Huku Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo

15/01/2018

Fan Xing Mji wa Zhumadian, Mkoa wa Henan

Katika siku za nyuma, nilikuwa nimeunganishwa na dada mmoja kufanya kazi kwa wajibu fulani. Kwa sababu nilikuwa na majisifu na mwenye kiburi na sikutafuta ukweli, nilikuwa na mawazo kiasi ya kabla kuhusu dada huyu ambayo niliweka moyoni mwangu daima na sikuzungumza waziwazi naye. Tulipotengana, sikuwa nimeingia katika ukweli wa uhusiano wa kufanya kazi wenye kuridhisha. Baadaye, kanisa lilinipangia kufanya kazi na dada mwingine nami nikaweka azimio mbele ya Mungu: Kuanzia sasa kuendelea, sitatembea katika njia za kufeli. Nimejifunza mafundisho yangu na hivyo kwa sasa wakati huu bila shaka nitakuwa na mawasiliano ya wazi zaidi na dada huyu na kufikia uhusiano wa kufanya kazi wenye kuridhisha.

Kila wakati kulikuwa na mgongano au pengo kati yetu tulipokuwa tukifanya wajibu wetu pamoja, ningechukua fursa ya kwanza kuwasiliana na dada na kuzungumza kwa dhati. Ningemwuliza ni vipengele vipi nilikuwa nikifanya kwa njia isiyofaa. Dada huyo kisha angeonyesha kuwa nilikuwa na kiburi na mwenye majisifu na kwamba siku zote ningekataa mitazamo yake katika mawasiliano yetu. Alisema wakati mwingine ningeonyesha hali zake na kumpachika jina bila haki, na kwamba wakati wa mikusanyiko, nilifanya maamuzi yote kuhusu kusoma neno la Mungu. Nilikubali kwa kichwa mambo haya yote dada alisema juu yangu. Nilidhani: “Kwa kuwa unasema mimi nina kiburi, basi nitazungumza kwa unyenyekevu zaidi kuanzia sasa na kuendelea na kuzingatia kwa makini hasa kuzungumza kwa hekima na busara. Ikiwa nitatambua matatizo yoyote unayo, basi nitayadunisha wakati ninapoyataja. Ikiwa hutayatambua, basi sitayazungumzia. Wakati wa mikusanyiko, nitakula na kunywa chochote utakachoniambia nikule na ninywe, na nitasikia kila kitu unachosema. Si hili litatatua kila suala? Kisha hutasema kwamba siwezi kufanya kazi na mtu yeyote kwa sababu ya kiburi changu.” Baada ya haya, nilianza kuweka hili katika vitendo. Kabla ya kuzungumza, ningefikiri vile ningeweza kuepuka kukana wazo la dada. Wakati mitazamo yetu hayakulingana pamoja, ningekubali kushindwa na mtazamo wake na kutekeleza wazo lake. Nilipomwona dada akifanya jambo kwa njia isiyo sahihi, singemfafanulia kwa waziwazi. Lakini baada ya kipindi cha muda cha kutenda kwa namna hii, niligundua kuwa itikadi yangu ya “nyima mwili na weka ukweli katika matendo” haikuwa imebadilisha uhusiano wetu hata kidogo. Badala yake, iliimarisha mawazo yake yaliyotungwa kabla kunihusu. Kwa kuona matokeo hayo, nilihisi nimekosewa. Niliwaza: “Tayari nimejitahidi kadri niwezavyo kuweka ukweli katika matendo, mbona haifanyi kazi? Dada huyu si rahisi kupatana na yeye, hana wepesi wa kuhisi hata kidogo.” Kwa hiyo, nilizama katika uhasi na moyo wangu ukahuzunika sana.

Siku moja, kiongozi mmoja alitujia kukagua kazi yetu na kuuliza jinsi hali zetu zilivyokuwa wakati wa kipindi hiki. Kisha nikaeleza vile hali yangu ilivyokuwa. Baada ya kusikiliza, kiongozi huyo alisema: “Hii mbinu yako haiweki ukweli katika matendo. Wewe ni mchafu ndani. Unatenda hivi kwa madhumuni yako mwenyewe na hautendi kulingana na ukweli.” Baada ya haya, tulisoma vifungu viwili vya maneno ya Mungu. Mungu alisema: “Upande wa nje, inaonekana kana kwamba unatia ukweli katika vitendo, lakini kwa kweli, hali ya matendo yako haionyeshi kwamba unatia ukweli katika vitendo. Kuna watu wengi ambao, punde tu wanayo mienendo fulani ya nje, huamini. ‘Je, kwani sitimizi wajibu wangu? Je, sikuacha familia na kazi yangu? Je, kwani sitii ukweli katika vitendo kwa kutimiza wajibu wangu?’ Lakini Mungu hatambui kwamba unatia ukweli katika vitendo. Wale wote ambao matendo yao yamechafuliwa na nia na malengo ya kibinafsi hawatendi ukweli. Kusema kweli, aina hii ya mwenendo huenda itashutumiwa na Mungu; haitasifiwa au kukumbukwa na Yeye. Kulichangua hili zaidi, unafanya uovu na mwenendo wako unampinga Mungu. Kutoka nje, mambo haya unayoyafanya yanaonekana kuambatana na ukweli: Hukatizi wala kusumbua chochote na hujafanya maharibifu yoyote ya kweli au kukiuka ukweli wowote. Kinaonekana kuwa chenye mantiki na cha maana, ilhali asili ya matendo yako inahusika na kufanya uovu na kumpinga Mungu. Kwa hivyo unapaswa kupambanua kama kumekuwa na mabadiliko katika tabia yako na kama unatia ukweli katika vitendo kwa kutazama nia nyuma ya matendo yako kulingana na maneno ya Mungu. Haiamuliwi na maneno au maoni ya kibinadamu. Badala yake, inategemea Mungu kusema kama unakubali mapenzi Yake au la, kama matendo yako yana uhalisi wa ukweli au la, na kama yanafikia mahitaji Yake na viwango Vyake au la. Kujipima tu dhidi ya matakwa ya Mungu ndiyo sahihi” (“Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). “Mawazo ya binadamu kwa kawaida yanaonekana mazuri na sahihi kwa watu, na yanaonekana kana kwamba hayawezi kukiukaukweli kwa kiasi kikubwa sana. Watu huhisi kwamba kufanya mambo kwa jinsi hii kutakuwa kuweka ukweli katika matendo; wanahisi kwamba kufanya mambo kwa jinsi hiyo kutakuwa kumtii Mungu. Hakika, hawamtafuti Mungu kwa kweli au kumwomba Mungu kulihusu, na hawajitahidi kulifanya vizuri kulingana na mahitaji ya Mungu, ili kuridhisha mapenzi Yake. Hawamiliki hali hii ya kweli, wala hawana hamu kama hiyo. Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo watu hufanya katika kutenda kwao. Unamwamini Mungu, lakini humweki Mungu moyoni mwako. Hii sio dhambi vipi? Je, hujidanganyi mwenyewe? Ni aina gani za athari ambazo unaweza kuvuna ukiendelea kuamini jinsi hiyo? Isitoshe, umuhimu wa imani unaweza kuonyeshwa vipi?” (“Kutafuta Mapenzi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Kutenda Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilijaribu kuelewa maneno yake Mungu na kuyalinganisha na hali yangu inayodaiwa kuwa “kuweka ukweli katika matendo.” Moyo wangu ulichangamka. Hivyo, njia niliyokuwa nikifanya mambo haikukusudiwa kukidhi Mungu. Ilikusudiwa kulinda hadhi yangu bure. Niliogopa kiongozi huyo angesema asili yangu ilikuwa na dosari, kwamba sikutafuta ukweli, na kuwa sikufanya kazi vyema na yeyote. Aidha, nilifikiri ilikuwa ni kisingizio cha kurahisisha uhusiano wangu na dada na kujinasua kwa aibu na uchungu uliosababishwa na mgogoro huo. Nilidhani ingekomboa ile taswira ambayo watu wengine walikuwa nayo kunihusu na kuwaruhusu kuona kuwa nilikuwa nimebadilika. Inaweza kuonekana kuwa kile kilichodaiwa kuwa “kuweka ukweli katika matendo” kwangu kilikuwa kwa madhumuni yangu mwenyewe. Yote yalitendwa mbele ya wengine na hayakuanzishwa kwa msingi wa kutafuta kumridhisha Mungu. Sikujidharau na kwa kweli kuunyima mwili kwa sababu sikuwa na ufahamu wa asili yangu ya majisifu na kiburi. Katika kutafakari juu ya kufanya kazi na dada, ni kwa sababu sikutambua asili yangu ya kujisifu na kiburi, na kwa sababu nilijiheshimu na nilikuwa nafikiri kila wakati kuwa nilikuwa bora zaidi kuliko wengine nilipozungumza, bila kujua nilikuwa nimesimama kwenye kiweko nikidunisha wengine. Wakati wa kushughulikia mambo, nilipenda kuwa msimamizi; nilifanya mambo kwa njia yangu mwenyewe, na kamwe sikuwahi kutafuta maoni ya watu wengine. Wakati dada alipoonyesha haya matatizo niliyokuwa nayo, sikutafuta ukweli uliofanana ili kuchambua na kuelewa hali ya asili yangu. Hata zaidi, sikutafuta jinsi ninapaswa kuiweka katika vitendo kulingana na mahitaji ya Mungu na kwa mujibu wa ukweli. Nilibadili tu matendo machache ya nje, nikifikiria kuwa kwa kuwa niliacha kufanya mambo ambayo yalikuwa mabaya, nilikuwa nikiweka ukweli katika matendo. Kwa kweli, kila kitu nilichokuwa nikifanya kilikuwa ukweli kulingana na mawazo yangu mwenyewe. Vyote vilikuwa ni vitendo vya nje na havikuwa na chochote kuhusu neno la Mungu. Mungu hangetambua kuwa nilikuwa nikiweka ukweli katika matendo. Kwa sababu sikuwa natenda kulingana na mahitaji ya Mungu na sikuwa natenda kwa mujibu wa ukweli, na kila kitu nilichofanya kilifanyika ili kukidhi tamaa zangu za kibinafsi na kufikia malengo yangu mwenyewe, kwa hiyo matendo yangu yalikuwa mabaya machoni pa Mungu; ilikuwa kumpinga Mungu.

Baada ya kutambua hili, niliunganisha neno la Mungu kwa makusudi ili nipate kuelewa asili yangu potovu katika maisha. Wakati nilionyesha upotovu wangu au nilipotambua kuwa hali yangu haikuwa sahihi, nilifichua waziwazi nafasi yangu na nikaichunguza na kutafuta chanzo kulingana na neno la Mungu. Nilipofanya hili, kunena kwangu na matendo yangu yakawa ya kawaida, na nilijua nafasi ambao nilipaswa kusimama. Nikawa na heshima kwa watu na kutii kwa uvumilivu. Kuunyima mwili kukawa sio kugumu sana na tukaweza kuwa mawasiliano ya dhati. Ushirikiano wetu ulikuwa umekuwa wa kuridhisha tena zaidi kuliko siku za nyuma.

Kupitia uzoefu huu, nimepata kuelewa kwamba kuweka ukweli katika vitendo lazima kuwekwe kwa msingi wa neno la Mungu na lazima kuanzishwe kwa kanuni za kweli. Mtu akiacha neno la Mungu, basi kila kitu kinakuwa kitendo cha nje, yaani, kuweka ukweli wa mawazo yao wenyewe katika matendo. Hata ikiwa ningefanya mambo vizuri na kwa usahihi, bado haingechukuliwa kama kuweka ukweli katika vitendo, na hata zaidi haingeleta mabadiliko kwa tabia ya maisha yangu. Kuanzia sasa kuendelea, bila kujali ni nini ninachofanya, nataka maneno ya Mungu kuwa kanuni za matendo yangu na kuweka neno la Mungu kikamilifu katika vitendo ili mwenendo wangu utalingana na ukweli na mapenzi ya Mungu na kupata kuridhika kwa Mungu.

Iliyotangulia: Ubia wa Kweli

Ikiwa una matatizo au maswali yoyote katika imani yako, tafadhali wasiliana nasi wakati wowote.

Maudhui Yanayohusiana

Ukombozi wa Moyo

Na Zheng Xin, Marekani Mnamo Oktoba ya 2016, mimi na mume wangu tulikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho wakati tulikuwa ughaibuni....

Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Asante Mungu kwa kunurishwa huku, ambako kumeniinua kutoka kwa upofu. Kama sivyo, ningekuwa bado ningehadaiwa na udanganyifu wangu mwenyewe—nikiinuka mbele na tamaa pofu kwelekea kwa mauti yangu ya karibu sana. Ni gutuko lililoje la kushangaza!

Roho Yangu Yakombolewa

Na Mibu, Uhispania “Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi...

Uzoefu wa Kutenda Ukweli

Hengxin Jiji la Zhuzhou, Mkoa wa Hunan Sio muda mrefu mno uliopita, nilisikia “Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha,” jambo...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp