Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu)

25. Mungu anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa maelfu ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu Atabadilisha namna anavyomfahamu na mtazamo wake Kwake, ili kwamba maarifa yake juu ya Mungu yaweze kuanza upya, na hivyo moyo wake usafishwe upya na kubadilishwa. Kushughulika na nidhamu ndiyo njia, na ushindi na kufanya upya ndiyo malengo. Kuondoa mawazo ya kishirikina aliyo nayo mwanadamu kuhusu Mungu asiye dhahiri ndilo limekuwa kusudi la Mungu milele, na hivi karibuni limekuwa suala la haraka Kwake. Ni matumaini Yangu kwamba watu wote watalifikiria jambo hili zaidi. Wabadilishe jinsi kila mtu anavyopitia uzoefu ili kwamba kusudi hili la haraka la Mungu liweze kufanyika hivi karibuni na hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani iweze kuhitimishwa kwa matokeo mazuri. Onyesheni uaminifu wenu kama mnavyopaswa, na ufariji moyo wa Mungu kwa mara ya mwisho. Ni matumaini Yangu kwamba hakuna ndugu yeyote atakayekwepa jukumu hili au kulitekeleza kwa namna isiyo ya dhati.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (7)" katika Neno Laonekana katika Mwili

26. Mungu anakuja katika mwili wakati huu kwa mwaliko, na kutokana na hali ya mwanadamu. Yaani, Anakuja kumpatia mwanadamu kile kinachohitajika. Atamwezesha kila mtu, wa tabia au jamii yoyote, kuona neno la Mungu na, kutoka katika neno Lake, kuona uwepo na udhihirishaji wa Mungu na kukubali ukamilishaji wa Mungu. Neno lake litabadilisha mawazo na mitazamo ya mwanadamu ili kwamba sura ya kweli ya Mungu ikite mizizi kabisa katika moyo wa mwanadamu. Hili ndilo tamanio pekee la Mungu duniani. Haijalishi jinsi gani asili ya mwanadamu ilivyo kuu, jinsi gani asili yake ilivyo duni, au jinsi mwanadamu alivyotenda huko nyuma, Mungu hajali haya. Anatumainia tu mwanadamu kuisafisha kabisa taswira ya Mungu aliyo nayo moyoni mwake na kuijua asili ya binadamu, hivyo kuubadilisha mtazamo wa kiitikadi wa mwanadamu. Anatarajia kuwa mwanadamu ataweza kuwa na shauku ya kina kwa Mungu na kuwa na mahusiano ya milele na Yeye. Hiki ndicho Mungu anachohitaji kutoka kwa mwanadamu.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (7)" katika Neno Laonekana katika Mwili

27. Maarifa ya maelfu kadhaa ya miaka ya utamaduni wa kale na historia vimeifunga fikra na dhana na mtazamo wa mwanadamu kwa nguvu sana kiasi cha kutoweza kupenyeka na kutoweza kubadilishwa. Mwanadamu anaishi katika ngazi ya kumi na nane ya kuzimu, kana kwamba amefukuzwa na Mungu hadi kwenye jela, asiweze kuona mwanga tena. Fikra za kishirikina zimemkandamiza mwanadamu kiasi kwamba mwanadamu anaweza kupumua kwa shida sana na hivyo anakosa hewa. Hawana nguvu hata kidogo ya kupinga, kimya kimya anaendelea kuvumilia na kuvumilia…. Hakuna hata mmoja aliyewahi kujaribu kupigana au kusimama kwa ajili ya uadilifu na haki; anaishi maisha ambayo hayana tofauti na maisha ya mnyama, huku akinyanyaswa na kushambuliwa na mabwana wa ushirikina, mwaka baada ya mwaka, siku baada ya siku. Mwanadamu hajawahi kufikiria kumtafuta Mungu ili kufurahia furaha duniani. Ni kana kwamba mwanadamu amekandamizwa, kama majani ya majira ya kupukutika, yaliyonyauka na kukauka kabisa. Mwanadamu amepoteza kumbukumbu na anaishi kuzimu bila matumaini ikiwakilisha ulimwengu wa kibinadamu, akisubiri ujio wa siku ya mwisho ili kwamba aweze kuangamia pamoja na kuzimu, kana kwamba siku ya mwisho anayoitamani sana ni siku atakayofurahia pumziko la amani. Maadili ya kishirikina yameyapeleka maisha ya mwanadamu "Kuzimu," kiasi kwamba mwanadamu ana uwezo mdogo hata zaidi wa kupinga. Ukandamizaji wa aina mbalimbali ulimlazimisha mwanadamu kuzama chini kabisa Kuzimu polepole na kutanga mbali kabisa na Mungu. Sasa, Mungu amekuwa mgeni kabisa kwa mwanadamu, na mwanadamu bado anafanya haraka kumwepuka wanapokutana. Mwanadamu hamtambui na anamtenga kana kwamba mwanadamu hajawahi kumjua wala kumwona hapo mbeleni. … Maarifa ya utamaduni wa kale vimemwondoa mwanadamu kutoka katika uwepo wa Mungu kimyakimya na kumwelekeza mwanadamu kwa mfalme wa mashetani na wana wake. Vitabu Vinne na Maandiko Bora Tano vimeipeleka fikra na mawazo ya mwanadamu katika enzi nyingine ya uasi, na kumfanya mwanadamu kuendelea kuwaabudu wale walioandika Vitabu hivyo na Maandiko Bora, wakikuza zaidi mtazamo wake juu ya Mungu. Mfalme wa mashetani alimtupa Mungu nje kutoka katika moyo wa mwanadamu bila huruma bila yeye kujua, huku akifurahia kuuchukua moyo wa mwanadamu. Baada ya hapo na kuendelea mwanadamu alimiliki roho mbaya na ya uovu akiwa na sura ya mfalme wa mashetani. Alijawa na chuki juu ya Mungu, na uovu wa mfalme wa mashetani ukasambaa ndani ya mwanadamu hadi akamalizwa kabisa. Mwanadamu hakuwa na uhuru tena na hakuweza kujiondoa kutoka kwa mtego wa mfalme wa mashetani. Kwa hiyo, mwanadamu angeweza kuendelea kukaa pale tu na kufungwa, ajisalimishe kwake na kujitiisha kwake. Zamani sana, alipanda mbegu ya kutoamini kuwa kuna Mungu ndani ya moyo mchanga wa mwanadamu, akimfundisha mwanadamu dhana za uongo kama vile, "jifunze sayansi na teknolojia, tambua Vipengele Vinne vya Usasa, hakuna Mungu duniani." Si hivyo tu, alitangaza kwa kurudiarudia, "Hebu tujenge makazi mazuri sana kwa kufanya kazi kwa bidii, akiwaomba wote kujiandaa toka wakiwa watoto kuitumikia nchi yao." Mwanadamu amepelekwa mbele yake bila kujitambua, na bila kusita akajichukulia sifa (akimrejelea Mungu akiwa Amewashikilia binadamu wote katika mikono Yake). Hajawahi kuhisi aibu au kuwa na hisia yoyote ya aibu. Aidha, bila aibu aliwanyakua watu wa Mungu na kuwaweka katika nyumba yake, akirukaruka kama panya mezani na kumfanya mwanadamu amwabudu kama Mungu. Yeye ni jahili kweli! Anaropoka tuhuma hizo za kushtua, "Hakuna Mungu duniani. Upepo upo kwa ajili ya sheria za asili; mvua ni unyevunyevu unaoganda na kudondoka kwenye ardhi kama matone; tetemeko la ardhi ni mtikisiko wa uso wa ardhi kwa sababu ya mabadiliko ya jiolojia; ukame ni kwa sababu ya ukavu hewani kwa mwingiliano wa kinyuklia katika uso wa jua. Haya ni matukio ya asili. Ni sehemu gani ambayo ni tendo la Mungu?" Hata anaropoka[a] kauli pujufu kama hizi: "Mwanadamu alitokana na sokwe wa zamani, na dunia leo imeendelea kutokana najamii ya kale ya takribani miaka bilioni moja iliyopita. Ama nchi inaendelea au inaanguka inaamuliwa na mikono ya watu wake." Mwanadamu amemning'iniza ukutani miguu juu kichwa chini na kumweka mezani ili atunzwe vizuri na kuabudiwa. Anapokuwa anapiga kelele kwamba "Hakuna Mungu," anajichukulia kuwa ni Mungu, na kumsukumia mbali Mungu nje ya mipaka ya dunia bila huruma. Anasimama katika sehemu ya Mungu na kutenda kama mfalme wa mashetani. Ni upuuzi mkubwa kiasi gani! Anamsababisha mtu kuteketezwa na chuki yenye sumu. Inaonekana kwamba Mungu ni adui wake mkubwa na Mungu hapatani naye kabisa. Anafanya hila zake za kumfukuza Mungu wakati anabakia bila kuadhibiwa na huru[13]. Huyo kweli ni mfalme wa mashetani! Tunawezaje kuvumilia uwepo wake? Hatapumzika hadi awe ameisumbua kazi ya Mungu na kuiacha ikiwa imeharibika na kuwa katika hali ya shaghalabaghala kabisa[14], kana kwamba anataka kumpinga Mungu hadi mwisho, hadi samaki afe au wavu ukatike. Anampinga Mungu kwa makusudi na kusogea karibu zaidi. Sura yake ya kuchukiza ilifunuliwa kabisa toka zamani na sasa imevilia damu na kugongwagongwa[15], ipo katika hali mbaya sana, lakini bado hapunguzi hasira yake kwa Mungu, kana kwamba anatamani angemmeza Mungu kabisa kwa mara moja ili kutuliza hasira moyoni mwake. Tunawezaje kumvumilia, huyu adui wa Mungu anayechukiwa! Ni kumalizwa kwake na kuondolewa kabisa ndiko kutahitimisha matamanio yetu ya maisha. Anawezaje kuruhusiwa kuendelea kukimbia ovyo ovyo? Amemharibu mwanadamu kiasi kwamba mwanadamu hajui mahali pa raha zote, na anakuwa hafifu na ambaye hajitambui. Mwanadamu amepoteza uwezo wa kawaida wa kufikiri wa kibinadamu. Kwa nini tusitoe sadaka uhai wetu wote kumwangamiza na kumchoma na kuondoa kabisa hofu ya hatari inayobakia na kuiruhusu kazi ya Mungu kuufikia uzuri usiotarajiwa hivi karibuni? Genge hili la waovu limekuja miongoni mwa wanadamu na kusababisha hofu na msukosuko. Wamewaleta wanadamu wote katika ukingo wa jabali, wakipanga kwa siri kuwasukumia chini wavunjike vipande vipande na kuteketeza maiti zao. Wana matumaini ya kuharibu mpango wa Mungu na kushindana na Mungu katika jaribio ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda[16]. Hiyo ni rahisi kwa vyovyote vile! Msalaba umeandaliwa, mahususi kwa ajili ya mfalme wa mashetani ambaye ni mwenye hatia ya makosa maovu sana. Mungu si wa msalaba tena na Amekwishamwachia Shetani. Mungu aliibuka mshindi muda mrefu uliopita na Hahisi tena huzuni juu ya dhambi za binadamu. Ataleta wokovu kwa binadamu wote.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (7)" katika Neno Laonekana katika Mwili

28. Kutoka juu hadi chini na kuanzia mwanzo hadi mwisho, amekuwa akiisumbua kazi ya Mungu na kutenda kinyume Chake. Mazungumzo yote ya urithi wa utamaduni wa kale, maarifa ya thamani ya utamaduni wa kale, mafundisho ya imani ya Tao na imani ya Confucius, na maandiko bora ya Confucius na ibada ya kishirikina vimempeleka mwanadamu kuzimu. Sayansi na teknolojia ya kisasa, na vilevile maendeleo ya viwanda, kilimo, na biashara havionekani popote. Badala yake, anasisitiza ibada za kishirikina zilizoenezwa na "masokwe" wa kale kuingilia, kupinga na kuharibu kazi ya Mungu kwa makusudi. Hajamtesa mwanadamu hadi leo hii, bali anataka kummaliza[17] mwanadamu kabisa. Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. Kuna wachache sana ambao wako tayari kumpokea Mungu na kuukaribisha ujio wa Mungu kwa furaha. Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii; wakiwa na visu na mapanga mikononi, wanajipanga katika pambano kumwangamiza Mungu. Sanamu zimetapakaa nchi nzima ya shetani ambapo mwanadamu anafundishwa kila mara kuwa hakuna Mungu. Juu ya nchi hii kunatoka harufu mbaya sana ya karatasi inayoungua na ubani, ni harufu nzito sana inayosababisha kukosa hewa. Inaonekana kuwa ni harufu ya uchafu unaopeperuka wakati joka anapojisogeza na kujizungusha, na ni harufu ambayo lazima mwanadamu hawezi kujizuia kutapika. Licha ya hiyo, kunaweza kusikika pepo waovu wakikariri maandiko. Sauti hii inaonekana kutoka mbali kuzimu, na mwanadamu hawezi kujizua kusikia baridi ikiteremka chini ya uti wake. Katika nchi hii sanamu zimetapakaa, zikiwa na rangi zote za upinde wa mvua, ambazo zinaibadilisha nchi kuwa ulimwengu unaometameta, na mfalme wa mashetani anakenua, kana kwamba njama yake mbovu imefanikiwa. Wakati ule ule, mwanadamu hana habari kumhusu, wala mwanadamu hajui kwamba shetani amekwisha mharibu kiasi kwamba hawezi kuhisi na ameshindwa. Anatamani kumfutilia mbali Mungu mara moja, kumtukana na kumwangamiza tena, naye anajaribu kuharibu na kuvuruga kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu "kuingilia kati" kazi yake miongoni mwa wanadamu wa duniani? Anawezaje kumruhusu Mungu kuufichua uso wake wa chuki? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kati kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu, aliyejawa kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kutawala nguvu yake duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? Akiwa na roho mbaya, bado anaamini kwamba yeye ni mzuri kupita kiasi. Genge hili la washiriki jinai! Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani[18] na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu, na wamemharibu mwanadamu kiasi kwamba mwanadamu anafanana na wanyama wabaya wasioweza kuvumilika, wala hana tena hata chembe ya mwanadamu asilia mtakatifu. Hata wanatamani kutawala kama madikteta duniani. Wanakwamisha kazi ya Mungu ili kwamba isiweze kusonga mbele hata kidogo na kumfunga mwanadamu kana kwamba wapo nyuma ya kuta za shaba na chuma cha pua. Baada ya kufanya dhambi nyingi sana na kusababisha shida nyingi sana, wanawezaje kutarajia kitu chochote tofauti na kusubiri kuadibu? Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanaupinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, kwa kuwa mfalme wao amepanda kwenye kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakiwaongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi ili watikise vichwa vyao na kuchochea vurugu[19]. Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu wa wafalme wote, bila kutambua kwamba wao si chochote zaidi ya nzi juu ya kitu kilichooza. Si hivyo tu, wanatoa maoni ya kashfa dhidi ya uwepo wa Mungu kwa kuwategemea wazazi wao nguruwe na mbwa. Nzi wadogo wanadhani wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi mwenye meno[20]. Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, ilhali wazazi wao ni nguruwe na mbwa wachafu mara bilioni kuliko wao wenyewe? Bila kutambua hali yao wenyewe ya kuwa duni, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na kiburi na wanajiinua kila mahali kuhusu uzuri wao na mvuto wao wenyewe, wanamtupia mwanadamu uchafu wao kwa siri. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao wenyewe, na hivyo wanautesa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea kisa cha ndani cha ulimwengu wa kidini). Mwanadamu hajui kwamba, ingawa mbawa za nzi ni nzuri na za kupendeza, hata hivyo ni nzi mdogo tu aliyejaa uchafu na kujawa na vijidudu. Kwa kutegemea uwezo wa wazazi wao nguruwe na mbwa, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya kuungwa mkono kabisa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliozidi. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza tena kazi yao ya utesaji, wakiendeleza kazi yao ya muda wa maelfu kadhaa ya miaka. Kikundi hiki cha waliopotoka hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu hata zaidi. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Wao ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani inamfanya Mungu atoe sauti kuu, na Hawezi kujizuia kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize. Ili mwanadamu ampende Mungu ni lazima aelewe mapenzi Yake na furaha na huzuni Yake, vilevile na kile Anachokichukia zaidi. Hii itakuza zaidi kuingia kwa mwanadamu. Kadri mwanadamu anavyoingia kwa haraka, ndivyo moyo wa Mungu unavyoridhika; kadri mwanadamu anavyomtambua kwa uwazi mfalme wa mashetani, ndivyo mwanadamu anavyosogea karibu zaidi kwa Mungu, ili kwamba matamanio yake yaweze kutimizwa.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (7)" katika Neno Laonekana katika Mwili

29. Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, ubadilishwe, hivyo kuokoa roho yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na Shetani; ni ili kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu. Weka pembeni mazungumzo kuhusu jinsi maisha na uzoefu wa mwanadamu yalivyo ya kiburi au ya kina; mioyo ya watu itakapokuwa imeamshwa, watakapokuwa wameamshwa kutoka katika ndoto zao na kujua kikamilifu madhara yaliyoletwa na joka kuu jekundu, kazi ya huduma ya Mungu itakuwa imekamilika. Siku ambayo kazi ya Mungu itakuwa imekamilika ni wakati ambapo mwanadamu ataanza rasmi kutembea kwenye njia ya imani sahihi katika Mungu. Wakati huu, huduma ya Mungu itakuwa imekamilika: Kazi ya Mungu kuwa mwili itakuwa imekamilika kabisa, na mwanadamu atakuwa ameanza rasmi kufanya kazi ambayo anapaswa kufanya—atatekeleza huduma yake. Hizi ni hatua za kazi ya Mungu. Hivyo, mnapaswa kutafuta kwa kupapasa njia yenu ya kuingia katika misingi ya kuyajua mambo haya. Haya yote ndiyo mnayopaswa kuyaelewa.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (8)" katika Neno Laonekana katika Mwili

30. Kuingia kwa mwanadamu kutakuwa bora tu wakati ambapo mabadiliko yametokea ndani kabisa mwa moyo wake, maana kazi ya Mungu ni wokovu kamili wa mwanadamu—mwanadamu aliyekombolewa, ambaye bado anaishi chini ya nguvu za giza, na ambaye hajawahi kuzinduka—kutoka katika eneo hili la kusanyiko la mapepo; ni ili kwamba mwanadamu aweze kuwekwa huru dhidi ya milenia ya dhambi, na kupendwa na Mungu, kulikanyaga kabisa joka kuu jekundu, kuanzisha ufalme wa Mungu, na kuupumzisha moyo wa Mungu haraka, ni kutoa mawazo bila woga, bila kubania, kwa chuki inayowaghadibisha, kuondoa kabisa vijidudu hivyo, kuwafanya muache maisha haya ambayo hayana tofauti na maisha ya ng'ombe au farasi, ili msiwe watumwa tena, ili msiweze kukanyagwa tena au kuamrishwa na joka kuu jekundu; hamtakuwa tena wa taifa hili lililoanguka, hamtakuwa tena wa joka kuu jekundu la kuchukiza, hamtafungwa nalo tena. Kiota cha mapepo hakika kitachanwachanwa na Mungu, na mtasimama kando ya Mungu—nyinyi ni wa Mungu, na sio wa dola hii ya watumwa. Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga joka huyu mwovu wa zamani wa kuchukiza, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote; Mungu hatamhurumia hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote[21], Atamharibu kabisa.

kutoka katika "Kazi na Kuingia (8)" katika Neno Laonekana katika Mwili

31. Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanazunguka kila pembe, wakihadaa na kudanganya, wakitoa shutuma zisizokuwa na msingi[22], wakiwa wakatili na waovu, wakiukandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo imeijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa visivyo kawaida[23]. Nani awezaye kuuona ulimwengu zaidi ya anga? Shetani anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kukifunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa mashetani amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la mapepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yenye hasira, wakiogopa sana kwamba Mungu atawapata kwa ghafula na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha bila mahali pa amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamewahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa mapenzi ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili bado Amefichwa kabisa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo mashetani hawana huruma nao ni katili, inawezekanaje mfalme wa mashetani anayeua watu kwa kufumba na kufumbua, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na pia mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, na hawana hata chembe ya wema, na wanawajaribu watu wasio na hatia na kuwa watu wasio na uwezo wa kuhisi. Wahenga wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umewaacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote ni njama za kufunika dhambi! Nani ambaye ameikumbatia kazi ya Mungu? Nani ametoa maisha yake au kumwaga damu kwa ajili ya kazi ya Mungu? Kwa kizazi baada ya kizazi, kutoka kwa wazazi hadi watoto, mwanadamu aliye katika utumwa amemfanya Mungu mtumwa bila heshima—hii inawezaje kutoamsha hasira? Maelfu ya miaka ya chuki imejaa moyoni, milenia ya utendaji dhambi zimeandikwa katika moyo–inawezekanaje hii isichochee ghadhabu? Mlipize Mungu, mwondoe kabisa adui Yake, usimruhusu kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ni wakati: Mwanadamu amepata nguvu kwa muda mrefu, ametumia nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa ajili ya hili, kuuchana uso uliojificha wa pepo huyu na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kumwacha Shetani huyu wa zamani. Kwa nini kuweka kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini kutumia hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali viko wapi? Haki iko wapi? Faraja iko wapi? Wema uko wapi? Kwa nini kutumia mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini kutumia nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini asimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini kumbana Mungu hadi Anakosa mahali ya kupumzisha kichwa Chake? Wema uko wapi miongoni mwa wanadamu? Ukarimu uko wapi miongoni mwa wanadamu? Kwa nini kusababisha matamanio makubwa kiasi hicho katika Mungu? Kwa nini kumfanya Mungu kuita tena na tena? Kwa nini kumlazimisha Mungu kumhofia Mwana Wake mpendwa? Kwa nini jamii hii ya giza na mbwa walinzi wake wasimruhusu Mungu kuja bila kizuizi na kuzunguka dunia ambayo Aliiumba? Kwa nini mwanadamu haelewi, mwanadamu anayeishi katika maumivu na mateso? Mungu amevumilia mateso makubwa kwa ajili yenu, kwa maumivu makubwa Amemtoa Mwanawe wa pekee, mwili na damu Yake, kwenu—hivyo kwa nini bado hamuoni? Katika mtazamo mzima wa kila mtu, mnakataa ujio wa Mungu, na kukataa urafiki wa Mungu. Kwa nini mnakosa busara kiasi hicho? Mko tayari kuvumilia uonevu katika jamii ya giza kama hii? Kwa nini, badala ya kujaza tumbo zenu kwa milenia ya uadui, mnajishindilia "kinyesi" cha mfalme wa mashetani?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (8)" katika Neno Laonekana katika Mwili

32. Hatua za kazi ya Mungu duniani zinahusisha shida kubwa: Udhaifu wa mwanadamu, upungufu, utoto, ujinga na kila kitu cha mwanadamu—kila moja imepangwa kwa uangalifu sana na kuangaliwa kwa hadhari sana na Mungu. Mwanadamu anaonekana wa kutisha hivi kwamba hakuna mtu anayeweza kuthubutu kumtega au kumchokoza; anapoguswa tu anarudisha pigo, au vinginevyo anaanguka chini na kupoteza mwelekeo wake, na ni kana kwamba, akipoteza umakini kidogo tu, anarudia uovu tena, au anampuuza Mungu, au anakimbia kwa baba yake nguruwe au mama yake mbwa ili ajiingize mambo machafu ya mwili wake. Ni kizuizi kikubwa kiasi gani! Katika kila hatua ya kazi Yake haswa, Mungu anawekwa katika majaribio, na takribani kila hatua inaleta hatari kubwa. Maneno yake ni ya kweli na ya uaminifu, na bila uovu, lakini nani yuko tayari kuyakubali? Nani yuko tayari kutii kikamilifu? Inamhuzunisha Mungu. Anafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya mwanadamu, Anasongwa na wasiwasi kuhusu maisha ya mwanadamu, na Anauonea huruma udhaifu wa mwanadamu. Amevumilia shida nyingi katika kila hatua ya kazi Yake, kwa kuwa kila neno Analozungumza; Hajui la kufanya daima, naye hufikiria juu ya udhaifu, ukaidi, utoto wa mwanadamu, na vile alivyo hatarini … wakati wote tena na tena. Nani amewahi kujua hili? Anaweza kuwa na imani na nani? Nani angewezakufahamu? Anachukia dhambi za mwanadamu daima, na ukosefu wa ujasiri, uoga wa mwanadamu, naye anahofia hatari aliyo nayo mwanadamu, na kutafakari njia zilizopo mbele ya mwanadamu; siku zote, Anapoangalia maneno na matendo ya mwanadamu, inamfanya kuwa na huruma, hasira, na siku zote vitu hivi vinamletea maumivu moyoni Mwake. Hata hivyo, wasio na hatia wamekuwa sugu; kwa nini lazima Mungu afanye vitu kuwa vigumu kwao siku zote? Mwanadamu dhaifu ameondolewa kabisa uvumilivu; kwa nini Mungu awe na hasira isiyopungua kwa mwanadamu? Mwanadamu dhaifu na asiye na nguvu hana tena uchangamfu hata kidogo; kwa nini Mungu anamkaripia kwa ukaidi wake siku zote? Nani anayeweza kuhimili matishio ya Mungu mbinguni? Hata hivyo, mwanadamu ni dhaifu, na yupo katika dhiki sana, Mungu ameisukuma hasira Yake ndani kabisa moyoni Mwake, ili kwamba mwanadamu ajiakisi taratibu. Ilhali mwanadamu, aliye katika matatizo makubwa, hazingatii hata kidogo mapenzi ya Mungu; amekanyagwa na mfalme mzee wa mashetani, na bado haelewi kabisa, siku zote anajiweka dhidi ya Mungu, au si moto wala baridi kwa Mungu. Mungu amezungumza maneno mengi sana, lakini nani ambaye ameyazingatia? Mwanadamu haelewi maneno ya Mungu, lakini bado hashtuki, bila kuwa na shauku, na hajawahi kuelewa kabisa hulka ya Shetani wa kale. Watu wanaishi Kuzimu, jahanamu, lakini wanaamini wanaishi katika kasri lililo chini ya bahari; wanateswa na joka kuu jekundu, lakini bado wanadhani wamependelewa[24] na nchi ya joka; wanadhihakiwa na Shetani lakini wanadhani wanafurahia ustadi wa hali ya juu wa mwili. Ni wachafu na mafidhuli kiasi gani! Mwanadamu amekutana na bahati mbaya, lakini haijui, na katika jamii hii ya giza anapatwa na ajali baada ya ajali[25], lakini bado hajazinduka kutokana na jambo hili. Ni lini atakapoachana na wema wake wa kibinafsi na tabia ya mawazo ya kiutumwa? Kwa nini hajali moyo wa Mungu kiasi hicho? Je, anajifanya haoni ukandamizaji na shida hii? Je, hatamani kuwe na siku ambayo atabadilisha giza kuwa nuru? Je, hatamani zaidi kurekebisha uonevu dhidi ya haki na ukweli? Je, yuko tayari kutazama tu bila kufanya chochote watu wakitupilia mbali ukweli na kupindua ukweli? Je, anafurahia kuendelea kuvumilia matendo haya mabaya? Je, yuko radhi kuwa mtumwa? Je, yuko tayari kuangamia mkononi mwa Mungu pamoja na mali za taifa hili lililoanguka? Azma yako iko wapi? Malengo yako yako wapi? Heshima yako iko wapi? Maadili yako yako wapi? Uhuru wako uko wapi? Je, uko radhi kutoa maisha yako yote kwa ajili ya joka kuu jekundu, mfalme wa mashetani? Je, unafurahi kumwacha akutese hadi kufa? Kina chake ni vurugu na giza, watu wa kawaida, wanaoteseka na mateso kama hayo, wanaililia mbingu na kulalamikia nchi. Ni lini mwanadamu ataweza kuwa na ujasiri? Mwanadamu amekuwa kimbaumbau na amekonda, anawezaje kuridhika na Shetani huyu katili na dikteta? Kwa nini asiyatoe maisha yake kwa Mungu mapema iwezekanavyo? Kwa nini bado anayumbayumba, ni lini ataweza kumaliza kazi ya Mungu? Hivyo akiwa ameonewa na kunyanyaswa bila sababu yoyote, maisha yake yote hatimaye yatakuwa bure; kwa nini ana haraka hivyo ya kufika, na haraka hivyo ya kuondoka? Kwa nini hahifadhi kitu kizuri cha kumpa Mungu? Je, amesahau milenia ya chuki?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (8)" katika Neno Laonekana katika Mwili

33. Mungu amekuwa mwili wakati huu kufanya kazi hii, kukamilisha kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kuifunga enzi hii, kuihukumu enzi hii, kuwaokoa waliozama kabisa dhambini kutoka katika ulimwengu wa bahari ya mateso na kuwabadilisha kabisa. Wayahudi walimsulubisha Mungu msalabani, hivyo kuhitimisha safari za Mungu kwenda Uyahudi. Muda mfupi baadaye, Mungu mwenyewe Alikuja kati ya wanadamu kwa mara nyingine tena, na kuwasili kimyakimya katika nchi ya joka kuu jekundu. Kwa kweli, jumuiya ya kidini ya serikali ya Kiyahudi ilikuwa imetundika picha ya Yesu katika kuta zao kwa muda mrefu, na kwa vinywa vyao watu walilia "Bwana Yesu Kristo." Hawakujua kwamba kitambo sana Yesu alikubali amri ya Baba Yake kurudi miongoni mwa wanadamu kukamilisha hatua ya pili ya kazi Yake ambayo haijakamilika. Kwa hivyo, watu walipigwa na butwaa walipomwangalia: Alikuwa Amezaliwa katika ulimwengu ambamo enzi nyingi zilikuwa zimepita, na Alionekana miongoni mwa wanadamu kwa umbo la yule ambaye ni wa kawaida kabisa. Kwa kweli, kadiri enzi zilivyopita, mavazi Yake na umbo lote vimembadilika, kana kwamba Alikuwa Amezaliwa upya. Watu wangewezaje kujua kuwa ni Bwana Yesu Kristo Yule Aliyeshuka msalabani na Aliyefufuliwa? Hana hata chembe ya jeraha, jinsi tu Yesu hakuwa Anafanana na Yehova. Yesu wa leo Hajaathiriwa na nyakati zilizopita kwa muda mrefu. Watu wangewezaje kumjua? Watu wenye mashaka kama "Tomaso" siku zote ana mashaka kuwa ni Yesu Aliyefufuka, siku zote anataka kuona makovu ya misumari katika mikono ya Yesu kabla hajatulia; bila kuyaona, siku zote angekuwa na mashaka, na hana uwezo wa kuweka miguu yake katika ardhi na kumfuata Yesu. Maskini "Tomaso"—angewezaje kujua kuwa Yesu amekuja kufanya kazi Aliyoagizwa na Mungu Baba? Kwa nini Yesu anapaswa kuwa na makovu ya msalaba? Je, makovu ya kusulubiwa ni alama za Yesu? Amekuja kufanya kazi kwa ajili ya mapenzi ya Baba Yake; kwa nini Aje Akiwa Amevaa na kujipamba kama Myahudi wa miaka maelfu ya miaka kadhaa iliyopita? Je, umbo ambalo Mungu analichukua katika mwili linaweza kuzuia kazi ya Mungu? Je, hii ni nadharia ya nani? Kwa nini, Mungu anapofanya kazi, lazima iwe kulingana na mitazamo ya mwanadamu? Kitu pekee ambacho Mungu anapania katika kazi Yake ni ili kazi hiyo iwe na matokeo. Hafuati sheria, na hakuna kanuni katika kazi Yake–mwanadamu angewezaje kuielewa? Ingewezekanaje mitazamo ya binadamu itambue kazi ya Mungu? Hivyo ni vizuri zaidi kutulia vizuri: Msihangaike na mambo madogomadogo, na usichukulie pakubwa mambo ambayo ni mapya tu kwenu—hii itakuzuia kujitania na watu kukucheka. Umemwamini Mungu kwa miaka yote hii lakini bado humjui Mungu; hatimaye unajitumbukiza katika kuadibu, wewe, ambaye umewekwa katika "kiwango cha juu kabisa[26]," umejiweka katika madaraja ya walioadibiwa. Ni bora zaidi usitumie mbinu zako za kijanja kujigamba kuhusu hila zako; je, mtazamo wako finyu unaweza kumwelewa Mungu kweli, Anayetazama kutoka milele hadi milele? Je, uzoefu wako wa juujuu unaweza kuelewa kabisa mapenzi ya Mungu? Usiwe na majivuno. Hata hivyo, Mungu sio wa duniani—sasa inawezekanaje kazi Yake iwe kama ulivyotarajia?

kutoka katika "Kazi na Kuingia (8)" katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

13. "Anabakia bila kuadhibiwa na huru" inaonyesha kwamba shetani anapagawa na kucharuka.

14. "Shaghalabaghala kabisa" inahusu jinsi tabia ya shetani ya ukatili haivumiliki kwa watu.

15. "Imevilia damu na kugongwagongwa" inahusu sura mbaya ya kutisha ya mfalme wa pepo.

16. "Jaribio ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda" ni istiara ya mipango mibaya ya shetani yenye kudhuru kwa siri, ya uovu. Inatumiwa kwa dhihaka.

17. "Kummaliza" inahusu tabia ya kidhalimu ya mfalme wa pepo, ambaye huwaangamiza watu wote.

18. "Kigeugeu duniani" inaonyesha kwamba ikiwa mtu ni tajiri na mwenye nguvu, watu hujipendekeza naye, na kama mtu hana hela na hana nguvu, watu humpuuza. Kifungu hiki kinahusu udhalimu wa ulimwengu.

19. "Kuchochea vurugu" inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

20. "Nyangumi mwenye meno" imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

21. "Kiongozi wa uovu wote" inahusu shetani mkongwe. Kirai hiki kinaonyesha kutopenda kabisa.

22. "Wakitoa shutuma zisizokuwa na msingi" inahusu mbinu ambazo shetani hutumia huwadhuru watu.

23. "Inalindwa visivyo kawaida" inaonyesha kuwa mbinu ambazo shetani hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.

24. "Wamependelewa" inatumiwa kuwadhihaki watu wanaoonekana wagumu na hawajitambui.

25. "Anapatwa na ajali baada ya ajali" inaonyesha kuwa watu walizaliwa katika nchi ya joka kubwa jekundu, na hawawezi kuwa na ujasiri.

26. "Kiwango cha juu kabisa," inatumiwa kuwadhihaki wale wanaomtafuta Mungu kwa bidii.

a. Maandishi ya asili yanasoma "Wengine hata wanapaaza sauti."