Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

647 Kweli Unajua Kazi ya Mungu?

1 Ni nani amewahi kukubali ukweli? Ni nani amewahi kumkaribisha Mungu kwa mikono yote? Nani amewahi kutamani uwepo wa Mungu? Tabia ya mwanadamu imeoza tangu zamani sana, na unajisi wake umefanya hekalu la Mungu lisitambulike tangu zamani sana. Mwanadamu, wakati akiendelea kufanya kazi yake, amekuwa akimdharau Mungu. Ni kana kwamba upinzani wake kwa Mungu umeandikwa kwenye jiwe, na haubadiliki, na matokeo yake ni bora alaaniwe kuliko kuendelea kuteseka “kwa kufanyiwa vibaya” na maneno na matendo yake. Inakuwaje watu kama hawa wamjue Mungu? Wanawezaje kupata pumziko kwa Mungu? Na wanawezaje kufaa kuja mbele za Mungu?

2 Bila shaka, hakuna chochote kibaya kujitoa kwa mpango wa usimamizi wa Mungu—lakini kwa nini watu daima huweka kazi ya Mungu na ukamilifu wa Mungu akilini mwao huku wakitoa kwa dhati damu na machozi yao wenyewe? Roho ya watu ya kujitokea kwa dhati, bila shaka, ni ya thamani—lakini wangejuaje kwamba “hariri” wanayoisokota haiwezi kabisa kuwakilisha kile Mungu alicho? Nia nzuri za watu, bila shaka, ni za thamani na adimu—lakini wangewezaje kumeza “hazina ya thamani mno”?

3 Kila mmoja wenu anapaswa kufikiria juu ya maisha yenu ya zamani: Kwa nini hamjawahi kuwa mbali na kuadibu na laana ya kikatili? Kwa nini watu daima “huwa na uhusiano wa karibu” na maneno adhimu na hukumu yenye haki? Je, Mungu anawajaribu kwa kweli? Je, Mungu anawasafisha kwa makusudi? Na watu huingiaje katikati ya usafishaji? Je, wanajua kazi ya Mungu kweli? Ni mafunzo gani ambayo watu wamejifunza kutoka kwa kazi ya Mungu na kuingia kwao wenyewe? Watu wasisahau kusihi kwa Mungu, wawe na ufahamu katika kazi ya Mungu, waiamini kwa dhati, na kusimamia vizuri kuingia kwao wenyewe.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi na Kuingia (9)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Ni Muhimu Sana Kumjua Mungu wa Vitendo

Inayofuata:Amini Kwamba Mungu Hakika Atamfanya Mwanadamu Mkamilifu

Maudhui Yanayohusiana

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  1 Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…

 • Nimeuona Upendo wa Mungu

  1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako, nikiishi maish…

 • Umuhumi wa Maombi

  1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, ku…

 • Nitampenda Mungu Milele

  1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na hasi, m…