Nimejifunza Kukubaliana na Wengine

25/08/2020

Mwenyezi Mungu anasema, “Kiburi ndicho chanzo cha upotovu wa mwanadamu. Kadiri watu wanavyozidi kuwa na kiburi, ndivyo wanavyozidi kuwa na uelekeo wa kumpinga Mungu. Tatizo hili ni kubwa kiasi gani? Siyo tu kwamba watu wenye tabia ya kiburi humfikiria kila mtu mwingine kuwa duni kuwaliko, lakini lililo baya zaidi, wao hata huwa na mtazamo wa udhalilishaji kwa Mungu. Hata ingawa, kwa nje, watu wengine wanaweza kuonekana kana kwamba wanamwamini Mungu na kumfuata, hawamchukulii kama Mungu hata kidogo. Wao huhisi sikuzote kuwa wanamiliki ukweli na wanajipenda mno. Hiki ndicho kiini na chanzo cha tabia ya kiburi, na hutoka kwa Shetani. Kwa hivyo, tatizo la kiburi lazima litatuliwe. Kuhisi kuwa wewe ni bora kuliko wengine—hilo ni jambo dogo. Suala la muhimu ni kwamba tabia ya kiburi ya mtu humzuia mtu kumtii Mungu, sheria Yake, na mipango Yake; mtu kama huyo daima huhisi kuwa na uelekeo wa kushindana na Mungu kuwatawala wengine. Mtu wa aina hii hamchi Mungu hata kidogo, sembuse kumpenda Mungu au kumtii. Watu ambao ni wenye kiburi na wenye majivuno, hasa wale ambao ni wenye kiburi mno hadi kiwango cha kupoteza akili zao, hawawezi kumtii Mungu katika imani yao Kwake, na hata hujiinua na kujishuhudia wenyewe. Watu kama hao ndio humpinga Mungu zaidi. Kama watu wanataka kufikia mahali ambapo wanamcha Mungu, basi lazima kwanza watatue tabia zao za kiburi. Kadiri unavyotatua tabia yako ya kiburi kikamilifu, ndivyo utakavyokuwa na uchaji zaidi kwa Mungu, na ni hapo tu ndipo utakapoweza kumtii Yeye na uweze kupata ukweli na kumjua” (Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Nilijua kila mara kwamba tabia yangu ilikuwa ya kiburi, lakini sikuwahi kuelewa maneno haya: “Kiburi ndicho chanzo cha upotovu wa mwanadamu. Kadiri watu wanavyozidi kuwa na kiburi, ndivyo wanavyozidi kuwa na uelekeo wa kumpinga Mungu.” Pia, sikuwahi kulenga kutafuta ukweli ili kuitatua. Ni wakati tu ambapo nilivuruga kazi ya kanisa kwa sababu ya kiburi changu, kwa sababu nilishaua ukuu wangu, na kuwalazimisha watu wafanye kile nilichowaambia katika wajibu wangu, ndipo mwishowe nilianza kuthamini maneno ya Mungu na kuona jinsi kiburi kinaweza kuwafanya watu watende maovu na kumpinga Mungu. Wakati huo tu ndipo nilipolenga kutafuta ukweli ili kutatua tabia yangu ya kiburi.

Ilikuwa mnamo Mei 2018 kanisa liliponipa wajibu wa uandishi. Nilipoanza mara ya kwanza, nilihisi kwamba sikuwa na uwezo hata kidogo. Nilimwomba na kumtegemea Mungu mara nyingi katika wajibu wangu na kushiriki juu ya kanuni za kuhariri makala pamoja na kina dada niliofanya kazi nao. Baada ya muda fulani, nilihisi kana kwamba nilielewa vizuri kanuni na ustadi wa kitaalamu wa kuhariri makala na kwamba nilikuwa na uwezo a kufanya kazi hiyo. Kadiri muda ulivyopita, niliacha kulenga sana kutafuta kanuni za ukweli katika wajibu wangu. Nilipohariri makala nilisikiliza maoni ya wengine mara chache na nikashikilia maoni yangu mara nyingi. Wakati mmoja kulikuwa na makala ambayo hayakuwa na mfuatano bayana wa mawazo. Dada wawili walisema kwamba tulipaswa kushiriki kulingana na maneno na kanuni za Mungu na tuandike mfuatano wa mawazo kabla ya kuyabadilisha. Niliwaza “Je, tunahitaji kweli kutafuta maneno na kanuni za Mungu? Tumekuwa tukifanya wajibu huu kwa miaka mingi sasa, kwa hivyo tunapaswa kuweza kutatua tatizo dogo kama hili!” Niliwaeleza wengine mfuatano wa mawazo yaliyokuwa katika makala hayo kama nilivyoelewa na nikawasisitizia sababu ya maoni yangu kuwa sahihi. Kwa sababu ya kusisitiza kwangu, kina dada hao hawakutafuta maneno na kanuni za Mungu bali waliandika makala hayo kulingana na ufahamu wangu. Wakati mwingine tulikuwa tukishiriki juu ya maana ya makala fulani wakati ambapo kina dada walipendekeza tutafute vifaa vya kujifunza kuhusu kuandika ambavyo tungesoma. Nilipinga sana wazo hili na nikawaza, “Sote tumehariri makala kiasi cha kuridhisha, kwa hivyo kuna haja gani ya kusoma zaidi? Mfuatano wa mawazo katika uandishi ni kitu unachozoea. Unajaribu tu kurekebisha kitu ambacho hakijaharibika.” Nilitafuta kisingizio chochote cha kukwepa wazo hilo na nikawafundisha yale niliyojua kuhusu uandishi ili wote waweze kukubaliana nami. Mwishowe, dada hao wawili hawakuwa na chaguo lingine ila kukubaliana na hayo.

Siku moja, dada mgeni alikuja kuhariri makala pamoja nami. Niligundua kwamba alikuwa mgeni katika imani na hakuwa amewahi kufanya kazi ya uandishi hapo awali. Pia, nilipomjua vizuri, niligundua kwamba hakuwa hodari katika muundo wa lugha kama mimi. Niliwaza, “Nimekuwa nikifanya wajibu huu kwa muda mrefu zaidi kukushinda na ninaelewa mengi zaidi juu ya kanuni na ujuzi kukushinda. Unahitaji tu kufanya kile ninachosema kuanzia sasa.” Wakati mmoja, niliona kwamba hakuwa amehariri makala fulani kulingana na mawazo yangu. Nilihisi wasiwasi sana na nikawaza, “Una tatizo gani? Nimefanya ushirika nawe kwa utondoti. Kwa nini husikilizi? Hili halikubaliki. Lazima niwe mkali kwako.” Na kwa hivyo nilielekeza kidole kwenye skrini ya kompyuta na nikasema kwa sauti ya kukaripia, “Sasa unafanya nini? Mawazo katika makala haya hayafuatani vizuri! Nimekuwa hapa kwa muda mrefu na ninajua zaidi juu ya kanuni na ujuzi kukuliko. Kama tu ungeyahariri kama nilivyokuambia, usingefanya makosa kama haya.” Uso wa dada huyo ulibadilika na kuwa mwekundu na akainamisha kichwa chake bila kusema lolote. Nilipomwona akiwa amefadhaika sana, nilihisi vibaya kidogo na nikawaza, “Kwa nini nilimnenea kwa namna hiyo na kumfedhehesha?” “Sitafanya hivyo tena.” Lakini muda mfupi baadaye, tulipokuwa tukijadili makala fulani, nilitumia muda mrefu kushiriki na yule dada mawazo yangu mwenyewe lakini bado hakuyahariri kama nilivyomwambia. Nilikasirika sana na nikawaza, “Mapendekezo ninayotoa ya uhariri yanakubaliwa na washiriki wa timu wa muda mrefu na hata mtu anayesimamia anakubali, hivyo kwa nini usifanye tu kile ninachosema? Hapana, lazima nifikirie jinsi ya kukufanya unisikilize.” Kisha nikashiriki naye mara nyingi na kuacha mara tu alipokubali mapendekezo yangu. Mbali na hayo, hata wakati wa kufanya ibada za kila siku, nilitumia imani yangu ya muda mrefu na ufahamu wangu mkubwa kama visingizio vya kumwambia asikilize mahubiri fulani wakati mmoja na kisha asome sura fulani za maneno ya Mungu wakati mwingine mpaka hakujua cha kufanya tena. Haya yalipokuwa yakiendelea, dada huyo aliishia kuhisi kwamba alizuiwa sana nami. Alikuwa msemi na alipenda kutabasamu sana mwanzoni na alieleza maoni yake mwenyewe mara nyingi. Lakini sasa alikuwa mnyamavu na mwenye huzuni na alizungumza mara chache sana. Alikuwa pia hasi na hakutaka kufanya wajibu wake huko tena. Nilifadhaika nilipomwona akiwa katika hali kama hiyo na nikadhani kwamba sikupaswa kumtendea hivyo. Lakini pindi tatizo fulani lilipoibuka, sikuweza kujizuia kudhihirisha kiburi changu.

Muda mfupi baadaye, nilipata malengelenge mengi kinywani mwangu na hata ikawa vigumu kula. Zaidi ya hayo, sikuweza kuhisi kazi na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Sikuwa na lolote la kusema nilipomwomba Mungu na sikupata nuru yoyote kutoka katika maneno ya Mungu. Nilihariri makala machache tu baada ya zaidi ya mwezi moja. Nilikuwa nikihisi wasiwasi kila wakati, kwa hivyo nilikuja mbele za Mungu kuomba kwamba Ananielekeze ili nijue hali yangu mwenyewe. Baadaye, nilisoma baadhi ya maneno ya Mungu yaliyonukuliwa katika makala niliyokuwa nikihariri ambayo yalifunua hali yangu halisi. Maneno ya Mungu yanasema, “Mnatekeleza wajibu wenu, wakati unapita, na mnapata mafanikio kiasi, lakini hamjakuwa na maendeleo yoyote katika kuingia kwenu katika uzima. Hamjafaulu, na yote mnayoelewa ni hayo mafundisho machache tu, na, kwa muda mrefu, hamjakuwa na ufahamu wa uhalisi wa ukweli. Katika hali kama hii, je, mtafanya nini na mtafichua tabia zipi potovu? (Kiburi na majivuno.) Je, mtakuwa wenye kiburi na majivuno hata zaidi, au mtasalia jinsi mlivyo? (Tutakuwa wenye kiburi na majivuno hata zaidi.) Sababu ya hilo ni nini? (Tutafikiri kwamba tuna sifa zinazostahili.) Je, ni kwa msingi upi ndio mnaamua kwamba mna sifa zinazostahili? Je, inaamuliwa kwa msingi wa muda ambao mmekuwa mkitekeleza wajibu wenu na kiasi cha uzoefu ambao mmepata katika utekelezaji wa wajibu huo? Polepole lakini kwa hakika, je, mtaanza kujiweka katika madaraja kulingana na ukubwa wa cheo? … Wakati ambapo watu hawana sifa zinazostahili, wao hujua kwamba wanapaswa kuwa wenye kutahadhari na waangalifu, na wao hujikumbusha wasifanye makosa; punde wanapokuwa na rasilimali za kutumia, wanakuwa wenye kiburi na wanadhani kwamba wao ni wazuri. Punde mtu anapofikiria ana rasilimali za kutumia, uhusiano wake na Mungu hauwi wa kawaida tena, na hii ni ishara ya hatari” (Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, nilikumbuka nilipoanza kufanya wajibu wa uandishi. Sikujua chochote kuhusu kanuni au ustadi, lakini nilijitambua kiasi. Niliweza kujiachia na kutafuta na kujifunza pamoja na dada zangu. Baada ya muda fulani, nilidhani kwamba nilikuwa nimeelewa baadhi ya kanuni na nikaanza kuona matokeo katika wajibu wangu. Kufumba na kufumbua, nilianza kujionyesha, nikifikiri kwamba nilikuwa na ubora mzuri wa tabia na ukuu na kwa hivyo nilianza kuwadharau kina dada zangu. Sikusikiza tena mapendekezo yao na walipotaka kutafuta kanuni au kurejea vifaa vya kusoma, nilidhani kwamba hakukuwa na haja na kwamba walipaswa kufanya tu kile nilichosema. Nilimdharau yule dada mgeni hata zaidi. Nilidhani kwamba kwa sababu nilikuwa nimefanya wajibu huu kwa muda mrefu sana na nilielewa mengi zaidi, alipaswa kuheshimu ukuu wangu na kukubaliana na mawazo yangu. Wakati ambapo hakufanya hivyo, nilimkaripia hadi akakubali mapendekezo yangu. Hata nilimlazimisha asome yale niliyomtaka asome wakati wa ibada. Nilimzuia hadi kufikia wakati ambapo alikuwa hasi, mwenye uchungu na hakutaka kufanya wajibu wake tena. Sikuwa nikifanya wajibu wangu, nilikuwa nikifanya uovu! Nilikuwa nikitumia uzoefu wangu kwa faida yangu, na kuzidi kuwa mwenye kiburi, nikiwazuia wengine, kuwadhuru na kuwakandamiza kila wakati. Ingawa nilijua hali yangu ilikuwa mbaya, nilikuwa mkaidi na nilikataa kutafuta ukweli au kutafakari juu yangu mwenyewe. Wakati huo tu ndipo nilipogundua jinsi roho yangu ilivyokuwa na giza na kwamba nilikuwa mgonjwa. Mungu alikuwa Akinifundisha nidhamu na hata zaidi, Akinilinda. Mungu alikuwa Akitumia hali hii kunilazimisha nije mbele Yake na kutafakari juu yangu mwenyewe. Nilipofikiri juu ya madhara ambayo kiburi changu kilikuwa kimemsababishia dada yangu, nilifadhaika sana na nilihisi hatia. Sikuwa na ubinadamu hata kidogo! Nilikuja mbele za Mungu upesi kuomba na kutubu. Baadaye, kwenye mkutano mmoja, nilishiriki juu ya upotovu ambao nilikuwa nikionyesha na jinsi nilivyoufahamu, na nikamwomba radhi mno dada yangu. Mbali na yeye kutofanya jambo hilo kuwa tatizo kubwa, pia alizungumza juu ya matukio aliyopitia. Nilihisi ghafla kana kwamba mioyo yetu ilikuwa imevutwa pamoja. Baada ya hapo, tulipofanya kazi pamoja katika wajibu wetu, tuliweza kushiriki kwa pamoja na kufidiana upungufu wetu. Mawazo katika makala pia yalianza kuwa bayana zaidi tulipokuwa tukiyahariri na tulifanya kazi haraka sana. Kisha niliona kwamba kwa kutoishi kulingana na tabia yangu potovu na kufanya kazi vizuri na wengine, nilituzwa kwa mwongozo na baraka za Mungu.

Siku moja wakati wa ibada, nilisoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama kiburi na majivuno, vingekuwa ndani yako, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho, na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utayabadilisha mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno! Kutatua matendo yao maovu, lazima kwanza watatue matatizo ya asili yao. Bila mabadiliko katika tabia, haitawezekana kuleta suluhu ya kimsingi kwa shida hii. Unapokuwa na uelewa fulani wa Mungu, unapoweza kuona upotovu wako mwenyewe na kutambua uhafifu na ubaya wa kiburi na majivuno, basi utahisi chuki, kughadhabishwa na kutatizwa. Utaweza kufanya mambo kwa ufahamu kumridhisha Mungu na kwa kufanya hivi, utahisi utulivu. Utaweza kwa ufahamu kutoa ushuhuda kwa Mungu na kwa kufanya hivi, utahisi raha. Kwa ufahamu utajifichua mwenyewe, huku ukifunua ubaya wako, na kwa kufanya hivi, utahisi vizuri ndani yako na kujihisi kuwa katika hali iliyoboreka ya akili” (Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Maneno ya Mungu yalinionyesha kwamba asili yangu ya kiburi na majivuno ilikuwa chanzo cha upinzani wangu kwa Mungu. Kwa sababu ya kudhibitiwa na asili yangu ya kiburi, nilijiona sana kila mara. Nilihisi kana kwamba nilikuwa na uwezo wa kufanya kazi na nilielewa mengi zaidi ya mtu mwingine yeyote, na kwa hivyo nilitaka kuwa na kauli ya mwisho siku zote. Maoni ya kina dada zangu yalipotofautiana na yangu, nilikataa kuyakubali na nikawalizimishia maoni yangu mwenyewe hadi wakayakubali. Dada zangu walipotaka kutafuta ukweli na kurejelea vifaa vya kusoma vya uandishi, niliwazuia na kuwalazimisha wakubali maoni yangu badala yake. Je, sikuwa nikiwatawala kimwinyi, nikiwadhibiti na kusimama mahali pasipostahili? Maneno ya Mungu pekee ndiyo ukweli na kanuni za mwenendo wa mwanadamu, na ndiyo tunayopaswa kuyatii na kuyakubali. Lakini sikuwaruhusu dada zangu watafute kanuni za ukweli au kumtii Mungu, lakini badala yake, niliwalazimisha wafanye kile nilichosema, kana kwamba maneno yangu yalikuwa ukweli. Nilijaribu kubadilisha ukweli kwa maoni na mawazo yangu mwenyewe. Je, sikuwa nikijaribu kujisawazisha na Mungu? Shetani hufuata kanuni kama vile, “Mimi ni bwana wangu mwenyewe kotekote mbinguni na ardhini na “Acha wale wanaokubaliana nami waneemeke na wale wanaonipinga waangamie.” Yeye hutaka kila mara kuwadhibiti wanadamu na kuchukua nafasi ya Mungu. Nilikuwa pia nikiishi kulingana na sumu hizi za Shetani, nikitaka kila wakati kuwa mkuu, kutawala na kuwa na kauli ya mwisho. Mbali na kuwadhuru dada zangu, pia niliharibu kazi ya kanisa. Tabia yangu ya kishetani ilikuwa mbaya sana. Nilikuwa nikitembea kwenye njia ya kumpinga Mungu na niliikosea sana tabia Yake! Tabia ya Mungu yenye haki ilinijia. Bila kazi ya Roho Mtakatifu, ilikuwa kana kwamba nilikuwa kama kipofu, nilishindwa kuelewa tatizo lolote na sikufanikisha chochote katika wajibu wangu. Nilipokabiliwa na ukweli huo, niliinamisha tu kichwa change na kukubali kwamba hata kama kulikuwa na mafanikio kidogo katika wajibu wangu, yote yalikuwa matendo ya Mungu. Nilikuwa tu nimeshirikiana kidogo. Lakini sikujijua hata kidogo na nilikuwa mwenye kiburi na kuwaamrisha hapa na pale watu bila kufikiria. Kwa kweli sikujijua hata kidogo. Nilihisi aibu sana nilipofikiria juu ya hayo. Niliamua kufanya kazi vizuri na wengine tangu wakati huo, kutoishi tena kulingana na tabia yangu ya kiburi, kujifunza jinsi ya kujiachia na kukubali mapendekezo ya wengine zaidi.

Wakati mmoja, tulipokuwa tukichambua mfuatano wa mawazo katika makala fulani, Dada Zhang aliibua baadhi ya mawazo ambayo yalistahili lakini kwa mara nyingine nilimtaka afanye kile nilichofikiri. Mara tu nilipokuwa karibu kusisitiza sababu ya mawazo yangu kuwa sahihi, niligundua ghafla kwamba nilikuwa nikidhihirisha tabia yangu ya kiburi tena na kujaribu kumlazimisha dada yangu afanye kile nilichosema. Nilikumbuka jinsi nilivyowaumiza kina dada zangu na kuathiri wajibu wangu hapo awali kwa sababu nilikuwa nikiishi kulingana na tabia yangu ya kiburi. Sikutaka kufanya hivyo tena, kwa hivyo nilimwomba na kumwita Mungu moyoni mwangu. Nilikumbuka ushirika mmoja wa Mungu wakati huo. Baada ya Mungu kumtaka Adamu awape majina viumbe wote wenye uhai, Mungu alitwaa majina hayo na kuwapa viumbe hao wenye uhai. Maneno ya Mungu yanasema, “Mungu Alimpa binadamu werevu naye binadamu akautumia werevu wake aliopewa na Mungu kufanya mambo. Kama kile binadamu anafanya ni kizuri machoni mwa Mungu, basi kinathibitishwa, kutambulika, na kukubalika na Mungu bila ya utathmini au upinzani wowote. Hili ni jambo ambalo hakuna mtu wala roho wa maovu, wala Shetani, anaweza kufanya. Je, mnauona ufunuo wa tabia ya Mungu hapa. Je, mwanadamu, mwanadamu aliyepotoshwa, au Shetani anaweza kuwakubali wengine kuwawakilisha katika kufanya mambo huku wakitazama? Bila shaka la! Je, wanaweza kupigania cheo na yule mtu mwingine au nguvu nyingine ambayo ni tofauti na wao? Bila shaka wangefanya hivyo! Na kwa muda huo, kama angekuwa ni mtu aliyepotoshwa au Shetani aliyekuwa na Adamu, bila shaka wangekataa kile ambacho Adamu alikuwa akifanya. Ili kuthibitisha kwamba wanao uwezo wa kufikiria kwa uhuru na wanayo maono yao binafsi na ya kipekee, wangekataa kabisa kila kitu alichofanya Adamu: ‘Unataka kukiita hivyo? Kwa kweli, sitakiita hivyo, nitakiita hivi; ulikiita Tom lakini mimi nitakiita Harry. Lazima nionyeshe ustadi wangu.’ Haya ni aina gani ya asili? Hii ni asili ya kiburi kisicho na mipaka? Lakini Mungu anayo tabia kama hii? Je, Mungu alikuwa na upinzani wowote usiokuwa wa kawaida kwa mambo haya ambayo Adamu alifanya? Jibu ni bila shaka la! Kati ya tabia ambayo Mungu anafichua, hakuna hata chembe ya ubishi, ya kiburi, au kujigamba kwa nafsi. Hilo liko wazi kabisa hapa” (Neno Laonekana katika Mwili). Niliguswa sana nilipokuwa nikitafakari maneno ya Mungu. Adamu aliwapa majina viumbe wote wenye uhai na Mungu akakubali kile ambacho Adamu alikuwa amefanya bila kubadilisha chochote. Mwanadamu hutumia akili aliyopewa na Mungu kufanya vitu vizuri na Mungu hukubali vitu hivi na haingilii. Niliona kwamba Mungu ni mnyenyekevu na Aliyejificha na kwamba Hajionyeshi hata kidogo. Kiini cha Mungu ni kizuri na chema! Hata hivyo, mimi ambaye ni duni kuliko funza, nilikuwa tu mwenye kiburi na majivuno na nilishaua ukuu wangu. Nilitaka kila mara kuitawala timu na kuwalazimisha wengine wafanye kile nilichosema—sikuwa na aibu! Kwa mintarafu ya yale yaliyokuwa tu yametokea sasa, niliona waziwazi kwamba maoni ya Dada Zhang yalistahili zaidi kuliko yangu, lakini bado nilitaka kuyapuuza na kumlazimisha afanye kile nilichotaka. Sikuwa kabisa na hisia kutokana na kiburi changu! Nilipofikiria haya, nilijichukia na nilitaka kujizaba makofi machache makali. Nilimwomba Mungu kimyakimya, nikisema jinsi nilivyotaka kujiachia na kufanya yale ambayo dada yangu alipendekeza. Kwa hivyo niliwaambia hao kina dada wengine, “Mawazo ya Dada Zhang yanastahili na ni bora kuliko yangu. Hebu tufanye yale anayopendekeza.” Wale kina Dada wengine walikubali nilichosema. Tulihariri makala hayo baadaye na chini ya mwongozo wa Mungu, kazi ilienda kwa utaratibu na ikamalizika baadaye kidogo. Sote tulihisi uhuru mkubwa. Dada wawili walinena nami baadaye, wakisema, “Umebadilika. Hushikilii mawazo yako mwenyewe sana na unaweza kukubali mapendekezo ya wengine.” Nilipowasikia wakisema haya, nilimshukuru Mungu kwa dhati!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Kila Neno la Mungu ni Maonyesho ya Tabia Yake

Ni sasa tu ninapoelewa kwamba kama napenda kuielewa tabia ya Mungu, ni lazima nijaribu kwa bidii kuelewa na kutafuta ukweli ndani ya kila sentensi ya Mungu. Kwa njia hii, hakika nitafaidika sana. Kuanzia leo kwendelea, natamani kuzingatia kuweka juhudi nyingi zaidi katika maneno ya Mungu, na kutafuta hivi karibuni kuwa mtu ambaye ana ufahamu kiasi wa Mungu.

Maneno ya Mungu Yameniamsha

Kwa sababu ya kutoa nuru kwa maneno ya Mungu, nimeamka kutoka kwa dhana na mawazo yangu, nikigundua kwamba mimi si mtu ambaye yuko tayari kukubali kuadibu na hukumu ya Mungu. Kumenifanya pia nione ya kwamba niko katika ukingo wa hatari.