Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kurudi kwa Mwana Mpotevu

13

Wang Xin Mjini Harbin

Katika mwaka wa 1999, nilikuwa kiongozi kutokana na mahitaji ya kazi ya kanisa. Ingawa nilijisikia sana kwamba sikustahili hiyo kazi wakati kwanza nilipoanza, baada ya muda, kutokana na asili yangu ya kiburi na ya kujidai, tahadhari yangu ya awali polepole ilibadilika na kuwa ya kujiinua mwenyewe na kushuhudia kujihusu. Nilijali kuhusu chakula, nguo, na raha, kwa ulafi nikijiingiza katika baraka za hadhi yangu. Mimi hata nilitaka kuwa sawa na Mungu. Hatimaye, mwishowe nilifukuzwa na kutumwa nyumbani. Ilikuwa tu ni baada ya hili nilipopata mwamko na kutambua kwamba “hadhi” ilikuwa imenifanya kukata tamaa juu ya Mungu na ukweli; “hadhi” ilikuwa imenifanya kuanzisha ufalme wangu binafsi; “hadhi” ilikuwa imenigeuza kuwa mpinga Kristo; “hadhi” ilinifanya nishike njia ya kifo. Ilikuwa ni hapo tu nilipogundua kwamba nilikuwa nimepotea mbali sana na njia sahihi na tayari nilikuwa nimeanguka katika kina kirefu sana.

Nikiangalia nyuma, hali yangu ya kuanguka ilianza wakati kazi yangu ya injili ilipoanza kuonyesha matokeo fulani. Wakati huo, nilifikiria kuwa nilikuwa kitu muhimu na nikaanza kuzungumza katika hali ya kujinata na kuridhika na mimi mwenyewe, na mara nyingi nilizungumza na sauti kwa watu ndani ya upeo wa kazi yangu. Baadaye, dada mmoja niliyekuwa nimeunganishwa naye akadakiza juu ya upungufu wangu, akisema kuwa mimi nilionyesha aina ya tabia ya kiburi na uwenda wazimu nilipozungumza. Niliikubali tu juu juu, lakini siyo moyoni mwangu. Mwishowe, bado nilifikiria njia za aina zote za kukanusha kwa njia isiyo dhahiri upungufu alioudakiza. Katika siku baada ya haya, nilianza kuzungumza kwa ajili ya hadhi yangu, bila kuhisi kamwe wasiwasi moyoni mwangu kwa kushindwa kumtosheleza Mungu. Badala yake, mara nyingi nilihisi kuvunjika moyo kwa sababu watu wengine hawakuridhishwa nami. Hatua kwa hatua, roho yangu ilikufa ganzi na kukosa hisia. Wakati tu nilikuwa bado sijajua kabisa kwamba nilikuwa nikifuata njia mbovu, kiongozi fulani alinipa barua. Ilisema: “Fulani, kwa vile sasa umekuwa kizito, hata toni ya sauti yako imebadilika. Wewe ni sawa sana na viongozi wa serikali kote duniani. Utaondolewa hivi karibuni.” Nini? Hii haimaanishi kuwa nitapoteza maisha yangu ya baadaye na kudura? Baada ya kusoma maneno haya, nikawa na maumivu makali yenye uchungu, lakini sikuchunguza asili yangu au kutambua vyema kutoka kwayo huduma ya Mungu na mawazo Yake, na zaidi ya hayo sikuelewa matokeo ya kuendelea jinsi hii. Kisha, ugonjwa mkubwa ulinikumba ghafla. Katika hali hii na mazingira, nilihisi kwamba nilikuwa nimeshuka kabisa katika hali ya kufa moyo. Fikira zangu zilikuwa katika mvurugiko na nilikuwa na hofu ya kupoteza wajibu wangu. Nilikuwa pia na hofu ya kuondolewa na kutokuwa na siku za baadaye, na vile vile kufukuzwa na kutumwa nyumbani. Nilikuwa nimejawa na maombi ya kufedhehesha kwa Mungu. Ingawa nilitambua kuwa nilijali sana juu ya hadhi, nilikuwa chini ya udhibiti wa Shetani kabisa na singeweza kujinasua mwenyewe. Kwa kweli nilitumia uwezo wangu kama kiongozi kuwadhibiti ndugu wa kiume na kike kufanya mambo ya kibinafsi kwa ajili yangu, nikiwafanya kunisaidia kupata daktari ili nipate kutafuta njia ya kuondokwa na ugonjwa wangu haraka. Moyo wangu ulitawaliwa na wazo moja: sipaswi kupoteza hadhi yangu na sipaswi kupoteza wajibu wangu. Nilianza kufurahia heshima maalum, nikala virutubishi vyema vya afya, na pia nikapokea chakula kizuri kutoka kwa ndugu wa kiume na kike bila swali. Hata hivyo, nilifikiria kwa ujinga: Sifanyi hili kwa ajili ya kufurahia; ninafanya hivi kuponya ugonjwa wangu ili usicheleweshe kazi yangu, na kwa hiyo halijumuishwi kama lililozidi. Mwishowe, sikukosa kupona tu lakini ugonjwa wangu ukawa mbaya hata zaidi.

Baadaye, kulingana na hali yangu, viongozi wakaniruhusu nirudi nyumbani ili kutafakari mwenyewe, wakisema kuwa ugonjwa wangu ni suala la akili.

Niliposikia habari kwamba walikuwa wananiacha nirudi nyumbani ili nitafakari mwenyewe, nilihisi kama nilikuwa nimepigwa na radi. Miguu yangu ilikuwa dhaifu sana sikuweza kusimama, na karibu hata sikuwa na nguvu za kutosha kupumua. Nilidhani: Yamefika kikomo. Si miaka hii yote ya kufuatilia imekuwa bure? Ni matarajio gani ambayo bado ninayo? Nitaendelea kuishije katika siku zijazo?

Baada ya kurudi nyumbani, nilikuwa nimechanganyikiwa mchana kutwa. Matarajio yangu ya zamani na ahadi zote zilikuwa zimetoweka. Niliangalia umri wangu mwenyewe na kisha jinsi familia yangu ilikuwa imebadilika kwa kipindi cha miaka: Ndugu zangu wote waliolewa na kuoa, wakati nilikuwa mtu wa kipekee asiyehitajika na ambaye watu hawangemwelewa. Wakati huo, nilihisi nimekuwa mwenye ukiwa na nisiyejiweza kwa kiwango fulani, na hivyo niliishi kila siku na malalamiko, masikitiko, na lawama, bila chembe ya faraja. Ingawa wakati mwingine ningekumbuka juu ya utamu wa kazi ya Roho Mtakatifu na nyakati za furaha za kupitia kazi ya Mungu, nilivyozidi kufikiri juu yake ndivyo nilivyozidi kuteseka na kujuta. Halafu ningelia kwa sauti kubwa, nikijiuliza: Je, barabara yangu ya kuamini katika Mungu itafikia mwisho hivi? Nitakufa tu nikihisi uchungu jinsi hii? Siwezi! Nilikuwa na maumivu mengi kiasi kwamba kwa kweli nilipendelea kifo kuliko kuishi. Nilipiga magoti na kulia, nikimwita kwa sauti kubwa na kumwomba Mungu: “Ewe Mungu! Kila dakika baada ya kukuondokea Wewe imekuwa haivumiliki kabisa. Sasa ninaelewa kwa undani kwamba kile ninachohitaji ni Wewe, na siyo vitu vya mwili kama chakula, mavazi, hadhi, na raha …. Mambo haya yataniletea tu maumivu na kuadibiwa, kuteseka fikira, mashtaka dhidi ya dhamiri yangu, shutuma na wasiwasi. Ewe Mungu! Ninajichukia na kujidharau kwa sababu ya kutothamini fursa ya kufanywa mkamilifu ambayo Wewe ulinifadhili. Hakika sitaki kukuacha Wewe! Ewe Mungu! Nitaitembeaje njia yangu ya baadaye? Ninastahili kufanya nini? Tafadhali nionyeshe njia sahihi. Ninawezaje kuyaridhisha malengo Yako chini ya hali hizi?” Moyo wangu ulikuwa unalia, na mwili wangu wote ulikuwa ukitetemeka. Machozi ya majuto, hali ya kuwiwa, na majuto yote yakisokotana. Wakati huo, nilipata ladha ya kile ambacho mtu aliyeshindwa na Mungu huhisi baada ya kutelekezwa na Mungu kwa sababu ya kuikosea tabia Yake! Katikati ya kilio changu cha mara kwa mara na majuto, nilihisi Mungu akinirudia polepole. Kisha Mungu akanipa nuru: “Ungefanya nini kama ungekuwa upate uzoefu wa majaribio kama ule wa watendaji-huduma? Bila kujali ni wakati upi, ni lazima ufuate kwa moyo mmoja na fikra … kutafuta mabadiliko ya tabia mpaka kazi ya ulimwengu wote ikamilike.” Halafu pia nilikumbuka kwamba Mungu alisema wakati mmoja: “Bila kujali iwapo unakosea bila kupenda ama kutokana na asili ya uasi, kumbuka tu: Harakisha na uuzindukie uhalisi! Endelea kwa bidii; bila kujali ni hali gani inayotokea, lazima uendelee kwa bidii. Mungu anafanya kazi ili kuwaokoa watu…” (“Mapenzi ya Mungu ni Kuwaokoa Watu kwa Kiwango Kikubwa Sana Kinachowezekana” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Mbele ya neno la Mungu lisilochoka, moyo wangu hatua kwa hatua ulipona. Niliona matumaini, nilielewa nia za Mungu, na sikuwa tena nimechanganyikiwa kuhusu ni njia gani mbele yangu niliyostahili kuchukua. Hivi sasa, Mungu anataka mimi niwe mfuasi mwaminifu, niweze kutafuta mabadiliko ya kitabia kwa uthabiti, na kutoka wakati huu na kwendelea niweze kumaliza barabara niliyokuwa sijamaliza kuitembea kama kiumbe aliyeumbwa, kutokuwa nikiomba kitu chochote tena kutoka kwa Mungu. Katika hatua hii, nilifikiri juu ya maneno ambayo Mungu alisema baada ya majaribio ya watendaji-huduma, ambayo maana yake ni: Mtu kwa kweli hateseki kiasi hicho chote kama kwa hakika yuko radhi kuwa kiumbe aliyeumbwa … Ndiyo, chanzo cha mateso yangu ni upotovu wangu. Nia ya asili ya Mungu ilikuwa kutomwacha mtu ateseke sana. Ni kwamba tu sikutaka kuwa kiumbe aliyeumbwa. Siku zote nilijaribu kuepuka ukweli ili kutembea njia yangu mwenyewe, daima kutaka kuwa Mungu, na kuwafanya watu kunichukua kama Mungu. Ninawezaje basi kukosa kuteseka sana? Wakati huu, mimi mwenyewe nilipitia nguvu ya neno la Mungu—lingeweza kunifanya nifufuke kutoka kwa wafu, kunifanya nizivunje nguvu zote za kifo. Sasa matatizo yote ndani ya moyo wangu yalitatuliwa na neno la Mungu. Kama mvua nzuri baada ya ukame wa muda mrefu, kila kitu kilikuwa kibichi sana, kilichokombolewa sana, cha nzuri sana. Ndiyo! Mungu, nilikuwa kwa asili kiumbe wa kuumbwa aliyetengenezwa na Wewe. Kwa kuwa nilifanywa na Wewe nitamilikiwa wa Wewe na kukuabudu Wewe. Huu ni wajibu wangu na jukumu langu. Siipaswi kuuliza chochote zaidi kutoka Kwako na ni lazima nitii tu mbele ya tabia Yako ya haki. Wewe kuniruhusu nirudi nyumbani kutafakari mwenyewe ni zawadi Yako kubwa kabisa ya upendo na ulinzi kwangu. Niliteswa na ugonjwa kwa sababu ya kutotii kwangu na kwa sababu niliichukiza tabia Yako. Kulingana na matendo yangu nilipaswa kulaaniwa na Wewe muda mrefu uliopita, lakini kutokana na neema Yako, Wewe umeniruhusu kuwa hai leo.

Uzoefu huu umeacha alama kubwa katika kina cha nafsi yangu, ukinifanya kutoweza kuusahau kwa maisha yangu yote. Kila wakati nikikumbuka tukio moja baada ya jingine nikishambuliwa, ningekuwa mwenye hadhari kubwa na kuhamasishwa. Mimi kamwe sitamkosea Mungu tena na kumhuzunisha Mungu. Bila ya stahamala na uvumilivu wa Mungu, singekuwa napumua leo! Ewe Mungu! Asante! Katika kazi Yako nimefurahia utamu wake na furaha awali, lakini pia nimeonja tabia Yako isiyokosewa. Zaidi ya hayo, nimepitia jinsi ilivyo kuwa mwana mpotevu na joto la kurudi kwa kukumbatio Lako tena. Matendo Yako yanawezaje kutonifanya nionyeshe sifa zangu za dhati zaidi?