Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

09/04/2019

Na Bong, Philippines

Yaliyomo

Nataka Kuwa Tajiri

Maisha ya Kubadilisha Afya kwa Pesa

Namsikia Mungu Akiita Kwa Sauti

Maneno ya Mungu Yaniongoza Kuona Madhara ya Shetani

Napambana Kuondoa Vifungo vya Pesa na Kuja Kufahamu Mamlaka ya Mungu

Ninahisi Shukurani Kubwa kwa Ajili ya Upendo wa Mungu na Kuendelea Mbele kwenye Maisha Mapya

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Nataka Kuwa Tajiri

“Mwalimu mkuu, tafadhali mpe mwanangu fursa na kumruhusu afanye mtihani!” Macho ya mama yangu yalimsihi mwalimu mkuu alipokuwa akizungumza kwa sauti ya kutetemeka kidogo.

Bila kuonyesha hisia, mwalimu mkuu akasema, “Hapana, shule ina kanuni. Mtoto anaweza kufanya mtihani tu wakati ada ya mtihani imelipwa!”

Mama yangu alionekana mwenye kutayahari na kumsihi mwalimu mkuu, akisema, “Mwalimu mkuu, najua hili ni gumu sana kwako shuleni pia, lakini nina watoto wengi na sisi huweza kuishi kwa shida tu. Hatuwezi kwa kweli kumudu kulipa ada hii ya mtihani. Mbona nisiiandikie shule cheti cha ‘Naahidi Kulipa Deni’, umruhusu mwanangu afanye mtihani, nami nitajua jinsi ya kuwalipa haraka iwezekanavyo….”

Mwalimu mkuu alimtazama mama yangu na kuwaza kwa muda kidogo. Akionekana kana kwamba hakuwa na uchaguzi mwingi, alisema, “Sawa, vizuri!”

…………

Sitawahi kusahau wakati niliendelea kwenye shule kuu ya kati ambapo, kwa sababu familia yangu haikuweza kulipa ada ya mtihani, mama yangu alimwomba mwalimu mkuu wa shule kuniruhusu kufanya mtihani na ilimbidi kuandika cheti cha “Naahidi Kulipa Deni”. Nilihisi kuudhika sana wakati huo. Katika jamii hii ambako pesa hutawala bila kupingwa, kama huna pesa zozote basi huwezi kufanikisha chochote, na kimyakimya nikafanya azimio: Baada ya kuwa mtu mzima, nitajitahidi kuchuma pesa, kuwa tajiri na kubadili majaliwa yangu mwenyewe!

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Maisha ya Kubadilisha Afya kwa Pesa

Baada ya kuhitimu kutoka shule kuu ya kati, ili nipate kutimiza ndoto zangu haraka ilivyowezekana, nilijiandikisha kwenye shule ya ufundi na kujifunza kurekebisha magari. Nilipokuwa nikihudhuria shule hiyo, nilifanya kazi kwa bidii ili kujifunza maarifa ya kitaalamu. Wale wanafunzi wenza walipokwenda kufurahia wakati wao wa ziada mchana, bado nilikuwa hapo nikijifunza ujuzi wa mashine; kila mtu mwingine alipokuwa amelala usiku, nilikaa macho nikisoma na kujifunza kwa bidii.

Baada ya kuhitimu, nilikwenda jijini Manila ili kukuza ujuzi wangu. Kwa sababu sikuwa na washirika na hati yangu ya kuhitimu haikutoka kwa shule inayojulikana, hata hivyo, nilipoomba kazi, hakuna aliyekuwa tayari kuniajiri. Nilihisi kama sikuwa na chaguo jingine ila kwenda kufanya kazi kwa kampuni ya kurekebisha magari ya mjomba wangu. Ili kuchuma pesa zaidi, nilitengeneza magari na kumsaidia mjomba wangu kufanya hesabu zake. Nilifanya kazi kila siku kutoka macheo hadi magharibi, na mara nyingi ningekuwa bado nikifanya kazi ya ziada wakati watu wengine walipomaliza na kwenda nyumbani.

Nilipofunga ndoa, nilikuwa na watoto watatu. Sikutaka watoto wangu wawe maskini kama nilivyokuwa, na kwa hiyo nilifanya kazi kwa bidii hata zaidi. Nilifanya kazi kila siku kutoka saa moja asubuhi hadi saa moja jioni, na baada ya kazi niliendesha tuk tuk ya umeme, nikiwabeba watu kila mahali ili kuchuma pesa kiasi za ziada. Hatimaye nilirudi nyumbani karibu saa nane usiku na nililala takriban saa tatu au nne tu usiku kila usiku. Si hivyo tu, lakini nilitumia zile siku nne za likizo nilizokuwa nazo kila mwezi kufanya kazi ya pili kama dereva wa teksi ili kuchuma pesa kidogo za ziada. Ingawa tayari nilikuwa muumini wa Bwana, nilihudhuria mikutano tu nilipokuwa na wakati wa ziada wakati huo na wakati mwingine nilihisi kuwa na deni la Bwana, lakini nilipoona familia yangu haikuishi maisha mazuri, ningeanza tena kufanya kazi kwa bidii sana ili kuchuma pesa.

Baada ya miaka kadhaa ya kazi ngumu, hatimaye niliweza kununua nyumba na gari. Jambo ambalo halikuwa zuri sana, hata hivyo, lilikuwa kwamba, kwa sababu nilikuwa nimefanya kazi usiku kwa muda mrefu sana na nilikuwa nimejikaza sana, nilishikwa na shinikizo la damu. Daktari aliniambia niendee matibabu na nisifanye kazi ya kupita kadiri tena. Nikajiwazia: “Sina afya njema tena na kama siwezi kuchuma pesa zozote zaidi wakati ujao, hilo linamaanisha kwamba matumaini yangu kuwa tajiri sasa yamevunjika?” Nilipofikiria jambo hili, nilikata tamaa. Sikuwa tayari kukata tamaa hivyo, hata hivyo, kwa hiyo nilikwenda kwa matibabu na kuendelea kuchuma pesa mchana na usiku. Ni wakati tu nilipohisi mgonjwa kimwili nilipolazimika kukaa nyumbani na kutotoa gari nje. Lakini kila wakati nilipopumzika, niliona kwamba ningechuma pesa kidogo na basi singekuwa radhi kupumzika, na kwa hiyo ningevumilia ugonjwa wangu na kuendelea kuendesha gari. Mwishowe, ugonjwa wangu ukawa mbaya zaidi na nilikuwa dhaifu sana kiasi kwamba sikuweza tena kufanya kazi. Sikuwa na chaguo wakati huo ila kuacha kazi na kupumzika, na kutegemea kutumia dawa ili kujiendeleza kuishi …

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Namsikia Mungu Akiita Kwa Sauti

Siku moja mwezi wa Juni, mwaka wa 2016, Mchungaji Jess na mkewe walikuja kutuona. Wakasema kuwa Bwana Yesu alikuwa amekwisha kurudi, na kwamba alikuwa akitekeleza hatua mpya ya kazi. Walisema kwamba Yesu alikuwa ametekeleza kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema na kwamba, ingawa dhambi zetu zilikuwa zimesamehewa na Bwana, kwa sababu tulikuwa tumepotoshwa sana na Shetani, asili yetu ya dhambi na ya kishetani ilikuwa imebakia dhabiti ndani yetu. Walisema chini ya utawala wa asili yetu ya dhambi, mara nyingi tuliweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu, na tulifungwa na kubanwa na dhambi. Kutokana na mahitaji yetu kama wanadamu wapotovu, katika siku za mwisho Mungu kwa mara nyingine alikuwa Amepata mwili ili kutekeleza hatua moja ya kazi ya kumhukumu na kumtakasa mwanadamu kwa maneno, na hatua hii ya kazi ilikuwa ikitekelezwa kwa msingi wa kazi ya ukombozi. Mungu alikuwa Amekuja kutuokoa kabisa kutoka kwenye vifungo vya dhambi, na hili kabisa lilikuwa utimilifu wa unabii wa BibliaLazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

Niliposikia ushirika wa Mchungaji Jess, moyo wangu ulihisi kuguswa sana. Nilifikiria jinsi, licha ya kuwa nimemwamini Bwana kwa miaka mingi, sikuwa nimewahi kuondoa vifungo ya dhambi, lakini bado nilikuwa nikifuata mielekeo ya kijamii na kufuatilia maisha ya anasa za mwili…. Mara chache, ningejihisi kuwa na deni la Bwana, lakini sikuweza hasa kujidhibiti—kwa kweli nilikuwa na dhambi iliyokuwa dhabiti ndani yangu! Kadiri niliyosikiliza, ndivyo nilvyozidi kuhisi kuwa ushirika wa Mchungaji Jess ulitoka kwa Mungu, na kwa hiyo nikaamua kumsikiliza kwa dhati. Mchungaji Jess baadaye alinitolea ushuhuda kuhusu kazi ya Bwana Yesu aliyerudi—Mwenyezi Mungu—na alitupa ushirika juu ya vipengele vya ukweli kama vile hatua tatu za kazi ya Mungu kuwaokoa wanadamu, siri ya kupata mwili, jinsi Mungu hutekeleza kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho ili kumtakasa na kumbadili mwanadamu na jinsi Mungu huamua hatima ya mwisho ya wanadamu. Nikawa na hakika kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi, na mke wangu na mimi tukakubali kwa furaha kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho.

