604 Kuwa na Hekima na Utii Mipangilio Yote ya Mungu

1 Mungu hataki kuwashinda watu kupitia kuadibu; Hataki kila mara kuwatawala watu kabisa. Anataka watu watii maneno Yake na kufanya kazi kwa mtindo wa nidhamu, na kupitia hili kuridhisha mapenzi Yake. Lakini watu hawana aibu na kila mara huasi dhidi Yake. Naamini kwamba ni bora zaidi kwetu kutafuta njia rahisi sana ya kumridhisha Yeye, yaani, kutii mipango Yake yote, na ikiwa utatimiza hili kwa kweli utakamilishwa. Je, hili si jambo rahisi, la kufurahisha?

2 Fuata njia unayopaswa kufuata bila kufikiria kile ambacho wengine wanasema au kufikiria sana. Je, una siku zako za baadaye na jaala yako mikononi mwako? Wewe kila mara hukimbia na kutaka kufuata njia ya kidunia, lakini mbona usitoke nje? Kwa nini wewe huyumbayumba katika njia panda kwa miaka mingi na kisha unaishia kuichagua njia hii tena? Baada ya kutangatanga kwa miaka mingi, ni kwa nini umerudi sasa katika nyumba hii ingawa hukutarajia kufanya hivyo? Je, hili ni jambo lako mwenyewe tu? Ikiwa unapanga kuondoka, ngoja tu uone ikiwa Mungu atakuruhusu, na uone vile Roho Mtakatifu atakusisimua—jionee mwenyewe.

3 Kusema kweli, hata ukipata taabu, lazima uivumilie ndani ya mkondo huu, na ikiwa kuna mateso, lazima uteseke hapa leo na huwezi kwenda penginepo. Unaliona kwa dhahiri? Ungeenda wapi? Hii ni amri ya Mungu ya usimamizi. Unafikiria haina maana kwa Mungu kuchagua kundi hili la watu? Katika kazi ya Mungu leo, Yeye hakasiriki kwa urahisi, lakini watu wakitaka kuvuruga mpango Wake Anaweza kubadilisha sura Yake mara moja na kuigeuza kutoka kuwa yenye kung’aa hadi ya kuhuzunisha. Kwa hiyo, Nakushauri kutulia na kutii mipango ya Mungu, mruhusu akufanye uwe mkamilifu. Hii ndiyo njia pekee ya kuwa mtu stadi.

Umetoholewa kutoka katika “Njia … (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 602 Asili Yako ni Potovu Sana

Inayofuata: 605 Mungu Atumai Kwamba Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwaminifu kwa Maneno Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki