Nimepata Makazi ya Kweli

28/12/2019

Na Yangyang, Marekani

Nilipokuwa mwenye umri wa miaka mitatu, baba yangu alifariki. Wakati huo, mama yangu alikuwa tu amemzaa kaka yangu mdogo, na bibi yangu, kutokana na ushirikina, alisema kwamba mama yangu na kakangu mdogo ndio waliosababisha kifo cha baba yangu. Kutokana na kukosa chaguo bora, mama alilazimika kumpeleka kakangu mdogo nyumbani kwa baba yake ili aishi, kwa hivyo tangu mwanzoni mwa kumbukumbu zangu za zamani sana nilikuwa nikiishi pamoja na babu na bibi yangu. Ingawa babu na bibi yangu walinitendea vizuri, bado nilihisi mpweke na nilitaka sana kuwa pamoja na mama yangu na kakangu mdogo. Nilitamani sana aina ile ile ya upendo wa mama ambayo watoto wengine walipokea. Kwa kweli, kile nilichokuwa nikitaka hakikupita mipaka—nilichotaka tu ni familia ya kweli, mama ambaye alinipenda sana, ambaye angeweza kushiriki nami hisia zake za kweli. Lakini hata ombi hili dogo liligeuka kuwa tumaini la kupita kiasi, kwani niliweza tu kumuona mama yangu mwishoni mwa wiki. Kila nilipokuwa na shida shuleni, mama hakuwahi kuwa karibu name pia; nilikuwa kama jani la nyasi kando ya barabara ambalo halikumpendeza mtu yeyote. Baada ya muda, nilijidhalilisha sana, nilihifadhi kila kitu moyoni mwangu na sikuweza kuchukua hatua ya kuingiliana na wengine. Nilipokuwa mwenye umri wa miaka 16, watu wengine katika kijiji changu walienda ughaibuni kwa ajili ya kazi, na nilitamanishwa na wazo hilo. Niliwaza moyoni: Hali yangu nyumbani si nzuri sana. Nikienda ughaibuni, basi naweza kupata riziki yangu mwenyewe, na hata kuipa familia yangu mapato yangu kiasi. Kwa njia hiyo ningeweza kusaidia familia yangu kuishi vizuri kiasi.

Mnamo Agosti mwaka wa 2000, nilikuja Marekani kufanikiwa peke yangu. Hapa Marekani, ningeamka asubuhi na mapema na kufanya kazi mchana kutwa hadi usiku mkuu, na hakukuwa na mtu kando yangu ambaye ningeweza kushiriki naye mawazo yangu. Nilishikilia kuwa shupavu kwa nje, lakini kwa ndani, nilihisi mpweke na mwenye ukiwa sana. Wakati wowote nilipohisi hivi, niliikosa sana familia yangu, na nilitamani hata zaidi kuweza kuwa na familia yenye furaha.