Mara tu baada ya mimi kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, kwa shauku nilihudhuria mikutano, ningesoma maneno ya Mungu wakati wowote nilipopata fursa, nilijihisi kuwa karibu sana na Mungu na hali ya roho yangu ikawa bora zaidi na zaidi. Lakini baada ya muda mfupi, nilipoona kwamba familia yangu ilihitaji pesa kwa ajili ya vitu vingi sana, nilifikiri ilinilazimu nianze kuchuma pesa kwa haraka. Haingefaa kutokuwa na pesa, hivyo nikaanza kufanya kazi kwa bidii mara nyingine tena. Wakati mwingine, kazi ilikinzana na mikutano yangu ya kanisa na ningechagua kuchuma pesa badala yake, na hivyo nilihudhuria mikutano bila taratibu tu. Mke wangu na ndugu zangu katika kanisa walinipa ushirika mara nyingi, wakisema kuwa kazi ya siku za mwisho ilikuwa hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu. Ilitulazimu tulenge kufuatilia ukweli, walisema, raha za kimwili hazikuwa na thamani, kwamba ilitosha kuwa na chakula na mavazi, na kwamba ilikuwa sawa kufanya kazi saa za kawaida tu. Walinisihi sana nisifuatilie utajiri na raha za kimwili sana kiasi kwamba singekuwa hata na wakati wa kuhudhuria mikutano, kwa kuwa hivyo huenda ningepoteza fursa yangu ya kupata ukweli. Lakini moyo wangu ulikuwa tayari umetwaliwa na fedha na sikuzingatia kabisa yale ndugu zangu waliyoyasema; niliendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuchuma pesa.

Baadaye, nilifanya kazi kwa kampuni ya mjomba wangu wakati wa mchana na kuendesha teksi yangu usiku ili nichume pesa kidogo za ziada. Mwezi mmoja ulipita kwa njia hii, kisha miezi miwili, kisha mitatu…. Ili kuchuma pesa, daima nilikuwa nikisukumiza na kuharakisha. Katika wakati huu, teksi yangu ingekuwa na shida karibu kila siku, lakini sikuwahi kumwomba Mungu au kuingia ndani ya roho yangu kwa ajili ya kujitafakari mwenyewe ili kugundua sababu ni nini. Wakati mmoja baadaye, nilikuwa nakaribia tu kutoka na teksi yangu wakati injini iliharibika. Nikifikiri kwamba kuharibika kwa aina hiyo hakungeweza kutengenezwa kwa haraka, nilirudi nyumbani. Nilipokuwa nikitembea kwelekea nyumbani, sikuweza kujizuia kushangaa: “Tangu nilipoanza kujishughulisha sana kuchuma pesa, sijahudhuria mikutano ya mara kwa mara, na ninahisi kama ninajitenga zaidi na zaidi na Mungu. Kila siku, kichwa changu kinajazwa na mawazo ya jinsi ya kuchuma pesa zaidi na jinsi ya kuishi maisha mazuri zaidi. Sijawahi kufikiria jinsi ninavyoweza kuhudhuria mikutano au jinsi ninavyoweza kusoma maneno ya Mungu zaidi na kuuelewa ukweli zaidi. Injini ya gari langu imeharibika ghafla leo—inaweza kuwa kwamba mapenzi mazuri ya Mungu yamesababisha hili?”

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Maneno ya Mungu Yaniongoza Kuona Madhara ya Shetani

Baada ya kufika nyumbani, niliona kuwa mke wangu hakuwa hapo, hivyo nikaenda kanisani kumtafuta. Nilitukia tu kukutana na dada wawili na, walipopata habari kwamba gari langu lilikuwa na tatizo nalo, walifanya ushirika nami, wakisema, “Ndugu, wewe ni Mkristo, na wakati unapokumbana na masuala unapaswa kuyapokea kutoka kwa Mungu! Daima umekuwa ukifanya kazi kwa bidii ili uchume pesa kwa muda sasa, hujahudhuria mikutano mara kwa mara na moyo wako unajitenga zaidi na zaidi na Mungu. Gari lako limeharibika leo na mapenzi ya Mungu yamesababisha hili. Unapaswa kutuliza moyo wako na kutafuta kwa bidii. Fikiria kwa uangalifu: Pesa huchumwa tu kwa sababu tunataka kuzichuma? Kwa kweli tuna uwezo wa kudhibiti majaliwa yetu wenyewe? Kama tunayaelewa maswali haya, basi tutajua ni mtazamo upi wa kuchukua kwa pesa.” Kisha wakaniomba kusoma kifungu cha maneno ya Mungu: “Majaliwa ya mwanadamu yanadhibitiwa na mikono ya Mungu. Wewe huna uwezo wa kujidhibiti mwenyewe: Licha ya mwanadamu yeye mwenyewe daima kukimbilia na kujishughulisha, anabakia bila uwezo wa kujidhibiti. Kama ungejua matarajio yako mwenyewe, kama ungeweza kudhibiti majaliwa yako mwenyewe, ingekuwa wewe bado ni kiumbe?” (“Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baada ya kusoma kifungu hiki, hawa dada basi walinipa ushirika kuhusu kipengele cha ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya majaliwa ya wanadamu. Baada ya kusikiliza jambo hili, nilihisi kujazwa kila aina ya hisia tofauti: “Ndiyo,” niliwaza. “Sisi wanadamu ni viumbe wa Mungu, na majaliwa yetu yanatawaliwa na kudhibitiwa na Mungu. Mungu pia huamua kabla kiasi cha pesa tunachoweza kuchuma maishani mwetu, lakini sikutambua ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya majaliwa ya wanadamu, lakini badala yake kwa lengo moja tu nilichuma pesa kwa kazi yangu mwenyewe ya bidii, na kujifanya kuwa tajiri, nikijaribu kubadili majaliwa yangu mwenyewe na kujitahidi kujiweka huru kutoka kwa utawala wa Mungu—kwa kweli mimi ni mwasi na mpumbavu sana!” Baada ya kufikia utambuzi huu, niliwaambia wale dada, “Tangu nilipoacha kuhudhuria mikutano mara kwa mara ili nichume pesa, nimetumia pesa zote ambazo nimechuma nikiendesha teksi yangu kwa kurekebisha gari lenyewe. Wakati huu, pesa nitakazolazimika kutumia kununua injini mpya zitakuwa ndizo pesa zote nilizochuma nikiendesha gari langu kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Hili limenifanya kwa hakika nije kutambua kwamba kwa kweli hatuwezi kudhibiti majaliwa yetu wenyewe, na iwapo ninaishi kama masikini au tajiri au ni kiasi gani cha pesa nilicho nacho haiamuliwi tu kwa jitihada zangu za mtu mmoja, lakini badala yake huamuliwa na ukuu wa Mungu. Mungu anatumia suala la injini ya gari langu kuharibika leo ili kunibembeleza nirudi mbele Yake, kunifanya ntambue ukuu Wake na ili kwamba nisipambane tena peke yangu. Ni lazima nijifunze jinsi ya kumtii Mungu na kufanya kufuatilia ukweli kuwa kipaumbele changu. Jambo sahihi tu la kufanya ni kuaminisha kuchuma pesa mikononi mwa Mungu!”

Baada ya kusikia nikisema hili, mmoja kati ya dada hao akasema, “Mungu ashukuriwe! Ndugu, kwamba unaweza kupata ufahamu wa aina hiyo wa jambo hili ni kwa uongozi wa Mungu! Lakini ikiwa tunataka kuwa huru kabisa dhidi ya utumwa ambao pesa hutuathiria, ni lazima tuwe na utambuzi kuhusu njia na hila za udanganyifu ambazo Shetani hutumia ili kutumia pesa kutupotosha na kutudhuru, ni lazima tupate ufahamu kamili wa uovu na ubaya wa Shetani na tuelewe juhudi za uangalifu ambazo Mungu hutumia kutuokoa. Hebu tusome kifungu kingine cha maneno ya Mungu kinachohusu kipengele hiki.” Alipokuwa akisema haya, huyo dada akanisomea kifungu kimoja cha maneno ya Mungu: “‘Pesa inaifanya dunia izunguke’ ni falsafa ya Shetani, na inaenea miongoni mwa wanadamu wote, katika kila jamii ya binadamu. Mnaweza kusema kwamba ni mwenendo kwa sababu umewekwa ndani ya moyo wa kila mtu. Tangu mwanzo kabisa, watu hawakuukubali msemo huu, lakini kisha waliukubali bila kusema walipokutana na maisha halisi, na wakaanza kuhisi kwamba maneno haya kweli yalikuwa ya kweli. Je, huu si mchakato wa Shetani kumpotosha mwanadamu? … Hivyo baada ya Shetani kutumia mwenendo huu kuwapotosha watu, unaonyeshwa vipi kwao? Hamhisi kwamba hamtaishi katika dunia hii bila pesa yoyote, kwamba hata siku moja haiwezekani? Hadhi ya watu inatokana na kiasi cha pesa wako nayo na pia heshima yao. Migongo ya maskini imekunjwa kwa aibu, ilhali matajiri wanafurahia hadhi zao za juu. Wanatenda kwa njia ya kujigamba na wana majivuno, wakiongea kwa sauti kubwa na kuishi kwa kiburi. Msemo na mwenendo huu unaleta nini kwa watu? Si watu wengi wanaona kupata pesa kunastahili gharama yoyote? Si watu wengi hutoa Heshima na uadilifu wao wakitafuta pesa zaidi? Si watu wengi hupoteza fursa ya kufanya wajibu wao na kumfuata Mungu kwa sababu ya pesa? Si hii ni hasara kwa watu? (Ndiyo.) Si Shetani ni mbaya kutumia mbinu hii na msemo huu kumpotosha mwanadamu kwa kiwango kama hicho? Si hii ni hila yenye kijicho? Unaposonga kutoka kuukataa huu msemo maarufu hadi mwishowe kuukubali kama ukweli, moyo wako unaanguka kabisa chini ya mshiko wa Shetani, na hivyo unakuja kuishi naye bila kusudi. Msemo huu umekuathiri kwa kiwango kipi? Unaweza kujua njia ya ukweli, na unaweza kujuua ukweli, lakini huna nguvu ya kuufuatilia. Unaweza kujua kwa hakika kwamba maneno ya Mungu ni ukweli, lakini huko radhi kulipa gharama au kuteseka ili kupata ukweli. Badala yake, kwako, ni afadhali utoe siku zako za baadaye na kudura yako kwenda kinyume na Mungu hadi mwisho kabisa. Licha ya kile Mungu anasema, licha ya kile Mungu anafanya, licha ya kiasi unagundua kwamba upendo wa Mungu kwako ni wa kina na mkubwa, bado ungeendelea kwa njia hiyo kwa ukaidi na kulipa gharama ya msemo huu. Hiyo ni kusema huu msemo tayari unadhibiti tabia na fikira zako, na unaona afadhali hatima yako idhibitiwe na msemo huu kuliko kuyatoa yote. Watu wanafanya hivi, wanadhibitiwa na msemo huu na kutawaliwa nao. Hii si athari ya Shetani kumpotosha mwanadamu? Hii si filosofia na tabia potovu ya Shetani ikikita mizizi kwa moyo wako? Ukifanya hivyo, si Shetani amefikia lengo lake? (Ndiyo.)” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Baada ya kusoma kifungu hiki, huyo dada alitoa ushirika, akisema, “Maneno ya Mungu yanazungumza kwa dhahiri juu ya chanzo asili cha sababu ya sisi kutii utumwa wa pesa, na hutuambia athari kubwa zinazotungoja tukifuatilia pesa. Baada ya wanadamu kushawishiwa na kupotoshwa na Shetani, Shetani alitumia aina zote za falsafa na semi kama vile ‘Pesa ni kitu cha kwanza,’ ‘Pesa siyo kila kitu, lakini bila hiyo, huwezi kufanya chochote,’ ‘Mtu hufa kwa ajili ya fedha; ndege hufa kwa ajili ya chakula’ na ‘Pesa ni muhimu sana ulimwenguni’ kutudanganya na kutupotosha. Baada ya kukubali falsafa na semi hizi, sisi huona pesa kuwa muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote, tukiamini kwamba tunaweza tu kupata mahali pa usalama katika jamii ikiwa tuna pesa, na kisha tutafurahia maisha ya utajiri. Kwa hiyo sisi hupambana na kujitahidi na kufanya kazi kwa bidii ya ajabu sana ili kuchuma pesa, na tunakuwa na tamaa zaidi na zaidi. Tunapokuwa na pesa, sisi hutaka pesa zaidi, na bila sisi kujua tunazidi kuwa watumwa wa pesa. Sisi hutumia muda wetu wote kuchuma pesa, sisi huharibu afya yetu ya mwili, na huwa hatufuatilii njia ya kweli hata tunapojua vizuri kabisa kwamba ni njia ya kweli. Halafu hatujihisi tena kutaka kumwabudu Mungu au kutafuta kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Kutoka kwa hili, tunaweza kuona kwamba Shetani hutumia semi hizi mbovu za maisha ili kutupotosha na kutudhuru, kutunasa kabisa katika wavu wake, na hivyo kutufanya tukatae kuwepo kwa Mungu, kukataa ukuu wa Mungu, kumuepuka Mungu na kumsaliti Mungu, na kuwa imara chini ya udhibiti wake na kufungwa naye ili tupoteze wokovu wa Mungu—hii ndiyo nia ya msingi ya Shetani ya kuwapotosha wanadamu. Na bado hatuna ukweli na hatuwezi kubaini njama danganyifu za Shetani, lakini tunatawaliwa kabisa tu. Haya yanapoendelea, sisi huwa mbali na Mungu zaidi na zaidi, na wakati kazi ya Mungu itakapofika mwisho tutakuwa tumechelewa kujuta. Ni lazima tuitunze nafasi tuliyo nayo leo ili kuokolewa na Mungu! Ingawa Shetani hutudhuru na kutupotosha kwa njia kama hizo, Mungu yuko hapo daima, akituokoa kimya kimya. Tunaponaswa katika mtego wa pesa na hatuwezi kutoka, Mungu huizindua mioyo yetu mizito kupitia kutushughulika na kutufundisha nidhamu, kutufanya tuweze kutuliza mioyo yetu na kutafuta kuelewa mapenzi Yake. Kutoka nje, gari lako kuharibika linaonekana kama jambo baya, lakini ndani yake kumefichwa upendo na wokovu wa Mungu kwa ajili yako!”

Kupitia ufunuo wa maneno ya Mungu na ushirika wa dada yangu, hatimaye nilielewa kwamba nilikuwa nimeona fedha kama muhimu sana, kiasi kwamba nilikosa kuzingatia afya yangu mwenyewe kwa ajili ya pesa na kwamba hata nilikuwa nimemuepuka Mungu. Ilidhihirika kuwa yote haya yalikuwa matokeo ya kuwa chini ya vifungo na madhara ya semi za maisha za Shetani, na niliwaza jinsi hili lilikuwa kweli. Kwa sababu, wakati nilipokuwa mdogo, nilikuwa nimeonja uchungu wa kutokuwa na pesa na kuangaliwa kwa dharau na wengine, na nilikuwa nimekubali falsafa na semi za Shetani, kama vile “Pesa ni kitu cha kwanza,” na “Pesa siyo kila kitu, lakini bila hiyo, huwezi kufanya chochote,” nilikuwa nimeamini kwamba pesa zingeweza kutatua tatizo lolote na nilikuwa nimefanya azimio kuwa tajiri, na hivyo, bila kujali jinsi kazi yangu ilivyokuwa ngumu au ya kuchosha kiasi gani, sikujali hata kidogo, hata kama ningepoteza afya yangu mwenyewe. Hasa, baada ya kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, nilijua kwamba Mungu alikuwa akionyesha maneno Yake na kufanya kazi Yake ya hukumu ili kumtakasa na kumbadili mwanadamu, na hatimaye kumwongoza mwanadamu kwenye hatima yake mazuri. Pia nilijua kwamba hatua hii ya kazi ilikuwa hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu kuwaokoa wanadamu, na kwamba ilikuwa muhimu sana kwetu kupata wokovu. Na bado sikuwa nimeutunza wokovu wa Mungu, lakini nilikuwa nimewazia kupata pesa zaidi tu na kuwa na vitu vizuri vya kufurahia, na hatimaye sikuweza kuhudhuria mikutano mara kwa mara ili kumwabudu Mungu, na moyo wangu ukawa mbali na Mungu zaidi na zaidi. Wakati huu, Mungu alikuwa amenisaidia kupitia ndugu wa kiume na wa kike, na Alikuwa amenipa makumbusho kupitia gari langu kuwa na shida mara nyingi, lakini sikuwa nimezingatia mapenzi ya Mungu hata kidogo, lakini nilitenda tu ari yangu mwenyewe kwa hiari na kumwasi Mungu. Je, haya yote hayakusababishwa na kutegemea semi za maisha za Shetani ili kuishi? Isingekuwa kwa injini ya gari langu kuharibika, singekuwa nimeshiriki katika kujichunguza na kutafuta mapenzi ya Mungu, na si ningekuwa basi ningepoteza fursa yangu ya kupata wokovu wa Mungu na kuishi maisha yangu yote katika majuto? Nilikuwa nimeharibiwa sana na falsafa hizo za shetani! Mungu ashukuriwe, kwa sababu ulikuwa ni mwongozo wa maneno ya Mungu ulioniwezesha kuona kuwa hizo falsafa na semi hizo zilikuwa tu uongo wa uasi uliokusudiwa kuwadanganya na kuwapotosha wanadamu, na niliona kwa dhahiri kusudi bovu la Shetani la kumpotosha mwanadamu. Kuanzia wakati huo kwendelea, sikuwa tena tayari kudanganywa au kufungwa na Shetani, lakini nilitaka kurudi mbele ya Mungu mara nyingine tena na kuhudhuria mikutano kwa dhati, kufuatilia ukweli na kumwabudu Mungu.

