30. Kupitia Dhiki, Upendo wa Mungu Uko Pamoja Nami

Na Li Ling, Jimbo la Henan

Jina langu ni Li Ling, na nilifikia umri wa miaka 76 mwaka huu. Nilipata imani katika Bwana Yesu mnamo mwaka wa 1978 baada ya kuugua, na katika kipindi hicho nilipokea neema Zake nyingi. Hii ilinitia msukumo wa kumfanyia Bwana kazi kwa shauku; nilikwenda mahali pote nikitoa mahubiri na kushiriki injili, na vile vile kuwakaribisha ndugu nyumbani kwangu. Kanisa letu lilikua kwa upesi sana na kuwa mkutano wa zaidi ya watu 2000, na kwa sababu hiyo, serikali ya Chama cha Kikomunisti cha China ilianza kutukandamiza muda mfupi baadaye. Polisi walikuja na kuipekua nyumba yangu mara kadhaa ili kujaribu kunizuia kuitenda imani yangu na kueneza injili, na kila walipokuja, wangechukua chochote cha thamani na kitu chochote kilichoweza kuchukuliwa—hata taa za globu. Zaidi ya hayo, nilikamatwa na maafisa wa Idara ya Usalama wa Umma (PSB) na kuzuiliwa mara nyingi. Nilikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho mnamo mwaka wa 1996, na miaka miwili baadaye nilipata kukamatwa na kuteswa tena na serikali ya CCP, lakini wakati huu kuliwa na wasiwasi zaidi. Nilipata uzoefu wa moja kwa moja wa jinsi ilivyokuwa vigumu sana mtu kumwamini Mungu katika nchi inayomkana Mungu kama China. Licha ya shida hizi zote, bado nilihisi wokovu na upendo wa Mungu kwangu.

Usiku wa manane siku moja mnamo Mei 1998, muda mfupi baada ya saa nane usiku, sauti ya mtu akiponda kwenye mlango wangu ilinishtusha kutoka katika usingizi mzito. Singeweza kujizuia kuwa na wasiwasi na nikawaza, “Labda ni polisi! Kuna ndugu watano hapa kutoka nje ya mji waliokuja kueneza injili. Nawezaje kuwalinda?” Nilijawa na hofu. Kabla hata ya kufika mlangoni, polisi waliupiga mlango teke ukafunguka kwa kishindo kikubwa. Mkuu wa Idara ya Usalama wa Kisiasa ya PSB, akiwa na bunduki mkononi, na maafisa wa polisi zaidi ya dazeni wenye virungu vya umeme wakaingia kwa kishindo. Punde tu alipovuka kizingiti afisa mmoja alinigeukia, akanipiga teke kikatili na kunipigia ukelele, “Ala! Umekamatwa mara nyingi sana, lakini bado una kiburi cha kumwamini Mungu! Zingatia maneno yangu, nitahakikisha kwamba utapoteza kila kitu ulicho nacho na familia yako kuangamizwa!” Maafisa wabaya walianza kusema kwa sauti kubwa katika vyumba vya kulala. “Polisi, amkeni sasa hivi!” Bila hata kusubiri ndugu wengine wavae mavazi yao, walitutia pingu kwa pamoja, wawili kwa wawili, wakatupekua, na pia wakachukua pete ambayo nilikuwa nimevalia. Kisha walianza kupekua mahali pote, hata kupekua ghala langu la unga na kumimina unga wote kwenye sakafu. Walirusha vitu tu kwenye sakafu nzima. Waliishia kuchukua vinasasauti kumi na moja, runinga moja, kipepeo kimoja, taipureta moja, na vitabu zaidi ya 200 vya maneno ya Mungu. Hata walifungua ili kudadisi vijikabati vya mwanangu na kuiba yuani zaidi ya elfu moja alizokuwa amepokea tu kama mshahara wake. Punde tu maafisa dazeni moja au takribani kiasi hicho walikuwa karibu kutupeleka sote kwenye kituo cha polisi, mwanangu alikuwa akirejea nyumbani kutoka kazini. Mara alipoona kwamba mshahara wake ulikuwa umeibwa alikimbia kwa maafisa na kuwaomba warumdishie pesa zake. Mmoja wa maafisa alisema kwa hila, “Tutaziangalia kwenye kituo, na ikiwa ni zako, tutakurudishia.” Lakini badala yake, jioni hiyo walikuja kumkamata mwanangu kwa ajili ya uhalifu wa “kuzuia shughuli rasmi.” Kwa bahati nzuri, alikuwa tayari ameenda mafichoni, vinginevyo angekamatwa vilevile.

Polisi walivipeleka vitabu na vitu vingine vilivyokuwa vimechukuliwa ngawira hadi kituoni, na kisha wakatuzuilia sisi sote sita tukiwa mmoja mmoja kwenye Idara ya Usalama wa Umma ya Kaunti usiku kucha. Nilipokuwa nimeketi hapo, sikuweza kupata kuwa na hali ya utulivu kwa muda mrefu. Nilikumbuka wakati nilipokamatwa mnamo mwaka wa 1987; nilidhulumiwa kimwili na kwa matusi na polisi na kuteswa hadi kuwa katika hali mahututi. Niliona pia kwa macho yangu mwenyewe mwanamume kijana aliyekuwa na umri wa miaka takribani 20 akipigwa na polisi hadi kufa kwa muda wa chini ya masaa mawili, na mwanamke mmoja alisema kuwa alikuwa amebakwa na maafisa wawili kwa zamu wakati wa kuhojiwa. Maafisa pia wangewaweka watu kwenye benchi za mateso, kuwachoma kwa nyundo ya kulehemia, na kutia umeme katika ndimi zao kwa kutumia virungu vya umeme hadi kufikia kiwango ambacho hapakuwepo na damu iliyosalia. Walitumia kila aina ya mbinu za kudharaulika, na za kikatili ili kuwatesa watu—ni kitendo kiovu mno cha ukatili. Kwa kukamatwa kwangu mara nyingi nilipitia mimi mwenyewe mateso haya ya kikatili na yasiyokuwa na huruma kutoka kwa upande wa polisi. Wanaweza kutenda ukatili wowote. Kuwa tena kwenye “lango hili la kuzimu” na kuwasikia polisi wakisema kwamba “nitateswa kinyama” kuliniacha nikiwa nimetishika sana. Walikuwa wamechukua vitu vingi sana nyumbani kwangu siku hiyo na pia walikuwa wamewakamata ndugu wengine kadhaa. Hawangeniruhusu kabisa niondoke kwa urahisi. Na kwa hivyo nilimwomba Mungu moyoni mwangu. “Ee Mungu! Najua kuwa tumeanguka mikononi mwa polisi leo kwa idhini Yako. Nahisi dhaifu sana kwa sababu wote ni pepo wanaokosa kabisa ubinadamu wowote, na kwa hivyo nakuomba Unipe ujasiri na hekima, na Unipe maneno yanayofaa ya kusema. Niko tayari kuwa shahidi Kwako—kwa hakika sitakuwa Yuda na kukusaliti! Natumai hata zaidi Uweze kuwalinda wale wengine ambao walikamatwa ili waweze kusimama kidete katika hali hii. Mungu, Wewe ndiye Mfalme wa ulimwengu wote, na matukio yote, vitu vyote viko chini ya utawala na mipango Yako. Naamini kwa dhati kwamba mradi niweze kukutegemea kwa kweli, hakika Utatuongoza kushinda ushawishi mwovu wa Shetani.” Mungu alinipa nuru nilipokuwa nikisali, Akanikumbusha maneno haya Yake: “Maisha ya kuzidi uwezo wa binadamu ya Kristo tayari imeonekana, hakuna kitu chochote unachopaswa kuhofia. Shetani yuko chini ya miguu yetu na muda wao ni mdogo. … Kuwa mwaminifu Kwangu zaidi ya yote, songa mbele kwa ujasiri; Mimi ni mwamba wako wa nguvu, Nitegemee Mimi!” (“Sura ya 10” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinijaza imani. Ni kweli—Mungu ni mwenye uweza na Shetani atashindwa daima mikononi mwa Mungu. Bila ruhusa ya Mungu hawezi kugusa hata unywele kichwani mwangu. Niliwaza kuhusu jinsi nilivyokuwa nimekamatwa mara nyingi na serikali ya CCP tangu kupata imani kwangu; si nilikuwa nimeshinda changamoto hizi mara kwa mara chini ya ulinzi wa Mungu? Niliwaza pia kuhusu nabii Danieli, jinsi yeye na marafiki zake watatu walivyosingiziwa na watu wabaya, kisha wakatupwa katika tundu la simba na kuchomwa katika tanuri ya moto, yote kwa sababu walilitetea jina la Yehova na kumwabudu Yehova Mungu. Hata hivyo, walikuwa na ulinzi wa Mungu na hawakudhuriwa. Nilipokuwa nikiwaza kuhusu haya yote, ghafla ujasiri ulijaa ndani yangu na nilihisi kujawa na nguvu. Nilijua kuwa bila kujali jinsi Shetani alivyonitesa au kuniumiza, Mungu akiwa mlinzi wangu hodari wa nyuma, sikuwa na lolote la kuogopa. Nilikuwa tayari kutegemea imani yangu na kushirikiana na Mungu, kuwa shahidi kwa Mungu mbele ya Shetani.

Polisi walianza kunihoji asubuhi iliyofuata. Afisa ambaye alikuwa amenihoji mara kadhaa hapo awali alinikodolea macho, akazaba sehemu ya juu ya meza na kufoka, “Kwa hivyo, ni wewe tena, jike zee. Umeanguka mikononi mwangu tena. Ikiwa hutafichua unachojua wakati huu utajiingiza kwenye shida kubwa! Zungumza! Wanatoka wapi wale watu wote ambao walikuwa wakiishi nyumbani kwako? Kiongozi wa kanisa ni nani? Vitabu hivyo vilitoka wapi? Taipureta ni ya nani?” Sikuweza kujizuia kuanza kuhisi woga; afisa huyo alikuwa mkatili mno, mwenye kutisha sana, na hangesita kumpiga mtu hadi afe. Niliinamisha kichwa changu kwa woga na kunyamaza, wakati wote nikimwomba Mungu kimya kimya aulinde moyo wangu. Alipoona kwamba sikuwa nikizungumza, afisa huyo alianza kunifokea matusi. “Wewe ajuza mzee, hakuna maana ya kumtishia nguruwe aliyekufa kwa maji moto!” Alinikimbilia huku akipiga ukelele na kunipiga teke la kuruka kwenye mfupa wa kidari. Niliruka nyuma mita kadhaa na kuanguka sakafuni kwa kishindo, nikatazama juu. Niliumia sana kiasi kwamba sikuweza kupumua. Huku asitake kuniacha, alinishambulia, akaniinua kutoka kwenye sakafu kwa mavazi yangu na akasema, “Wewe jike zee pumbavu! Sitakuruhusu ufe leo, lakini nitahakikisha kwamba maisha yako hayana maana kuyaishi. Utaishi maisha ya kuteseka!” Akisema hivyo, alinipitishia shoti ya umeme kwa kutumia kirungu chake cha umeme; nilipoona kikitoa mwanga wa samawati, nilihisi hofu sana. Nilimwomba Mungu kimya kimya tena na tena, na hapo ndipo nikakumbuka maneno Yake mengine: “Ni lazima uyavumilie yote, lazima uviachilie vitu vyote ulivyo navyo, na kufanya kila kitu unachoweza kunifuata Mimi, kulipa gharama zote kwa ajili Yangu. Huu ndio wakati Nitakujaribu, je, utatoa uaminifu wako Kwangu? Je utanifuata Mimi hadi mwisho wa barabara kwa uaminifu? Usiwe na hofu; kwa msaada Wangu, ni nani angeweza daima kuzuia barabara? Kumbuka hiki! Kumbuka! Kila kitu ambacho hutokea ni kwa kusudi Langu njema na yote yako chini ya uangalifu Wangu. Je, kila neno na tendo lako linaweza kufuata neno Langu? Wakati majaribio ya moto yatakuja juu yako, utapiga magoti na kuomba msaada? Au wewe utajikunyata, bila uwezo wa kusonga mbele?” (“Sura ya 10” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). Kupitia maneno ya Mungu, sikuhisi tu kuwa thabiti na aliyejasirishwa, lakini pia nilipata ufahamu wa mapenzi Yake. Jaribio nililokuwa nikipitia wakati huo huo lilikuwa wakati wa Mungu wa kunijaribu. Afisa huyo alikuwa akinitesa kimwili ili kujaribu kunifanya nimsaliti Mungu, lakini mapenzi ya Mungu yalikuwa nitoe ibada na upendo wangu Kwake. Alikuwa akiweka tumaini Lake juu yangu, na kwa hivyo sikuweza tu kushindwa na mwili na kuviabudu vikosi vya Shetani. Nilijua kwamba nilipaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu na kuwa na ushuhuda mkubwa Kwake. Afisa huyo alinipiga kwa nguvu kwa kirungu chake na wimbi baada ya wimbi la mkondo wa umeme lilipitia ndani yangu, likiulazimisha mwili wangu kushikamana na kukunjamana kwa umbo la mpira. Alipokuwa akinipitishia shoti ya umeme alinifokea, “Zungumza! Ikiwa hutazungumza nitakupitishia shoti ya umeme hadi ufe!” Nilikaza meno yangu na bado sikusema neno. Alipoona haya, alishindwa kujizuia kwa ajili ya ghadhabu. Wakati huo, nilichukia pepo huyo wazimu kwa moyo wangu wote. Mwanadamu aliumbwa na Mungu; kumwamini na kumwabudu bila shaka ni sawa na ni jambo lifaalo, lakini CCP kinampinga Mungu kabisa, kikiwatesa na kuwakandamiza waumini kikatili, bila hata kunihurumia, mwanamke mkongwe wa miaka 60. Hata walitaka kusababisha kifo changu! Kadiri walivyoniumiza zaidi ndivyo nilivyozidi kukaza meno yangu kwa chuki na niliapa moyoni mwangu: Hata nikifa, nitashuhudia kwa Mungu. Sitakuwa msaliti ambaye anaishi maisha ya aibu, na kuchochea dhihaka za Shetani. Afisa huyo alijichosha akinipiga na kunipigia kelele, kwa hivyo alipoona bado sikusema chochote, mmoja wa maafisa alijaribu kunibembeleza: “Tayari wewe ni mzee hivi—haya yote ni kwa ajili ya nini? Tuambie tu kile tunachotaka kukijua, ni nani aliyekupa vitu hivyo na watu hao wanaishi wapi kisha tutakupeleka nyumbani.” Mungu alinipa nuru ya kubaini udanganyifu huu wa Shetani, kwa hivyo bado sikusema chochote. Alipoona kwamba sikufungua kinywa changu aligeuka ghafla kuwa mkatili na kuanza kunitisha. “Sema ukweli na hutapata kifungo kibaya vile, la sivyo, utapata mateso makali zaidi. Usipozungumza utapata kifungo cha miaka 12 na utafungwa maisha yako yote!” Nilihisi mvumo kichwani mwangu nilipomsikia akisema ningefungwa kwa miaka 12 na nikawaza, “Niko katika hali duni ya mwili singeweza kustahimili mwaka mmoja, sembuse 12. Labda nitaishia kufia gerezani.” Wazo la kuishi siku zangu zote zilizosalia katika gereza lenye giza bila jua lilinifanya nihuzunike sana. Je, ningeweza kuvumilia bila maisha ya kanisa na riziki ya maneno ya Mungu? Huku nikihisi kutokuwa na matumaini, nilimwomba Mungu kimya kimya. Alinipa nuru mara moja, Akanikumbusha maneno haya kutoka Kwake: “Kwa kila kitu kinachotokea ulimwenguni, hakuna kitu Nisichokuwa na usemi wa mwisho kukihusu. Ni kitu gani kilichopo ambacho hakiko mikononi Mwangu?” (“Sura ya 1” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Ni kweli! Kudura za wanadamu zimo mikononi mwa Mungu, na matukio yote na vitu vyote viko chini ya sheria na mipango Yake. Bila kubagua, yale ambayo Mungu anasema ni sharti yatiiwe; Mungu asiporuhusu niende gerezani, polisi hawana ushawishi wowote kuhusu jambo hilo, lakini Akifanya hivyo, basi nitakubali kwenda gerezani bila malalamiko. Petro aliweza kutii hukumu ya Mungu na kuadibu Kwake, majaribio na taabu. Hakuwa na chaguo yeye mwenyewe, na alijisalimisha kwa Mungu na kutii mpangilio wa Mungu. Mwishowe alisulubishwa kichwa kikiangalia chini kwa ajili ya Mungu—alitii hadi kufa na kuwa mtangulizi wa upendo kwa Mungu. Nilijua kuwa nilihitaji kujifunza kutokana na mfano wa Petro siku hiyo na kujiweka mikononi mwa Mungu. Hata kama ningepata kifungo cha maisha, bado nililazimika kumtii Mungu. Polisi waliishia kunipeleka kwenye kituo cha uzuiliaji.