Nilipokuwa na umri wa miaka 21, nilipata kumjua mume wangu nilipokuwa nikifanya kazi kwenye mkahawa. Alikuwa mtu mzuri na aliyewapenda sana wazazi wake, kwa hivyo nilikuwa na maoni mazuri juu yake. Wakati mmoja, nilitengua mguu wangu kwa kuotokuwa mwangalifu, na kwa mshangao wangu, aliacha kazi yake ili kunitunza, jambo ambalo lilinifanya niguswe sana. Nilianza kumtegemea polepole. Mnamo Aprili mwaka wa 2008, tulifunga ndoa. Nilihisi kama kwamba nilikuwa nimempata mtu ambaye ningemwaminia maisha yangu, na mwishowe nilihisi kana kwamba nilikuwa na familia yangu mwenyewe. Nilihisi furaha sana moyoni mwangu, na kile nilichokuwa nimetarajia kwa miaka mingi mwishowe kilikuwa kimetimia. Baada ya kufunga ndoa, mimi na dada ya mume wangu tulishirikiana ili kuanzisha kampuni ya vifaa vya ujenzi, lakini kwa kuwa mimi pekee katika familia yetu ndiye niliyeelewa Kiingereza, kampuni nzima ilikuwa ikiendelezwa tu na mimi. Nilikuwa nikimtunza kila mtu katika familia yangu na kusimamia kampuni hiyo. Kupitia miaka kadhaa ya kujitahidi sana, sio tu kwamba niliweza kumsaidia mume wangu kulipa madeni yake ya zamani, lakini pia niliweza kukusanya akiba kiasi kwa ajili ya familia yangu. Hapo awali, nilidhani kwamba juhudi zangu zingenifanya nipate kuheshimiwa na familia ya mume wangu, lakini hali halisi ilikuja kama dharau. Mara tu biashara ilipoanza kupata mafanikio kiasi, tulipanga kupata mtoto, lakini sikuweza kuwa mjamzito. Kwa hivyo nilikunywa dawa nyingi na kuwatembelea madaktari wengi, lakini sikuweza kuwa na tumaini hata kidogo. Mume wangu alikuwa mtoto wa kiume wa kwanza katika familia yake, na wazazi wake na jamaa wengine walisikitishwa sana nasi kwa sababu hatukuwa tumewapa mjukuu. Huku akikabili shinikizo la aina hii, mtazamo wa mume wangu kwangu pia ulibadilika sana. Wakiiga hilo, kila mtu katika familia ya mume wangu basi akabadilisha mitazamo yake kwangu. Dada mkubwa wa mume wangu mara nyingi alisema mambo ili kunitenga, na hata alipotosha ukweli ili kusema mambo mabaya kunihusu mbele ya mume wangu. Nilihisi kwamba nilikuwa nimekosewa, kwa hivyo nilimwambia mume wangu jinsi nilivyokuwa nikihisi. Sio tu kwamba hakuwa na huruma kwangu, lakini wakati mwingine alinipigia kelele vilevile, jambo ambalo lilinifanya nihisi uchungu hata zaidi na kukosewa. Baadaye, tulienda hospitalini kwa sababu ya uchunguzi mwingine, na hatimaye tukagundua kwamba kwa kweli ni mume wangu aliyekuwa na tatizo. Lakini hii haikuwa ya maana tena, kwa sababu baada ya miaka kadhaa ya ugomvi, uhusiano wetu ulikuwa umeanza kuharibika. Kuanzia mwanzoni mwa mwaka wa 2012, mume wangu alikuwa akirudi China mara nyingi kutembelea madaktari na kutekeleza biashara, huku akija tu nyumbani mara moja kila baada ya miezi sita. Kila wakati aliporudi, ilikuwa tu ili kuchukua pesa, akiniambia kuwa kampuni aliyokuwa akiendesha nchini China ilihitaji ufadhili wa kutosheleza gharama zake, lakini hakunijali kabisa. Kwa njia hii tulikuwa pamoja kwa zaidi ya miaka mitatu kwa shida, na uhusiano wetu uliharibika zaidi.

Mnamo Septemba mwaka wa 2015, tuliishia mwishowe kutangua ndoa. Kilichonisononesha zaidi ni kwamba, tulipokuwa tukigawanya mali yetu, mume wangu alivuka mipaka kiasi cha kumwambia wakili anilazimishe nitie saini mkataba uliosema kwamba, mahakama isingeidhinisha talaka yetu, basi ningelazimika kumpa mali yangu yote kabla ya wiki moja kuisha. Wakili mwingine alinifanya nifikirie jambo hilo kwa uangalifu: Ikiwa ningetia saini mkataba huu, jambo hilo lingekuwa hasara sana kwangu, na akasema kwamba angeweza kunisaidia kuandika mkataba ambao ungenipa masurufu. Kuona mume wangu akiwa hasimu sana na asiye na huruma kulinifanya niishiwe na hamu kabisa. Kuanzia kwanza kupendana hadi kuolewa, kwa karibu muongo mmoja nilimpa mume wangu na familia hii kila kitu, kitu ambacho hakuna kiasi cha pesa au mali kinachoweza kulinganishwa nacho. Lakini sasa, kwa sababu mume wangu hakuweza kunipa mimba, yeye na familia yake walinilaumu, na wakageukia kuwa wasio na huruma kwangu, bila kuzingatia hata kidogo hisia zangu. Nilichopata kama malipo ya kile nilichowekeza kilikuwa maumivu mengi na mahangaiko ya moyo. Nilihisi mchovu. Sikutaka lolote lililohusiana na familia hii tena. Nilitaka tu kuondoka katika makazi haya haraka iwezekanavyo na kwenda mbali sana na watu hawa ambao walikuwa wameniumiza sana. Kwa hivyo, bila kusita hata kidogo, nilitia saini ya jina langu.

Baada ya talaka yangu, nilihisi kutojiweza kabisa. Sikujua ni nani ambaye ningeweza kumwamini, na sikujua ni nani ambaye ningeweza kwenda kwake kushiriki naye hisia zangu. Kila nilipofikiria juu ya ndoa yangu iliyokosa kufaulu, ilinifanya niwe na huzuni na simanzi sana. Nilichunguza tena nafsi yangu ya sasa. Ili kupata mtoto, nilikuwa nimekunywa dawa nyingi sana zilizokuwa na homoni kiasi kwamba nilikuwa nimeongeza nusu ya uzito wangu wa awali. Niliogopa sana kwamba wengine wangeniona sasa nikitaabika, katika hali hii ngumu ambayo nilikuwamo ndani yake. Kwa nje, nilijifanya kuwa hodari, lakini moyoni mwangu nilihisi dhaifu mno. Kweli nilitamani sana siku ambayo ningeweza kuishi maisha ambayo roho yangu ingeweza kuwekwa huru. Ni wakati huu ndipo nilianza kuwa na hamu ya kumwamini Mungu.

Muda mfupi baada ya hili, nilikutana na Carmen siku moja nilipokuwa katika duka la ununuzi akinunua nguo. Alikuwa na shauku kubwa ya kunisaidia, na tukabadilishana nambari za simu. Baadaye, niliona ujumbe ambao alichapisha kwenye WeChat, na nikagundua kuwa alikuwa Mkristo. Carmen mara nyingi alishiriki nami upendo wa Mungu kwa mwanadamu, na nilihisi kuguswa sana moyoni mwangu. Niligundua polepole kuwa mimi, ambaye siku zote nilikuwa msiri sana, nilikuwa tayari kutoa hisia zangu na kuingiliana na watu wengine. Mimi na Carmen tulipopata kujuana, mateso yote ambayo nilikuwa nimehisi moyoni mwangu hii miaka mingi iliyopita yalitoka. Carmen alielewa sana mateso yangu, na alishiriki nami uzoefu uliofanana na huo ambao alikuwa amepitia. Nilihisi kuwa nilikuwa nimekutana na mtu aliyejali kwa kweli, na jambo hilo lilitia moyo wangu ukunjufu. Siku moja, Carmen alinialika nyumbani kwa dada mwingine ambapo nilikutana na Ndugu Kevin na dada wengine kadhaa kutoka Kanisa la Mwenyezi Mungu. Nilipokuwa nao, nilihisi kuwa walikuwa tofauti sana na watu ambao nilikuwa nimekutana nao hapo zamani. Kila nilipokuwa na watu wengine, hata kama walikuwa jamaa au marafiki zangu, nilihisi kana kwamba sikueleweka kwa hakika nilipotoa hizia zangu kwao. Badala yake, niliona wasiwasi kuwa bahati zangu mbaya zingedhihakiwa nao, kwa hivyo sikutaka kushiriki na mtu yeyote hisia zangu. Hata hivyo, nilipokuwa na Carmen na hawa wengine, nilihisi mtulivu sana, kwani wote waliweza kuelewa mateso yangu, na pia walishiriki nami uzoefu wao wenyewe. Sikuwahi kufikiria jinsi ambavyo ningeweza kutoa hisia zangu kwa dhati na kuzungumza na watu wote waliokuwa hapa mara ya kwanza nilipokutana nao na jinsi ambavyo sote tulishiriki uzoefu wetu sisi kwa sisi. Nilihisi kama kwamba ndugu hawa walinichukulia kama jamaa kuliko jinsi familia yangu ilivyonichukulia, jambo ambalo sikuwahi kufurahia hapo awali katika maisha yangu yote ulimwenguni humu kwa miongo kadhaa iliyopita, na lilinifanya nihisi kuguswa sana ndani yangu.

Baadaye, sote tulikutana ili kutazama Hadithi ya Xiaozhen kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu, na moyo wangu ulisismuliwa. Hadithi iliyokuwa katika filamu hiyo ilikuwa kweli kabisa: Alipokuwa mtoto, mhusika mkuu aliyekuwa katika filamu hiyo alicheza na marafiki zake pasipo ubaya kabisa, lakini mara walipokua na kuanza kuwa na masilahi yaliyopingana, mioyo ya watu wote ilianza kubadilika. Walianza kupangiana njama, na hata wakawa maadui na kupigana. Hakukuwa na mapenzi tena au urafiki wowote hata kidogo. Sikuwa na budi kufikiria miaka hiyo yote ambayo mimi na mume wangu tulijitahidi pamoja. Hata hivyo, kwa sababu hatukuweza kupata mtoto, uhusiano wetu ulivunjika, na mwishowe mume wangu kwa kweli alishindania kila senti kutoka kwangu ilipofika wakati wa kugawa mali yetu. Ilinifanya nifikiri kuhusu jinsi watu walivyo wabaya sana; wakati wowote maslahi yao yanapokuwa hatarini, hisia zote husahaulika. Kwa bahati nzuri, mhusika mkuu katika filamu hiyo anampata Mungu mwishowe, na kurudi kwa familia ya Mungu, ambapo Mungu anakuwa Yule wa pekee ambaye anaweza kumtegemea, na yeye hayuko mpweke tena, wala haendelei kuhisi kuwa na shaka na kutojiweza. Nilihisi kuguswa sana baada ya kuona haya, macho yangu yakijawa na machozi. Niliwaza moyoni: “Xiaozhen aliporudi kwa Mungu, alivua barakoa ambayo alikuwa amevaa ili kuendelea kuishi; aliishi katika uwepo wa Mungu kwa kweli, akapokea wokovu Wake, na akaweza kuishi maisha yenye ukombozi na uhuru. Mwenyezi Mungu hakika ataniokoa pia, ili niweze kuishi kwa furaha kama Xiaozhen.” Katika filamu hiyo, nilimsikia Mwenyezi Mungu akisema: “Wanadamu, baada ya kuuwacha utoaji wa uzima kutoka kwa Mwenye uweza, hawajui azma ya kuishi, lakini hata hivyo wanaogopa kifo. Hawana usaidizi wala msaada, lakini bado wanasita kufumba macho yao, na wanajitayarisha kuendeleza uwepo wa aibu ulimwenguni humu, magunia ya miili wasio na hisia za roho zao wenyewe. Unaishi hivi, bila matumaini, kama vile wafanyavyo wengine, bila lengo. Kuna aliye Mtakatifu tu katika hekaya atakayekuja kuwaokoa watu ambao, wakiwa wanapiga kite katika mateso yao, wanatamani sana kufika Kwake. Hadi sasa, imani hii haijafikiwa kwa wale ambao hawana fahamu. Hata hivyo, watu bado wanaitaka sana. Mwenye uweza ana rehema kwa watu hawa ambao wameteseka sana. Wakati uo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na fahamu, maana imembidi Asubiri sana kupata jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kutafuta, kuutafuta moyo wako na roho yako, kukuletea chakula na maji na kukuzindua, ili usione kiu na kuhisi njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo utarudisha ghafla kumbukumbu yako: ukitambua ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, lakini wakati fulani usiojulikana ukapoteza mwelekeo wako, wakati fulani usiojulikana ukaanguka barabarani ukiwa hujitambui na tena wakati fulani usiojulikana ukampata ‘baba.’ Isitoshe, unagundua kuwa Mwenye uweza amekuwa hapo muda huo wote, akiangalia, akisubiri kurejea kwako, kwa muda mrefu sana” (“Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusikia maneno haya, ilikuwa kana kwamba mama yangu alikuwa akiniita, na ilionekana kana kwamba nilikuwa nimerudi upande wa mama yangu, ambapo nilihisi ukunjufu usio na kifani moyoni mwangu. Ilitukia kwamba, Mungu alikuwa kando yangu siku zote akinilinda, Akingojea kurudi kwangu. Sikuwa tena peke yangu. Mungu alijua hali yangu iliyokuwa mbaya na mahitaji yangu. Wakati wangu wa shida zaidi, roho yangu ilipouma zaidi, kupitia ndugu hawa kunihubiria injili, Alinirudisha ndani ya nyumba ya Mungu, ambapo nilipokea wokovu wa Mungu na kufurahia upendo ambao Mungu anao kwangu. Wakati huo, nilihisi kama mtoto aliyepotea ambaye hatimaye alikuwa amepata makazi, ambaye alikuwa ameipata familia yake, na nilihisi sana furaha ya kweli!

Baada ya haya, nilianza kuishi maisha ya kanisa na, kupitia kusoma neno la Mwenyezi Mungu, nilihisi kuwa nilikuwa nimepata kitu ambacho ningeweza kukitegemea kabisa, na kwamba sasa nilikuwa na kusudi na mwelekeo katika maisha yangu. Hata hivyo, kwa kuwa nilielewa kidogo sana juu ya ukweli, kila nilipofikiri kuhusu ndoa yangu iliyokosa kufaulu, bado ningehisi maumivu moyoni mwangu. Nilichukia jinsi familia ya mume wangu ilivyonitendea, na kila wakati nilipofikiria juu ya jambo hilo, nilipata maumivu makali. Kwa hivyo, nilimwomba Mungu juu ya shida zangu, na nilitoa hisia zangu kwa ndugu na kushiriki nao kuhusu matatizo yangu, nikitafuta ukweli ili kuyatatua. Wakati mmoja, Ndugu Kevin alishiriki nami kifungu hiki cha maneno ya Mwenyezi Mungu: “Mwanadamu ametembea katika enzi hizi tofauti pamoja na Mungu, lakini bado hafahamu kwamba Mungu huongoza hatima ya mambo yote na viumbe hai au jinsi Mungu hupanga na kuelekeza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Kuhusu sababu, siyo kwa sababu matendo ya Mungu hayafahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu, kiasi ya kwamba, mwanadamu anabaki katika huduma ya Shetani wakati ule ule anapomfuata Mungu—na hata halitambui hili. Hakuna anayetafuta nyayo za Mungu kwa vitendo au kuonekana Anakoonyesha, na hakuna aliye na hiari ya kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani, yule mwovu, ili kurekebishwa kufuatana na dunia hii na kanuni za kuwepo ambazo watu waovu hufuata. Wakati huu, moyo na roho za mwanadamu hutolewa ushuru kwa shetani na kuwa riziki ya Shetani. Hata zaidi, moyo wa binadamu na roho yake zimekuwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na uwanja wake wa kuchezea unaofaa. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni za kuwa binadamu, na wa thamani na maana ya kuwepo kwa binadamu. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu, na yeye huacha kumtafuta na kumsikiza Mungu. Wakati upitavyo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu na yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu kisha huanza kupinga sheria na amri za Mungu na moyo na roho zake hufishwa…. Mungu humpoteza mwanadamu ambaye Alimuumba mwanzoni, na mwanadamu hupoteza mzizi wa mwanzo wake: Hii ndiyo huzuni ya hii jamii ya wanadamu” (“Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kisha Ndugu Kevin alishiriki juu ya hili, akiniambia: “Sababu ya maisha yetu kujaa maumivu ni kwamba sisi hukubali dhana, maoni na semi za maisha za Shetani, na kwa kuwa tumedhuriwa na kupotoshwa na Shetani. Kwa kweli, wanadamu wamepotoshwa na Shetani kwa maelfu ya miaka. Kwa muda mrefu sasa, tumezoea vitu vyote ambavyo Shetani hutia ndani yetu polepole. Sisi hutegemea sheria za Shetani za kuendelea kudumu ili kuishi, zikitufanya tupuuze vyote isipokuwa faida zetu wenyewe, tuwe wenye ubinafsi, duni na wasio na dhamiri. Familia ya mume wako wa awali iliweza kukutendea jinsi walivyokutendea kwa sababu wao pia walidhibitiwa na fikira za kikabaila kama vile ‘Endeleza ukoo wa mababu wa mtu,’ ‘Kuna njia tatu za kukosa mapenzi ya mtoto kwa wazazi, kutokuwa na wana wa kiume ndiyo mbaya zaidi,’ na ‘Walee watoto ili utunzwe uzeeni’ ambazo zilikuwa zimetiwa ndani yao polepole na Shetani. Na mumeo alipokuwa akigawa mali yenu, hakuzingatia hata kidogo miaka yako yote ya kuwa pamoja kama mume na mke na hili pia lilikuwa yeye kuathiriwa na kudhibitiwa na sheria za kuendelea kuishi kama vile ‘Pesa ni kitu cha kwanza’ na ‘Mbingu huwaangamiza wale ambao hawajiwakilishi’ na akawa mbinafsi na asiyejali. Kwa sababu ya kupotoshwa na Shetani, watu hawawezi kuelewana kabisa, na hakuna furaha hata kidogo maishani mwetu. Mateso yote tunayopitia husababishwa na mateso ya Shetani. Familia zetu zote huteswa na Shetani vile vile, jamii yote ya binadamu inamilikiwa na Shetani, na haiwezi kufanya lolote kuhusiana na kudhuriwa na Shetani. Kwa hivyo, bila mwongozo wa Mungu, watu ambao wanaishi kulingana na falsafa na semi za Shetani wanaishi maisha ambayo hayana furaha ya kweli. Tunachohitaji sana maishani mwetu si utajiri wa kidunia au upendo wa familia zetu, lakini badala yake ni wokovu wa Mungu. Tunachohitaji ni kupata ruzuku ya neno la Mungu. Ni Mungu pekee anayeweza kutuongoza tuachane na upotovu na mateso ya Shetani, na kurudisha dhamiri na mantiki yetu, Akituwezesha kuishi kama watu wa kweli na kupata uhuru na ukombozi.” Baada ya kusikiliza ushirika wa Ndugu Kevin, ghafla niligundua: Kwa hivyo si mimi tu ambaye nimeishi kwa uchungu, lakini badala yake jamii nzima ya wanadamu imedanganywa na Shetani na kupotoshwa na Shetani, na sote tunapambana kwa maumivu. Watu wanaweza kujitenga na mateso ya Shetani, na kushinda mateso haya kwa kuja tu mbele za Mungu na kukubali wokovu wa Mungu. Hii ndiyo njia pekee ya kupata furaha na uhuru. Mara nilipoelewa hili, akili yangu ilihisi kutokuwa na shaka, na nilihisi kukombolewa kabisa.

Mara nilipofahamu sababu asili ya mwanadamu kuishi kwa uchungu, niligundua kuwa chuki kati yangu na familia ya mume wangu wa zamani ilikuwa imesababishwa na mateso ya Shetani, na nilikuwa tayari hata kujaribu kuwasamehe na kuacha kuwa na kisasi dhidi yao. dhidi yao. Nilipoanza kutia neno la Mungu kwenye vitendo, nilihisi furaha zaidi moyoni mwangu. Siku moja mnamo Agosti mwaka wa 2016, nilikutana na mume wangu wa zamani mtaani. Tulisalimiana na nilihisi waziwazi moyoni mwangu kuwa sikumchukia tena, kwa sababu nilijua kwamba alikuwa ameishi na mateso ya Shetani, kwamba alikuwa amedanganywa na kuteswa na Shetani. Kama ningekuwa na fursa, ningeeneza injili ya Mungu ya siku za mwisho kwake, ili yeye pia aweze kuja mbele za Mungu na kupokea wokovu wa Muumba. Wakati huo, nilihisi kuwa Mungu kwa kweli ni wa kupendeka sana, na kwamba neno la Mungu ni ukweli. Almradi tuje mbele za Mungu na kupokea wokovu Wake, basi tunaweza kujikomboa toka kwa vifungo vya Shetani na kupata uhuru na ukombozi, na kuishi maisha ya furaha na baraka.

Kila wakati ninapotazama video ya densi na wimbo iitwayo Furaha Katika Nchi ya Kanaani, mimi huhisi furaha sana, na ninahisi kama kwamba maneno ya wimbo huu yanaeleza vizuri kabisa jinsi ninavyohisi: “Nimerudi kwa familia ya Mungu, mchangamfu na mwenye furaha. Mikono yangu imemshika mpendwa wangu, moyo wangu ni miliki Yake. Japo nimepitia Bonde la Machozi, nimeyaona mapenzi ya Mungu. Mapenzi yangu kwa Mungu hukua siku baada ya siku, Mungu ndiye chanzo cha furaha yangu. Nikiduwazwa na uzuri wa Mungu, moyo wangu umeshikizwa kwa Mungu. Siwezi kumpenda Mungu vya kutosha, nyimbo za sifa huchemka moyoni mwangu.” Ninapokumbuka njia ambayo nimefuata, bila kujali nilichopitia njiani, Mungu alikuwa kando yangu siku zote akinilinda na, mwishowe, Aliniongoza nirudi ndani ya familia Yake. Sasa, kila siku ninafurahia kunyunyiziwa na kukimiwa na neno la Mwenyezi Mungu. Maumivu ambayo nilihisi ndani yangu yametoweka, na nimepata mwelekeo katika maisha yangu na kupata uhuru na furaha ya kweli. Shukrani kwa Mungu kwa kuniokoa. Nitajitahidi kufuatilia ukweli na kutimiza wajibu wangu kama kiumbe kadiri niwezavyo ili kulipisha upendo wa Mungu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Nimepata Furaha ya Kweli

Na Zhang Hua, Kambodia Nilizaliwa katika familia ya kawaida ya ukulima. Ingawa familia yangu haikuwa tajiri, baba na mama yangu walipendana...

Niliupata Mwanga wa Kweli

Bila kufahamu, chini ya uongozo wa maneno ya Mungu, nikaanza pia kutafuta mabadiliko katika tabia yangu na kuona vitu kulingana na maneno ya Mungu; pia nilikuwa na ufahamu wa na nilijua jinsi ya kutofautisha asili mbaya ya mkondo wa jamii na taratibu na njia ambazo Shetani humdanganyia mtu.