Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

`

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi”

1. Kwa kupotoshwa na Shetani, wanadamu hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya ushindi ni kuupata ushuhuda na utukufu na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi. Mwanadamu atashindwa vipi? Atapata kushindwa kwa kutumia hii kazi ya maneno kumshawishi mwanadamu kabisa; kwa kutumia toba, hukumu, kuadibu, na laana isiyo na huruma kumhini kabisa; na kwa kuweka wazi uasi wa mwanadamu na kwa kuhukumu upinzani wake ili ajue udhalimi wa mwanadamu na uchafu wake, mambo ambayo yatatumiwa kuangazia tabia ya haki ya Mungu. Kwa kiwango kikubwa, ni matumizi ya maneno haya yatakayomshinda mwanadamu na kumshawishi kabisa. Maneno ndiyo njia ya kumshinda mwanadamu na wote wanaokubali ushindi watakubali mapigo na hukumu ya maneno. Harakati ya sasa ya kunena ni harakati ya ushindi. Ni kwa njia gani watu watashirikiana? Ni kwa kushiriki haya maneno ipasavyo na kuyafahamu. Watu hawawezi kujipatia ushindi wao wenyewe. Ni lazima, kwa kushiriki haya matamshi, wapate kufahamu uovu na uchafu wao, uasi na udhalimu wao, na waanguke chini mbele ya Mungu. Ikiwa waweze kufahamu mapenzi ya Mungu kisha uyaweke katika vitendo, na zaidi, uwe na maono, na ikiwa waweza kuyasikia maneno haya kikamilifu na usitende kulingana na mapenzi yako, basi utakuwa umeshindwa. Na itakuwa ni haya maneno yamekuwezesha kushindwa. Je, ni kwa nini wanadamu walipoteza ushuhuda? Ni kwa sababu kamwe hakuna aliye na imani kwa Mungu au anamshikilia Mungu rohoni mwake. Kuwashinda wanadamu kunamaanisha watu wairudie hii imani. Mara zote watu wanauegemea ulimwengu, wakiwa na matumaini mengi sana, wakitaka mengi sana kwa ajili ya maisha yao ya usoni, na wakiwa na mahitaji badhirifu mengi. Mara zote wanaifikiria na kuipangia miili yao wala hawatamani kutafuta njia ya imani kwa Mungu. Roho zao zimetekwa na Shetani, wameacha kumheshimu Mungu, na wametoa mioyo yao kwa Shetani. Ila mwanadamu aliumbwa na Mungu. Hivyo, mwanadamu amepoteza ushuhuda, kwa maana kwamba amepoteza utukufu wa Mungu. Kusudi la kumshinda mwanadamu ni kuurejesha utukufu wa mwanadamu wa kumheshimu Mungu.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

2. Kazi ya sasa ya ushindi ni kazi inayokusudiwa kuweka wazi itakavyokuwa hatima ya mwanadamu. Ni kwa nini Ninasema kuwa kuadibu na hukumu ni hukumu mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe cha siku za mwisho? Hulioni hili? Ni kwa nini kazi ya ushindi ni hatua ya mwisho? Je, si kudhihirisha hatima ya kila tabaka la wanadamu? Si kuruhusu kila mtu, katika harakati ya kazi ya ushindi ya kuadibu na hukumu, kuonyesha tabia zake na kisha kuwekwa katika aina yake baadaye? Badala ya kusema kuwa huku ni kuwashinda wanadamu, ni sawa na kusema kuwa huku ni kuonyesha hatima ya kila aina ya mwanadamu. Yaani, huku ni kuhukumu dhambi zao halafu kuonyesha matabaka mbalimbali ya wanadamu, na kwa njia hiyo kubaini ikiwa ni waovu au ni wenye haki. Baada ya kazi ya ushindi, kazi ya kutuza mazuri na kuadhibu maovu inafuata: watu wanaotii kabisa, yaani walioshindwa kabisa, watawekwa katika hatua nyingine ya kusambaza kazi ulimwenguni kote; wasioshindwa watawekwa gizani na watapatwa na majanga. Kwa hivyo mwanadamu ataainishwa kulingana na aina yake, watenda maovu watawekwa pamoja na maovu, wasiuone mwangaza tena, na wenye haki watawekwa pamoja na mazuri, ili kupokea mwangaza na kuishi milele katika mwangaza. Mwisho wa vitu vyote u karibu, mwisho wa mwanadamu umebainishwa wazi machoni mwake, na kila kitu kitaainishwa kulingana na aina yake. Ni vipi basi wanadamu wataepuka kuathiriwa na kuanishwa huku? Kudhihirishwa kwa mwisho kwa kila jamii ya mwanadamu kutafanywa hatima ya kila kitu ikikaribia, na kutafanywa kipindi cha kazi ya ushindi wa ulimwengu mzima (ikiwemo kazi yote ya ushindi kuanzia kazi ya sasa). Kudhihirishwa huku kwa mwisho wa mwanadamu kunafanywa mbele ya kiti cha hukumu, katika harakati ya kuadibu na harakati ya kazi ya ushindi ya siku za mwisho.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

3. Hatima ya mwanadamu si kitu kilichoamuliwa kabla tangu uumbaji wa dunia. Hii ni kwa sababu mwanzoni kulikuwa na jamii moja tu ambayo kwa pamoja iliitwa” wanadamu,” na kwa sababu mwanadamu alikuwa bado hajapotoshwa na Shetani, na wanadamu wote waliishi katika mwangaza wa Mungu, bila giza kuwaandama. Lakini baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, kila jamii na aina ya watu walitapakaa ulimwenguni kote—kila jamii na aina ya watu waliotokana na ukoo mmoja ujulikanao kwa pamoja kama “wanadamu” uliojumuisha mwanamke na mwanamume. Wote walipotoshwa na mababu zao kutoka kwa nia za mababu zao wa awali—wanadamu waliojumuisha mwanamke na mwanamume (yaani, Adamu na Hawa asilia, mababu wa awali). Wakati huo, watu wa pekee duniani walioongozwa na Yehova walikuwa Waisraeli. Watu wa aina mbalimbali waliotokana na Israeli nzima (yaani kutoka ukoo asilia) wakati ule walipoteza uongozi wa Mungu. Watu hawa wa mwanzo, bila ufahamu wowote wa masuala ya ulimwengu wa wanadamu, walienda na mababu zao kuishi katika maeneo waliyodai kumiliki, mpaka wa leo. Kwa hivyo hawatambui walipotoka vipi kutoka kwa Yehova na jinsi wametiwa najisi mpaka leo na uchafu wa kila aina ya pepo wachafu na roho waovu. Waliopotoshwa zaidi na kutiwa sumu mpaka leo hii, yaani ambao hawawezi kukombolewa, hawatakuwa na njia nyingine ila tu kufuata mababu zao—pepo wachafu waliowapotosha. Wale wanaoweza kukombolewa watakwenda mahala stahili kwa mwanadamu, yaani sehemu iliyotengwa kwa ajili ya waliokombolewa na—walioshindwa. Kila kitu kitafanywa ili kukomboa wanaoweza kukombolewa, ila wale wasiosikia, wasioweza kutibika, chaguo lao pekee litakuwa kuwafuata mababu zao kwenye shimo la kuadibu lisilo na kikomo. Usidhani kuwa hatima yako iliamuliwa kabla tangu mwanzo na kudhihirishwa tu sasa. Ikiwa unadhani hivyo, je, umesahau kuwa katika uumbaji wa mwanadamu hakukuumbwa jamii tofauti ya Kishetani? Je, umesahau kuwa ni aina moja tu ya mwanadamu, yaani Adamu na Hawa, ndiyo iliumbwa (ikiwa na maana kwamba ni mwanamume na mwanamke tu ndio waliumbwa)? Ungalikuwa uzao wa Shetani kutoka mwanzo, je, hilo halingemaanisha kuwa Yehovah Alipomuumba mwanadamu Alijumuisha jamii ya Kishetani? Je, Angefanya jambo kama hilo? Alimuumba mwanadamu kwa ajili ya ushuhuda Wake; Alimuumba mwanadamu kwa ajili ya utukufu Wake. Angeumbaje kwa kukusudia jamii ya vizazi vya Shetani ili kumuasi kwa makusudi? Je, Yehova Angeweza kufanya hili? Ikiwa ndiyo, ni nani angeweza kumwita Mungu Mwenye haki? Nikisema sasa kuwa baadhi yenu mwishowe mtaenda na Shetani, haimaanishi kuwa mlikuwa na Shetani toka mwanzo; ila inamaanisha mmejishusha chini sana hivi kwamba japo Mungu Amejaribu kuwakomboa, bado mmekosa kuupata ukombozi. Hakuna lingine ila kuwaweka katika jamii moja na Shetani. Hii ni kwa sababu hamwezi kukombolewa, si kwamba Mungu si mwenye haki kwenu, yaani, Mungu Hajawaunganisha na Shetani na baadaye kuwaweka katika jamii moja na Shetani kutaka mteseke kwa makusudi. Huo si ukweli wa ndani wa kazi ya ushindi. Ikiwa unaamini hilo, basi ufahamu wako unaegemea upande mmoja!

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

4. Hatua ya mwisho ya ushindi ni ya kukomboa watu na vilevile kudhihirisha mwisho wa kila mtu. Inaweka wazi upotevu wa watu kupitia hukumu na kwa njia hiyo kuwafanya watubu, waamke, na kufuata uzima na njia ya haki ya maisha ya mwanadamu. Ni ya kuamsha mioyo ya waliolala na wapumbavu na kuonyesha, kwa hukumu, uasi wao wa ndani. Hata hivyo, ikiwa watu hawako tayari kutubu, hawako tayari kufuata njia ya haki ya maisha ya mwandamu na hawawezi kuutupa uozo wao, basi watakuwa vifaa visivyoweza kukombolewa vya kumezwa na Shetani. Hii ndiyo maana ya ushindi—kuwakomboa watu na vilevile kuwaonyesha mwisho wao. Mwisho mzuri, mwisho mbaya—yote inadhihirishwa na kazi ya ushindi. Ama watu watakombolewa au kulaaniwa yote yanadhihirishwa wakati wa kazi ya ushindi.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

5. Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia ushindi. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maana nyingine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. Vinginevyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, watu wa kila mataifa vilevile watapitia kazi ya ushindi. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake?

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

6. Sasa hivi Ninatumia kazi ya hawa watu walio Uchina kudhihirisha tabia zao zote za uasi na kuufunua ubaya wao wote. Huu ndio usuli wa kusema kila Ninachotaka kusema. Baadaye Nitafanya hatua nyingine ya kazi ya kushinda ulimwengu wote. Nitatumia hukumu Yangu kwenu kuhukumu udhalimu wa kila mtu duniani kote kwa sababu nyie watu ndio wawakilishi wa waasi miongoni mwa wanadamu. Wasiojikakamua watakuwa foili[a] na vyombo vya kuhudumu tu, ila watakaojikakamua watatumika vizuri. Ni kwa nini Ninasema watakuwa foili[a] ? Ni kwa sababu maneno na kazi Yangu ya sasa vinalenga usuli wenu na kwa sababu mmekuwa wawakilishi na kielelezo cha uasi miongoni mwa wanadamu. Baadaye Nitapeleka maneno haya yanayowashinda kwa nchi za kigeni na kuyatumia kuwashinda watu wa huko, ila hamtakuwa mmeyafaidi. Je, hilo halitawafanya foili[a] ? Tabia potovu za wanadamu wote, matendo ya uasi ya mwanadamu, maumbile na sura mbaya za mwanadamu, zimeratibiwa zote katika maneno yanayotumiwa kuwashinda nyinyi. Baadaye Nitayatumia kuwashinda watu wa kila taifa na kila dhehebu kwa sababu nyinyi ni mfano, kielelezo. Hata hivyo, Sikupanga kuwaacha kwa makusudi; mkikosa kufanya vizuri katika utafutaji wenu na kwa hivyo kuthibitisha kuwa hamsadiki, hamtakuwa tu chombo cha kuhudumu na foili[a] ?