Katika kituo cha uzuiliaji, nilihisi kama nilikuwa jahannamu. Hakukuwa na dirisha kwenye seli, hakukuwa na taa za umeme, na zaidi ya watu 20 walikuwa wamesongamana ndani ya seli moja yenye ukubwa wa mita za mraba 10 tu. Tulilazimika kula, kunywa, na kwenda haja ndani ya seli. Kulikuwa na vidimbwi vidogo vya maji pande zote sakafuni na kulikuwa na mikeka kadhaa iliyovingirishwa, lakini hapakuwa na blanketi au shuka. Sisi sote tulilazimika kujinyoosha kwenye vidimbwi hivyo vya maji ili kulala. Kulikuwa na ndoo ya choo kwenye kona, na kulikuwa na mbu na nzi kila mahali. Uvundo ulikuwa mbaya sana hadi nikashindwa kupumua; kila mtu aling’ang’ania nafasi karibu na lango la chuma ili aweze kupata hewa kupitia kipenyo cha upana wa chini ya futi mmoja. Kulikuwepo na joto jingi kweli katika msimu wa joto na kulikuwa na watu wengi waliosongamana ndani ya seli hiyo ndogo, wafungwa wengi sana wangetembea uchi, bila kuvaa chochote. Mara nyingi vita vilizuka kati ya wafungwa juu ya mambo madogo madogo na kila wakati walikuwa wakitumia lugha chafu. Lishe yetu ya kila siku ilitengenezwa kwa supu ya unga ambayo haikuwa imeiva vya kutosha pamoja na tambi nyembamba, na mboga zilizochemshwa bila mafuta au chumvi yoyote. Wakati wote kulikuwa na uchafu uliaoachwa chini ya bakuli, na wafungwa wote waliugua ugonjwa wa kuendesha. Siku moja wakati wa kuitwa majina tulipokuwa nje kupata hewa safi, niliripoti namba ya mfungwa isiyo sahihi kwa bahati mbaya. afisa wa marekebisho alikasirika, akisema kwa sauti kuu, “Jitazame, makuruhi sana! Na unamwamini Mungu!” Kisha akachukua kiatu chake cha ngozi na kunipiga nacho usoni mara kumi, akiuacha uso wangu ukiwa umejawa na mavilio ya damu. Wafungwa wenzangu wote wa seli wakati huo walijipata taabani kwa sababu yangu, na wote walipigwa mara kumi. Nyuso zao zote zilijawa na mavilio ya damu, pia; walikuwa wakifunika nyuso zao na kulia kwa maumivu. Kuanzia wakati huo afisa wa marekebisho alinilazimisha nifue sare na mashati yao, pamoja na matandiko. Mmoja wa walinzi wakuu aliendesha hosteli nyumbani kwake na angeleta matandiko yote ambayo yalikuwa yametolewa ili niyaoshe, na mara yalipokuwa safi nililazimika kuyarekebisha yote kwa mkono. Nilikuwa mchovu sana mwisho wa kila siku hadi mwili wangu wote ulikuwa wenye uchungu na maumivu; kwa kweli nilihisi kama niliyekuwa nikishindwa kuvumilia. Katika siku chache tu mikono yangu ilivimba. Wakati mwingine wakati sikuweza kwa kweli kustahimili na nilipumzika kwa muda, afisa wa marekebisho alinikaripia kwa ukali, kwa hivyo sikuwa na chaguo ila kuendelea kufanya kazi, nikilia. Ilipofika wakati wa kupumzika usiku, hata ingawa nilikuwa na usingizi na uchovu wa mwili, bado sikuweza kulala vizuri. Mikono yangu ilikuwa na uchungu na maumivu na mgongo wangu uliumia sana hata sikuweza kuunyoosha. Miguu yangu pia ilikuwa imekufa ganzi. Hata hivi leo naweza tu kunyanyua mikono yangu juu digrii arobaini au hamsini—siwezi hata kuinyoosha kuwa wazi. Nilipata shida kubwa za njia ya utumbo kutokana na kufanya kazi ngumu sana bila kupata chakula cha kutosha, na kusababisha niendeshe mara kwa mara. Aidha, majeraha yaliyoachwa kutokana na kupigwa na wale maafisa wabaya wa polisi hayajawahi kupona kabisa. Afya yangu ilizidi kuzorota zaidi na zaidi. Baadaye nilianza kupata homa kidogo ya kudumu na walinzi wa gereza walikataa kuniruhusu nipate matibabu. Bila kujijali, nilidhoofika na kuwaza, “Katika umri huu mateso ya aina hii yakiendelea naweza kufa hapa siku yoyote sasa.” Hali ya ukiwa na kutojiweza ilijaa moyoni mwangu na kwa uchungu wangu nikamwomba Mungu. “Ee Mungu, mimi ni dhaifu mno hivi sasa na sijui mapenzi Yako ni yapi. Mungu, naomba Uniongoze ili niweze kuwa shahidi Kwako katika hali hii na kukuridhisha.” Nilimwita Mungu kutoka moyoni mwangu kila mara, na bila mimi kutambua, Mungu alinipa nuru, nikakumbuka wimbo wa maneno ya Mungu. Niliimba wimbo huu kimya kimya: “Mungu amefanyika kuwa mwili wakati huu kufanya kazi hii, kukamilisha kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kuifunga enzi hii, kuihukumu enzi hii, kuwaokoa waliozama kabisa dhambini kutoka katika ulimwengu wa bahari ya mateso na kuwabadilisha kabisa. Mungu amevumilia sana kulala bila kupata usingizi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi kupitisha siku Zake na mwanadamu, hajawahi kulalamikia uchakavu walionao wanadamu, hajawahi kumlaumu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha Yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na Aliingia mwenyewe ‘jahanamu’ na ‘kuzimu,’ katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu” (“Kila Hatua ya Kazi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Uzima wa Mwanadamu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Nilipokuwa nikiimba kimya kimya machozi yalitiririka usoni pangu mfululizo, na nikafikiria jinsi Mungu alivyo mkuu, na bado Amejinyenyekeza mara mbili ili kuwa mwili, Akivumilia mateso na fedheha isiyo na mwisho ili Awaokoe wanadamu. Sio tu kwamba amekabiliana na ukinzani na kuhukumiwa na wanadamu wapotovu, lakini pia Amepata ukandamizwaji na kuandamwa na CCP. Mungu hana hatia na kuteswa Kwake ni ili wanadamu waweze kuishi maisha mema na ya furaha katika siku zijazo. Maumivu na fedheha Aliyovumilia yamekuwa makubwa, lakini Hajawahi kunung’unika juu yake au kumlalamikia mtu yeyote. Uchungu ambao nilikuwa napitia wakati huo ulikuwa baraka ya Mungu iliyonijia, chanzo cha hayo yote ni mapenzi ya Mungu. Ilikuwa hivyo ili kwamba niweze kubaini kiini kiovu cha pepo hao na kisha kuasi dhidi ya Shetani, kuepukana na ushawishi muovu wa Shetani na kupata wokovu kamili. Hata hivyo, sikuwa nimeelewa nia njema ya Mungu, nikawa hasi na dhaifu baada ya mateso madogo tu. Nilipolinganisha hii na upendo wa Mungu, niliona kwamba nilikuwa mbinafsi na mwasi kupindukia. Na kwa hivyo niliweka azimio langu kuwa bila kujali hali ni ya kuleta huzuni au ngumu jinsi gani, ningemridhisha Mungu na singefanya tena lolote kumsononesha. Niliapa juu ya maisha yangu kuwa nitakuwa shahidi kwa Mungu. Mara nilipojitiisha, niliona matendo ya Mungu. Baada ya polisi kunifungia, Mungu alimwinua dada yangu, ambaye hakuwa muumini, kulipa polisi faini ya yuani 16,000 na yuani nyingine 1,000 kwa ajili ya chumba na malazi yangu, na nikaachiliwa.

Ijapokuwa nilipitia mateso ya mwili kwa muda wa miezi mitatu gerezani, nilikuwa nimeona tabia ya kweli ya kundi la pepo wa CCP na ukinzani wao kwa Mungu. Kufungwa mara nyingi na serikali ya CCP pia kulinipa ufahamu fulani halisi wa kazi ya Mungu, uweza na hekima Yake, na upendo Wake. Niliona kwamba Mungu ananilinda na kunitunza wakati wote, na Yeye kamwe haniachi, hata kwa muda mfupi. Nilipokuwa nikipitia mateso ya kila aina ya pepo hao na nilikuwa na maumivu makali, ni maneno ya Mungu ambayo yaliniongoza muda baada ya muda kushinda madhara na uharibifu wa Shetani, yakinipa imani na ujasiri wa kushinda ushawishi mbaya wa giza. Nilipokuwa dhaifu na asiyejiweza, yalikuwa ni maneno ya Mungu ambayo yalinipa nuru na kuniongoza mara moja, yakiwa kama nguzo ya kweli kwangu na kuandamana nami kupitia siku moja isiyovumilika baada ya nyingine. Kupitia ukandamizaji na shida kama hii kumeniruhusu nipate hazina ya maisha ambayo haiwezi kupatikana wakati wa amani na faraja. Kupitia uzoefu huu, azimio langu katika imani yangu limeimarika na bila kujali ni aina gani ya vitu vya ukatili nitakavyovikabili wakati ujao, nitafuatilia ukweli na nitafuatilia uzima. Nampa Mungu moyo wangu kwa sababu Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na Yeye ndiye Mwokozi wangu wa pekee.

Iliyotangulia: 29. Naja Kutofautisha Waziwazi kati ya Upendo na Chuki kwa Kupitia Uchungu wa Mateso

Inayofuata: 31. Ukingoni mwa Kifo, Mwenyezi Mungu Alikuja Kunisaidia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

24. Kuinuka Kupitia Ukandamizaji wa Giza

Maneno ya Mungu yalinipa kitu imara cha kutegemea! Kiliniruhusu kufurahia nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu wakati wa maumivu yangu ya kuzidi kiasi na udhaifu, ambayo ndiyo iliyokuwa njia ya pekee ambayo ningeweza kupita kipindi hiki cha giza na kilichorefuka kupita kiasi Ingawa nimepata uzoefu wa kukamatwa na kuteswa mara nyingi na serikali ya CCP, na mwili wangu umepitia ukatili usio na huruma na mateso, kwa kweli naelewa ukweli mwingi ambao sikuufahamu katika siku za nyuma na ninaona kwa dhahiri tabia ya kishetani ya uovu unaopinga maendeleo wa serikali China. Nimepata uzoefu pia wa upendo wa kweli wa Mwenyezi Mungu kwangu na nimeonja hekima inayoweza ya Mwenyezi Mungu na matendo ya ajabu. Huniamsha kutafuta kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu. Leo, bado ninatimiza wajibu wangu katika kanisa kama nilivyofanya zamani; mimi humfuata Mungu katika njia sahihi ya uzima, mimi hutafuta ukweli na hutafuta kuishi maisha ya maana.

1. Upendo wa Mungu Ulikuwa Nami Katika Gereza la Giza la Ibilisi

Wakati huo, licha ya mimi kuteswa na kukandamizwa na ibilisi waovu, na kuwa ukingoni mwa kifo mara kadhaa, Mwenyezi Mungu alitumia mkono Wake wa nguvu kuniongoza na kunilinda, kunirudisha kwa uhai, na kunipeleka kwa usalama…. Kupitia hili, kwa kweli nilipitia uvukaji mipaka na ukuu wa nguvu ya uhai wa Mungu, na kupata utajiri wa thamani wa maisha niliyotunikiwa na Mungu.

4. Kutoka kwa Mateso Kunatoka Harufu Nzuri ya Upendo

Katika uzoefu wangu wa vitendo, kwa kweli nimekuja kufahamu kwamba mamlaka na nguvu ya maneno ya Mungu ni kubwa sana, kwamba uhai ambao Mungu humpa mwanadamu ni usio na mwisho na kwamba unaweza kushinda nguvu zote ovu za Shetani! Katika mateso, nilitambua ulikuwa ni upendo wa Mungu ulionifariji na kunipa moyo, na uliniweka dhidi ya kupotea njia yangu. Bila kujali mahali ambapo naweza kuwa ama ni hali za aina gani ninazojipata kwazo, Mungu daima ananichunga, na upendo Wake daima uko nami.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki