26. Uvukaji Mipaka na Ukuu wa Nguvu ya Mungu ya Maisha

Na Lin Ling, Jimbo la Shangdong

Nilizaliwa katika familia masikini ya mashambani, na kwa sababu familia yetu ilikosa uwezo au hadhi, nilidharauliwa na wengine tangu utotoni, na mara nyingi nilidhulumiwa. Kila wakati hili lilipofanyika, nilihisi kufedheheka na mwenye taabu, na nilitamani siku ambayo mwokozi angekuja kubadilisha majaliwa yangu. Baada ya kufunga ndoa, kwa sababu maisha yalikuwa magumu, na mwanangu alikuwa mgonjwa mara kwa mara, majirani wangu walinizungumzia kuhusu kumwamini Yesu, na nilipopata habari kuwa Bwana Yesu anaweza kuwaokoa wale wanaoteseka kutokana na mateso na shida zao, niliguswa sana. Nilihisi kuwa hatimaye nilikuwa nimepata Mwokozi wangu, na kwa hivyo kuanzia hapo nilimwamini Yesu, na nilihudhuria mikutano kwa shauku na kusikiliza mahubiri kila mahali nilipoweza. Lakini baadaye, niligundua kuwa makanisa daima yalikuwa ya kuhuzunisha zaidi, na kwamba wivu, mabishano, na njama kati ya waumini vilizidi kuongezeka. Haikuwa tofauti na jamii kwa ujumla. Sikuweza kujizuia kusikitika, imani ambayo nilihisi mwanzoni ilipungua polepole, na sikuhudhuria mikutano tena.

Mnamo mwaka wa 2000, dada mmoja alinihubiria injili ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Nilipopata habari kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerejea, maneno hayakuweza kuelezea furaha niliyohisi moyoni mwangu. Kila siku, kila nilipokuwa na wakati, nilikuwa na neno la Mungu mkononi mwangu na nililisoma kama vile mtu ashindaye na njaa hula. Unyofu katika maneno ya Mungu ulinichangamsha na kunifariji. Nilihisi utunzaji, rehema, na wokovu wa Muumba, na roho yangu yenye shauku ilipata kunyunyuziwa na riziki. Baada ya hapo, niliishi miongoni mwa familia kubwa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, ambapo nilihudhuria mikutano na kutekeleza wajibu wangu pamoja na ndugu zangu. Sisi sote tulijitahidi kufuatilia ukweli pamoja na kunyunyuziwa na maandalizi ya neno la Mwenyezi Mungu, kulikuwa na upendo baina ya ndugu zangu, na sote tulisaidiana. Hakukuwa na njama, udanganyifu, au dharau la umaskini na upendo wa mali, au kuwepo kwa dhuluma au ukandamizaji. Katika Kanisa la Mwenyezi Mungu, nilifurahia kwa kweli furaha na shangwe ambayo sikuwahi kuona hapo awali. Hata hivyo, kwa sababu nilimwamini Mwenyezi Mungu, nilikamatwa na kuteswa kikatili na serikali ya CCP, na kisha kufungwa gerezani kwa muda wa mwaka mmoja. Katika pango hilo la pepo lenye giza, neno la Mwenyezi Mungu ndilo lilinipa imani na nguvu, na ndilo lililoniongoza polepole kumshinda Shetani na kukataa kudhibitiwa na vizuizi vya kifo.

Usiku wa tarehe 24 Agosti, mwaka wa 2009, nilikuwa nimekwenda tu kulala, nilipoamshwa ghafla na kubisha kwa ukali mlangoni. Kabla sijapata wakati wa kujibu, polisi 7-8 waliuvunja mlango na kuingia ndani ya chumba hicho. Mara tu walipoingia, walisema kwa sauti kubwa, “Usisonge! Ondoka kitandani na uandamane nasi!” Kabla hata sijapata muda wa kuvaa nguo zangu, nilisikia mwaliko sauti wa kibodi cha kamera huku nikipigwa picha. Polisi kisha wakapekuapekua nyumba hiyo kwelikweli walipokuwa wakichunguza, bila kukosa kupekua hata kipande kimoja cha karatasi. Muda si muda, nyumba ilikuwa imevurugika, kana kwamba imechakurwa na majambazi. Kila kitu kilikuwa kwenye sakafu, na hakukuwa na mahali pa kutembea. Baadaye, polisi watatu walinipeleka kwa nguvu kwenye gari lililokuwa likisubiri nje.

Baada ya kunipeleka kwenye kituo cha polisi, walinilazimisha kusimama nikitazama ukuta. Afisa mmoja wa polisi alinihoji kwa sauti kali, akisema, “Tuambie ukweli kuhusu imani yako katika Mwenyezi Mungu! Je, wajibu wako ni upi kanisani? Kiongozi wako ni nani? Yuko wapi? Tuambie kila kitu!” Nilisema, bila woga, “Sijui chochote!” Kero lao lilibadilika kuwa ghadhabu mara moja. Walinipiga mateke wakinitupia matusi kwa sauti kubwa na kunitisha kwa nguvu, “Ukituambia, tutakuachilia, lakini ikiwa sivyo, tutakupiga hadi ufe!” Walipokuwa wakizungumza, walinisukuma hadi kwenye kiti cha chuma kilichokuwa na nguzo kuu ya kuzuia, ambacho kisha walikifunga kwa uthabiti. Nilipoona jinsi polisi hawa waovu walivyonikamata kwa utumiaji nguvu wa namna hiyo, na vile vile sura za kikatili na macho ya hasira waliyonielekeza, na jinsi walivyonitendea, mwanamke asiye na utetezi, kana kwamba nimetenda makosa mabaya, singeweza kujizuia kushikwa na hofu na kuogopa. Niliwaza, “Je, wanapangaje kunitesa? Ikiwa kweli watanitesa au kunipiga, nitafanya nini?” Singeweza kujizuia kumwomba Mungu moyoni mwangu, “Mwenyezi Mungu! Kimo changu kweli ni kidogo sana, na, kwa nikiwa nimezungukwa na nguvu za uovu za Shetani, nimeogopa. Ninakusihi Unipe imani na nguvu. Unilinde, ili nisisujudu kwa Shetani na pepo hawa, na ili niweze kusimama kidete na kukushuhudia Wewe!” Wakati huu ndipo nilipokumbuka maneno ya Mungu, “Unapaswa kujua kwamba vitu vyote vilivyo katika mazingira yanayo wazunguka vipo hapo kwa ruhusa Yangu, Mimi napanga yote. Oneni wazi na muridhishe moyo Wangu katika mazingira Niliyokupa. Msiogope, Mwenyezi Mungu wa majeshi hakika atakuwa pamoja nawe; Yeye anawasaidia na Yeye ni ngao yenu” (“Sura ya 26” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Ndiyo, kila kitu kilichonitokea siku hiyo kilikuwa na ruhusa ya kiti cha enzi cha Mungu, kwa hivyo ingawa nilikuwa nimenaswa katika pango la pepo na nilikabiliwa na kikundi cha ibilisi wakali, wa shetani, sikuwa nikipigana peke yangu; Mwenyezi Mungu alikuwa nami. Ningeweza kumtegemea, na Alikuwa tegemeo langu thabiti, kwa hivyo cha kuogopa kilikuwa kipi? Nilipofikiria mambo haya, sikujiona tena mwepesi kutishwa au mwoga, nilikuwa na nguvu ya kupigana na Shetani hadi mwisho, na niliapa kuwa ningesimama kidete na kumhuhudia Mungu hata kama ingenigharimu maisha yangu!

Baada ya hayo, polisi walianza kujaribu kupata ungamo kutoka kwangu kwa kutumia nguvu kwa njia ya mateso. Asubuhi ya siku ya kwanza, walinitia pingu, na kisha polisi wakanipeleka kupimwa damu, walinivuta kwa nguvu, na kusababisha ncha kali za pingu kuung’ata mwili wangu. Muda si muda, ngozi kwenye vifundo vya mikono yangu ilitoboka, na uchungu ulikuwa wa kuumiza na mkali sana. Baada ya hapo, walinitia pingu kwenye rejeta, na kwa ajili ya kuogopa kuwa ningekimbia, walikaza pingu sana hadi vifundo vya mikono yangu vikasagika kuwa fujo lenye damu. Maafisa hawa waovu wa polisi walinihoji mara kwa mara, wakijaribu bila mafanikio kunilazimisha nitoe habari za kanisa, lakini kwa sababu kila mara nilisema kuwa sijui chochote, walighadhibishwa na kukasirika. Mmoja wao alisogea mbele kwa hasira na akanipiga kofi usoni kwa nguvu. Niliona vimulimuli mara moja, karibu nizimie, meno yangu yaligongana kwenye ufizi wangu, na machozi yalitiririka kutoka machoni mwangu pasipo kutaka. Afisa wa polisi aliponiona nikilia lakini bado nimekataa kuzungumza, alikunja uso kwa hasira, na kuzivuta kikatili nywele zangu kadhaa zilizo kwenye komo la uso wangu na kuzizungusha mikononi mwake, na kisha akabamiza kisogo changu ukutani. Pigo hili kali lilinifanya niwe na kizunguzungu na masikio yangu kuwangwa. Hasira yake ikiwa bado haijapungua, alinipiga kofi mara kadhaa mfululizo na kusema kwa sauti kubwa, “Nitakuliza! Hilo ndilo unalopata kwa kutozungumza!” Alipokuwa akiongea, alinikanyaga kwenye miguu yangu kwa viatu vyake. Baada ya kupokea mapigo na mateso makali ya pepo hawa, nilikuwa nahisi uchungu na ulegevu kote. Nililala sakafuni, bila kusonga, kana kwamba nilikuwa karibu nife. Walipoona hali yangu, polisi walinifokea mfululizo wa mapayo na kuondoka, wakibamiza mlango walipokuwa wakitoka. Katika majira ya alasiri, walinipiga kwa ukatili vile vile walipokuwa wakijaribu kunilazimisha nitoe habari za kanisa. Baada ya raundi kadhaa za hayo, nilihisi kizunguzungu na kichefuchefu, na mwili wangu uliumia sana hadi ilihisi kuwa tayari kusalimu amri. Nilihisi kana kwamba ningeweza kufariki wakati wowote. Lakini polisi hao wabaya hawakupunguza mahojiano hata kidogo. Wakiwa na ukosefu wa ubinadamu, walitumia kiberiti cha plastiki kuzichoma nyaya zangu, na kusababisha malengelenge mawili makubwa mara moja. Iliumiza sana sikuweza kujizuia kulia. Nikihisi uchungu, niliketi sakafuni na kuwatazama polisi hawa wabaya, kila mmoja wao akinikodolea macho kwa ghadhabu ya kinyama kama pepo wa kuzimu waliotamani sana kunichana vipande vipande, na sikuweza kujizuia kuhisi dhaifu. Nilimlalamikia Mungu kimyakimya, “Mwenyezi Mungu, polisi hawa wabaya wataacha kunitesa lini? Siwezi kuvumilia zaidi….” Nilihisi dhaifu sana nilikuwa tayari kuzimia, na sikuweza kujizuia kuwaza, “Je, itakuwaje nikiwaambia tu jambo moja? Basi sitalazimika kuteseka….” Lakini kisha nikafikiria papo hapo, “Nikisema hata jambo moja, mimi ni Yuda, linalomaanisha kwamba ninamsaliti Mungu.” Ugomvi mkali ulizuka moyoni mwangu, na ikawa wakati huo ndipo nikakumbuka maneno ya Mungu, “Mnafaa kufanya yale ambayo yanawapendeza watu wote, na yale ambayo yana manufaa kwa binadamu wote, na yale yanayofaidi hatima yenu wenyewe, la sivyo, yule atakayeteseka katika maafa hatakuwa mwingine ila wewe” (“Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili). “Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu” (“Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalikuwa ujio wa ghafla wa utambuzi. Sikuweza kujizuia kushtushwa na mawazo yangu ya awali. Niliakisi, “Mateso ya Shetani yamenipata leo, na badala ya kufikiria kuhusu jinsi ya kumtegemea Mungu kushinda pepo hawa na kusimama kidete na kumshuhudia Yeye, badala yake nilikuwa nikijali mwili wangu. Je, hilo halinifanyi kuwa mbinafsi na wa kudharauliwa? Mungu ni mwenye haki na mtakatifu, na ikiwa ningewauza ndugu zangu na kuwa Yuda wa aibu, je, singekuwa nikiikosea tabia ya Mungu, na hivyo kujiangamiza? Mapenzi ya Mungu katika kuwaruhusu polisi hawa waovu kunitesa leo ni kuniwezesha kuona waziwazi asili ya uovu ya CCP ya kumpinga Mungu bure na kuwa adui na Mungu, ili niweze kuugeuza moyo wangu kwa Mungu, kudumisha uaminifu wangu kwa Mungu, na kusimama kidete na kumshuhudia Mungu.” Baada ya kufikia maamuzi haya, nilijutia na kujiona mwenye hatia kwa ajili ya kutotii kwangu. Nilitamani kutubu kwa Mungu. Bila kujali polisi waliniumiza au kunitesa jinsi gani, nilikataa kuufurahisha mwili wangu. Nilitaka tu kutii mipango na utaratibu wa Mungu, kuvumilia shida zote, na kusimama kidete na kumshuhudia Mungu ili nithibitishe uaminifu wangu Kwake kupitia matendo yangu. Hata kama ingenigharimu maisha yangu, singekuwa Yuda na kumsaliti Mungu! Ilimradi nilikuwa bado nina uhai ndani yangu, singeweza kamwe kujisalimisha au kukukabali kushindwa na Shetani! Jioni hiyo, polisi hawa wabaya waliniamuru niketi sakafuni na miguu yangu ikiwa imenyooshwa sana, kisha wakainua mikono yangu kwa nguvu, ikiwa imetiwa pingu mgongoni mwangu, juu hewani, na papo hapo nilihisi maumivu makali mikononi mwangu na kwenye vifundi vya mikono yangu ambavyo tayari vilikuwa vimejeruhiwa. Polisi, wasioweza kujizuia kwa ajili ya ghadhabu, waliitia feni kwenye mwendo wa kasi sana na kunielekezea, ikapuliza mkondo wa hewa baridi juu ya mwili wangu. Nilihisi baridi sana na kutetemeka kila wakati, na meno yangu yalitatarika kinywani. Nilikuwa na hedhi wakati huo, na badala ya kuniruhusu nibadilishe kisodo changu, polisi hawa wabaya walinishurutisha “niimalize” katika chupi langu. Lakini hata na hayo, polisi hawa waovu hawakukoma. Walileta ufito wa tawi la mti laini na kunichapa nao kote, kila pigo likiacha alama yenye damu. Ilikuwa chungu sana hadi nilijaribu kujinyonganyonga mwili ili kuepuka, lakini waliponiona nikikwepa kipigo, polisi walinipiga kwa nguvu zaidi, wakifanya hivyo walisema, “Hebu tuone ikiwa sasa utazungumza! Leo usiku nitakuacha ukiwa kiwete aliyetambarika!” Ukatili na ubaya wa maafisa hawa waovu wa polisi ulikuwa wa kuchukiza mno, lakini kwa ajili ya mwongozo na ulinzi wa Mungu, sikujisalimisha kwao, na hawakupata chochote katika raundi hiyo ya mahojiano.

Miongoni mwa siku nyingi za mahojiano ya kikatili, afisa mmoja kutoka kwenye Brigedi ya Usalama wa Kitaifa aliendelea kujifanya kuwa “askari mzuri,” akijaribu bila mafanikio kunishawishi nisaliti kanisa kwa kutumia mbinu zenye huruma. Alikuwa na sura ya kuvutia, ya upole, akanipa maji, akaniletea tufaha, akiwa na wema wa uwongo alisema, “Ni aibu sana kuteseka namna hii katika umri mdogo sana hivi. Tuambie tu kile tunachotaka kujua, na linaweza kukoma. Unaweza kwenda nyumbani. Mume wako na mwana wako wanatarajia kukuona!” Hapo awali nilidhani kuwa alionekana mzuri, lakini alikuwa mkatili na mbaya zaidi kuliko yeyote kati yao. Alipogundua kuwa singemwambia, sura yake iligeuka na kuwa kemeo kali, ikifichua kabisa asili yake ya ukatili, na alianza kunitesa kwa ukatili zaidi na bila huruma. Alinipeleka katika ukumbi mkuu wa kituo cha polisi, ambako alinilazimisha niketi peke yangu pembeni kwa saa mbili kwenye hewa yenye kibaridi, na kisha baada ya kurudi na kunikemea, alidhani sijamjibu kwa sauti ya kutosha, kwa hivyo alinilazimisha ninyooshe miguu yangu, na kisha akakanyaga kwa nguvu vifuu vya magoti yangu, kisha aliinyanyua kwa ukali mikono yangu ambayo ilikuwa imetiwa pingu mgongoni mwangu. Nilisikia mwaliko kutoka kwenye kiuno changu, kisha nikasikia maumivu makali sana na nilipiga mayowe, baada ya hapo nilipoteza hisia zote kwenye kiuno changu. Sikudhani kamwe kuwa uyowe wangu ungemkasirisha ibilisi huyu. Alimfokea kwa ukali mmoja wa vibaraka wake, “Leta kitambaa na ukishindilie mdomoni mwake ili asipigie mayowe tena!” Alileta kitambaa kilichonuka, kichafu na kukishindilia katika kinywa changu, ambacho kilinifanya nitake kutapika. Alinifokea, “Kishikilie kwa meno yako! Usithubutu kukiangusha kitambaa!” alipokuwa anaendelea kukishindilia kinywani mwangu. Nilipokabiliwa na wanyama hawa wabaya, hakukuwa na kitu moyoni mwangu isipokuwa chuki kali. Niliwachukia sana sikuwa na machozi. Baadaye, afisa huyu mwovu aliendelea kunihoji, na alipoona kwamba bado singemwambia, kwa mara nyingine tena aligandamiza miguu yangu huku akiinua mikono yangu yenye pingu hewani. Ilikuwa chungu sana hadi nikaanza kutokwa na kijasho chembamba, na pasipo kutaka nilipiga mayowe tena. Alipoona kuwa bado siwezi kuongea, aliwaambia vibaraka wake, “Mchukueni!” Polisi wawili wabaya walininyanyua kutoka chini, lakini wakati huo kiuno changu hakingeweza kuinuka sambamba. Ilinibidi nitembee polepole, mgongo ukiwa umeinama, hatua moja kwa nyingine. Nikiwa katika uchungu mwingi, udhaifu, kukosa tumaini, na kutojiweza kuliniingia akilini mwangu tana. Sikujua ningeweza kuvumilia kwa muda gani, hivyo mara kwa mara nilimwomba Mungu moyoni mwangu, nikiomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu, ili hata kama ingenilazimu kufa, singemsaliti.

Baada ya hapo, niliona kuwa Mwenyezi Mungu alifahamu udhaifu wangu kwa kila njia, na alikuwa amenirehemu na kunilinda kisiri wakati wote. Polisi hawa wabaya walipokuja kunihoji tena, walinitisha, “Ikiwa hutazungumza, tutakupeleka mahali pengine na kukuweka kwenye kiti cha umeme. Mara tu tutakapowasha umeme, utapoteza fahamu, na hata ikiwa hutakufa, utakuwa mlemavu!” Niliposikia maneno ya afisa huyo muovu, sikuweza kujizuia kuogopa. Nilidhani kuwa singeweza kuhimili kutendewa unyama kama huo, kwa hivyo nilimwomba Mungu kwa upesi, na wakati huo, nikakumbuka maneno ya Mungu “Watu wanapokuwa tayari kuyatoa maisha yao, kila kitu huwa hafifu, na hakuna anayeweza kuwashinda. Ni nini kingekuwa muhimu zaidi kuliko uzima?” (“Sura ya 36” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Ndiyo, maisha yangu yalikuwa mikononi mwa Mungu. Mungu anayadhibiti na kuyatawala, na ikiwa ningeishi au kufa halikuwa jambo la kuamuliwa na polisi. Ikiwa ningehatarisha maisha yangu kwa kweli, ningemshinda Shetani. Wakati huo, nilikuwa nimejawa na imani, na nilikuwa tayari kuhatarisha maisha yangu, kuyaweka mikononi mwa Mungu, na kutii mipango na utaratibu wa Mungu. Kamwe sikufikiri kwamba wakati huo, ningemsikia mmoja wa wale polisi wabaya akisema kwamba kiti cha umeme kilikuwa hata kimeharibika, na kwamba umeme huwezi kuwashwa. Wakati huo, nilihisi kwa kina kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa nami kila wakati. Hata ingawa nilikuwa katika pango la pepo, Mungu alibaki nami. Aliniruhusu nipitie mateso, lakini hakuruhusu pepo hawa wa kishetani wachukue maisha yangu. Nilimshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya ulinzi Wake wa kimiujiza, na kwa kuniwezesha kutoroka! Imani yangu iliendelea kuwa thabiti, na nilikuwa tayari kuvumilia mateso yoyote ili nisimame kidete na kumshuhudia Mungu. Polisi hawa waovu na majinuni walinitesa na kunihoji kwa muda wa siku sita na usiku tano, bila kuniruhusu kula, kunywa maji, au kulala. Hili liliniruhusu nione waziwazi kuwa serikali ya CCP ni kikundi tu cha majambazi na wanagenge. Kuwa katika mtego wao kulimaanisha kuwa katika mtego wa pepo wakatili, wakali sana, na bila utunzaji na ulinzi wa Mwenyezi Mungu, wangenitesa hadi nife. Licha ya kwamba polisi hawa wabaya hawakuniruhusu nile, ninywe, au nilale kwa muda wa siku nyingi, na pia walinitesa kwa njia zote, kamwe sikuhisi kiu, njaa, au uchovu wowote. Maafisa wa Brigedi ya Usalama wa Kitaifa walisema hawajapata kumwona mtu mchanga akistahimili kwa muda wa siku nyingi hivyo. Nilielewa kwa undani kwamba hii ilikuwa ni nguvu kubwa ya maisha ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa ikiegemeza kipande changu cha mwili, ikinipa uzima, na kunipa nguvu ya kuendelea hadi mwisho. Kama vile Bwana Yesu alivyosema, “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu” (Mathayo 4:4). Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema, “Mungu hutumia maisha Yake kukimu vitu vyote vilivyo hai na visivyo na uhai, na kuleta yote kwa utaratibu mzuri kwa mujibu wa uwezo na mamlaka Yake. Huu ni ukweli ambao hauwezi kuwazika au kueleweka na yeyote, na kweli hizi zisizoeleweka kwa fikira zetu ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha” (“Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Baada ya hapo, polisi walipoona kuwa mbinu za kikatili hazikuwa zinafaulu, waliamua kujaribu mbinu zenye huruma. Mkuu wa Brigedi ya Usalama wa Kitaifa alikuja yeye mwenyewe kunihoji. Alinivua pingu kwa kujipendekeza na kwa upole, na kunialika niketi, na alisema kwa sauti ya “upole”, “Wewe ni mjinga sana. Wewe si afisa wa aina yoyote au mkuu katika kanisa. Walikusaliti, na uko hapa unatupinga kwa niaba yao. Je, inastahili kweli? Pia, ikiwa unamwamini Mwenyezi Mungu, katika siku zijazo mwana wako atawekewa mipaka kutahiniwa ili kuingia katika chuo kikuu, kujiunga na jeshi, au kuwa mtumishi wa umma. Na mumeo hakujali. Anaweza kuwa tayari ameshapata mtu mwingine na kukuacha…. Ukweli ni kwamba, tayari tunajua kila kitu kuhusu hali yako. Hata kama hutatuambia chochote, tunaweza kukushtaki kwa kosa bado, kwa sababu hii ni nchi ya CCP. Tunaamua kinachojiri. Pia tunaamua tutakuzuilia kwa muda wa siku ngapi. Hata ukifa hapa, hakuna kitakachotutendekea, kwa hivyo ingekuwa vyema kama ungekiri! China ni tofauti na nchi zingine. Hata kama hutatuambia chochote, bado tunaweza kukushtaki kwa kosa na kukuhukumu.” Niliposikia njia zote tofauti alizojaribu kunishawishia kwa wema, moyo wangu ulipepesuka kwa kusisimka, na nilihuzunika sana. Sikujua la kufanya, kwa hivyo niliomba moyoni mwangu, “Mwenyezi Mungu! Unajua kimo changu ni kidogo sana kwamba ninakosa mengi. Sijui jinsi ya kupitia au kukabiliana na hali kama hizi. Ninaomba mwongozo Wako.” Wakati huo ndipo nilipopata mwelekeo tena katika maneno ya Mungu: “Nyakati zote, watu Wangu wanapaswa kujihadhari dhidi ya hila danganyifu za Shetani … kitu ambacho kitawazuia kuingia katika mtego wa Shetani, wakati mtakapokuwa na majuto ya kuchelewa sana” (“Sura ya 3” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). “Kwa ajili Yangu, si lazima pia usikubali kushindwa na nguvu zozote za giza. Tegemea hekima Yangu ili kutembea kwa njia kamili; usiruhusu njama za Shetani kuchukua umiliki” (“Sura ya 10” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yaliuchangamsha moyo wangu, na nilipata njia ya utendaji. Nilijiwazia, “Hakika! Huyu alikuwa Shetani aliyekuwa akitumia ndoano za kihisia kunipotosha na kunidanganya. Ninapaswa kufahamu hila zake, nimshinde kwa hekima, na nisijiruhusu kudanganywa. Vitu vyote na mambo yote yamo mikononi mwa Mungu. Hata kama nitakaa gerezani kwa muda mrefu hadi mihimili iliwe na kutu, sharti kamwe nisijisalimishe kwa Shetani na kumsaliti Mungu!” Sasa, nilielewa wazi zaidi kuhusu nilichopaswa kufanya. Nilipokabiliwa na shari na majaribu yake, niliketi kimya, nikasali, na kuutuliza moyo wangu mbele za Mungu. Kisha, nilimwambia kwa hasira, “Nitakushtaki! Sio tu kwamba umejaribu kunitesa ili nikiri, laikini pia umenituhumu kwa kosa la uongo!” Kwa kicheko kibaya cha chinichini alisema, “Sijakupiga. Enenda ukanifungulie mashtaka. Hii ni nchi ya CCP. Hakuna atakayekutetea.” Uongo wake ulinifanya nidharau serikali mbaya ya CCP kwa moyo wangu wote. Na ibilisi huyu mzee hakujali sheria au maadili. Baada ya hapo, alileta fungu kubwa la vitambulisho vya ndugu zangu ili nivitambue, akiniuliza ikiwa niliwajua na alitumaini bure kuwa ningewasaliti. Nilijibu kwa uchungu, “Simjui hata mmoja wao!” Aliposikia hivyo, uso wake uligeuka zambarau kwa ajili ya hasira. Aliona kwamba kwa kweli sitamwambia chochote, na aliondoka akiwa amenuna. Alasiri hiyo, walinipeleka kizuizini, na walinitisha vikali, wakisema, “Kizuizini tutakushurutisha uchutame kando ya maji na uambue vitunguu saumu, na baada ya siku chache za kufanya hivyo, mikono yako yote itaoza!” Walikenua na kucheka kwa majivuno walipokuwa wakizungumza, na katika sura zao za kinyama, niliona uso muovu wa Shetani, katili na mkali!