Baadaye, niliuratibu tena muda wangu: ningepata jioni mbili kila juma kukutana na ndugu wa kiume na wa kike ili kushiriki maneno ya Mungu na, wakati sikuhudhuria mikutano, ningetenga muda wa kusoma maneno ya Mungu na kutafakari ukweli. Baadaye, moyo wangu ulihisi utulivu na amani, uhusiano wangu na Mungu ukawa wa karibu zaidi na zaidi, na kile kilichonishangaza kweli kilikuwa kwamba ugonjwa wangu pia ulianza kupungua.

Napambana Kuondoa Vifungo vya Pesa na Kuja Kufahamu Mamlaka ya Mungu

Muda mfupi baadaye, Mungu alinijaribu. Siku moja, kanisa lilinipangia kazi ambayo ilihitaji siku kadhaa kutekeleza. Nilijua kwamba Mungu alikuwa akiniinua kwa kunipa kazi hii na kwa kweli nilitaka kuianza, lakini wakati uliohitajika kuitekeleza kazi yangu ilitukia tu kukinzana na kazi yangu. Niliwazia jinsi malipo yangu ya rehani na karo za watoto wangu vilivyopangwa, na katika siku mbili ilinibidi niwape watoto wangu karo zao. Kama singefanya kazi kwa siku chache, singekuwa na pesa za kutosha kulipia yote. Papo hapo nilihisi kama nilikuwa katika hali fulani ya kuleta mfadhaiko na sikujua cha kufanya ili niwe na matokeo mema, na hivyo nikamwomba Mungu na kumwambia matatizo yangu. Baadaye, nikasoma katika sehemu ya maneno ya Mungu “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III”: Kitu cha kwanza ambacho mtu lazima aelewe, wakati ambapo anapokanyaga guu lake hapa duniani, ni binadamu hutoka wapi, kwa nini watu wako hai, nani anayeamuru hatima ya binadamu, ni nani anayekidhi mahitaji ya binadamu, na Aliye na ukuu juu ya uwepo wa binadamu. Maarifa haya ndiyo njia ya kweli ambayo kwayo mtu huishi, msingi muhimu kwa kuwepo kwa binadamu.” “Ikiwa mtu anayaona maisha kama fursa ya kupitia ukuu wa Muumba na kujua mamlaka yake, ikiwa mtu anayaona maisha yake kama fursa nadra ya kutekeleza wajibu wake akiwa binadamu aliyeumbwa na kutimiza kazi yake maalum, basi mtu atakuwa ana mtazamo sahihi wa maisha, ataishi maisha yaliyobarikiwa na yanayoongozwa na Muumba, atatembea kwenye nuru ya Muumba, atajua ukuu wa Muumba, atakuwa katika utawala Wake, atakuwa shahidi wa matendo Yake ya kimiujiza na mamlaka Yake” (Neno Laonekana katika Mwili).

Baada ya kusoma maneno ya Mungu, nilielewa kwamba Mungu aliwaumba wanadamu na kutupa pumzi ya uzima, kwamba Yeye hutupa kila kitu tunachohitaji ili kuishi na anashikilia ukuu juu ya majaliwa yetu, na Yeye huonyesha ukweli ili kutuongoza kwenye njia sahihi katika maisha. Kama viumbe walioumbwa, tunapaswa kutekeleza wajibu wa kiumbe aliyeumbwa mbele ya Mungu ili kulipizia upendo wake, tunapaswa kupata uzoefu wa kazi Yake katika maisha yetu halisi, na kupitia na kujua mamlaka ya Mungu. Nikikumbuka ya zamani, daima nilikuwa nikitegemea tamaa zangu ovyo za makuu na jitihada za nafsi ili kutembea njia ya watu wa kidunia katika ukimbizaji wa pesa, na yote niliyojiletea yalikuwa ni maumivu, na nilipata hasara maishani mwangu. Sasa, sikuweza tena kuwa kama nilivyokuwa wakati huo wa awali—napaswa kufuatilia ukweli, nitafute mapenzi ya Mungu katika hali zilizonikabili kila siku, nitende maneno ya Mungu na kutii ukuu wa Mungu, kwa maana ni hii tu iliyokuwa njia ya kweli katika maisha na ni ukimbizaji kama huu tu ambao ungeweza kupata sifa za Mungu. Baada ya kupata ufahamu huu, nikamwomba Mungu: “Ewe Mungu! Sasa ninaelewa mapenzi Yako. Nataka kutii na kutekeleza wajibu wangu. Nataka pia kufanya azimio mbele Yako, kwamba bila kujali ni hali gani zitakazoweza kunikabili siku zijazo, daima nitatafuta ukweli kutoka ndani ya maneno Yako, nitende kulingana na matakwa Yako, nitii ukuu na mipango Yako na kutekeleza wajibu wangu kama kiumbe aliyeumbwa. Naomba kwamba Uniongoze.” Baada ya kuomba, moyo wangu ukawa mtulivu na nikaamua kuwa ningetekeleza wajibu wangu kwa dhati.

Siku mbili baadaye, mke wangu aliniambia kuwa mwana wetu alihitaji shilingi elfu saba za karo yake, kwa hiyo nilikichukua kipande cha mapambo ya vito ambacho nilikuwa nimekinunua zamani kutoka kwenye duka la rahani na kukirudisha kwenye duka hilo hilo ili kukiweka rahani. Sikutazamia kamwe meneja wa duka hili anipe shilingi 18,000 kwa kipande hicho! Lilikuwa jambo la kushangaza kwangu, kwa kuwa meneja wa duka hili la rahani wakati wowote alilipa tu kiasi kidogo cha pesa. Nilifikiri kwamba kipande hicho cha mapambo kingenipa kiasi kisichozidi shilingi 11,000 tu, lakini sasa meneja huyu kwa kweli alikuwa amenipa shilingi elfu saba zaidi ya hizo na zilitosha hasa kulipa karo ya mwanangu. Kwa kweli nilikuja kufahamu kwamba mamlaka ya Mungu yalitawala na kusimamia vitu vyote, kwamba Mungu alipanga vitu vyote kwa ajili ya maisha yetu na kwamba hatukuwa na sababu ya kuwa na wasiwasi au kujisumbua. Niliweza tu kutoa shukrani zangu na sifa kwa Mungu.

Maisha ya Kikristo: Huenda Nisiwe Tajiri, lakini Nina Bahati Sana

Ninahisi Shukurani Kubwa kwa Ajili ya Upendo wa Mungu na Kuendelea Mbele kwenye Maisha Mapya

Siku moja, nilisoma maneno haya ya Mungu: “Kile ambacho Mungu anataka kuona ni kwamba moyo wa mwanadamu unaweza kufufuliwa. Njia hizi ambazo anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu ni za kuamsha bila kikomo moyo wa mwanadamu, kuamsha roho ya mwanadamu, kumwacha mtu kujua alipotoka, ni nani anayemwongoza, kumsaidia, kumkimu, na ni nani ambaye amemruhusu mwanadamu kuishi hadi sasa; ni ya kuwacha mwanadamu kujua ni nani Muumbaji, ni nani wanapaswa kuabudu, ni njia gani wanapaswa kutembelea, na mwanadamu anapaswa kuja mbele ya Mungu kwa njia gani; yanatumika kufufua moyo wa mwanadamu polepole, ili mwanadamu ajue moyo wa Mungu, aelewe moyo wa Mungu, na aelewe utunzaji mkuu na wazo nyuma ya kazi Yake kumwokoa mwanadamu. Wakati moyo wa mwanadamu umefufuliwa, hataki tena kuishi maisha ya uasherati, tabia potovu, lakini badala yake kutaka kufuatilia ukweli kwa kuridhishwa kwa Mungu. Wakati moyo wa mwanadamu umeamshwa, anaweza basi kujinusuru kutoka kwa Shetani, kutoathiriwa tena na Shetani, kutodhibitiwa na kudanganywa na yeye. Badala yake, mwanadamu anaweza kushiriki kwa makini katika kazi ya Mungu na maneno Yake ili kuridhisha moyo wa Mungu, na hivyo kupata uchaji wa Mungu na kuepuka uovu. Hili ndilo lengo la awali la kazi ya Mungu” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI” katika Neno Laonekana katika Mwili). Ni baada tu ya uzoefu wangu nilipoelewa hatimaye kwamba Mungu alikuwa amepanga hali hizi ili kuzindua moyo wangu na roho yangu, na kunifanya kufuata njia sahihi katika maisha ya kumtii Mungu, kumcha Mungu na kuepuka maovu, na kuishi katika baraka za Mungu—hii yote ilikuwa jitihada ya bidii ya Mungu! Nilikumbuka ya zamani niliyokuwa nimepitia, kutoka kuingia katika hali ngumu na ya hatari ya pesa na kupata ugonjwa mbaya hadi kuwa na bahati ya kusikia injili ya Mungu ya siku za mwisho na kuja mbele ya Mungu, kisha mara nyingine tena kwenda katika ukimbizaji wa pesa na kunaswa katika wavu wa Shetani. Ndugu zangu wa kiume na wa kike walinipa ushirika kuhusu maneno ya Mungu, nilikuja kupata maarifa kiasi ya Mungu kuhusu ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya majaliwa ya wanadamu, na pia nilikuja kupata maarifa kiasi juu ya nia mbovu ya Shetani katika kutumia uongo wa uasi ili kuwapotosha watu, na ni hapo tu nilipoanza kuacha pesa kidogo kidogo, na nilielewa kuwa ni kutenda maneno ya Mungu na kutii ukuu wa Mungu tu iliyokuwa njia sahihi ya kufuata katika maisha…. Ili kuuzindua moyo wangu na kuniokoa dhidi ya kudhuriwa na Shetani, Mungu alinilipia thamani kubwa ya kujitahidi na Alinionyesha huruma. Kila hatua niliyochukua, iwe nilisikiliza na nilikuwa mtiifu, au iwe nilimuepuka na kumepuka Mungu, Mungu daima alitumia njia zilizofaa zaidi kuniokoa. Kwa kweli nilikuja kufahamu jinsi upendo wa Mungu ulivyo halisi na jinsi moyo wa Mungu ulivyo mzuri na mwema! Isingekuwa wokovu wa Mungu, ningekuwa bado ninaishi katika mtego wa Shetani, nikiwa nimenaswa katika kizingia cha pesa, bila kujua kabisa kile ambacho madhara ya Shetani yalikuwa yakinigeuza kuwa. Nilipokuja kwenye ufahamu huu wa upendo wa Mungu, nilithamini sana jinsi ilivyokuwa heshima ya kweli na bahati njema kwangu kuweza kuja mbele ya Mungu—Mungu alikuwa amenipa neema na kunionyesha fadhili! Nilitaka tu kutumia muda na nguvu zaidi katika siku zijazo kuhudhuria mikutano, kusoma maneno ya Mungu na kumwabudu Mungu, kujihami na ukweli zaidi, na kufanya kazi yangu vizuri kulipizia upendo wa Mungu. Mshukuru Mungu na kumsifu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Nilifurahia Karamu Kubwa

Xinwei Mkoa wa Zhejiang Juni 25 na 26, mwaka wa 2013 zilikuwa siku zisizosahaulika. Eneo letu lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na wafanyakazi wa…

Kutupa mbali Minyororo ya Shetani

Kabla ya kumwamini Mungu, bila kujali chochote nilichokuwa nikifanya, sikuwahi kutaka kubaki nyuma. Nilikuwa tayari kukubali shida yoyote ili mradi ingemaanisha ningeinuka juu ya kila mtu mwingine zaidi. Baada ya kumkubali Mungu, mtazamo wangu uliendelea kuwa sawa, kwa sababu niliamini kikamilifu msemo, “Ni kwa kupitia ugumu wa hali ya juu zaidi tu ndipo mtu anaweza kuushinda ukawaida,” na kuona mtazamo wangu kama ushahidi wa msukumo wangu. Wakati Mungu alinifichulia ukweli, hatimaye niligundua kuwa nilikuwa nikiishi chini ya pingu za Shetani, nikiishi chini ya miliki yake.