Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ulinzi Bora Zaidi wa Mungu kwa Wanadamu

12

Mji wa Kuiqian Rizhao, Mkoa wa Shandong

Kituo changu katika maisha, au hadhi, kilikuwa kitu ambacho sikuweza kamwe kukiachilia, na wakati Mungu alitengeneza mazingira yaliyonifichua, nilikuwa hasi, nikilalamika, na kukata tamaa tu. Ni kwa njia ya kusafishwa baada ya kusafishwa tu nilipopata kuelewa nia nzuri za Mungu, na kwamba kunijaribu Kwake hakukuwa kwa nia ya kunitesa. Badala yake, kulikuwa ni kunitakasa na kunifanya kuwa mkamilifu, kuniruhusu nielewe kwamba kuamini katika Mungu kwa ajili ya kituo kunaweza tu kuniangamiza, hivyo kuniruhusu mimi kuyaachilia maoni yasiyofaa ya kufuatilia, na kuwa na lengo sahihi la kufuata.

Baada ya kuhudumu kama kiongozi katika kanisa kwa muda kiasi, nilipandishwa cheo kuwa mshirika wa kiongozi wa wilaya. Baada ya muda mfupi, nilipandishwa cheo tena na nikaaminishwa cheo cha kiongozi wa wilaya. “Kupanda” huku kwa mfuatano kulinifanya nitie bidii hata zaidi kutekeleza wajibu wangu, nitarajie kwa hamu siku ambayo kazi hata zaidi zingeaminishwa kwangu. Tumaini hili likawa msukumo wa kufuatilia kwangu. Hata hivyo, nilipokuwa tu nikiwaza juu ya “upandaji” wangu wa hatua kwa hatua, nilibadilishwa! Wakati huo nilisetwa—nilihisi kwamba nilikuwa nimepoteza kituo changu na njia yangu ya imani kwa Mungu ilikuwa imefika mwisho wake. Nilikuwa na maumivu kiasi kwamba nilifikiria kuliacha kanisa. Hata nilifikiria kuhusu kufa. Baadaye, kupitia kupata nuru kutoka kwa maneno ya Mungu, hatua kwa hatua nilitoka kwa uhasi huo. Maneno yake yalikuwa: “Milima inaposonga, je, inaweza kubadili mkondo kwa ajili ya kituo chako? Maji yanaposonga, je, yanaweza kukoma tu kabla ya kufikia kituo chako? Je, mbingu na dunia zinaweza kubadilishwa na kituo chako?” (“Tamko la Ishirini na Mbili” katika Neno Laonekana katika Mwili). Wakati huo, ingawa nilitambua kwamba kutamani kwangu hadhi kulikuwa na ushawishi mkubwa na kwamba imani katika Mungu haipaswi kuwa ufuatiliaji wa hadhi, sikuwa na ufahamu wowote wa kweli kujihusu: na nilijiwazia: mimi sitafuatilia hadhi tena; bila kujali ni kazi gani nimepangiwa, nitatii na hivyo ndivyo. Baadaye, kanisa lilinipangia kuhubiri injili na kuwatunza waumini wapya. Nilikubali yote haya. Kwa hiyo, niliamini kwamba nilikuwa nimeachilia hamu yangu ya hadhi.

Baada ya muda mfupi, nilihama kutoka kuwatunza waumini wapya na kuwa tena kiongozi wa kanisa. Wakati huo, hiyo hamu ndani sana ya moyo wangu ya “kurudi” ilikuwa inasisimka. Chini ya utawala wa tamaa hiyo, niliweka kila kitu kwa kuringa, nikitumaini kwamba uongozi ungeona “mabadiliko” yangu. Ilipofika wakati wa kugawa wilaya za kanisa, singejizuia kufikiri: Wakati huu huenda wakaniruhusu kuwa mshirika wa kiongozi wa wilaya. Hata hivyo, mpango wa Mungu kwa mara nyingine tena ulivunja ndoto yangu ya hadhi, na mimi niliishia kuwa shemasi wa ushirikiano wa kanisa jingine. Nikiwa nimekikabiliwa na uhalisi huu, nilielewa visivyo, nikalalamika, na kwa ghafla mapambano ndani ya moyo wangu yakachemka: Ee Mungu, wengine pia wana upotovu wao na hufanya makosa katika kazi zao, lakini bado wanafanya kazi kama viongozi. Nimetoa kwa kiwango sawa na watu wengine katika kila hali—mbona Mungu hanitumii? Mbona nina bahati mbaya sana? Mara nyingine tena, nilishuka katika maumivu ya kusafishwa. Katikati ya giza, ni maneno ya Mungu yaliyoniongoza: “Wewe huoni pigo baada ya pigo na kufundishwa nidhamu baada ya kufundishwa nidhamu kama ulinzi bora zaidi, bali unayaona kama uchokozi usio na busara kutoka Mbinguni au adhabu ya kufaa kwako. Wewe ni mjinga sana! … Kurudi unakoona kama katili hakujaubadilisha moyo wako kabisa, wala hakujaumiliki moyo wako. Badala yake, kumeudhuru tu. Wewe umeona tu ‘kuadibu huku katili’ kama adui yako katika maisha haya lakini hujapata chochote. Wewe ni wa kujidai sana! Wewe huamini mara chache kwamba unapitia aina hizi za majaribio kwa sababu wewe ni mwenye kustahili dharau sana, badala yake, wewe huamini kwamba ni wa bahati mbaya sana na zaidi ya hayo, wewe husema kwamba Mimi kila mara Hutafuta makosa madogo madogo kwako” (“Je, Wale Wasiojifunza na Wasiojua Chochote si Wanyama tu?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalichoma moyo wangu kama upanga mkali. Ilikuwa kweli! Nyakati hizo zote za kujikwaa—sikuwa nimepata chochote kutoka kwayo. Kila wakati nilipopoteza kituo changu, nilihisi kama nilikuwa ninakaribia kufa kama kwamba kwa kupoteza kituo changu, nilikuwa nimepoteza maana ya maisha. Hadhi ilikuwa imekuwa jeraha langu la kufa. Lakini kutokana na kurudi huku kadhaa, sikuwa kwa kweli nimejielewa, na nilikuwa nimeelewa nia za dhati za Mungu kidogo hata zaidi. Sikuwa nimeelewa kwamba kujaribiwa kwangu na Mungu kulikuwa ni kwa ajili ya kuzuia kutamani kwangu hadhi, ili niweze kuwa na ufuatiliaji sahihi. Badala yake, nilimuelewa Mungu visivyo, nikalalamika, na kuamini kwamba Yeye alikuwa akinitesa kwa azma, Akijaribu kuyafanya mambo yawe magumu kwangu, na nikaamini kuwa nilikuwa sina bahati. Kwa kweli nilikuwa muhali sana, mpumbavu sana!

Baadaye, niliona katika ushirika kutoka kwa Mungu: “Hata hivyo, upotovu ndani ya asili ya binadamu ni lazima uondolewe kupit majaribu. Katika hali yoyote usiyoipita, ni katika hizi hali ambamo ni lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili ujue upotovu wako mwenyewe. … Katika hali zozote zile bado ungali mtumwa wa Shetani, katika hali zozote bado ungali na tamaa zako mwenyewe, matakwa yako mwenyewe—ni katika hali hizi ambamo unapaswa kuteseka” (“Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Kwa kuangalia maneno ya Mungu, kufikiria juu ya kusafishwa baada ya kusafishwa kulikonijia, hatimaye nilielewa nia njema za Mungu, na ningeweza kuonja upendo mkuu wa Mungu na wokovu. Ingawa nilikuwa mwenye kiburi na ujinga na sikuwa na ufahamu wa moyo wa Mungu, Yeye alifanya mazingira ili kunijaribu muda baada ya muda, Akinilazimisha, katikati ya maumivu ya kusafishwa, kutambua upotovu wangu mwenyewe, majisifu yangu mwenyewe na kuwa muhali, na kwamba hamu yangu ya hadhi ilikuwa kubwa mno. Yeye aliniongoza kuacha kutawaliwa na kituo changu, Yeye aliniongoza kutofuatilia tena hadhi. Jinsi Nilivyojaribu zaidi kulielewa, ndivyo nilivyohisi zaidi kuwa upendo wa Mungu kwangu ulikuwa mkubwa kweli, wakati nilikuwa kipofu na mjinga. Nilimwelewa visivyo na kumlaumu Mungu, na kwa kweli niliujeruhi moyo Wake. Wakati huo, mimi sikujizuia ila kumwaga machozi ya majuto na kuanguka chini mbele ya Mungu katika sala: Ee Mungu! Asante kwa upendo Wako na wokovu kwangu. Kama singepata kuadibu huku na hukumu kutoka Kwako, ningekuwa kwa njia isiyorudi ya maangamizi yangu mwenyewe kwa sababu ya kufuata kwangu hadhi. Majaribio Yako na usafishaji Wako kwangu ni ulinzi mkubwa na wokovu kwangu. Ee Mungu! Nimeelewa nia Zako nzuri kwangu, na niko radhi kuviacha vikwazo hivi vya kufuatilia ukweli, kutafuta zaidi ya mapenzi Yako katika mazingira Unayotengeneza, kuufuata ukweli, kufuata mabadiliko katika tabia, kuwa kiumbe mwangalifu sana, razini, kutoruhusu kazi Yako ndani yangu kuwa bure.