Wimbo wa Kusifu | Mfano Halisi wa Nguvu ya Uzima ya Mungu

07/07/2020

Wote wanaokuja duniani humu lazima wapitie maisha na kifo,

na wengi wao walipitia mzunguko wa kifo na kuzaliwa upya,

mzunguko wa kifo na kuzaliwa upya.

Wale wanaoishi watakufa hivi karibuni na wafu watarejea karibuni.

Yote haya ni mwendo wa maisha uliopangwa na Mungu kwa kila kiumbe hai.

Hata hivyo, njia hii na mzunguko huu

hasa ni ukweli ambao Mungu anataka binadamu aone:

kwamba uzima aliopewa mwanadamu na Mungu hauna mipaka,

na hauzuiliwi na maumbile ya nje, wakati, au nafasi.

Hili ndilo fumbo la uzima aliopewa binadamu na Mungu,

na dhihirisho kwamba maisha yalikuja kutoka Kwake.

Ingawa watu wengi wanaweza kukosa kuamini kwamba maisha yalitoka kwa Mungu,

binadamu bila ya kufahamu hufurahia yote yatokayo kwa Mungu,

iwe wanaamini au wanakana uwepo Wake.

Iwapo siku moja Mungu kwa ghafla Atabadili moyo

na Atake kurudisha yote yaliyomo duniani

na kuchukua maisha Aliyotoa,

basi yote duniani yataisha.

Mungu hutumia maisha Yake kukimu vitu vyote vilivyo hai na visivyo na uhai,

na kuleta yote kwa utaratibu mzuri kwa mujibu wa uwezo na mamlaka Yake.

Huu ni ukweli ambao hauwezi kuwazika au kueleweka na yeyote,

na kweli hizi zisizoeleweka kwa fikira zetu

ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha,

ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Leave a Reply

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp