Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Tabia ya Mungu ni Haki na, Hata Zaidi, Upendo

16

Fang Xin, Beijing

Agosti 15, mwaka wa 2012

Tangu mwaka wa 2007, nilipoikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, ingawa nimeonekana juu juu kuwa na kazi nyingi sana kutekeleza majukumu yangu, sijaupa moyo wangu kwa Mungu, na mara nyingi nimehisi kufungwa kiasi cha msongo wa pumzi na masuala madogo ya familia. Kila wakati ninapowaza kuhusu ukweli kwamba binti yangu tayari ana umri wa miaka thelathini, na angali bado hajapata mwenzi wa kufaa, mimi hulalamika kwa Mungu; mwanangu wa kiume hujali tu kuhusu kujifurahisha, na licha ya kutokuwa na mapato yoyote, yeye hutumia pesa kwa ubadhirifu, kwa hiyo mimi hulalamika; na mme wangu mzee huenda kazini, lakini msimamizi wake huwa hamlipi–na mimi hulalamika kuhusu hili pia …. Mimi hulalamika kwa pande zote, na mara nyingi humwelewa Mungu visivyo. Inaonekana kama kwamba Mungu amekuwa wa kutonifanyia haki mno. Matokeo yake, nimekuwa nikiishi katika giza na mateso. Hata hivyo, sijajua kwamba ni lazima nimtafute Mungu, na nimekuwa mjinga kwa kina kuhusu jinsi hali yangu ni ya hatari. Nimejitahidi tu bila msaada katikati ya mateso yangu. Hata hivyo, Mungu anajua hali yangu kikamilifu. Yeye hutumia mbinu za kipekee kuniita na kuniokoa, Akinisababisha niamke kutoka kwa ndoto na kuyatoroka madhara na mateso ya Shetani.

Mnamo Agosti 1, mwaka wa 2012, mvua ilikuwa hasa nzito sana. Kiwango cha maji katika mto kilipanda kwa haraka, na kilikuwa tayari kimefika juu ya daraja. Kilikuwa kinaenda mbele wimbi baada ya wimbi, na hali ilikuwa ya kuogofya sana. Nilipokuwa tayari kuendesha skuta yangu ya umeme kupitia daraja lililokuwa limezamishwa, tairi yangu ya mbele ilikuwa imelifikia tu na nilikuwa nikifikiri juu ya kugandamiza nguvu ya mtambo ili kusonga mbele wakati, kwa mshangao wangu, maji yalikuwa ya kina sana na mawimbi juu sana. Kabla sijaonyesha hisia, skuta yangu–pamoja nami juu yake–ilizolewa na mkondo. Nilikuwa karibu tu kupiga ukelele, “Mwenyezi Mungu!” Kabla ya maneno haya yangeweza kutoka mdomoni mwangu, hata hivyo, maji yaliingia ndani ya kinywa changu, na nilikuwa nikigogomoa funda baada ya funda la maji. Wakati huo nilielewa ndani ya moyo wangu, na nilijua wazi akilini mwangu, kwamba hii ilikuwa hatima yangu ya mwisho. Nilikuwa naelekea kufa hapa. Maji yaliendelea kuingia kinywani mwangu, na nilijitahidi kumwita Mungu lakini sikuweza. Ghafla, nilikuwa na fursa. Nilitazama juu, uso wangu ukipenya uso wa maji, na wakati huo hatimaye niliweza kupiga ukelele kwa sauti ilyopwelea, “Mwenyezi Mungu, niokoe!” Punde baadaye, kama jani katika mkondo, nilijihisi kuelea dhidi ya mti mkubwa. Mara moja nilinyosha mikono yangu nje, nikaukumbatia mti ule, na niliweza kusimama. Wakati huu nilijihisi kusisimka hasa. Singejizuia kumwomba Mungu: “Mungu! Ilikuwa Wewe uliyeniokoa. Kutokana uchafu wangu na upotovu, Umeyang’oa maisha haya yangu kutoka kwa ukingo wa kifo na kunirudisha. Napenda kukupa Wewe shukrani zangu na sifa.”

