Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Maneno Bora zaidi ya Mungu Kuhusu Injili ya Ufalme

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

`

Wale Wasiopatana na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Watu wote wana tamaa ya kuona uso wa kweli wa Yesu na kutaka kuwa pamoja Naye. Naamini kuwa hakuna mmoja wa ndugu au dada anayeweza kusema kwamba yeye hana nia ya kumwona au kuwa pamoja na Yesu. Kabla ya nyinyi kumwona Yesu, yaani, kabla ya nyinyi kumwona Mungu Aliye kwenye mwili, mtakuwa na mawazo mengi, kwa mfano, kuhusu sura ya Yesu, njia Yake ya kuzungumza, njia Yake ya maisha, na kadhalika. Hata hivyo, wakati mnamwona hasa, mawazo yenu yatabadilika haraka. Ni kwa nini? Je, mnataka kujua? Hata ingawa fikira za mwanadamu hakika haziwezi kupuuzwa, haikubaliki kamwe mwanadamu kubadilisha kiini cha Kristo. Nyinyi mnamchukua Kristo kama asiyekufa, mhenga, lakini hakuna yeyote anayemchukua Kristo kama binadamu wa nyama na mwili aliye na kiini kitakatifu. Kwa hivyo, wengi wa wale ambao wanatamani usiku na mchana kumwona Mungu ni hasa maadui wa Mungu na hawapatani na Mungu. Je, huu si uovu kwa upande wa mwanadamu? Hata sasa bado mnadhani kwamba imani yenu na uaminifu umewafanya mstahili kuona uso wa Kristo, lakini Mimi Nawasihi kujihami kwa mambo zaidi yaliyo na umuhimu! Kwa maana katika wakati uliopita, uliopo na ujao, wengi wa wale ambao hupatana na Kristo wameanguka; wao wote wamechukua jukumu la Mafarisayo. Sababu yenu ya kushindwa ni nini? Ni kwa sababu katika fikra zenu kuna Mungu mkubwa, Atamanikaye. Lakini ukweli si kama vile mwanadamu atakavyo. Kristo si Mkubwa wa umbo, bali Yeye ni mdogo hasa; Yeye si mtu tu, bali ni mtu wa kawaida; Hana uwezo wa kupaa mbinguni tu, bali hana pia uhuru wa kuzunguka ardhini Atakavyo. Na hivyo watu humchukulia kama mtu wa kawaida; wao kufanya wanavyopenda wanapokuwa pamoja Naye, na kusema maneno kiholela wakiwa Naye, wakati huu wote wakingojea kurudi kwa "Kristo wa kweli." Mnamchukua Kristo aliyekuja tayari kama mtu wa kawaida na neno Lake kama lile la mtu wa kawaida. Kwa hivyo, hamjapata chochote kutoka kwa Kristo na badala yake mmeonyesha ubaya wenu kwenye mwangaza.

Kabla ya kuwasiliana na Kristo, unaweza kuamini kwamba tabia zako zimeweza kubadilishwa kabisa, na unaweza kuamini kwamba wewe ni mfuasi mwaminifu wa Kristo, na pia uamini kwamba wewe unastahili kupokea baraka za Kristo. Kwa kuwa umesafiri njia nyingi, umefanya kazi nyingi, na kuleta matunda mengi, hivyo ni lazima uwe mtu anayepata taji mwishowe. Hata hivyo kuna ukweli ambao hauujui: nafsi fisadi na uasi na upinzani wa mwanadamu huonekana wazi mara tu anapomwona Kristo, na uasi na upinzani unaoonekana wakati huu ni hakika na kamilifu kuliko wakati mwingine wote. Ni kwa sababu Kristo ni Mwana wa Adamu na ana ubinadamu wa kawaida ndio maana mwanadamu hamwogopi wala kumheshimu. Ni kwa sababu Mungu anaishi katika mwili ndio maana uasi wa mwanadamu huletwa katika mwanga kikamilifu na kwa uwazi. Kwa hivyo Nasema kwamba kuja kwake Kristo kumechimbua uasi wote wa wanadamu na kutupa asili ya mwanadamu katika afueni ya ghafla. Hii ni "kumvuta chui kutoka mlimani" na "kumvuta mbwa mwitu kutoka pangoni." Je, unaweza kusema kwamba wewe ni mwaminifu kwa Mungu? Je, unaweza kusema kwamba wewe huonyesha utiifu kamili kwa Mungu? Je, unaweza kusema kwamba wewe si muasi? Wengine watasema: Kila wakati ambao Mungu anajenga mazingira yangu, mimi daima hutii na kamwe huwa silalamiki. Kwa kuongezea, siweki fikra zozote juu ya Mungu. Wengine watasema: Kazi zote nilizowekewa na Mungu, mimi hufanya kwa ukamilifu kadri ya uwezo wangu na kamwe sijachoka. Kisha Nawauliza hivi: Je, mnaweza kulingana na Kristo wakati mnaishi pamoja naye? Na ni kwa muda gani nyinyi mnaweza kulingana na yeye? Siku moja? Siku mbili? Saa moja? Masaa mawili? Imani yenu inafaa pongezi, lakini hamna uthabiti wa kutosha. Wakati unaishi na Kristo kwa kweli, ukweli wako na umuhimu wako utawekwa wazi kwa maneno na matendo yako, na hivyo ndivyo tamaa yako ya kupindukia na utovu wa nidhamu na kutoridhika kwako kutafichuka. Mwishowe, kiburi chako kitakuwa kikubwa zaidi, na wakati wewe utakuwa hulingani na Kristo kama maji na moto, basi asili yako itawekwa wazi kabisa. Wakati huo, fikra zako haziwezi kufichika tena. Malalamiko yako, pia, yataonekana kwa ghafla, na ubinadamu wako mbovu utakuwa wazi kabisa. Hata hivyo, unaendelea kuupinga uasi wako mwenyewe. Na unaamini kwamba Kristo kama huyu si rahisi kukubali na Yeye ni mwingi wa ukali kwa binadamu, na ungependa kumtii kikamilifu kwake kama yeye angekuwa tofauti, na Kristo mwenye huruma. Mnaamini kwamba kuna sababu ya uasi wenu, kwamba nyinyi mnamwasi tu wakati Kristo amewasukuma mpaka hatua fulani. Kamwe hamjawahi kufahamu kwamba hammchukui Kristo kama Mungu, wala hamna nia ya kumtii. Badala yake, wewe kwa ukaidi unasisitiza Kristo afanye kazi Yake kulingana na mawazo yako, na katika kazi zozote ambazo hazijafanyika vile, unaamini kwamba Yeye si Mungu bali ni mwanadamu. Je, si kuna wengi kati yenu ambao wameridhika na Yeye katika hali hii? Ni nani huyo mnayemwamini? Na jinsi gani mnaweza kumtafuta?

Kila mara mnatumaini kumwona Kristo, lakini Nawasihi msijiinue wenyewe hivyo; kila mtu anaweza kumwona Kristo, lakini Nasema hakuna ambaye ni wa kufaa wa kumwona Kristo. Kwa sababu asili ya binadamu imejazwa na uovu, kiburi, na uasi, unapomwona Kristo, asili yako itakuharibu na itakuhukumu hadi kufa. Uhusiano wako na ndugu (au dada) hauwezi kuonyesha mengi kukuhusu wewe, lakini si rahisi hivyo unaposhiriki na Kristo. Wakati wowote, dhana yako inaweza kujiimarisha, kiburi chako kichipuke, na uasi wako kuzaa matawi. Jinsi gani na utu kama huu unaweza kujiunga na Kristo? Je, kweli unaweza kumchukua kama Mungu kila wakati wa siku zote? Je utakuwa na hali halisi ya utiifu kwa Mungu? Mnamuabudu Mungu wa ukuu ndani ya mioyo yenu kama Yehova na bali mnamchukua Kristo anayeonekana kama mwanadamu. Hisia zenu ni duni mno na ubinadamu wenu ni wa hali ya chini! Hamwezi kumwangazia Kristo kama Mungu milele; badala yake, nyinyi tu humvuta kwenu na kumwabudu kama Mungu wakati imewapendeza hivyo. Hii ndiyo sababu Ninasema nyinyi si waumini wa Mungu, lakini washirika wa wale ambao wanampiga vita Kristo. Hata watu ambao huonyesha wema kwa wengine hulipwa, lakini Kristo, ambaye anafanya kazi ya namna hiyo kati yenu, hapendwi wala kulipwa na mtu, wala hapati utiifu kutoka kwa mwanadamu. Je, hili si ni jambo la kusikitisha?

Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kumfanyia tendo mbaya, lakini katika uhusiano wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kweli, au kutii neno la Kristo; basi Ninasema kwamba wewe ni mdanganyifu mkubwa na mtenda dhambi katika dunia. Kama wewe ni hasa mtu mwema na mwaminifu kwa jamaa yako, marafiki, mke (au mume), wanao, na wazazi, na kamwe hujanyanyasa wengine, lakini huwezi kulingana na kuwa na amani na Kristo, basi hata iwapo utatuma vitu vyako vyote kama misaada kwa jirani zako au umemlinda vizuri baba yako, mama, na kaya, bado Nasema kwamba wewe ni mwovu, na mwenye hila pia. Usifikiri kwamba wewe unalingana na Kristo ikiwa unalingana na mwanadamu au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unaamini kwamba wema wako unaweza kujinyakulia baraka za Mbinguni? Je, unafikiri kwamba matendo mema yanaweza kubadilishwa na utii wako? Hakuna hata mmoja yenu anaweza kukubali ushughulikiaji na upogoaji na kupogoa, na wote huwa vigumu kukubali ubinadamu wa kawaida wa Kristo. Hata hivyo siku zote mnadai utiifu kwa Mungu. Imani kama yenu italeta adhabu ya kufaa. Wacheni kujihusisha katika ndoto za raha na kutaka kumwona Kristo, kwa maana nyinyi ni wadogo sana katika kimo, kiasi kwamba nyinyi hata hamstahili kumwona. Wakati umeuwacha kabisa uasi wako na unaweza kuwa na amani pamoja na Kristo, basi Mungu Atakuonekania bila shaka. Iwapo utaenda kumwona Mungu kabla ya kupogolewa au kupitia hukumu, basi ni dhahiri kuwa utakuwa mpinzani wa Mungu na utakuwa katika njia ya kuangamizwa. Asili ya mwanadamu ni kuwa kawaida yeye yuko na uhasama kwa Mungu, kwa kuwa watu wote wamepotoshwa kabisa na shetani. Hakuna kizuri kinachoweza kuja kwa mtu mwenye mpotovu kujihusisha na Mungu. Vitendo vyote na maneno ya mwanadamu kwa hakika vitafichua upotovu wake; na wakati yeye anaingia katika ushirika na Mungu, uasi wake utaonekana katika nyanja zote. Binadamu kisha kwa kutojua anampinga Kristo, anamdanganya Kristo, na anamkataa Kristo; hapo ndipo mwanadamu huwa katika hali ya hatari zaidi. Ikiendelea hivyo, itambidi kupata adhabu.

Baadhi ya watu wanaweza kuamini kwamba kama kushirikiana na Mungu ni hatari, basi itakuwa busara kukaa mbali na Mungu. Ni nini, basi, watu wa namna hiyo wanaweza kupokea? Je, wanaweza kuwa waaminifu kwa Mungu? Hakika, kushirikiana na Mungu ni vigumu sana, lakini hiyo ni kwa sababu mwanadamu amepotoka na si kwa sababu Mungu hawezi kujiunga na mwanadamu. Ingekuwa bora kwenu kujishughulisha na juhudi zaidi za ukweli wa kuzijua nafsi zenu. Mbona hamjapata neema kwa Mungu? Kwa nini tabia zenu zina chukizo Kwake? Kwa nini maneno yenu ni ya chukizo Kwake? Nyinyi mnajisifu wenyewe kwa uaminifu wenu mdogo na mnataka malipo kwa ajili ya kujitoa kwenu kudogo; nyinyi huwadharau wengine wakati nyinyi mnaonyesha utiifu kidogo, na kuwa wa dharau kwa Mungu baada ya kufanya kazi ndogo ndogo. Mnataka utajiri na zawadi na pongezi kwa ajili ya kumpokea Mungu. Nyoyo zenu huumwa wakati mnatoa sarafu moja au mbili; wakati mnatoa kumi, mnataka kubarikiwa na kufanywa tofauti na wengine. Ubinadamu kama wenu kweli ni wa kukera kuzungumziwa au kusikizwa. Ni nini sifa ya maneno na matendo yenu? Wale ambao wanatekeleza wajibu wao na wale wasiofanya; wale ambao huongoza na wale hufuata; wale wanaompokea Mungu na wale wasiompokea; wale wanaotoa na wale wasiotoa; wale wanaohubiri na wale ambao hupokea neno, na kadhalika; watu wote hawa hujitakia sifa wenyewe. Je, hamuoni hili likiwa kichekesho? Hakika mnajua kwamba mnamwamini Mungu, lakini hamwezi kulingana na Mungu. Hakika mnajua kuwa nyinyi hustahili, lakini bado mnajigamba. Je, hamhisi kuwa hisia yenu imekuwa kama kwamba nyinyi hamwezi tena kujizuia? Jinsi gani mkiwa katika hali hiyo mnaweza kushirikiana na Mungu? Je, sasa nyinyi hamjionei hofu wenyewe? Tabia yenu tayari imekuwa kwamba hamwezi kulingana na Mungu. Imani yenu si ya upuuzi? Imani yenu si ya kipumbavu? Ni jinsi gani utaweza kushughulikia maisha yako ya baadaye? Ni jinsi gani utachagua njia ya kusafiria?

Iliyotangulia:Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Inayofuata:Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa

Unaweza Pia Kupenda