Sitapumbazwa Tena na Nia Njema

14/01/2018

Meng Yu Mji wa Pingdingshan, Mkoa wa Henan

Wakati mmoja nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, niliona kuwa ndugu fulani alikuwa akijaribu kuwafurahisha dada zake, maonyesho ya hali mbovu ya tabia yake machoni mwangu. Niliamua kutafuta fursa ya kumkumbusha haya mambo. Siku zilipita na nikaona utendaji wake wa wajibu ulikuwa wenye matokeo machache mazuri—ushahidi wa maoni yangu ya awali kumhusu. Kwa hiyo niliamua kuzungumza naye uso kwa uso. Hata hivyo, tulipogusia suala hili, alikataa kwa ukali maoni yangu yote na akajibu kwa ukali kwamba nilikuwa mwenye kukosoa sana. “Kwa miaka hii yote,” alisema, “wakati wowote unapowasiliana nami, unanikemea kwa mtazamo wa kudharau, na leo unasema kwa namna hiyo ya kudharau....” Mazungumzo hayo yakageuka kuwa mabaya zaidi kuliko yasiyozaa matunda—yalivunjika kwa kutokubaliana kabisa. Majibizo yake yaliniongoza kwa uamuzi mchungu, nikifikiri: “Niliwasiliana ili nisaidie, sio kukuaibisha kwa kufichua upungufu wako. Badala ya kusikiliza, ulinitafutia makosa na kunishutumu kuwa mwenye mtazamo wa kudharau. Sawa! Mimi nitakuacha uwe. Hata hivyo, nia zangu zilikuwa njema, na kukatalia kwako kunaonyesha tu kuwa hutafuti ukweli.” Tangu wakati huo, daima nimejichukulia kama yule ambaye alikuwa sahihi, wakati nikifikiri ndugu huyo ndiye aliyekuwa na makosa peke yake. Hata hivyo, hivi karibuni nilipata ufahamu kujihusu kwa njia ya kushughulikia watu, vitu na mambo ambavyo Mungu ameweka karibu nami.