Baada ya kuzuiliwa kwa mwezi mmoja kizuizini, polisi walidai kwamba ikiwa ningelipa yuani 20,000, ningeweza kwenda nyumbani. Nilisema sikuwa nazo, na kana kwamba ni kujadiliana, walisema 10,000 ingetosha pia. Niliposema kuwa sina senti zozote, kero lao lilibadilika kuwa hasira mara moja, na walisema kwa dhihaka, “Ikiwa huna pesa zozote, utapata kusomeshwa upya kupitia kazi! Utakapotoka, mume wako hata hatakutaka!” Nilisema kwa uthabiti “Sawa basi, sijali!” Na kwa hivyo, bila kufikiria, walinishtaki kwa kosa la “kuvuruga amani ya kijamii” na “kuzuia kutekelezwa kwa sheria” na kunihukumu mwaka mmoja wa kusomeshwa upya kupitia kazi. Hii ilinionyesha waziwazi zaidi kuwa serikali ya CCP ni ibilisi wa Shetani isiyojali maisha ya mwanadamu ambayo inafanya iwe adui wa Mungu! Katika jehanamu hii ya hapa duniani inayotawaliwa na pepo, ambapo Mungu huchukuliwa kama adui mkubwa chama kilichopo madarakani ni maandiko na sheria takatifu, na wale wanaoishi chini ya mamlaka yake hawana haki za kibinadamu au uhuru wowote, sembuse uhuru wa kidini! Wakati huo, sikuweza kujizuia lakini kukumbushwa maneno ya Mwenyezi Mungu, “Ni kutoa mawazo bila woga, bila kubania, kwa chuki inayovimbisha kifua chenu, kuondoa kabisa vijidudu hivyo, kuwafanya muache maisha haya ambayo hayana tofauti na maisha ya ng’ombe au farasi, ili msiwe watumwa tena, ili msiweze kukanyagwa tena au kuamrishwa na joka kuu jekundu; hamtakuwa tena wa taifa hili lililoanguka, hamtakuwa tena wa joka kuu jekundu lenye chuki, hamtafungwa nalo tena. Kiota cha pepo hakika kitachanwachanwa na Mungu, na mtasimama kando ya Mungu—nyinyi ni wa Mungu, na sio wa milki hii ya watumwa. Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga mwovu huyu, joka wa zamani mwenye chuki, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote; Mungu hatamhurumia hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote,[1] Atamharibu kabisa” (“Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Wakati huo, nilijawa na huzuni na hasira, kwa sababu niliona jinsi serikali ya China ilivyokuwa yenye kudhuru kwa siri, ya hila, na danganyifu. Inadai kufuata kauli mbiu kama vile “uhuru wa itikadi za kidini, kulinda haki halali na masilahi ya raia,” lakini kisirisiri, inavuruga kwa upotovu kazi ya Mungu, inawakamata, inawapiga, inawatoza faini, na kuwaua wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu wakati wowote itakapo, na pasipo na huruma huwalazimisha watu kumkataa Mungu, kumsaliti Mungu, na kujisalimisha kwa utawala wake muovu. Wanadamu waliumbwa na Mungu, na ni kawaidia na haki kumwamini Mungu na Kumwabudu, lakini serikali ya CCP inayopinga maendeleo inakwenda kinyume na mbingu na maumbile, ikijaribu kukinga ujio wa Mungu wa kweli. Inawatesa kinyama waumini katika Mungu, kwa kutumia vitisho, vishawishi, madai ya uwongo, kutesa ili kukubali, na mateso. Makosa yake ni ya kuchukiza, ya kutisha, na ya kinyongo! Ukatili na uovu wake ulinifanya niichukie, na niliazimia zaidi ya wakati mwingine wowote kufa kabla ya kuifuata, na imani na azimio langu la kumfuata Mwenyezi Mungu na kutembea kwenye njia sahihi maishani lilikuwa thabiti zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Mnamo Agosti mwaka wa 2010, niliachiliwa baada ya kukamilisha kifungo changu. Niliporudi nyumbani, niligundua kuwa wakati nilipokuwa nikitumikia kifungo changu, mume wangu pia alikuwa akichunguzwa na polisi kwa muda wa mwaka mmoja. Katika mwaka huo, jioni kungekuwepo na polisi mara kwa mara ambao walifuatilia matendo yake nyuma ya nyumba yetu, wakimdadisi, na kupeleleza nyumba, ikifanya iwe vigumu kwa mume wangu kurudi nyumbani au kuwa na mahali ambapo angeweza kujisikia salama. Wakati wa mchana, ilibidi afanye kazi nje, na usiku alilazimika kulala katika rundo la kuni karibu na nyumba yetu, ikimfanya asiweze kulala vizuri. Baada ya kuachiliwa, niligundua kuwa vibaraka hawa wa polisi pia walieneza uvumi kijijini kunihusu, wakamchochea kila mtu kijijini aniache, na wakamtuma mkurugenzi wa Wanawake wa Kijiji anichunguze. Pia waliniambia niandikishe taarifa ya kuahidi kwamba sitaondoka mjini. Walininyima uhuru wote wa kibinafsi. Baada ya kukaa nyumbani kwa muda wa mwezi mmoja, nililazimishwa tena na maafisa wa polisi 3–4 kwenda kwenye Brigedi ya Usalama wa Kitaifa kuhojiwa. Walinifunga tena kwenye kiti cha chuma na kujaribu kunilazimisha niwaambie habari kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu. Familia yangu ilipokuja kunitoa, walisema kwa kiburi, “Ikiwa mnataka aachiliwe, mnahitajika kulipa faini ya yuani 20,000, au mumshurutishe atueleze habari kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu. La sivyo, atahukumiwa kifungo cha miaka mitano ya kuelimishwa upya kupitia kazi!” Familia yangu haikuwa na kiasi hicho cha pesa, kwa hivyo ilibidi warudi nyumbani wakiwa na kero la kutojiweza. Nilielewa kwa undani kwamba pepo hawa walitaka tena kutumia kukamatwa kwangu kunilazimisha nimsaliti Mungu, kwa hivyo moyoni mwangu nilimwomba Mungu katika sala kwa haraka, “Mwenyezi Mungu, Shetani anatekeleza tena hila zake leo, akitarajia bila mafanikio kuwa atanilazimisha nikusaliti, lakini siwezi kumruhusu anidanganye. Bila kujali nitalazimika kufanya kazi kwa miaka mingapi, nitakuwa shahidi ili Nikuridhishe”. Nilipokuwa tu nikiapa moyoni mwangu kuwa shahidi bila kujali ningehitajika kuteseka kiasi gani, niliona kazi za miujiza ya Mungu: Polisi wabaya walipoona kwamba hawangepata lolote kutoka kwa mahojiano yao, waliniachilia jioni hiyo. Nilimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunifungulia njia, na kuniokoa tena kutoka katika mfumbato wa Shetani.

Katikati ya mateso ya kikatili ya serikali ya CCP, kamwe sikuweza kuthubutu kufikiria kuwa ningeibuka na maisha yangu. Bila mwongozo wa neno la Mwenyezi Mungu, bila utunzaji na ulinzi wa Mwenyezi Mungu, na bila nguvu isiyoisha niliyopewa na Mungu, maisha yangu dhaifu yangekuwa yameangamizwa na kumezwa wakati wowote na ibilisi hawa wa kinyama, na singeweza kamwe kusimama kidete mbele ya Shetani. Hili lilinifanya nielewe kwa kweli mamlaka na uwezo wa maneno ya Mwenyezi Mungu, liliniwezesha kuhisi kuvuka mpaka na ukuu wa nguvu ya maisha ya Mwenyezi Mungu, na liliniwezesha nipate upendo wa kweli wa Mungu na utoaji karimu wa maisha kwangu! Ni Mwenyezi Mungu aliyeniongoza mara kwa mara kushinda majaribu ya Shetani, kushinda woga wangu wa kifo, na kuibuka kutoka katika jehanamu hiyo ya dunia. Nilipitia kwa undani kwamba upendo wa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu ni wa kweli, kwamba Mwenyezi Mungu pekee ndiye niwezaye kumtegemea, na kwamba Yeye ndiye wokovu wangu wa pekee. Nimeapa kiapo kikubwa cha kumwacha na kumkataa Shetani, kufuatilia ukweli, na kumfuata Mwenyezi Mungu milele na kutembea katika njia ya furaha, njia inayofaa ya maisha!

Tanbihi:

1. “Kiongozi wa uovu wote” inahusu ibilisi mkongwe. Kirai hiki kinaonyesha kutopenda kabisa.

Iliyotangulia: 25. Kuzinduka Katikati ya Mateso na Dhiki

Inayofuata: 27. Majonzi Yalivutia Upendo Wangu kwa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

1. Upendo wa Mungu Ulikuwa Nami Katika Gereza la Giza la Ibilisi

Wakati huo, licha ya mimi kuteswa na kukandamizwa na ibilisi waovu, na kuwa ukingoni mwa kifo mara kadhaa, Mwenyezi Mungu alitumia mkono Wake wa nguvu kuniongoza na kunilinda, kunirudisha kwa uhai, na kunipeleka kwa usalama…. Kupitia hili, kwa kweli nilipitia uvukaji mipaka na ukuu wa nguvu ya uhai wa Mungu, na kupata utajiri wa thamani wa maisha niliyotunikiwa na Mungu.

8. Mateso na Majaribio—Baraka za Kufadhiliwa

Baada ya kuwa na uzoefu wa mwaka mmoja wa shida katika jela, naona kwamba mimi ni mdogo sana wa kimo na kwamba nakosa ukweli mwingi sana. Mwenyezi Mungu kwa kweli amefidia upungufu wangu kupitia mazingira haya ya kipekee na ameniruhusu kukua. Katika dhiki yangu, Amenifanya kupata utajiri wa thamani mno katika maisha na kuelewa ukweli mwingi ambao sikuufahamu katika siku za nyuma na kuona kwa dhahiri sura mbaya kwa Shetani, pepo, na kiini cha kupinga maendeleo cha upinzani wake kwa Mungu. Nilitambua uhalifu wake muovu wa kumtesa Mwenyezi Mungu na kuwaua Wakristo. Nilipitia kwa dhati wokovu na huruma kubwa Mwenyezi Mungu aliyokuwa nayo kwangu, mtu mpotovu, na nimehisi kwamba nguvu na maisha katika maneno ya Mwenyezi Mungu yanaweza kunipa mwanga na kuwa maisha yangu na kunielekeza kumshinda Shetani na kwa ushupavu kutoka nje ya bonde la uvuli wa mauti. Vivyo hivyo, pia niligundua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayeniongoza kwenye njia sahihi ya uzima. Ni njia ng’avu ya kupata ukweli na uzima!

2. Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe

Katika kipindi hicho cha mateso, maneno ya Mungu yalikuwa yameandamana na mimi kupitia mchana na usiku za kudhikisha, maneno ya Mungu yalikuwa yameniruhusu kubaini njama janja za Shetani na kutoa ulinzi wa wakati wa kufaa. Maneno ya Mungu yalikuwa yamenifanya kuwa mwenye nguvu na ujasiri, yakiniruhusu kushinda mateso yao katili mara kwa mara tena. Maneno ya Mungu yalikuwa yamenipa nguvu na imani, yalikuwa yamenipa ujasiri wa kupigana na Shetani hadi mwisho kabisa….

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki