Imani na Maisha

Makala 26

Toba ya Afisa

Nilianza kuishi maisha ya kanisa, na nikagundua kuwa Kanisa la Mwenyezi Mungu lilikuwa tofauti kabisa na ulimwengu. Ndugu husoma maneno ya Mungu na hufanya ushirika juu ya ukweli. Wao hutafuta kutenda kulingana na maneno ya Mungu na ukweli, kuwa waaminifu na wanyofu, na kuwa wenye mioyo safi. Nilihisi kana kwamba nilikuwa nimekuja mahali pa utakatifu, na nilihisi uhuru na uachiliwaji ambao sikuwahi kuhisi hapo awali.