Wakati huo tu, nilipokuwa nikishikilia ule mti na kutazama kuelekea mtoni, nilishangaa kuona kwamba licha ya jinsi mawimbi yalivyokuwa makubwa na jinsi mkondo ulivyokuwa na nguvu, Mungu alikuwa amesababisha maji kunisukuma kwa upande mwingine, akiniacha katika eneo la takribani mita mia moja kutoka daraja lililokuwa limezamishwa. Mungu amejaa maajabu sana! Nilichukua muda wa kujiimarisha, na kisha nikajivuta kwa shida kuelekea pwani na kupanda ukingoni. Kisha nikatazama kuelekea mtoni, nikitarajia kuona ambako skuta yangu ya umeme ilikokuwa imeishia, lakini sikuweza kuipata. Yote niliyoweza kuona yalikuwa ni mawimbi yaliyokuwa yakipanda na kushuka, meusi yakitapakaa na kupita.

Nilipofika nyumbani na kulala juu ya kitanda changu, mandhari ya kufyonzwa na maji kuteremka mto na mkondo mkubwa yaliendelea kucheza akilini mwangu. Nikamshukuru Mungu kwa kuniokoa wakati huu wa hatari, na sikufikiri juu ya mambo mengine. Siku moja, nilisoma kitu ambacho kimeandikwa katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingilia Katika Maisha: “Ikiwa unaamini maneno ya Mungu, ‘Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi,’ basi utakuwa na imani. ‘Bila kujali muktadha ni upi, mimi nitamtii Mungu, nitamridhisha Mungu, nitakuwa shahidi, hili ni muhimu kuliko yote.’ Kama una imani hii hakuna haja ya kulichunguza. Unapaswa kuwa shahidi moja kwa moja, kumridhisha Mungu moja kwa moja, na kuweka ukweli katika matendo; huwezi kumtelekeza Mungu.” Ghafla nilijua kwamba ilikuwa ni nia njema za Mungu kwa maafa ya siku hiyo kunipata. Sio tu kuwa Alikuwa Ameyatumia ili kuniruhusu nipate uzoefu na kutambua matendo yenye nguvu zote ya Mungu katika mafuriko hayo, lakini pia Alikuwa Ametumia maafa haya ili kunitakasa na kunibadilisha. Niliwaza kuhusu jinsi nilivyokuwa nimetumia maisha yangu kulalamika kwa Mungu kwa ajili ya watoto wangu na mume wangu, na kimyakimya nilikuwa nimempinga Yeye; kama ningekuwa nimezolewa na mafuriko wakati huo, basi “ningeachia huru” kabisa watoto wangu, mume wangu, na mali yangu yote. Kwa kukabiliwa na maafa, si vitu hivi vyote vilikuwa bure kabisa? Mungu alikuwa ametumia maafa hayo kunizindua kwa matumaini kwamba ningeweza kuaminia kaya yangu yote kwa Mungu, na kutumia muda zaidi kufanya liwezekanalo kutafuta ukweli na wokovu. Huu ulikuwa ndio upendo ambao Mungu alikuwa nao kwangu. Kama maafa hayo hayangekuwa yamenifika, nisingekuwa nimechukua hatua ya kuja mbele ya Mungu, sembuse labda kurudi kwa Mungu. Kama Mungu alivyosema, “Inapokuja kwa hali ya maisha ya mwanadamu, mwanadamu bado hajapata maisha halisi, yeye bado hajaona kupita katika udhalimu, ukiwa, na hali duni ya dunia—na hivyo, kama haingekuwa ujio wa maafa, watu wengi bado wangekumbatia hali halisi ya dunia, na bado wangejishughulisha katika ladha ya ‘uzima.’ Je, hii si hali halisi ya dunia? Je, hii si sauti ya wokovu Ninayonena kwa mwanadamu? Kwa nini, miongoni mwa wanadamu, hakuna kamwe aliyenipenda kwa kweli? Ni kwa nini mwanadamu ananipenda tu katikati ya kuadibu na majaribu, lakini hakuna mwanadamu Anayenipenda chini ya ulinzi Wangu? Mimi Nimetoa kuadibu Kwangu mara nyingi juu ya mwanadamu. Wao wanaiangalia, kisha wanaipuuza, na hawawezi kujifunza na kutafakari juu yake kwa wakati huu, na hivyo yote yanayokuja juu ya mwanadamu ni hukumu isiyo na huruma. Hii ni mojawapo tu ya mbinu Zangu za kazi, lakini bado ni kwa ajili ya kumbadili mwanadamu na kumfanya aweze kunipenda” (“Tamko la Ishirini na Tisa” wa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika mwili). Tabia ya Mungu ni haki na, hata zaidi, upendo. Bila kujali Yeye hufanya nini, ni wokovu kwangu; ni kuniruhusu kumjua Yeye, kumtii Yeye, na kumpenda. Sasa, baada ya kupata uzoefu wa kazi ya Mungu na kufurahia ukarimu Wake, matumaini yangu tu ni kufanya liwezekanalo ili kutimiza majukumu yangu kama kiumbe kilichoumbwa ili kuulipa upendo wa Mungu, ili kuuridhisha moyo wa Mungu, na kutenda sehemu yangu katika kueneza injili ya ufalme wa Mungu.

Maudhui Yanayohusiana

 • Upendo wa Mungu ni wa Kweli Kabisa

  Katika siku za nyuma sikuweza kufungua kinywa changu kuhubiri, sikuthubutu kuzungumza. Kwa njia ya uzoefu huu mimi sitarudi nyuma tena; niko tayari kuweka jitihada zote kuchukua uzoefu wangu na kushuhudia. Kwa kuwa niliona na kupata uzoefu wa wokovu wa Mungu na upendo Wake wa kweli na halisi zaidi katika jaribio la maafa, ninawezaje kukosa kuwa na ushuhuda Kwake?

 • Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu

  Tungependa kuusema ukweli huu ulioshuhudiwa na macho yetu kwa kila mtu: Mungu ndiye msingi wa pekee wa kuwepo kwetu. Utukufu wote, utajiri, umaarufu na bahati katika dunia ni wa kupita kama mawingu ya muda mfupi. Wakati ambapo maji ya mafuriko yaliyameza maisha ya ubinadamu, maisha ya mwanadamu yalikuwa yasiyo ya maana sana na yalikuwa dhaifu. Hata watu matajiri na maarufu sana hawakuwa na nguvu. Tulipoomba msaada, ni Mungu peke yake angeweza kunyosha mkono wa wokovu, na kuwavuta wale wanaomwamini kwa kweli kutoka kwa poromoko la kifo.

 • Wakati wa Uzoefu Mmoja Niliona Ulinzi wa Mungu

  Kweli, wakati wa uzoefu huu, niliona kwa kweli Mungu akitutunza na kutulinda. Baada ya nyumba yetu kuchomeka, kama si kwa Mungu kuwahamasisha watu kadhaa kuja na kuuzima moto huo, basi kuitegemea nguvu za familia yetu peke yake hakungekuwa njia ya kuuzima moto. Upepo ulipokuwa ukisukuma moto chini kwelekea sehemu kuu ya nyumba yetu, kama si kwa Mungu kutumia nguvu Zake kuu kubadili mwelekeo wa upepo, basi vitabu vya kanisa, nafaka zetu na nyumba yetu yote ingekuwa imeteketezwa. Wakati mume wangu alipoukabili moto bila woga ili kuwaokoa nguruwe, kama haingekuwa ulinzi wa Mungu, chini ya ukali wa moto mkubwa kama huo ingewezekana kabisa kuwa mume wangu angechomeka hadi kufa, hangeweza kutoka nje tu bila kuumia hata unywele mmoja kichwani mwake. Tulivyozidi kuwasiliana kwa karibu, ndivyo tulivyozidi kuona nguvu kubwa ya Mungu na upendo. Hatukulalamika u, lakini mioyo yetu ilijaa shukrani isiyo na kikomo kwa Mungu.

 • Kupitia Utunzaji wa Uangalifu wa Mungu wa Wokovu wa Mwanadamu katika Maafa

  Kwa njia ya uzoefu huu nilielewa kweli kwamba Mungu hushusha maafa sio kuwaangamiza wanadamu lakini kuathiri wokovu wao. Kwa upande mmoja, Yeye hutupa tahadhari, watoto tulio vipofu na waasi ambao humwamini Yeye lakini bado tuko shingo upande na humdanganya na kumsaliti Yeye. Kwa upande mwingine, ni zaidi kuziokoa roho zote fukara ambazo kwanza zilikuwa Zake lakini bado zinaishi chini ya utawala wa Shetani. Njia hii ya wokovu ina utunzaji mwingi wa uangalifu wa Mungu.