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

7. Leo hii ni imani inayokuruhusu kushindwa, na kushindwa ndiko kunakufanya uamini kila tendo la Yehova. Ni kwa sababu tu ya imani unapokea kuadibu na hukumu ya aina hii. Kupitia kuadibu na hukumu hizi, umeshindwa na kukamilishwa. Bila aina hii ya kuadibu na hukumu upokeayo leo hii, imani yako ingekuwa bure. Kwa sababu humtambui Mungu, haijalishi unamwamini kiasi gani, imani yako itakuwa maonyesho matupu yasiyokuwa na misingi katika uhalisia. Ni baada ya kupokea aina hii ya kazi ya ushindi inayokufanya mtiifu kabisa ndipo imani yako inakuwa kweli na inayotegemewa, na roho yako kumrudia Mungu. Japo umehukumiwa na kulaaniwa sana kwa sababu ya hili neno “imani,” una imani ya kweli, na unapokea kitu cha kweli zaidi, halisi zaidi, na chenye thamani zaidi. Hii ni kwa sababu ni katika harakati ya hukumu tu ndipo unaona mahala pa mwisho pa viumbe wa Mungu; ni katika hukumu ndio unapata kuona kuwa Muumba Anapaswa kupendwa; ni katika kazi kama hiyo ya ushindi ndio unapata kuona mkono wa Mungu; ni katika ushindi huu unapata kutambua kikamilifu maisha ya mwanadamu; ni katika ushindi huu unapata kujua njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na kufahamu maana ya kweli ya “mwanadamu”; ni kupitia tu huu ushindi ndipo unaweza kuona tabia ya haki ya mwenye Uweza na uso Wake mzuri na mtukufu. Ni katika kazi hii ya ushindi ndipo unaweza kujifunza kuhusu asili ya mwanadamu na kufahamu “historia isiyokufa” ya mwanadamu; ni katika ushindi huu ndipo unapata kufahamu mababu za wanadamu na asili ya uovu wa mwanadmu; ni katika ushindi huu unapokea furaha na starehe pamoja na kurudi, nidhamu na maneno ya kuonya kutoka kwa Muumba kwa mwanadamu ambaye Alimuumba; katika kazi hii ya ushindi, ndipo unapokea baraka na majanga ambayo mwanadamu anapaswa kupokea… je, haya yote si kwa ajili ya hiyo imani yako ndogo? Je, baada ya kuvipata vitu hivi vyote imani yako haijakua? Hujapata kiwango kikubwa ajabu?

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

8. Labda utasema kuwa usingekuwa na imani, basi usingepata aina hii ya kuadibu au aina hii ya hukumu. Ila unapaswa kufahamu kuwa bila imani, si tu kwamba usingeweza kupokea aina hii ya kuadibu na ulinzi kutoka kwa mwenye Uweza, bali pia daima ungepoteza fursa ya kumwona Muumba. Usingejua asili ya mwanadamu na kufahamu umuhimu wa maisha ya mwanadamu. Japo mwili wako utakufa na roho yako kuondoka, bado hutayafahamu matendo yote ya Muumba. Aidha hutafahamu kuwa Muumba Alifanya kazi kubwa kiasi hicho duniani baada ya kumuumba mwanadamu. Kama mmojawapo wa hawa wanadamu Aliowaumba, je, uko tayari kutumbukia gizani kiasi hiki bila fahamu na kukumbana na adhabu ya milele? Ukijitenga na kuadibu na hukumu ya sasa, utapatana na kitu gani? Je, unafikiri ukishajitenga na hukumu ya sasa, utaweza kuepukana na haya maisha magumu? Je, si kweli kwamba ukiondoka “mahala hapa,” utakachokipata ni mateso machungu au majeraha kutoka kwa ibilisi? Je, waweza kukumbana na usiku na siku zisizostahimilika? Je, unafikiri kwamba kwa kuepuka hukumu sasa, unaweza kukwepa yale mateso ya siku zijazo? Ni kitu gani kitakukumba? Inaweza kuwa paradiso ya duniani unayoitarajia? Unafikiri unaweza kuepuka kuadibu kwa milele kwa baadaye kwa kuukimbia uhalisia kama ufanyavyo? Baada ya sasa, je, utaweza kuipata fursa na baraka kama hii tena? Je, utapata fursa na baraka utakapokuwa umekumbwa na misukosuko? Je, utapata fursa na baraka wanadamu wote waingiapo katika pumziko? Maisha yako ya furaha kwa sasa na hiyo familia yako ndogo yenye amani—vyaweza kuwa kibadala cha hatima yako? Iwapo una imani ya kweli, na unafaidi pakubwa kwa sababu ya imani yako, basi hayo yote ndiyo—wewe kiumbe—utafaidi, vilevile ndiyo ya pekee utakuwa nayo mwishoni. Aina hii ya ushindi ndiyo ya faida zaidi kwa imani na maisha yako.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

12. Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya ushindi kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Jinsi ambavyo mwenendo wa mtu ama mwili wake unavyobadilika haiamui ikiwa ameshindwa. Badala yake, ni wakati ambapo fikira zako, utambuzi wako, ufahamu wako unabadilika—yaani, ni wakati mielekeo yako ya kifikira inabadilika—ndipo huwa umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

13. Katika uwanja wa dini, watu wengi huteseka pakubwa maishani mwao mwote, kwa kuihini miili yao au kuubeba msalaba wao, au hata kuteseka na kustahimili hadi pumzi zao za mwisho! Wengine huwa wanafunga hadi siku ya kifo chao. Katika maisha yao yote wanajinyima chakula kizuri na mavazi mazuri, wakisistiza mateso tu. Wanaweza kuihini miili yao na kuinyima miili yao. Uwezo wao wa kustahimili mateso ni wa hali ya juu. Ila fikira zao, mawazo yao, mielekeo yao ya kiakili, na kwa hakika asili yao—hakuna kati yavyo kilichoshughulikiwa hata kidogo. Hawajifahamu. Picha ya Mungu akilini mwao ni ya kijadi na ya kidhahania, Mungu asiye yakini. Uamuzi wao wa kuteseka kwa ajili ya Mungu unaletwa na azma na asili yao chanya. Hata ikiwa wanamwamini Mungu, hawamfahamu Mungu wala kuyafahamu mapenzi Yake. Wanamfanyia Mungu kazi na kumtesekea Mungu kama vipofu. Hawawekei ung’amuzi thamani yoyote, na hawajishughulishi na jinsi ambayo huduma yao inatekeleza mapenzi ya Mungu. Aidha, hawajui jinsi ya kumpata na kumfahamu Mungu. Mungu wanayemhudumia si Mungu katika sura Yake asilia, ila ni Mungu waliyejifikiria, Mungu waliyemsikia, au Mungu wa kihadithi wanayemsoma katika maandiko. Hatimaye wanatumia mawazo yao na mioyo yao ya kiungu kumtesekea Mungu na kuifanya kazi ambayo Mungu Anapaswa kufanya. Huduma yao haiko sahihi, kiasi kwamba hakuna anayemtolea Mungu huduma kwa njia inayotekeleza mapenzi Yake. Haijalishi wako radhi kiasi gani kuteseka, mitazamo yao asilia ya huduma na picha ya Mungu akilini mwao havibadiliki kwani hawajapitia hukumu ya Mungu na kuadibu na usafishaji Wake na ukamilifu, na kwa sababu hakuna yeyote aliyewaongoza na ukweli. Japo wanasadiki kwa Yesu Mwokozi, hamna kati yao aliyewahi kumwona Mwokozi. Wamemsikia tu kwa hadithi na uvumi. Hivyo huduma yao ni sawa na kuhudumu mara mojamoja macho yao yakiwa yamefungwa kama kipofu akimhudumia baba yake. Ni nini kinaweza kupatikana kutokana na huduma kama hiyo? Na ni nani anaweza kuikubali? Huduma yao haibadiliki kamwe toka mwanzo hadi mwisho. Wanapokea mafunzo ya kibinadamu na kukita huduma yao katika uasilia wao na kile wanachokipenda wao. Hili laweza kuzalisha faida gani? Hata Petro, aliyemwona Yesu, hakujua jinsi ya kumhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi ya Mungu. Ni katika uzee wake ndipo alipopata ufahamu. Hili linaonyesha nini kuhusu mwanadamu kipofu ambaye hajapitia ushughulikiaji na hana upogoaji na ambaye hajawahi kupata yeyote wa kumwongoza? Je, huduma yako kubwa sasa si kama ile ya vipofu? Wale wote ambao hawajapokea hukumu, hawajapokea upogoaji na ushughulikiaji, na hawana mabadiliko—je, wao si waliokosa kushindwa kikamilifu? Wana manufaa gani watu kama hao? Ikiwa fikira zako, ufahamu wako wa maisha, na ufahamu wako wa Mungu hauonyeshi mabadiliko mapya na hautoi faida hata kidogo, hutatekeleza chochote kizuri katika huduma yako. Bila maono na bila ufahamu mpya wa kazi ya Mungu, huwezi kuwa mtu aliyeshindwa. Njia yako ya kumfuata Mungu itakuwa kama ile ya wale wanaoteseka na kufunga—itakuwa ya thamani ndogo! Hii ni kwa sababu kuna ushuhuda kidogo katika yale wayafanyayo ndipo Nasema huduma yao ni bure! Maisha yao yote, hao watu huteseka, hukaa gerezani kwa muda, na kwa kila wakati, hustahimili, husisitiza mapenzi na ukarimu, na kubeba msalaba wao. Wanatukanwa na kukataliwa na ulimwengu na hupitia kila ugumu. Wanatii hadi mwisho ila bado hawapati ushindi na hawawezi kutoa ushuhuda wa kutwaliwa. Wameteseka si haba, ila kwa ndani hawamfahamu Mungu kabisa. Hakuna fikira zao za zamani, mawazo ya zamani, vitendo vyao, uelewa wa wanadamu, na mawazo ya wanadamu yaliyoshughulikiwa. Kamwe hakuna uelewa mpya ndani yao. Hakuna hata chembe ya ufahamu wao wa Mungu ambao ni wa kweli au ni sahihi. Wamekosa kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Je, huku kwaweza kuwa kumhudumia Mungu? Japo ulimfahamu Mungu zamani, tuseme umeudumisha ufahamu huo hadi leo na kuendelea kukita ufahamu wako juu ya Mungu kwenye fikira na mawazo yako bila kujali Mungu Anafanya nini. Yaani, ikiwa huna ufahamu mpya na wa kweli kuhusu Mungu na ukose kutambua sura na tabia ya kweli ya Mungu. Ikiwa ufahamu wako wa Mungu bado unaongozwa na fikira za uhasama na ushirikina na bado una mawazo na fikira za mwanadamu. Ikiwa hii ndiyo hali, basi hujashindwa. Lengo langu la kukwambia sasa maneno haya yote ni kukupa fursa ya kufahamu na kutumia utambuzi huu kukuongoza katika ufahamu sahihi na mpya. Aidha yanalengwa kukwondolea mawazo ya zamani na utambuzi wa zamani ulio nao ili uweze kuwa na ufahamu mpya. Ikiwa unakula na kunywa matamshi Yangu kwa ukweli, basi ufahamu wako utabadilika kwa kiwango kikubwa. Bora tu udumishe moyo mtiifu kwa kula na kunywa matamshi ya Mungu, mtazamo wako utabadilika. Bora tu unaweza kukubali kuadibu kwa kila mara, fikira zako za zamani zitabadilika taratibu. Bora tu fikira zako za zamani zimebadilishwa kabisa na kuwa mapya, vitendo vyako vitabadilika ipasavyo. Kwa njia hii, huduma yako itaendelea kuwa yenye malengo zaidi, na itaweza kutekeleza mapenzi ya Mungu. Ukibadilisha maisha yako, ufahamu wako wa maisha, na mawazo yako mengi kuhusu Mungu, basi uasilia wako utadidimia taratibu. Hili, na hakuna jingine ila hili, ndilo tokeo baada ya Mungu kumshinda mwanadamu; haya ndiyo mabadiliko yatakayoonekana ndani ya mwanadamu. Ikiwa katika kumwamini Mungu, yote ujuayo ni kuutiisha na kuuhini mwili wako na kustahimili na kuteseka, na hujui wazi ikiwa unachokifanya ni sawa au la, bila kujali unamfanyia nani kazi, basi vitendo kama hivi vitaletaje mabadiliko?

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

14. Unapaswa kufahamu kuwa Ninachokitarajia kutoka kwako si kwamba mwili wako uwekwe katika kifungo au ubongo wako utawaliwe na kuzuiliwa kufikiria mawazo dhahania. Hili si lengo la kazi wala kazi inayopaswa kufanywa hivi sasa. …Unatakiwa kufahamu kazi ya Mungu na ugundue asili yako, uwezo wako, na yale maisha yako ya zamani. Hususani unapaswa kufikiria kuhusu vile vitendo vyako vyenye makosa vya zamani na mienendo yako ya kibinadamu. Ili Kubadilika, unapaswa kuanza kwa kubadilisha fikira zako. Kwanza, badilisha fikira zako za zamani kwa fikira mpya, na uruhusu fikira zako mpya ziongoze maneno na matendo yako na maisha yako. Hili ndilo ombi kwa kila mtu sasa hivi. Usitende kama kipofu au kufuata kama kipofu. Ni sharti uwe na msingi na lengo. Usijidanganye. Unapaswa ujue kabisa imani yako kwa Mungu ni kwa ajili ya nini, ina faida gani, na kitu gani unachopaswa kuingia kwacho sasa hivi. Ni muhimu kwamba uyafahamu haya yote.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