Siku kadhaa zilizopita, kanisa lilimpa mmoja kati ya ndugu zangu wadogo kazi mpya. Alikuwa katika hali mbaya awali, lakini tangu mpango huo, alibadilishwa kuwa mtu mpya, mwenye bidii zaidi katika akili na wa kujiamini zaidi katika neno. Siku moja, alizungumza nami kwa sauti, onyesho na namna ambayo iliniwacha nimekereka kwa kina. Nilijua kwamba aliwasiliana mapenzi Yake Mungu na kusema kweli kunihusu, lakini kata sikuweza kumsikiliza, sembuse kukubali kile alichosema. Nilipokuwa karibu kuripuka, ghafla nilijiona ndani yake na nikakumbuka sauti na onyesho niliyotumia miezi kadhaa iliyopita nilipowasiliana na ndugu yangu. Si ajabu nilifikiriwa mwenye mtazamo wa kudharau. Kile alichohisi kilikuwa cha kweli, na sasa hivi nimehisi yale maudhi sawa aliyopitia kutoka kwangu—kama hisia ya kuchefua ya kula mzoga wa nzi. Mungu alipanga mazingira kama hayo ili kuniwezesha kuona ukweli huu: Binadamu mwenye nia njema lakini tabia isiyobadilika hana mahali pa Mungu ndani ya moyo wake, kwa hivyo, kile anachofichua ni cha kawaida, na mfano halisi wa tabia yake ya kishetani. Wakati huo, nilikumbuka kitu kutoka kwa ushirika wake Kristo: “Umuhimu wa kujitafakari na kujijua ni huu: Kadiri unavyozidi kuhisi kuwa katika sehemu fulani umefanya vizuri au umefanya jambo linalofaa, na kadiri unavyofikiri kuwa unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu au kuweza kujivunia katika sehemu fulani, basi ndivyo inavyofaa zaidi kwako kujijua katika sehemu hizo na inavyofaa zaidi kwako kuzichunguza zaidi ili kuona ni uchafu gani uko ndani yako, pamoja na mambo gani ndani yako hayawezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu” (“Ni kwa Kutambua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Kwa hili, Mungu hukusudia kuwafundisha binadamu kuelewa ukosefu wa utakatifu katika maneno na matendo yao. Kwa sababu wanadamu kwa kawaida ni waasi na wamejawa na sumu za kishetani, matendo yao, isipokuwa yakosolewe na ukweli, kwa kawaida humpinga Mungu. Wale wanaofikiri kuwa tabia zao zinaambatana na ukweli na ni zisizolaumika, kwa kweli hawajabadilika katika tabia yao, na bado hawajakamilishwa na Mungu. Wao bado wanampinga Mungu kwa masuala ya asili yao ya ndani na wanafichua tabia yao ya kishetani. Kuna uchafu mwingi sana ndani ya wanadamu unaohitaji kuchambuliwa, kutambuliwa na kuzungumziwa. Sasa ninapoangalia nyuma kwa mawasiliano yangu na ndugu huyo, nilikuwa nimedhibitisha uhalali wa usahihi wangu kwa nia zangu njema, lakini nilikosa kuona kwamba nilichukua msimamo usio halisi katika mawasiliano yangu. Nilijiweka kama stadi wa ukweli, mtu ambaye anaweza kujua kama wengine wanatenda kwa kawaida, na nani ambaye anaelewa kikamilifu; Nilishurutisha msikilizaji wangu ili anikubali na kumpachika jina kama “asiye mfuatiliaji wa ukweli” kwa ishara kidogo ya kutokubaliana. Nimefichua nini? Ukaidi, ukatili, ukandamizaji, nidhamu—tabia ya Shetani inayochukiza na yenye kuchefua. Kuna tofauti yoyote kati ya yale ambayo nimefichua na ukandamizaji wa kisiasa katika matapo mengi ya kisiasa yanayoendelezwa mbele na joka kubwa jekundu? Joka kubwa jekundu halikutegemea chochote ila nia zake lenyewe wakati lilipoweka mashtaka na kuwatia watu kwenye ukandamizaji wa kikatili. Kwa kweli sikumwomba Mungu au kutafuta mwongozo Wake kabla ya kuwasiliana na ndugu yangu, wala sikuthibitisha kama kweli alikuwa mwenye makosa kabla ya kushawishika na fikira zangu za awali, kuona kuwa utendaji wake usio na mafanikio ulisababishwa na kuwepo chini ya ushawishi wa uovu, na kumsukuma kukubali kwake mashtaka hayo. Sasa ninatambua kuwa tabia yangu ya asili inafanana na ile ya joka jekundu kubwa—kila mwendo wangu, sura zangu na namna za kuongea zote zilijawa na tabia za kiburi ambazo hufichuliwa kwa kawaida kwa joka kubwa jekundu. Ninawezaje kuwa wa faida kwa wanadamu na tabia yangu mbovu? Roho Mtakatifu angewezaje kufanya kazi kupitia mimi? Bila kazi Yake, ninawezaje kutarajia kuzaa matunda kwa mawasiliano yangu? Sasa naona kuwa mawasiliano hayakuzaa matunda, sio kwa sababu ya kukataliwa kwa ukweli kwa ndugu yangu, lakini kwa sababu sikumweka Mungu moyoni mwangu na sikuwa mtu sahihi mbele ya Mungu. Nilichofichua hakikumsinya Mungu tu, ila pia wanadamu.

Kwa msaada wa kazi halisi ya Mungu, najijua na kuelewa kwamba kama wanadamu hawabadiliki katika tabia yao, hawana budi kufichua tabia potovu ya Shetani hata kama wanadhani kuwa wana nia njema na mienendo ya kufaa, na kisha wanapaswa kujielewa wenyewe. Kuanzia sasa kuendelea, nitajitahidi kulenga mabadiliko katika tabia za maisha yangu, kujijua na kubadili tabia yangu ya asili, kujizuia dhidi ya kutoa maoni kwa kutupia macho kijuujuu, kujiepusha na mwelekeo wa kuacha kutafuta kasoro ndani yangu wakati nina nia njema, kutafuta kujijua katika kila kitu, kufikia mabadiliko katika tabia na kuleta faraja kwa moyo wa Mungu.

Ikiwa una matatizo au maswali yoyote katika imani yako, tafadhali wasiliana nasi wakati wowote.

Maudhui Yanayohusiana

Maneno ya Mungu Yameniamsha

Kwa sababu ya kutoa nuru kwa maneno ya Mungu, nimeamka kutoka kwa dhana na mawazo yangu, nikigundua kwamba mimi si mtu ambaye yuko tayari kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu. Kumenifanya pia nione ya kwamba niko katika ukingo wa hatari.

Nimebahatika Kumhudumia Mungu

Na Gensui, Korea ya Kusini Mwenyezi Mungu anasema, “Ni kupitia nini ndiyo ukamilishaji wa Mungu kwa mwanadamu hutimizwa? Kupitia tabia Yake...

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp