Maneno ya Mungu ya Kila Siku | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II | Dondoo 39

Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu

Tangu wakati wa uumbaji, tabia ya Mungu imeenda sako kwa bako na kazi Yake. Haijawahi kufichwa kutoka kwa binadamu, lakini imewekwa kadamnasi na kwa dhahiri kabisa kwa binadamu. Ilhali, kwa kadri muda unavyopita, moyo wa binadamu umekua hata mbali zaidi na Mungu, na kwa kuwa upotovu wa mwanadamu umekuwa wa kina zaidi, binadamu na Mungu wamekuwa mbali na mbali zaidi kati yao. Kwa utaratibu lakini kwa uhakika, binadamu ametoweka kutoka kwa macho ya Mungu. Binadamu ameshindwa kuweza “kuona” Mungu, jambo ambalo limemwacha yeye bila “habari” zozote kuhusu Mungu; hivyo, hajui kama Mungu yupo, na hata anaenda mbali mno kiasi cha kukataa kabisa kuwepo kwa Mungu. Kwa hivyo, kutofahamu kwa binadamu kuhusu tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho si kwa sababu Mungu amefichwa kutoka kwa binadamu, lakini kwa sababu moyo wake umemgeukia Mungu. Ingawaje binadamu anamsadiki Mungu, moyo wa binadamu haupo na Mungu, na hajui chochote kuhusu namna ya kumpenda Mungu, wala hataki kumpenda Mungu, kwani moyo wake haujawahi kusonga karibu na Mungu na siku zote anamuepuka Mungu. Kutokana na haya, moyo wa binadamu umekuwa mbali sana na Mungu. Kwa hivyo moyo wake uko wapi? Kwa hakika, moyo wa binadamu haujaenda popote: Badala ya kuupatia moyo huo Mungu, au kuufichua kwa Mungu ili Aweze kuuona, amejiekea yeye mwenyewe. Hiyo ni licha ya ukweli kwamba baadhi mara nyingi wanamwomba Mungu na kusema, “Ee Bwana, utazame moyo wangu—unajua yote ninayofikiria,” na baadhi hata huapa kumruhusu Mungu kuwafikiria, kwamba waweze kuadhibiwa kama watavunja kiapo chao. Ingawaje binadamu anamruhusu Mungu kuangalia ndani ya moyo wake, hii haimanishi kwamba anaweza kutii mipango na mipangilio ya Mungu, wala kwamba ameacha hatima na matarajio yake na mambo yake yote katika udhibiti wa Mungu. Hivyo, licha ya viapo unavyotoa kwa Mungu au mwelekeo kwake Yeye, kwa macho ya Mungu moyo wako ungali umefungwa kwake Yeye, kwani unamruhusu Mungu tu kuangalia kwenye moyo wako lakini humruhusu Yeye kuudhibiti. Kwa maneno mengine, hujampa Mungu moyo wako kamwe, na unazungumza tu maneno yanayosikika kuwa matamu ili Mungu asikie; nia zako mbalimbali za kijanja, huku, unajificha kutoka kwa Mungu, unajificha usionekane na Mungu, pamoja na maajabu, njama, na mipango yako, na unashikilia matarajio na hatima yako mikononi mwako, ukiwa na hofu kubwa kwamba huenda yakachukuliwa na Mungu. Hivyo, Mungu hatazamii uaminifu wa binadamu kwake Yeye. Ingawaje Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, na Anaweza kuona kile ambacho binadamu anafikiria na anataka kufanya moyoni mwake, na Anaweza kuona ni mambo yapi yamewekwa ndani ya moyo wake, moyo wa binadamu haumilikiwi na Mungu, hajautoa ili udhibitiwe na Mungu. Hivi ni kusema, Mungu anayo haki ya kuangalia, lakini Hana haki ya kuudhibiti moyo huo. Kwenye nadharia za kibinafsi za binadamu, binadamu hataki wala hanuii kujiacha kwenye huruma za Mwenyezi Mungu. Binadamu hajajifungia tu kutoka kwa Mungu, bali kunao hata watu wanaofikiria njia za kusetiri mioyo yao, kwa kutumia mazungumzo matamu na sifa za kinafiki ili kuunda hali ya uongo na kupata uaminifu wa Mungu, na kuficha uso wao wa kweli dhidi ya kuonekana na Mungu. Nia yao ya kutomruhusu Mungu kuona ni kutoruhusu Mungu kuelewa namna walivyo kwa kweli. Hawataki kuitoa mioyo yao kwa Mungu lakini wanajihifadhia wao wenyewe. Maandishi madogo ya haya ni kwamba kile ambacho binadamu anafanya na kile ambacho anataka kimepangiliwa chote, kikapigiwa hesabu, na kuamuliwa na binadamu mwenyewe; haihitaji kushiriki au kuingilia kati kwa Mungu, na isitoshe hahitaji mipango na mipangilio ya Mungu. Hivyo, iwapo ni kuhusiana na amri za Mungu, agizo Lake, au mahitaji ambayo Mungu anamwekea binadamu, uamuzi wa binadamu unatokana na nia na maslahi yake mwenyewe, katika mazingira na hali yake mwenyewe ya wakati huo. Siku zote binadamu anatumia maarifa na maono ambayo amezoeana nayo, na akili zake binafsi ili kuamua na kuchagua njia anayofaa kutembelea na haruhusu uingiliaji kati au udhibiti wa Mungu. Huu ndio moyo wa binadamu ambao Mungu anaona.

Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona, anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye. Tangu Alipoanza kusimamia, Mungu amekuwa akisubiria binadamu kumpa moyo wake, kumwacha Mungu kuutakasa na kuufaa ipaswavyo, kumfanya yeye kumtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu, kumfanya yeye kumstahi Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu amewahi kutazamia mbele na kusubiria matokeo haya.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

God Puts His Hope Completely on Man

I

From the beginning until today, it’s only mankind who’s had a way to talk with God, converse with God. Among all creatures, all living things, it’s only mankind who words can bring and talk with God, converse with God. Since His management, God has been waiting for just one offering—the heart of man, that He may cleanse and equip it, and make man satisfying and loved by God, man satisfying and loved by God.

II

With ears for listening and eyes that see, ideas and language, a will that’s free, man can hear God, can walk with God. He can know God’s will, accept His task. And God desires man, wants man for His like-minded friend who’ll walk with Him. Since His management, God has been waiting for just one offering—the heart of man, that He may cleanse and equip it, and make man satisfying and loved by God, man satisfying and loved by God.

III

Oh God would make man love Him, shun evil and revere Him. This one thing He’s awaiting since all eternity. Since His management, God has been waiting for just one offering—the heart of man, that He may cleanse and equip it, and make man satisfying and loved by God, man satisfying and loved by God.

from Follow the Lamb and Sing New Songs

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana