha maisha yake, na kusema,

"Bila kujali kinachotokea,

hata kama ni lazima nife sitaacha azimio langu au kuachana na lengo hili."

Halafu hakutakuwa na shida ambayo inaweza kukuzuia,

na Mungu atakufanyia jambo hili.

Lazima uwe na mtazamo wa aina hii na ufahamu jambo linapotokea, na kusema,

"Bila kujali kinachofanyika,

yote ni sehemu ya kufanikisha lengo langu, na ni shughuli ya Mungu.

Kuna udhaifu ndani yangu, lakini mimi si hasi.

Ninamshukuru Mungu kwa upendo Anaonipa

na kwa kunipangia aina hii ya mazingira.

Ni lazima nisisalimu amri.

Kusalimu amri kwangu kungekuwa sawa na kufanya masikilizano na Shetani,

na ni sawa na kujiangamiza.

Kusalimu amri juu ya shauku na azimio langu kutakuwa sawa na kumsaliti Mungu."

Hii ni aina ya moyo ambao ni lazima uwe nao.

Bila kujali wengine wanavyosema au jinsi walivyo,

na bila kujali jinsi Mungu anavyokutendea, azimio lako halipaswi kubadilika.

Bila kujali wengine wanavyosema au jinsi walivyo,

azimio lako halipaswi kubadilika.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.

Tazama zaidi

Ikiwa una matatizo au maswali yoyote katika imani yako, tafadhali wasiliana nasi wakati wowote.

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp