Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

226 Nimeiona Haki ya Mungu

1 Baada ya kupitia hukumu mbele ya kiti cha Kristo, ghafla niliamka. Nilipokuwa mmoja wa watu wa dini, imani yangu nyingi kwa Bwana ilikuwa chafu. Ingawa niliacha kila kitu, na kufanya kazi kwa bidii kwa miaka mingi, nilikosa ufahamu wa kweli kumhusu Bwana, nilikuwa nimejaa dhana na mawazo. Nilidhani kuwa Mungu ni mwenye huruma na rehema, kwamba nilistahili kupokea neema kutoka kwa imani yangu katika Bwana. Kwa miaka, nilifuata mfano wa Paulo, kuteseka na kulipa gharama kwa ajili ya Bwana. Nilipofungwa na kupata maumivu makali kabisa, sikuwa Yuda. Yote ilikuwa kwa ajili ya kupata taji la utukufu na kupokea baraka za ufalme wa mbinguni. Katikati ya ufunuo na hukumu ya maneno ya Mungu, nilisujudu ardhini.

2 Hukumu ya maneno ya Mungu inafichua asili potovu ya wanadamu. Ingawa dhambi zetu zimesamehewa, asili yetu ya kishetani imekita mizizi sana. Licha ya kumfanyia Bwana kazi kwa bidii, tabia yangu ya kishetani hufunuliwa mara nyingi. Nina kiburi, mwenye kujivuna, nasema uwongo, ninachotaka ni kujitofautisha. Kufanya matendo madogo mazuri ni kwa ajili ya kubarikiwa tu, lakini sitendi ukweli. Kutumia rasilmali na kupitia ugumu kwa ajili ya Mungu ni kufanya biashara na Mungu. Maombi yangu kwa Mungu sio chochote ila udanganyifu, sina uchaji kwa Mungu. Ningewezaje, mchafu na mpotovu, kustahili kuishi mbele ya Mungu? Shukrani iwe kwa Mungu kwa kutoniacha; kwa kweli huu ni upendo Wake.

3 Baada ya kupitia hukumu, naona kuwa Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Mungu huamua miisho ya watu kulingana na ikiwa wana ukweli au la. Tabia ya haki ya Mungu imeonyeshwa, kwa ukamilifu wake, katikati ya hukumu Yake. Nimeionja tabia ya Mungu; ndani yake hakuna huruma tu, bali pia hukumu. Zamani, yote niliyosema na kufanya yalikuwa na tabia za kishetani. Kila siku nilimwomba Mungu na kukiri dhambi zangu, lakini sikufanya toba ya kweli. Ni hukumu ya Mungu iliyoitakasa tabia yangu potovu. Utakatifu na haki ya Mungu ni vizuri sana, vinavyostahili sifa za mwanadamu. Nitatekeleza wajibu wangu vizuri na nimpende na kumtii Mungu milele.

Iliyotangulia:Ni Mungu Ambaye Ameniokoa

Inayofuata:Siwezi Kumudu Bila Hukumu na Kuadibu kwa Mungu

Maudhui Yanayohusiana

 • Furaha Katika Nchi ya Kanaani

  1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu kuingia kati…

 • Nitampenda Mungu Milele

  1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na hasi, m…

 • Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

  Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya…

 • Umuhumi wa Maombi

  1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…