7. Baada ya Kusikitishwa na Pepo, Nagundua Hata Zaidi Jinsi Neema ya Mungu Ilivyo ya Thamani

Na Xu Qiang, Eneo Huru la Mongolia la Ndani

Jina langu ni Xu Qiang. Nilikuwa nikifanya kazi kama kontrakta wa uhandisi, nikiongoza timu kubwa za watu katika miradi ya uhandisi kila mwaka, na nilipata mapato mazuri. Machoni pa wenzangu, nilikuwa na familia yenye kila kitu, kazi taratibu, na matarajio yasiyo na kikomo; lazima walinifikiria kuwa mtu mwenye bahati nzuri zaidi. Hata hivyo, wakati huo huo nilipokuwa nikifurahia maisha yakinifu, siku zote nilikuwa na hisia zisizoelezeka za utupu. Hii ilikuwa kweli hasa katika juhudi zangu za mara kwa mara za kupata miradi: Nililazimika kujipendekeza kwa viongozi wa idara husika, nikijitahidi kusoma mawazo yao kupitia matendo yao na kila mara nikihitaji kutumia kiwango kinachofaa cha unyenyekevu na ubembelezaji ili nipate nilichotaka; la sivyo, singechuma pesa yoyote. Zaidi ya hayo yote, ilinibidi nishughulike na hila kati ya wafanyakazi wenzangu, walivyojilinda daima dhidi ya wao kwa wao, na kufikiria kwao. Yote haya yalinifanya nitafakari hata zaidi…. Kwa sababu hizi, nilihisi kuvunjika moyo sana na mchovu sana; nilionekana kugeuka kuwa karagosi, mashine ya kuchuma pesa, na nilikuwa nimepoteza kabisa heshima na uadilifu wangu wote. Hili liliendelea hadi mwaka wa 1999, nilipoikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Niliguswa sana na uhuru ulioletwa na maisha ya kanisa na wepesi na uaminifu wa ndugu zangu. Nilitaka sana kuishi maisha haya ya kanisa, kushiriki na ndugu zangu juu ya neno la Mungu na kuongea sisi kwa sisi juu ya uzoefu na maarifa yetu binafsi wa maneno ya Mungu. Pia nilithamini nyakati kama hizi sana. Nilipoendelea kusoma matamko ya Mungu na kushiriki katika usharika, nilipata kuelewa ukweli mwingi, na roho yangu ilipata uhuru mkubwa. Nilifurahia hasa kwamba hatimaye nilikuwa nimepata njia ya kweli ya kuishi, na nilikuwa nimepata furaha ya kweli. Moyo wangu ulijaa shukrani kwa Mungu: Isingekuwa kwa sababu ya Mungu kuniokoa kutoka katika bahari ya ulimwengu ya mateso, nisingekuwa na chochote cha kutazamia maishani. Baadaye, nilianza kueneza injili kwa bidii, kwa furaha na bila kuchoka nilijishughulisha na wale watu waliokuwa wakiichunguza njia ya kweli na kuwawezesha pia kuisikia sauti ya Mungu na kupata wokovu wa Mwenyezi Mungu.

Hata hivyo, katika nchi inayompinga Mungu ya Uchina, raia hawana demokrasia yoyote au haki za binadamu, na wale wanaomwamini Mungu na kumwabudu Mungu wanakabiliwa hasa na kulazimishwa na kuteswa na serikali ya Chama cha Kikomunisti cha China. Kwa sababu ya imani yangu katika Mungu, mimi pia nilikamatwa na serikali ya CCP na kuteswa na kunyanyaswa kwa ukatili, na nilishinda karibu miaka miwili ya maisha mabaya sana katika jela ya CCP…. Baada ya kupitia kipindi hiki kigumu na chungu cha maisha yangu, niliona waziwazi kiini cha kishetani cha upingaji wa hasira wa serikali ya CCP dhidi ya Mungu na chuki ya ukweli, na nikapata ufahamu wa kina zaidi wa ukweli kwamba maneno ya Mungu ndiyo ukweli. Maneno Yake yangeweza kuwa maisha yangu, na yangeweza kunielekeza njia mbele yangu. Isingekuwa kwa sababu ya mwongozo wa kila wakati wa maneno ya Mungu, yakinipa nguvu na imani, nisingeweza kuwa bado hai leo. Sitasahau kamwe neema ya wokovu wa Mungu katika maisha yangu yote!

Ilikuwa asubuhi ya Desemba 18, mnamo 2005, na nilikuwa katikati ya mkutano na ndugu zangu. Ghafla, mlipuko wa sauti kali sana za kishindo zilisikika kutoka mlangoni. Kabla hatujapata muda wa kufikiria, zaidi ya maafisa kumi wa polisi waliingia kwa kishindo, kila mmoja wao akitazama kwa hasira na sura katili machoni mwao. Kikosi maalum cha polisi walichokuwa wamehamasisha kilionekana kama tukio kutoka katika filamu ambapo mtoro wa kuogofya sana alikuwa anakamatwa. Bila kutoa maelezo yoyote, walivua viatu vyetu kutuzuia kukimbia, na kisha wakatoa mishipi yetu na kuifunga mikono yetu nyuma ya migongo yetu. Walituibia vitu vyetu vyote vya binafsi, vikiwemo simu zetu za rununu, saa, pesa taslimu na kadhalika. Polisi kisha walitufokea tupige magoti kwa foleni dhidi ya ukuta, na kama yeyote kati yetu angekuwa mpole wa kusonga, walitusukuma na kutupiga mateke, wakitulazimisha twende chini sakafuni. Baada ya hayo, walifanya upekuzi kamilifu, wakipindua fanicha na kupekua nyumba nzima; baada ya muda, ilikuwa imeharibiwa kabisa. Baada ya kutazama yote haya, niliuliza kwa hasira, “Hatujavunja sheria zozote, hivyo kwa nini mnatukamata?” Nilishangazwa sana polisi aliponivamia, akanipiga chini mpigo mmoja na kunipigia kelele.” Tunawakamata nyinyi watu mnaomwamini Mungu! Hatutaweza kulala vizuri hadi tumkamate kila mmoja wenu!” Ulipukaji huu wa ghadhabu ulinishangaza nikanyamaza, na pia ilinimakinisha: Mungu ndiye serikali ya CCP ilichukia zaidi, kwa hivyo ingewezaje kutuachilia sisi waumini? Nilikuwa kipofu na mjinga sana! Katika wakati huo, nilianza kumwomba Mungu kimya kimya, nikimsihi Atulinde ili tuweze kuwa mashahidi na kutuzuia tusimsaliti. Muda mfupi baadaye, polisi aliyekuwa akitulinda akanihoji: “Nani aliyewaambia mhubiri dini yenu kila mahali? Kiongozi wenu ni nani?” Nikasema, “Kueneza injili kwetu ni kwa hiari kabisa.” Akatusi, “Upuuzi! Usijaribu kukataa makosa yoyote kijana, la sivyo tutakuonyesha kilicho muhimu hivi karibuni!” Punde, nikamsikia polisi wa kike akipiga kelele kutoka katika chumba kingine, “Niletee sindano! Wewe jaribu kujificha kutoka kwangu tu….” Mara moja nilihisi woga mkubwa, kwa maana wakati huo niligundua kuwa dada mdogo hakuwepo; alikuwa amejaribu kujificha ili kuepa kukamatwa na polisi, lakini alikuwa amegunduliwa. Yule polisi wa kike alimshika na kutumia sindano kumchoma ndani na kucha zake za mkono na nyayo za miguu yake, na hata akaanza kuchomoa nywele zake kikatili kishungi kimoja kimoja. Mwishowe, walimwacha yule dada mdogo hapo, ambaye kufikia wakati huo alikuwa amezirai, na wakatukamata, pamoja na mali yote waliyokuwa wamepora, na kuondoka na sisi kwa kasi.

Ilipofika saa sita adhuhuri, polisi walikuwa wametuzuilia katika kituo cha polisi, ambapo punde walianza kutuhoji kila mmoja peke yake. Yule aliyekuwa ananihoji alikuwa afisa mwenye miraba minne mwenye nguvu, na mara tu nilipoingia kwenye chumba cha mahojiano alinifokea nipige magoti. Nikasema, “Namwabudu Mungu pekee; ni Bwana wa mbingu, ardhi na vitu vyote pekee Anayestahili kupigwa magoti. Nakataa kata kata kupiga magoti mbele yako!” Mara tu aliposikia haya, alinielekezea kidole na kunguruma, “Unapaswa kujua kuwa hapa ndani, hata mfalme wa kuzimu hana budi kutii! Unafikiria wewe ni nani? Tusipokufanya uteseke kidogo, hutajua ni nani aliye na mamlaka! Sasa, piga magoti!” Alipokuwa akisema haya kwa kelele, alinipiga teke nikaanguka chini. Baada ya hapo akaanza kunihoji: “Niambie ukweli: Wewe ndiye kiongozi wa kanisa, sivyo? Wewe huweka wapi vitabu vyako vya kanisa?” Nikiwa na wasiwasi, sikujua jinsi ya kujibu, kwa hivyo nilimwomba tu Mungu tena na tena Anipe hekima ya kupingana na polisi huyu mwovu. Baada ya kuomba, nilihisi mtulivu zaidi na mwenye nguvu mpya na nikajiwazia, “Ni afadhali nife kuliko kuwasaliti ndugu zangu. Siwezi kumsaliti Mungu!” Kwa hivyo, nilimwambia yule polisi, “Sijui kuhusu mambo haya yoyote unayoniuliza. Unataka niseme nini hasa?” Punde niliposema haya yule polisi mwovu alinipiga konde kwa nguvu kichwani, na kisha mara moja akaendelea kunipiga kwa nguvu kwa ngumi na miguu yake. Nilipigwa vibaya sana kiasi kwamba nikaduwaa na kichwa changu kikawa na kizunguzungu, kikiumia vibaya sana kiasi kwamba nilihisi kana kwamba fuvu lilikuwa limepasuka. Nilianguka sakafuni kichwa chini. Baada ya hapo, alishikilia daftari la injili walilokuwa wamepata kwangu mikononi mwake na kutishia, “Tazama, unaona? Tuna ushahidi, kwa hivyo hakuna haja ya kukataa kuongea. Sema! Wewe ndiye kiongozi, sivyo? Usingekuwa kiongozi, usingekuwa na maandishi haya!” Kuona kwamba singeongea, alijaribu njia nyingine, akisisitiza, “Usiwe kichwa ngumu; hebu shirikiana nasi. Tuambie unachojua, na utaruhusiwa kuondoka kesho.” Wakati huo tu, Mungu alinipa nuru kwamba nilikumbuka kifungu kimoja cha matamko Yake: “Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda. Kwa nje yataonekana kama mambo madogo; lakini haya mambo yakitendeka huonyesha kama unampenda Mungu au la. Ikiwa unampenda, utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako Kwake” (“Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yaliniruhusu kuona wazi kwamba hivi vilikuwa vita vya ulimwengu wa kiroho. Singehadaiwa na ujanja wa Shetani, na ilibidi niwe shahidi wa Mungu kabisa. Bila kujali ni kiasi gani kinachodaiwa kuwa ushahidi walichokuwa nacho mikononi, singeweza kufichua habari yoyote kuhusu kanisa. Huu ulikuwa ushuhuda wa upendo wangu kwa Mungu na kujitolea ninakopaswa kudumisha mbele za Mungu. Baada ya hapo, niliomba, na pole pole nikatulia. Haijalishi alinitesa kiasi gani, sikutamka neno lolote. Mwishowe, polisi huyo mwovu alikerwa sana hadi akafunga mlango kwa kishindo na kuondoka.

