Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu | Dondoo 506

Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu | Dondoo 506

107 |18/09/2020

Leo, watu wengi sana hawana ufahamu huo. Wao huamini kwamba mateso hayana thamani, wao hukanwa na ulimwengu, maisha yao ya nyumbani yamesumbuliwa, wao si wapendwa wa Mungu, na matazamio yao ni matupu. Kuteseka kwa watu wengine hufikia kiwango fulani, na fikira zao hugeukia kifo. Huu si upendo wa kweli kwa Mungu; watu kama hao ni waoga, hawana ustahamilivu, wao ni wadhaifu na wasio na nguvu! Mungu ana hamu ya mwanadamu kumpenda Yeye, lakini kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo kuteseka kwa mwanadamu huwa kwingi zaidi, na kadri mwanadamu anavyompenda Yeye, ndivyo majaribio ya mwanadamu huwa makubwa zaidi. Ikiwa unampenda Yeye, basi kila aina ya mateso yatakufika—na ikiwa humpendi, basi labda kila kitu kitaendelea kwa urahisi kwako, na kila kitu kinachokuzunguka kitakuwa kitulivu kwako. Unapompenda Mungu, utahisi kwamba mengi kandokando yako hayawezi kushindikana, na kwa sababu kimo chako ni kidogo sana utasafishwa; aidha, huwezi kumridhisha Mungu, na daima utahisi kwamba mapenzi ya Mungu ni ya juu sana, kwamba hayawezi kufikiwa na mwanadamu. Kwa sababu ya haya yote utasafishwa—kwa sababu kuna udhaifu mwingi ndani yako, na mengi yasiyoweza kuridhisha mapenzi ya Mungu, utasafishwa ndani. Lakini lazima muone kwa dhahiri kwamba utakaso hutimizwa tu kupitia usafishaji. Hivyo, katika siku hizi za mwisho lazima muwe na ushuhuda kwa Mungu. Haijalishi mateso yenu ni makubwa vipi, mnapaswa kuendelea hadi mwisho kabisa, na hata wakati wa pumzi yenu ya mwisho, bado lazima muwe waaminifu kwa Mungu, na kudhibitiwa na Mungu; huku pekee ndiko kumpenda Mungu kweli, na huu pekee ndio ushuhuda thabiti na mkubwa sana. Unapojaribiwa na Shetani, unapaswa kusema: “Moyo wangu ni wa Mungu, na Mungu tayari amenipata. Siwezi kukuridhisha wewe—lazima nitoe kila kitu changu ili kumridhisha Mungu.” Kadri unavyomridhisha Mungu, ndivyo Mungu hukubariki zaidi, na ndivyo nguvu za upendo wako kwa Mungu huwa kuu zaidi; kwa hiyo, vilevile, utakuwa na imani na azimio, na utahisi kwamba hakuna kilicho na thamani zaidi au cha maana kuliko kutumia maisha ukimpenda Mungu. Inaweza kusemwa kwamba mwanadamu anatakiwa tu kumpenda Mungu ili kuishi bila huzuni. Ingawa kuna nyakati ambazo mwili wako ni dhaifu na unazongwa na matatizo mengi ya kweli, katika nyakati hizi utamtegemea Mungu kweli, na ndani ya roho yako utafarijiwa, na utahisi hakika, na kwamba una kitu cha kutegemea. Kwa njia hii, utaweza kushinda hali nyingi, na kwa hiyo hutalalamika kuhusu Mungu kwa sababu ya uchungu unaopitia; utataka kuimba, kucheza, na kuomba, kukusanyika na kuwasiliana kwa karibu, kumfikiria Mungu, na utahisi kwamba watu wote, mambo, na vitu vilivyo kandokando yako ambavyo vimepangwa na Mungu vinafaa. Kama humpendi Mungu, yote ambayo unategemea yatakuwa yenye kero kwako, hakuna kitakachokuwa cha kufurahisha machoni mwako; ndani ya roho yako hutakuwa huru bali wa kudhulumiwa, moyo wako daima utalalamika kuhusu Mungu, na daima utahisi kwamba unapitia mateso mengi sana, na kwamba ni udhalimu sana. Kama hufuatilii kwa ajili ya furaha, bali ili umridhishe Mungu na kutoshtakiwa na Shetani, basi ukimbizaji kama huo utakupa nguvu nyingi za kumpenda Mungu. Mwanadamu anaweza kutekeleza yote yanayonenwa na Mungu, na yote ayafanyayo yanaweza kumridhisha Mungu—hii ndiyo maana ya kuwa na hakika. Kufuatilia ridhaa ya Mungu ni kuutumia upendo wa Mungu kutia maneno Yake katika vitendo; pasipo kutia maanani wakati—hata kama wengine hawana nguvu—ndani yako bado kuna moyo unaompenda Mungu, ambao unamtamani Mungu sana, na humkosa Mungu. Hiki ni kimo halisi. Jinsi ambavyo kimo chako ni kikubwa hasa hutegemea jinsi upendo wako kwa Mungu ulivyo mkuu, kama unaweza kusimama imara wakati unajaribiwa, kama wewe ni mdhaifu hali fulani inapokujia, na kama unaweza kusimama imara wakati ambapo ndugu zako wanakukataa; majilio ya ukweli yataonyesha hasa upendo wako kwa Mungu ukoje. Inaweza kuonekana kutoka kwa kazi nyingi ya Mungu kwamba Mungu kweli anampenda mwanadamu, ni hasa tu macho ya roho ya mwanadamu bado hayajafunguliwa kabisa, na hawezi kufahamu kazi nyingi ya Mungu, na mapenzi ya Mungu, na vitu vingi ambavyo ni vya kupendeza kuhusu Mungu; mwanadamu ana upendo kidogo sana wa kweli kwa Mungu. Umemwamini Mungu katika wakati huu wote, na leo Mungu amezuia njia zote za kutoroka. Kusema kwa kweli, huna chaguo lingine ila kuifuata njia sahihi, njia sahihi ambayo umeelekezwa kwayo kwa hukumu kali na wokovu mkubwa kabisa wa Mungu. Ni baada tu ya kupitia taabu na usafishaji ndiyo mwanadamu hujua kwamba Mungu ni wa kupendeza. Baada ya kupitia mpaka leo, inaweza kusemwa kwamba mwanadamu amekuja kujua sehemu ya kupendeza kwa Mungu—lakini hili bado halitoshi, kwa sababu mwanadamu amepungukiwa sana. Lazima apate uzoefu zaidi wa kazi ya Mungu ya ajabu, na zaidi ya usafishaji wote wa mateso uliowekwa na Mungu. Ni wakati huo tu ndiyo tabia ya maisha ya mwanadamu itaweza kubadilishwa.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Onyesha zaidi
Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Shiriki

Ghairi