15. Ufahamu wako wa matendo ya Mungu unapobadilika, unapokuwa na ufahamu mpya wa ukweli wa kila Anachokisema Mungu, na ufahamu wako wa ndani unapoinuliwa, maisha yako yanabadilika na kuwa bora. Kila kitu kinachofanywa na kusemwa na mwanadamu sasa ni cha utendaji. Haya si mafundisho ya kidini, ila kile ambacho watu wanahitaji kwa ajili ya maisha yao na kile wanachopaswa kumiliki. Hili ndilo badiliko linalotokea kwa mwanadamu wakati wa kazi ya ushindi, badiliko ambalo mwanadamu anapaswa kupitia, na ndiyo matokeo baada ya mwanadamu kushindwa. Ukibadilisha fikira zako, kuchukua mwelekeo mpya wa kimawazo, kubadilisha mawazo yako na nia zako na mantiki yako ya zamani, kuacha haya yaliyokita mizizi ndani yako, na kupata ufahamu mpya wa imani kwa Mungu, basi, shuhuda unazozitoa zitainuliwa na uwepo wako mzima, kwa kweli utakuwa umebadilika. Yote haya ndiyo ya kiutendaji zaidi, halisi zaidi, na vitu vya kimsingi kabisa—vitu vilivyokuwa vigumu kwa mwanadamu kushika hapo zamani na vitu ambavyo wasingeweza kukumbana navyo. Ndizo kazi ya kweli ya Roho.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

16. Katika hitimisho la kazi yote ya ushindi, ni muhimu kwamba nyinyi nyote mfahamu kwamba Mungu si Mungu wa Israeli tu, ila ni Mungu wa kila kiumbe. Aliumba wanadamu wote wala si Waisraeli tu. Ukisema kuwa Mungu ni Mungu wa Israeli tu au kwamba haiwezekani Mungu kupata mwili katika taifa lolote lililo nje ya Israeli, basi bado hujafikia ufahamu wowote katika harakati za kazi ya ushindi na hutambui kamwe kwamba Mungu ni Mungu wako. Kile unachokitambua ni kuwa Mungu Alitoka Israeli Akaenda Uchina na Analazimishwa kuwa Mungu wako. Iwapo huu ndio mtazamo wako wa vitu, basi kazi Yangu haijazaa matunda ndani yako na hujaelewa chochote Nilichokisema. Hatimaye, ikiwa utaandika ukoo Wangu, sawa na Mathayo, Nitafutie “babu” afaaye na Nitafutie mizizi sahihi—yaani kwamba Mungu ana koo mbili kwa sababu ya kupata Kwake mwili mara mbili—je, huo hautakuwa mzaha mkubwa zaidi duniani? Wewe “mtu mwenye nia njema” uliyenipatia ukoo, je, huwezi kuwa mtu uliyemgawa Mungu? Je, uko tayari kuubeba mzigo huu wa dhambi? Baada ya hii kazi yote ya ushindi, ikiwa huamini kwamba Mungu ni Mungu wa viumbe wote, ikiwa bado unadhani kwamba Mungu ni Mungu wa Waisraeli tu, je, wewe si mtu anayemkana Mungu waziwazi? Kusudi la kukushinda leo ni kukufanya utambue kuwa Mungu ni Mungu wako, na Mungu wa wengine, na muhimu zaidi ni Mungu wa wote wanaompenda, na Mungu wa viumbe wote. Ni Mungu wa Israeli na Mungu wa Misiri. Ni Mungu wa Waingereza na Mungu wa Wamarekani. Si Mungu wa Adamu na Hawa tu, bali pia Mungu wa kizazi cha Adamu na Hawa. Ni Mungu wa kila Kitu mbinguni na duniani.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

17. Familia ya Waisraeli na familia zote za Mataifa zimo mikononi mwa Mungu. Hakufanya kazi katika nchi ya Israeli pekee kwa miaka elfu kadhaa na kuzaliwa Uyahudi, ila leo Anashuka Uchina, nchi hii ambapo joka kuu jekundu limejikunja. Ikiwa kuzaliwa Uyahudi kunamfanya Mfalme wa Wayahudi, basi si kushuka kwake miongoni mwenu leo kunamfanya Mungu wenu? Aliwaongoza Waisraeli na alizaliwa Uyahudi na vilevile amezaliwa katika nchi ya Mataifa. Je, kazi Yake yote si ya wanadamu wote Aliowaumba? Je, Anawapenda Waisraeli mara mia moja na kuwachukia Mataifa mara elfu moja? Je, hayo siyo mawazo yako? Ni wewe ambaye humtambui Mungu; si kwamba Mungu Hakuwa Mungu wako. Ni wewe unayemkataa Mungu; si kwamba Mungu hapendi kuwa Mungu wako. Ni nani kati ya walioumbwa hayuko mikononi mwa mwenye Uweza? Kwa kukushinda leo, je, lengo lake si la kukufanya utambue kuwa Mungu ni Mungu wako? Iwapo bado unashikilia kuwa Mungu ni Mungu wa Waisraeli tu, na kuendelea kushikilia kuwa nyumba ya Daudi huko Israeli ni asili ya uzao wa Mungu na kuwa hakuna taifa tofauti na Israeli limewezeshwa “kuzalisha” Mungu, na hata zaidi kuwa hakuna familia ya Mataifa yenye uwezo wa kupokea kazi ya Yehova—ikiwa bado unafikiria namna hii, je, haikufanyi kuwa mshikiliaji wa ukaidi? Usikazie macho Israeli kila wakati. Mungu Yuko hapa miongoni mwenu leo. Vilevile msitazamie mbingu tu. Acheni kutamani Mungu wenu Aliye mbinguni! Mungu Ametua miongoni mwenu, basi Anawezaje kuwa mbinguni? Hamjaamini katika Mungu kwa muda mrefu, ilhali mna mawazo mengi kuhusu Mungu, kiasi kwamba mnathubutu kutofikiri hata kwa sekunde moja kuwa Mungu wa Israeli Anaweza ‘kuwatunukia’ na uwepo wake. Wala huthubutu kufikiri jinsi unavyoweza kumwona Mungu Akijitokeza binafsi, ikitiliwa maanani jinsi ulivyo mchafu. Aidha hujawahi kufikiri jinsi Mungu Anavyoweza kushuka miongoni mwa Mataifa. Anapaswa kushuka juu ya Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni na kuonekana kwa Waisraeli. Je, si watu wa Mataifa (yaani watu wa nje ya Israeli) ndio walengwa wa chuki Yake? Anawezaje kufanya kazi miongoni mwao? Haya yote ni mawazo yaliyokita mizizi ndani yenu ambayo mmeyakuza kwa miaka mingi. Kusudi la kukushinda leo ni kuyaharibu haya mawazo yenu. Kwa njia hiyo mmeweza kumwona Mungu Akijionyesha Mwenyewe miongoni mwenu—si katika Mlima Sinai au Mlima wa Mizeituni, bali miongoni mwa watu ambao Hajawahi kuwaongoza hapo awali.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

18. Baada ya Mungu kufanyia hatua mbili za kazi Yake Israeli, Waisraeli na watu wa Mataifa walishikilia wazo hili: Japo ni kweli Mungu Aliumba viumbe wote, yuko radhi kuwa Mungu wa Waisraeli tu, si Mungu wa Mataifa. Waisraeli wanaamini yafuatayo: Mungu Anaweza tu kuwa Mungu wetu, sio Mungu wenyu Mataifa, na kwa sababu hamheshimu sana Yehova, Yehova—Mungu wetu—Anawachukia. Zaidi, Wayahudi hao huamini hili: Bwana Yesu Alichukua sura yetu Wayahudi na ni Mungu Aliye na alama ya Wayahudi. Mungu Anafanyia kazi miongoni mwetu. Sura ya Mungu na sura zetu zinafanana; sura zetu na sura ya Mungu zinakaribiana. Bwana Yesu ni Mfalme wetu Wayahudi; watu wa Mataifa hawajawezeshwa kupokea wokovu mkubwa kiasi hicho. Bwana Yesu ni sadaka ya dhambi kwetu Wayahudi. Ni kwa misingi ya hatua hizi mbili za kazi ndipo Waisraeli na Wayahudi walijijengea haya mawazo mengi. Wanamdai Mungu kuwa wao tu, bila kuruhusu kwamba Mungu vilevile ni Mungu wa Mataifa. Kwa njia hii, Mungu Alikuwa pengo katika mioyo ya watu wa Mataifa. Hii ni kwa sababu kila mtu aliamini kuwa Mungu Hataki kuwa Mungu wa watu wa Mataifa na kuwa Anawapenda tu Waisraeli—Wateule wake—na Anawapenda Wayahudi hasa wafuasi waliomfuata. Je, wajua kuwa kazi Aliyoifanya Yehova na Yesu ilikuwa ni kwa ajili ya uzima wa wanadamu wote? Je, sasa mnatambua kuwa Mungu ni wa wale wote waliozaliwa nje ya Israeli? Je, Mungu Hayumo miongoni mwenu leo? Hii haiwezi kuwa ndoto, ama vipi? Je, huukubali uhalisia huu? Unathubutu kutoamini au kulifikiria. Licha ya jinsi unavyolitazama, je, Mungu Hayumo miongoni mwenu? Je, bado waogopa kuyaamini maneno haya? Kuanzia leo, je, wote walioshindwa, na wale wote wanaotaka kuwa wafuasi wa Mungu, si wateule wa Mungu? Je, nyote mlio wafuasi leo, si wateule nje ya Israeli? Je, nafasi yenu si sawa na ya Waisraeli? Je, hili silo mnalopaswa kutambua? Je, hili si lengo la kazi ya kukushinda? Kwa kuwa mwaweza kumwona Mungu, basi Atakuwa Mungu wenu milele, tangu mwanzo hadi siku za baadaye. Hatawaacha, mradi tu nyinyi nyote mko radhi Kumfuata na kuwa viumbe Wake waaminifu na watiifu.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

19. Kukamilishwa kuna maana gani? kushindwa kuna maana gani? Ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili apate kushindwa? Na ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili afanywe mkamilifu? Kushinda na kukamilisha yote yanakusudiwa kumfanyia kazi mwanadamu ili aweze kurudi katika asilia yake na awe huru na tabia zake potovu za Kishetani na ushawishi wa Kishetani. Huu ushindi huja mapema katika mchakato wa kumfanyia kazi mwanadamu, ikiwa na maana kwamba ni hatua ya kwanza ya kazi. Kukamilisha ni hatua ya pili, au hitimisho la kazi. Kila mwanadamu ni lazima apitie hali ya kushindwa; la sivyo hataweza kumfahamu Mungu na hawezi kujua kuwa kuna Mungu, yaani, hawezi kumtambua Mungu. Na iwapo mtu hamtambui Mungu, hataweza kufanywa mkamilifu na Mungu kwa sababu hatakuwa na vigezo vya kufanywa mkamilifu. Ikiwa humtambui Mungu, utawezaje kumfahamu? Utawezaje kumtafuta? Aidha, hutaweza kumshuhudia, wala kumtosheleza. Kwa hivyo, kila anayetaka kukamilishwa, hatua ya kwanza ni kushindwa. Hili ndilo sharti la kwanza. Ila, iwe ni kushinda au ukamilifu, kila moja ni lengo la mwanadamu afanyaye kazi na kubadilishwa na kazi hiyo, na kila moja ni kipengele katika kazi ya kusimamia mwanadamu. Hizi hatua mbili ndizo zinahitajika kumgeuza yeyote kuwa mtu mkamilifu; hakuna moja kati yazo inaweza kurukwa. Ni kweli kuwa “kushindwa” hakuonekani kuwa ni jambo zuri, ila ni kweli kuwa mchakato wa kumshinda mtu ni mchakato wa kumbadilisha mwanadamu. Baada ya kushindwa, unaweza kuwa hujapoteza tabia yako mbovu kabisa, ila utakuwa umeijua. Kupitia kazi ya ushindi, utapata kujua uduni wa uanadamu wako, na vilevile kufahamu utovu wako wa nidhamu. Japo hutaweza kuyaacha haya au kuyabadilisha ndani ya muda mfupi wa kazi ya ushindi, utayajua baadaye. Haya yanaujenga msingi wa ukamilifu wako. Kwa hivyo kushinda na kukamilisha yote yanafanywa kumbadilisha mwanadamu, kumtoa mwanadamu tabia zake mbovu za Kishetani ili ajitolee kikamilifu kwa Mungu. Ni kwamba tu kushindwa ni hatua ya kwanza katika kubadilisha tabia ya mwanadamu na pia hatua ya kwanza ya mwanadamu kujitoa kikamilifu kwa Mungu, hatua iliyo chini ya ukamilifu. Tabia za maisha ya mtu aliyeshindwa hubadilika kiasi kidogo kuliko ya mtu ambaye amepata ukamilifu. Kushindwa na kufanywa mkamilifu ni tofauti kabisa kwa kuwa ni hatua tofauti za kazi na kwa kuwa huhitaji vigezo tofauti kutoka kwa wanadamu, huku ushindi ukiwa na vigezo vya chini na ukamilifu ukiwa na vigezo vya juu. Walio wakamilifu ni wenye haki, watu watakatifu na safi; ni udhihirisho wa kazi ya kusimamia wanadamu, au matokeo ya mwisho. Japo si wanadamu wasio na doa, ni watu wanaotaka kuishi maishi ya thamani. Na walioshindwa je? Hukiri tu kwa vinywa vyao kuwa Mungu Yupo; wanakiri kuwa Mungu Amepata mwili, kwamba neno linaonekana katika mwili, na kwamba Mungu Amekuja duniani kufanya kazi ya hukumu na kuadibu watu. Aidha wanakiri kuwa hukumu na kuadibu kwa Mungu na mapigo Yake na usafishaji Wake ni faida kwa mwanadamu. Yaani, wameanza kuwa na sifa za uanadamu, na wana ufahamu mdogo kuhusu maisha ila si bayana. Kwa maana nyingine, wameanza tu kuwa na uanadamu. Haya ni matokeo ya kushindwa. Watu waingiapo katika njia ya ukamilifu, tabia zao za zamani zaweza kubadilishwa. Aidha, maisha yao huendelea kukua na taratibu hujitosa zaidi katika ukweli. Wanaweza kuchukia dunia na kuwachukia wale ambao hawapendi ukweli. Hususani hujichukia wao wenyewe, na hata zaidi ya hayo, wanajitambua vyema. Wana hiyari kuishi katika ukweli na hulenga kutafuta ukweli. Hawako radhi kuishi katika mawazo ya bongo zao, na huchukia kujitukuza, kujisifu na kujiinua kwa mwanadamu. Wananena kwa adabu ya hali ya juu, wanafanya mambo kwa utambuzi, ni wenye busara na watiifu kwa Mungu. Wakipata kuadibu na hukumu, hawaoni unyonge, bali hutoa shukrani. Hawawezi kuishi bila kuadibu na hukumu ya Mungu; wanaweza kupata ulinzi wake kupitia kuadibu na hukumu Yake. Hawafuati imani ya utulivu na furaha ya kutafuta mkate wa kuwashibisha. Wala hawafuati raha za kupita za kimwili. Hili ndilo wakamilifu huwa nalo.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

20. Unasema kwamba unatambua Mungu mwenye mwili na unatambua kuwa Neno linaonekana katika mwili, na bado unafanya mambo fulani kinyume, na hutendi jinsi Anataka utende, na humwogopi. Je, huku ni kumtambua Mungu? Unatambua Anachokisema ila unakataa kuyaweka katika vitendo hata yale mambo unayoweza kufanya na huzifuati njia zake. Je, huku ni kumtambua? Unamtambua ila mawazo yako ni kujikinga dhidi Yake, humheshimu. Ikiwa umeona na kuitambua kazi Yake na unafahamu kuwa Yeye ni Mungu, na bado unaendelea kuwa vuguvugu na bado hujabadilika hata kidogo, basi bado hujapata ushindi.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

21. Mtu aliyeshindwa hufanya chochote awezacho; anataka kuingia na kuufikia ukweli wa juu hata kama bado hana uwezo. Ni kwamba tu ana mipaka katika yale anayoweza kufanya, yaani, vitendo vyake vimefungiwa na kuwekewa mipaka. Lakini angalau anapaswa kufanya chochote katika uwezo wake. Ukifanya haya mambo, itakuwa ni kwa sababu ya kazi ya ushindi. Hata ukisema, “Kwa sababu Anaweza kunena maneno mengi ambayo mwanadamu hawezi, ikiwa si Mungu, ni nani?” Kuwa na mawazo kama haya hakumaanishi unamtambua Mungu. Ikiwa unamtambua Mungu unapaswa kuthibitisha kwa matendo. Ukiongoza kanisa lakini usiweze kutenda haki, na kutamani pesa na kufuja pesa za kanisa kisiri kwa faida yako—je, huku ni kutambua kuwa kuna Mungu? Mungu ni mwenye Uweza na wa kumcha. Unawezaje kukosa kuogopa kama kweli unatambua kuwa kuna Mungu? Unawezaje kuwa ulifanya kitu cha kuchukiza namna hiyo? Je, huko kunaweza kuitwa kuamini? Je, kweli wamtambua Mungu? Je, unamwamini Mungu? Unayemwamini ni Mungu asiye yakini; ndiyo maana huogopi! Wale wote wanaomtambua Mungu kikweli na kumfahamu wanamcha na wanaogopa kufanya chochote kinachompinga na chochote kinachoenda kinyume na dhamiri yao; hususani wanaogopa kufanya chochote kinachoenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Hili tu ndilo laweza kuwa ni kumtambua Mungu. Utafanya nini wazazi wako wakikuzuia kumwamini Mungu? Utampenda vipi Mungu ikiwa mume wako asiyekuwa muumini anakutendea mema? Aidha utampendaje Mungu ikiwa ndugu na dada zako wanakuchukia? Ikiwa unamtambua, basi utatenda ipasavyo na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi katika hali hizi zote. Ukikosa kutenda wazi na kusema tu kwamba unatambua uwepo wa Mungu, basi wewe ni msemaji tu. Unasema unamwamini na kumtambua. Je, unamtambua kwa njia gani? Unamwamini kwa njia gani? Je, unamwogopa? Unamheshimu? Unampenda moyoni mwako? Unapokuwa na huzuni bila yeyote wa kuelekea, unahisi Mungu ni wa kupendwa, halafu baadaye unasahau. Huku si kumpenda au kumwamini Mungu! Je, Mungu Anataka mwanadamu apate nini mwishoni? Hali zote Nilizozitaja, kama vile: kufikiri kuwa wewe ni mtu mkubwa, kwamba unaelewa mambo upesi, kuwadhibiti wengine, kuwadharau wengine, kuwahukumu watu kwa misingi ya sura zao, kuwadhulumu watu waaminifu, kutamani pesa za kanisa, na kadhalika—kuondokewa na sehemu ya tabia mbovu za kishetani kama hizo ndiko kunatakiwa kuonekana ndani yako baada ya wewe kushindwa.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

22. Kazi ya ushindi inayofanywa kwenu nyie ni ya umuhimu mkubwa sana. Kwa upande mmoja, kusudi la hii kazi ni kukikamilisha kikundi cha watu, yaani, kuwakamilisha na kuwa kundi la washindi, kama kundi la kwanza la watu waliofanywa wakamilifu, yaani matunda ya kwanza. Kwa upande wa pili, ni kuruhusu viumbe wa Mungu kufurahia mapenzi ya Mungu, kupokea wokovu mkubwa wa Mungu, na kupokea wokovu kamili wa Mungu, na kumfanya mwanadamu kufurahia si tu huruma na ukarimu wa upendo, ila muhimu zaidi ni kuadibu na hukumu. Tangu uumbaji wa dunia hadi sasa, Mungu katika kazi Yake Amekuwa na mapenzi, bila chuki yoyote kwa mwanadamu. Hata kuadibu na hukumu uliyoiona ni mapenzi pia, mapenzi ya kweli na ya dhati, mapenzi yanayomwongoza mwanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya mwanadamu. Kwa upande wa tatu, ni kushuhudia mbele ya Shetani. Kwa upande wa nne, ni kuweka msingi wa kueneza kazi ya baadaye ya injili. Kazi yote Aliyoifanya ni kumwongoza mwanadamu kwenye njia sahihi ya maisha ya wanadamu, ili kwamba wawe na maisha ya kawaida ya wanadamu, kwani mwanadamu hajui jinsi ya kuishi. Bila uongozi kama huo, utaishi maisha tupu yasiyo na maana wala thamani, na kamwe hutajua jinsi ya kuwa mwanadamu wa kawaida. Huu ndio umuhimu mkuu wa kumshinda mwanadamu.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

23. Nyinyi nyote mnaishi katika mahala pa dhambi na ufisadi; nyinyi nyote ni watu wafisadi na wenye dhambi. Leo hii hamwezi tu kumwona Mungu, ila la muhimu zaidi, mmepokea kuadibu na hukumu, mmepokea wokovu wa kina, yaani, mmepokea upendo mkubwa zaidi wa Mungu. Yote Ayafanyayo ni mapenzi ya dhati kwako; Hana nia mbaya. Anakuhukumu kwa sababu ya dhambi zako, ili kwamba uweze kujichunguza mwenyewe na upokee wokovu mkubwa. Haya yote hufanywa kufinyanga mwanadamu . Tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu Amekuwa Akifanya kila Awezalo kumwokoa mwanadamu, na hakika hayuko tayari kuwaangamiza kabisa wanadamu Aliowaumba kwa mikono Yake Mwenyewe. Sasa Amekuja miongoni mwenu kufanya kazi; je, huu si wokovu zaidi? Je, Angaliwachukia, Angaliendelea kufanya kazi ya kiwango hicho cha juu ili kuwaongoza Yeye Mwenyewe? Ni kwa nini Ateseke hivyo? Mungu hawachukii wala hana nia mbaya juu yenu. Mnapaswa kufahamu kuwa mapenzi ya Mungu ndiyo mapenzi ya kweli zaidi. Anawaokoa kupitia hukumu kwa sababu tu ya uasi wa mwanadamu; la sivyo, hawangepata wokovu. Kwa kuwa hamjui jinsi ya kuishi, na mnaishi katika mahala pa ufisadi na dhambi na ni mapepo wenye ufisadi na uchafu, Hana moyo wa kuwaacha mpotoshwe zaidi; wala Hana moyo wa kutaka kuwaona mkiishi mahala pachafu kama hapa, mkikandamizwa na Shetani apendavyo, Hana moyo wa kuwaacha mtumbukie Kuzimu. Anataka tu kulipata hili kundi lenu na kuwakomboa vilivyo. Hili ndilo kusudi kuu la kufanya kazi ya Ushindi miongoni mwenu—ni kwa ajili ya wokovu tu.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

24. Iwapo hamwezi kuona kuwa kila kitu mnachofanyiwa ni mapenzi na wokovu, mkidhani kuwa ni mbinu tu, njia ya kumtesa mwanadamu na kitu kisichoaminika, basi ni bora mrudi duniani mwenu mwendelee kupata mateso na ugumu wa maisha! Ikiwa mko tayari kuwa kwenye mkondo huu na kufurahia hukumu hii na wokovu huu wa ajabu, na kufurahia baraka hizi ambazo haziwezi kupatikana kokote katika ulimwengu wa wanadamu, na kufurahia mapenzi yake, basi bakieni kuwa wanyenyekevu kwenye mkondo huu kukubali kazi ya ushindi ili uweze kufanywa mkamilifu. Japokuwa kwa sasa mnapitia mateso na usafishaji kwa sababu ya hukumu, mateso haya ni ya thamani na ya maana. Japo kuadibu na hukumu ni usafishaji na ufichuzi usio na huruma kwa mwanadamu, uliokusudiwa kuadhibu dhambi zake na kuadhibu mwili wake, kazi hii haijanuiwa kukashifu na kuuzima mwili wake. Ufichuzi mkali wa neno ni kwa kusudi la kukuongoza kwenye njia sahihi. Wewe mwenyewe umeipitia sana kazi hii na, ni wazi, haijakuongoza kwenye njia mbaya. Yote ni kukuwezesha kuishi kulingana na na ubinadamu wa kawaida, yote ni kitu ambacho kinaweza kutimizwa na ubinadamu wa kawaida. Kila hatua ya kazi hufanywa kwa misingi ya mahitaji yenu, kulingana na udhaifu wenu, kulingana na kimo chenu, na hamjatwikwa mzigo usioweza kubebeka. Japo huwezi kuliona hili wazi kwa sasa, na unajihisi Ninakuwa mgumu kwako, japo unadhani kuwa Ninakuadibu na kukuhukumu na kukuadibu kila siku kwa kuwa Ninakuchukia, na ingawa unachokipokea ni kuadibu na hukumu, hali halisi ni kuwa yote ni mapenzi kwako, pia ni ulinzi mkubwa kwako. Ikiwa huwezi kung’amua maana ya ndani ya kazi hii, basi huna njia ya kuendelea katika uzoefu wako. Unapaswa kuliwazwa kwa sababu ya huo wokovu. Usikatae kuzirudia busara zako. Baada ya kusafiri umbali huu, unapaswa kuuona wazi umuhimu wa kazi hii ya Ushindi. Hupaswi tena kuyumba mbele na nyuma katika fikira zako.

kutoka “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kivilinganisha.

Iliyotangulia:Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno La Mungu Kuhusu “Fumbo La Kupata Mwili”

Inayofuata:Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili

Unaweza Pia Kupenda