Muda mfupi baadaye, polisi mwenye umri wa takribani miaka thelathini aliingia na kunisaidia niinuke polepole kutoka sakafuni na kukaa kwenye kiti. Hata alinipa kikombe cha maji, na kisha akasema, “Chukua, ndugu; kunywa maji kiasi. Umeteseka.” Nilishtuka: Ni nini kilichokuwa kinaendelea? Inawezekanaje mtu aniite “ndugu” mahali kama hapa? Kabla nipate muda wa kufikiria haya zaidi, aliendelea: “Ndugu, siku hizi tunahitaji kuishi kwa njia ya uhalisi zaidi, na tuweze kubadilika kabisa. Inapofikia mtu kama wewe, hawana budi ila kukupiga hadi kufa. Kusema kweli, nilikuwa nikimwamini Mungu pia, kwa hivyo najua kuwa na imani ni jambo jema—lakini kuteseka sana kwa sababu yake, sembuse kuweka maisha yako hatarini, halistahili! Ukihukumiwa, hilo litaweka alama mbaya kwa familia yako yote. Nadhani wazazi wako wawili bado wako hai? Ukishinda gerezani miaka michache, basi hawatakuwepo tena wakati wako wa kutoka. Familia yako itakufikiriaje? …” Mapenzi yangu kwa mama na baba yangu yalikuwa ya kina zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, kwa hivyo kila neno la mtu huyu liliniuma hadi ndani ya moyo wangu. Picha za wazazi wangu wakongwe zilivyopita akilini mwangu, ghafla nilihisi wimbi la giza na udhaifu ukinipitia, na nikawaza, “Ni kweli; nikihukumiwa kwenda gerezani, basi mama na baba watafanyaje? Nani atawatunza? …” Wazo hilo lilisababisha machozi yatiririke kutoka machoni mwangu, na singeweza kuyazuia. Mara moja polisi huyo aliidakia fursa hiyo, akijaribu kunishawishi zaidi kwa kusema, “Kwa hivyo, unapaswa kufanya kila uwezalo kushirikiana nao; ukifanya hivyo, kesho utaachiliwa huru.” Kusikia maneno haya ghafla kulinigutusha, na maneno haya wazi zaidi yakawaka akilini mwangu: Lazima usiwe Yuda anayemsaliti Mungu hata kidogo! Nusra niteleze! Polisi huyu mjanja alitumwa na Shetani mwenyewe, kunidanganya nimsaliti Mungu. Katika wakati huo, maneno ya Mungu pia yalinipa mwongozo: “Ni kwa uaminifu tu ndio unaweza kupinga hila ya Shetani” (“Sura ya 10” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Niligundua kuwa kila kitu ambacho polisi walikuwa wamesema kilikuwa ni ujanja wa shetani; walitaka kutumia hisia za mapenzi za mwili kunichochea nimsaliti Mungu. Singeweza kabisa kupumbazwa na udanganyifu wa Shetani. Papo hapo, nilimwomba Mungu kimya kimya, nikiamini kwamba maswala ya wazazi wangu yalikuwa juu Yake kuamua na yalikuwa mikononi Mwake kabisa. Nikiwaaminia kwa nguvu kubwa ya Mungu, niliamua kuwa na ushuhuda wa Mungu. Kwa uthabiti, nikamwambia yule mtu, “Asante kwa nia zako nzuri; nashukuru fadhila zako. Hata hivyo, sijui chochote kuhusu maswala ya kanisa.” Alipoona kwamba ujanja wake haukuwa umefaulu, ghafla polisi huyu mbaya alionyesha tabia yake halisi kwa kushikwa na hasira. Akinielekezea kidole, alifoka kwa chuki, “Subiri tu hapa kufa basi!” na kisha akaondoka. Takribani saa nane alasiri, polisi watatu au wanne walikuja. Waliniinua kutoka kwenye kiti na kunivuta kwa kola hadi mlangoni, ambapo walitumia pingu kunitundika kwenye mtambaapanya. Mwishowe, walitoa tamko la kejeli la “Haya, chukua muda wako na ‘ufurahie,’” na kisha wakaondoka. Sikuweza kugusa sakafu kwa miguu yote miwili kwa wakati mmoja; ningeigusa kwa mguu mmoja, nililazimika kuuinua mwingine. Kusonga kwa mwili wangu kulizisababisha pingu zikate ndani ya mwili wangu, na ulikuwa uchungu mwingi sana. Karibu saa moja baadaye, polisi hao waovu walirudi, wakiwa wameshashiba chakula na kinywaji. Kwa tabasamu la uovu, waliniuliza nilivyokuwa nikihisi. Kufikia wakati huo, kwa sababu ya uchungu, suruali na shati langu la pamba zilikuwa zimelowa jasho, na niliposhushwa chini, mikono yangu yote ilikuwa imevimba kama mikate na kufa ganzi kabisa. Genge hili la polisi waovu kweli walikuwa wenye kutisha na wasio na huruma. Niliwachukia kabisa na nilikuwa nimeona vema uovu na ukatili wa serikali ya CCP. Walikuwa kundi la pepo waliompinga na kumchukia Mungu, na chuki yangu kwa chama hiki kiovu ilikuwa inaongezeka kwa haraka.

Jioni hiyo, muda fulani baada ya saa moja, polisi hao waovu walinirundika mimi na dada zangu wanne ndani ya gari la polisi kutupeleka katika eneo lingine. Kila mmoja wa dada zangu alionekana kusawijika; ni wazi kuwa wao, pia, walipitia ukatili kama huo. Tulitiana moyo kwa kuangaliana na sura zilizojaa azimio. Tulipofika kizuizini, polisi waovu waliwaruhusu dada zangu wanne watoke kwenye gari, lakini niliambiwa nibaki ndani ya gari na punde tulianza kuenda tena. Nilipowauliza walipokuwa wananipeleka, polisi mmoja alisema akitabasamu kwa hila, “Hata ingawa hujatoa habari yoyote, bado tunajua kwamba wewe sio mtu mdogo kanisani. Hatukutaka kuwa wenyeji wabaya, kwa hivyo tunataka kukupeleka ule ‘kumbwe ya usiku wa manane.’…” Nikijua kwamba genge hili la polisi waovu halikuwa na malengo yoyote mazuri, sikuthubutu kutotahadhari hata kidogo. Niliendelea kumwomba Mungu kimya kimya anipe nguvu na anilinde dhidi ya kumsaliti. Muda mfupi baadaye, nilipelekwa katika Kikosi cha Usalama cha Kitaifa. Nilipokelewa na watu wawili wenye nguvu walionielekeza katika chumba cha mahojiano. Kuona vifaa vyote vya utesaji vilivyokuwa vimetapakaa sakafuni kama chui walio kimya na wenye njaa kali kulinitia fadhaa. Wakati huohuo, polisi mmoja mwovu alinifokea akisema, “Nasikia kwamba wewe ni mkaidi kabisa. Naam, tunapenda kushughulikia mzee kama wewe!” Punde baada ya kusema haya polisi wawili waovu waliruka mbele, wakipiga kelele walipokuwa wakikimbia, na kunikamata masikio, wakiyavuta kwa nguvu zao zote. Katika mwanga huo hafifu, niliona nyuso mbili zenye ukatili, zilizokunjika, na moyo wangu ukaanza kupiga bila kudhibitiwa. Katika wakati huo, nilimsikia polisi mwingine mwovu akiangua kicheko na kusema, “Ni bahati yako mbaya kuwa umekutana nami leo. Haya, acha tuanze kwa kukuosha.” Alipokuwa akisema hivyo, walinishikilia kwa uthabiti na kurarua kila kipande cha nguo mwilini mwangu. Nilisimama pale nikiwa uchi wa mnyama kwenye sakafu baridi kama barafu, mwili wangu wote ukitetemeka na meno yangu yakitatarika. Yule polisi mwovu akavuta bomba ndefu la mpira, akalilenga moja kwa moja kwangu, na kufungua kilango. Kufumba kufumbua nilikuwa nikisukumwa na mlipuko wa maji ya barafu ya kugandisha mifupa. Ulikuwa uchungu usiovumilika, kana kwamba kisu kilikuwa kikiichuna ngozi yangu; ilihisi tu kama kwamba damu iliyokuwa ikikimbia katika mwili wangu wote ilikuwa ikiganda. Muda mfupi baadaye, sikuweza kuhisi chochote. Huku wakinimwagia maji, polisi hao waovu waliendelea kunifokea vitisho: “Ikiwa unajua kilicho bora kwako, basi harakisha uongee; usipoongea, basi hutaishi kuona jua likichomoza kesho!” Nikijilazimisha kuvumilia uchungu huu, niliinamisha kichwa changu na sikusema chochote. Polisi mmoja mwovu alisaga meno yake na kusema kwamba atanipa joto, ambayo ilimaanisha kuwa angenipitishia umeme. Kufikia wakati huo nilikuwa nimeteseka sana kiasi kwamba sikuwa nimebaki na nguvu yoyote. Nikihisi kana kwamba kifo kilikuwa kikikaribia hatua kwa hatua, nilimwomba Mungu kwa kukata tamaa: “Mungu! Sina umuhimu wowote kuweza kukufanyia chochote, lakini leo nataka kutumia kifo changu kumdhalilisha Shetani. Ninachokuomba tu ni kwamba Uulinde moyo wangu ili usipotee kutoka Kwako kamwe, na ili nisikusaliti.” Polisi walilazimisha nifungue mdomo wangu na kuniingiza kitambaa kilicholowa ndani, mwisho mwingine wa kitambaa hicho uliunganishwa na waya ya umeme. Waliunganisha mwisho mmoja wa waya kwenye sikio langu, kisha yule aliyeshikilia swichi akaiwasha. Ghafla nilihisi damu yote mwilini mwangu ikipanda juu kwa haraka, na nilihisi kama kwamba kichwa changu kilikuwa karibu kulipuka. Ilikuwa uchungu sana nikahisi kama kwamba macho yangu yangepasuka, na kila neva mwilini mwangu ilikuwa ikishtuka na nilihisi kana kwamba ingekatika. Wakiniona katika uchungu mwingi mno, kundi hili la polisi waovu liliangua tu kicheko. Muda mfupi baadaye, nilizirai. Punde baada ya hapo, niligutushwa kwa kumwagiwa ndoo ya maji baridi. Nilipopata fahamu, kitambaa kilikuwa bado mdomoni mwangu. Polisi mmoja alinichekelea vibaya na kuuliza, “Inaonja vipi? Ikiwa unataka kusema jambo, tingisha tu kichwa chako.” Wakati huo tu, nilikumbuka kifungu cha neno la Mungu: “Watu wanapokuwa tayari kuyatoa maisha yao, kila kitu huwa hafifu, na hakuna anayeweza kuwashinda. Ni nini kingekuwa muhimu zaidi kuliko uzima? Hivyo, Shetani anakuwa hawezi kufanya chochote zaidi ndani ya watu, hakuna anachoweza kufanya na mwanadamu” (“Sura ya 36” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalilitia nguvu azimio langu la kuchagua kuwa shahidi badala ya kumwabudu Shetani. Niliwaza, “Fanya chochote unachotaka kwangu. Hata hivyo, nina maisha haya tu; mbaya zaidi, nitakufa, lakini usidhani hata kidogo kuwa utapata neno hata moja kutoka kwangu!” Sikumjibu polisi; nilifunga tu macho yangu, nikakataa kumwangalia. Kitendo hiki kilimkasirisha yule polisi mwovu, na akanishtua kwa wimbi lingine la umeme, lakini wakati huu wimbi la umeme lilikuwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali. Kwa kimya, nikalia, “Mungu! Niokoe! Siwezi kuvumilia zaidi!” Hapo tu, picha dhahiri ya kusulubiwa kwa Bwana Yesu ilitokea mbele ya macho yangu: wale polisi wenye kutisha wakigonga msumari wa nusu futi kwenye kiganja cha Bwana, wakitoboa ngozi, na wakitoboa mfupa…. Mateso ya Bwana Yesu yaliusababisha moyo wangu kuwa na uchungu usio na mwisho, na sikuweza kujizuia kutoa machozi. Moyoni mwangu, nilimwomba Mungu: “Mungu! Wewe ni mtakatifu; Wewe huna dhambi. Lakini ili kuleta wokovu kwa binadamu Ulijikabidhi Mwenyewe kwa wahuni hao na kuwaacha wakutundike msalabani na kutoa kila tone la damu Yako ili kutukomboa sisi wanadamu. Mungu, mimi ni mtu mpotovu sana, kitu ambacho kinapaswa kuangamizwa. Nimekubali wokovu Wako na nina bahati nzuri ya kuipitia kazi Yako, kwa hivyo nafaa kujitolea mwenyewe Kwako. Mungu, najua bila shaka kuwa Wewe uko kando yangu hivi sasa, ukiambatana nami katika mateso yangu. Umenipenda daima na kuwekeza nguvu ndani yangu. Niko tayari kutoa kila kitu changu ili nikuridhishe, ili Usilazimike tena kuteseka kwa niaba yangu au kuwa na wasiwasi juu yangu tena.” Wakati huo tu, wale polisi wawili waovu waliacha kunipitishia shoti ya umeme. Kwa kuona kwamba Mungu alikuwa amenihurumia katika udhaifu wangu, moyo wangu ulijawa na shukrani Kwake! Baada ya hapo, licha ya ukweli kwamba polisi hawakuacha kuniumiza, sikuhisi uchungu wowote tena. Nikijua kwamba Mungu alikuwa Akinilinda na Alikuwa ameyachukua mateso yangu kwa ajili yangu, nilihisi kuguswa sana na upendo na Mungu, na nikalia machozi bila kukoma. Baadaye, polisi mmoja aliingia, akanitazama, na kuwaambia wale polisi wawili waovu, “Hiyo inatosha; mmempiga vibaya sana, na bado hazungumzi. Nina hakika hajui chochote.” Ni hapo tu ndipo walipoacha kunitesa. Nilijua kuwa hii yote ilikuwa sehemu ya utaratibu na mipango ya ajabu ya Mungu; Mungu hakuwa ameliruhusu kundi hili la pepo liyamalize maisha yangu, na Alikuwa amemshawishi mtu aje kuwakomesha. Nilishukuru kwa dhati kwa ajili ya upendo wa Mungu.

Wakiwa wameshindwa, polisi hao waovu hawakunihoji tena, na takribani saa sita usiku, walinipeleka kizuizini. Mlinzi alinielekeza kwenye seli iliyokuwa na wahalifu zaidi ya thelathini, na alipofungua mlango kuniingiza ndani, nilimsikia akicheka kwa hamaki na kumweleza mfungwa mkuu, “Subiri kidogo, tulia; usipige kelele nyingi sana.” Mfungwa mkuu alinitazama kutoka juu hadi chini, akitabasamu, na kumwambia mlinzi, “Hakuna wasiwasi!” Kabla sijapata wakati wa kufanya chochote, sura ya mfungwa mkuu iligeuka na kuwa ya giza na aliwaamuru wale wengine kwa sauti ya chini, ya kutisha, akisema, “Kama kawaida, ndugu. Mshambulie!” Wafungwa wote walikaa vizuri na kunitazama kama chui akitazama windo lake, wakifanya nishikwe na woga mwingi. Punde mfungwa mkuu alipopunga mkono wake, wote walinishambulia kama kundi la mbwa mwitu wakali. Wakinishikilia chini, walirarua nguo zangu zote na kuanza kunipiga kwa nguvu zao zote kwa kutumia soli za viatu vyao. Mwishowe, walikuwa wamenipiga vibaya sana hadi nikazirai. Haikuwa hadi saa sita asubuhi siku iliyofuata ndipo nilipata fahamu. Niligundua kuwa nilikuwa nimefinyiliwa pembeni, mwili wangu wote ulikuwa umevimba vibaya sana, hata sikuweza kuvaa nguo yoyote. Na hivyo ndivyo nililala kwa siku sita mfululizo kwenye kitanda cha ubao mwili wangu wote ukiwa umeumia kupondwa sana. Juu ya hayo, ndani ya mdomo wangu ulikuwa umechomwa na shoti za umeme za polisi waovu wabaya hadi tishu zote zilikuwa zimeoza, na nilikuwa katika uchungu mwingi sana hata singeweza kumeza tonge la chakula. Wakihofia kwamba kufa kwangu kungewasababishia shida, walinzi waliwatuma wale wafungwa wengine kwa zamu wanilishe supu ya mboga.

Majeraha yangu yalipopona kiasi, wafungwa walichochewa na polisi waovu waendelee tena na uonevu na unyanyasaji wao. Mapema kila asubuhi, walinifanya nikariri kanuni za gereza; kama ningefanya kazi duni, wangenipiga. Walinifanya pia nisafishe, na kuwafulia nguo wafungwa wenye pesa. Ningefanya kosa dogo, ningepigwa mangumi na mateke. Walijua kuwa nilimwamini Mungu, kwa hivyo mara nyingi wangesema mbele yangu kwa makusudi mambo mengi yaliyomkufuru Mungu ili waniudhi, na pia walinidhalilisha, kama vile, “Je, si watu wanaomwamini Mungu huwa hawahisi uchungu wanapopigwa? Na huwezi kufanya kazi bila kuhisi uchovu? Hujali kiasi unachoteseka, sivyo? …” Ili wanitese, walinilazimisha nisafishe choo cha kuinama kwa mkono, jambo lililokuwa la kuchukiza sana kiasi kwamba lilinifanya nitake kutapika; hata walinifanya nisafishe vigae vya sakafu kwa mswaki wangu, na kwa makusudi walitupa mikate yangu iliyopikwa chooni. Mlinzi alipokuja kukagua usafi wa seli, alivua viatu vyake na kuzunguka katika seli akiwa amevalia soksi nyeupe. Ikiwa angegundua uchafu wowote kwenye soksi, angetandika. … Nikikabiliwa na mateso yasiyo na mwisho kutoka kwa polisi hao waovu na wale wafungwa, nilihisi kudhoofika kabisa na mwenye huzuni sana. Nilianza kuhisi kwamba ingekuwa afadhali kufa kuliko kuendelea kuishi namna hii. Nikiwa katika kina cha udhaifu na mateso yangu, maneno ya Mungu yalinipa imani na motisha ya kuendelea kuishi. Nilikumbuka kwamba Alikuwa amesema, “Pengine utayakumbuka maneno haya: ‘Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.’ Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale. Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu” (“Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania?” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinifundisha kwamba kuweza kudhalilishwa na kuteswa kwa sababu ya imani yangu ilikuwa ishara kwamba Mungu alikuwa amefanya jambo la kipekee na kuniinua—ilikuwa heshima kubwa sana kwangu! Hata hivyo, nilikuwa mwoga na sikuwa na maadili thabiti; kwa sababu nilikuwa nimepitia uchungu kiasi wa mwili na kufedheheshwa kidogo, nilikuwa nimepoteza imani yangu katika Mungu, na sikuwa tayari kuwa na ushuhuda ili kulipiza upendo wa Mungu kupitia mateso. Mungu alikuwa amelipa gharama kubwa sana ili kuniokoa, kwa hivyo ningewezaje kumlipiza kwa njia hii? Ningewezaje kwenda kinyume na dhamiri yangu namna hii na kujibu kwa uhasi namna hiyo? Haingefaa! Mimi singekuwa mtu dhaifu asiye na ujasiri hata kidogo; Singeleta aibu kwa jina la Mungu kabisa! Kwa hiyo, nilimwomba Mungu kwa haraka: “Mungu, nakushukuru kwa kunipa nuru na kunifanya nielewe maana ya mateso. Kwa sababu ya heshima Yako, niko tayari kuvumilia mateso ya kila aina; natamani kukuridhisha hata ikimaanisha niishi maisha yangu yote gerezani. Ninachoomba ni kwamba Ubaki nami, Unipe nuru na kuniongoza, na uniwezeshe kusimama imara na kukutolea ushuhuda mkuu wakati wote wa kuteswa na Shetani.” Baada ya kuomba, nilihisi niliyejawa na nguvu kabisa, na nilikuwa na ujasiri wa kuyakabili mazingira hayo magumu.

Wiki chache baadaye, polisi hao waovu walirudi kunihoji, wakisema kwamba sikuwa nimechelewa sana kushirikiana nao, na kutishia kwamba kama singefanya hivyo, mambo yangezidi kuwa magumu kwangu katika siku zijazo. Baada ya kupitia vikao vichache vya kuteswa kwa kikatili, nilikuwa nimewang’amua kitambo asili zao za kishetani na niliwachukia sana. Kwa hivyo, haijalishi walivyonishawishi, kunitishia, na kuniogofya, imani yangu haikutikisika hata kidogo. Baadaye, walianza kunihoji mara moja kila baada ya majuma mawili hadi mwishowe, walipoona kwamba hawangepata habari yoyote kutoka kwangu, walinihukumu miaka miwili ya mafundisho kupitia kazi kwa uhalifu wa “kusababisha machafuko kwa umma” na “kujihusisha na mikusanyiko isiyo halali.”

Mnamo Februari 24, mwaka wa 2006, nilipelekwa katika kambi ya kazi. Kwa sababu ya imani yangu katika Mungu, nilikuwa nimebandikwa jina “mhalifu wa kisiasa,” na walinzi wa gereza kwa makusudi walinipangia kazi ngumu zaidi, yenye kuchosha na yenye hatari zaidi ya tanuu la motofali ili nifanye kazi yangu ya marekebisho. Kazi yangu ilikuwa kuondoa matofali yaliyookwa kutoka katika tanuu, ambamo joto lilikuwa angalau nyusi 300 selisiasi (nyusi 572 Fahrenheiti). Asubuhi, joto lilikuwa la chini zaidi, lakini bado lilikuwa zaidi ya nyusi mia moja (nyusi 212 Fahrenheiti). Licha ya sisi kulazimika kufanya kazi kwa joto kama hilo, walinzi hawakutupa mavazi yoyote ya kazi ya kuzuia joto. Kofia za usalama tulizovaa zingeyeyuka baada ya dakika mbili tu za kuwa katika eneo la tanuu, na ili kuzuia kuchomeka, tulilazimika kushikilia pumzi yetu huku tukikimbia kuingia na kutoka kwa haraka iwezekanavyo. Kwa sababu hatukuwa na buti zenye kuzuia joto, tulipoingia kwenye eneo la tanuu, tulilazimika kubadilisha kati ya mguu tuliosimamia; ikiwa hatungekuwa waangalifu, miguu yetu ingepata majipu kutokana na kuungua. Wafungwa wapya hawakuwa wamezoea haya; baada ya kuingia, wasingeweza kubaki kwa zaidi ya sekunde tano kabla ya kukimbia nje tena. Nahodha wetu wa timu alipangia kila kiongozi wa kikundi awe na bomba la plastiki lililojazwa na mchanga; yeyote aliyekimbia nje angepigwa na bomba hilo. Ingawa aina hizi za mabomba hazikuwa ngumu kiasi cha kuvunja mifupa, zilisababisha alama kali za pigo kwenye ngozi. Wafungwa walilipa bomba hilo jina la utani “vipiga ngozi.” Tulipoingia katika eneo la tanuu, hatukuthubutu kupumua; kupumua kulikuwa ni kama kuvuta moto ndani ya mapua yetu. Baada ya kuondoa matofali machache, tulilazimika kuzivuta rukwama kwa haraka kutoka nje tena, na ikiwa mojawapo ya magurudumu lingelipuka, hatungeadhibiwa pekee, lakini wakati ungeongezwa katika vifungo vyetu, uliorekodiwa kama uhalifu wa “uharibifu wa vifaa vya uzalishaji na kukataa marekebisho.” Kama wafungwa, kazi yetu ya kila siku ilikuwa kujaza rukwama na matofali 115 makubwa na matofali 95 madogo. Katika joto kama lile, kazi hii haingewezekana kukamilisha, lakini walinzi hawakuuliza kwa nini hukuweza kuikamilisha; walikuuliza tu kwa nini una hisia za upinzani kuhusu kufanya kazi. Kwa sababu kufanya kazi katika moto kulinifanya nitoe jasho sana, niliishia kupata shida ya upungufu wa potasiamu. Nilianguka chini na kupoteza fahamu mara kadhaa, kwa hiyo wangenitupa juu ya ukuta wa tanuu ili nipoe kwa dakika chache. Baada ya kuamka, walinifanya ninywe kikombe cha maji ya chumvi, na kunilazimisha nirudi kazini. Huo ndio ulikuwa wakati wangu wa kwanza kujua maana ya kufika mwisho, kujua ugumu usiovumilika ulikuwa nini, na hisia ya kutaka kufa badala ya kuendelea kuishi ilikuwa ipi. Hapa, hakuna aliyejali kama ungeishi au kufa; nahodha wa timu alijali tu ikiwa kikundi chako kilimaliza kazi yake au la. Kama kingemaliza, hangesema chochote, na kama hakingemaliza, bado hangesema chochote, lakini angeelekeza tu kidole kwenye mlango wa tanuu kisha aondoke. Baada ya hapo, kiongozi wa kikundi angewaita watu wowote ambao walikuwa hawajamaliza kazi yao wasimame katika eneo la tanuu na kuwapa kichapo; mara walipoanguka chini, wangechomwa vibaya sana na ardhi moto kiasi kwamba majipu yaliibuka kwenye ngozi yao yote. Kwa kuongezea, ilibidi wafanye rukwama nyingine ishirini zilizojaa matofali kila siku, na hawangekoma hadi walie wakiomba huruma. Nikikabiliwa na mazingira ya aina hii, nilihisi dhaifu sana; siku chache tu za kuteswa zilihisi kama safari kupitia kuzimu. Akilini mwangu, miaka miwili ilihisi kama muda mrefu sana kweli. Sikujua jinsi ambavyo ningeweza kuendelea kuishi wakati huo wote, na nilikuwa na wasiwasi kuwa labda ningepigwa hadi niuwawe na polisi hao waovu au kuchomwa hadi kufa katika joto hilo kali. Kadiri nilivyofikiria zaidi juu ya matarajio yangu, ndivyo nilivyohisi kunaswa zaidi; nilihisi kuwa kweli singeweza kuvumilia katika gereza hili la pepo tena—kwa hivyo nilifikiria kuhusu kufa. Kila siku kuanzia wakati huo kuendelea, nilitafuta nafasi za “kuokolewa.”

Siku moja mwishowe, fursa yangu ilifika. Wakati lori lililojaa matofali lilikuwa likiondoka, nilijitupa chini yake kichwa kwanza. Hata hivyo, magurudumu ya gari ghafla yalisimama inchi chache kutoka nilipokuwa; ilivyotukia, lori lilikuwa limeharibika. Wafungwa wachache walinichomoa, na mlinzi mkuu akasema kuwa nilikuwa nakataa kukubali nidhamu na sikutaka kubadili tabia za zamani. Kisha akaanza kuniadhibu. Walisukuma kurungu cha umeme kinachotoa miale ya moto ndani ya shati langu upande wa mbele, na nilihisi uchungu sana kiasi kwamba nilianguka chini kwa misukomisuko mikali. Baada ya hapo, walinitia pingu mikono yangu ikiwa nyuma kwenye mlingoti wa simu na kunipiga kwa ukatili kwa virungu vya umeme. Baada ya chakula cha jioni, nilipigwa na umma ili kurekebisha na “kusahihisha” itikadi yangu. … Mateso haya yasiyoisha yalinifanya nihisi kiwango cha juu cha hofu, kukata tamaa, na kukosa msaada. Wakati tu nilikuwa nikipambana na swali la jinsi ningeendelea kuishi, kifungu cha maneno ya Mungu kilijitokeza akilini mwangu: “Haijalishi Mungu Anavyokuboresha, unabaki kuwa na imani kubwa na kutopoteza imani katika Mungu. Ufanye kile mwanadamu anafaa kufanya. Hiki ndicho Mungu Anahitaji kwa mwanadamu, na moyo wa binadamu unapaswa kuweza kurudi Kwake kikamilifu na kumwelekea katika kila wakati. Huyu ni mshindi. Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi” (“Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalileta mwale wa mwanga na joto moyoni mwangu, nilipokuwa tu karibu sana kukata tamaa yote. Ilikuwa kweli; mwishowe, Mungu alitaka kufanya kikundi cha washindi ambao wangeweza kudumisha imani yao na kujitolea Kwake katika mazingira yoyote magumu, waishi kulingana na maneno Yake na, hatimaye, kutoa ushuhuda mkuu na wenye nguvu kwa Mungu mbele ya Shetani. Sababu ambayo Shetani alikuwa ametumia kila njia inayowezekana kunitesa na kuniumiza ni kwamba alitaka kuchukua fursa ya udhaifu wangu, akinishambulia wakati nilikuwa chini na kunilazimisha nimsaliti Mungu—lakini singeweza kuwa ishara ya kufedheheshwa kwa Mungu! Upendo wa Mungu kwangu ulikuwa halisi na wa vitendo sana; nilipokuwa dhaifu kabisa na nikatamani kifo, Mungu alikuwa bado akinitazama kwa siri, Akinilinda na kuniweka hai. Haijalishi nilivyokuwa dhaifu, Hakuwahi kuwa na dhamira yoyote ya kuniacha; upendo Wake kwangu ulibaki vivyo hivyo tangu mwanzo, na bado Alikuwa akinipa nuru, Akinielekeza, na kunisaidia kupata suluhisho la uchungu. Singeweza kabisa kumsikitisha Mungu au kuumiza hisia Zake. Nilishukuru kwa mwongozo wa Mungu; ulikuwa umeniruhusu tena kung’amua ujanja wa Shetani na kurudi kutoka ukingoni mwa kifo. Singejizuia ila kuimba wimbo: “Nitatoa upendo na uaminifu wangu kwa Mungu na kukamilisha misheni yangu ya kumtukuza Mungu. Nimedhamiria kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu, wala kamwe sitashindwa na Shetani. Eh, kichwa changu kinaweza kupasuka na damu itiririke, lakini ujasiri wa watu wa Mungu hauwezi kupotea. Ushawishi wa Mungu umo moyoni, naamua kumwaibisha Shetani Ibilisi. Maumivu na shida vimeamuliwa kabla na Mungu, nitastahimili aibu ili kuwa mwaminifu Kwake. Kamwe sitamsababisha Mungu alie au kusumbuka” (“Natamani Kuiona Siku ya Utukufu wa Mungu” katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya).

Mara tu nilipotii na kuwa tayari kuvumilia mateso yote ili kumridhisha Mungu, Mungu alinifungulia njia: Kwa sababu nahodha wa timu alikuwa hajui kusoma na kuandika, alinifanya nimsaidie kujaza ripoti zake, na tangu wakati huo kuendelea, sikulazimika kufanya kazi nyingi ya kuhamisha matofali. Wakati fulani baadaye, dada mzee kutoka kanisani alinitembelea. Aliushika mkono wangu mikononi mwake na kusema kwa machozi, “Mwanangu, umeteseka. Ndugu zako wana wasiwasi sana juu yako, na sote tunakuombea kila siku. Lazima ubaki mwenye nguvu, na usisujudu mbele za Shetani. Lazima usimame imara na umshuhudie Mungu. Sote tunakungojea uje nyumbani.” Katika kuzimu huku kwa mwanadamu kwenye baridi na katili, mbali na maneno ya faraja ya Mungu, sikuwa nimewahi kusikia neno la ukunjufu kutoka kwa mtu yeyote. Kusikia maneno haya ya fadhila kutoka kwa ndugu zangu, maneno ambayo niliyasikia mara nyingi zamani, yalinipa faraja na kunitia moyo mno. Kwa muda mrefu baadaye, nilihisi kutiwa moyo na upendo wa Mungu; nilihisi kupumzika zaidi kiasi, na nilikuwa na uchangamfu wakati nilikuwa nikifanya kazi. Katika wakati wangu wote gerezani, siku hizo zilipita haraka sana. Hii ilikuwa kweli hasa katika miezi yangu minne ya mwisho. Siku zote nilikuwa wa kwanza katika orodha ya majina yaliyotangazwa kila mwezi ya wafungwa ambao vifungo vyao vimefupishwa. Katika miezi iliyopita, orodha hii ya majina ilijumuisha tu wafungwa wakuu, na viongozi wa timu; wafungwa wasio na pesa au nguvu yoyote hawakuwa. Kwa Mkristo kama mimi, ambaye serikali ya CCP ilimbandika jina “mhalifu wa kisiasa,” uwezekano ulikuwa wa chini hata zaidi kwamba ningetendewa hivyo. Kwa sababu hii, wafungwa wale wengine walinizunguka kila wakati na kuniuliza, “Uliwezaje?” Kila wakati hili lilifanyika, nilimshukuru Mungu moyoni mwangu, kwa sababu nilijua kuwa haya yalikuwa matokeo ya rehema Yake kuu kwangu; yalikuwa ni mapenzi ya Mungu yaliyonipa nguvu.

Mnamo 7 Septemba, mwaka 2009, niliachiliwa kwa msamaha wa mapema. Muda mfupi baadaye, nilirudi kanisani na kuanza tena maisha ya kanisa, na tena nilijiunga na ngazi za wale wanaoeneza injili. Baada ya kupitia muda huu wa shida, nilikuwa na azimio zaidi na nilikomaa zaidi kuliko hapo awali, na nilithamini hata zaidi nafasi ya kutekeleza wajibu wangu. Kwa sababu nilikuwa nimeona sura ya kweli ya upinzani wa serikali ya CCP dhidi ya Mungu na ukatili kwa watu, nilikuwa na hisia nzito hata zaidi juu ya jinsi wokovu wa Mungu ulivyo wa thamani. Mungu asingekuja binafsi, katika mwili, kufanya kazi ya kuleta wokovu kwa wanadamu, wale wote wanaoishi chini ya utawala wa Shetani wangeangamizwa na kumezwa naye. Kuanzia wakati huo kwendelea, wakati wowote nilipokuwa nikitimiza wajibu wangu, mtazamo wangu ulikuwa tofauti sana na jinsi ulivyokuwa zamani; nilihisi kuwa kazi ya kueneza injili na kuokoa roho za watu ilikuwa muhimu sana, na nilitaka kutoa uaminifu wangu wote na kutumia nguvu zangu zote kwa maisha yangu yote kuleta watu zaidi mbele za Mungu. Nilitaka kuwawezesha pia kuamka kutoka katika mkanganyo na udanganyifu wa serikali hii imkanayo Mungu, wakubali ruzuku ya uzima ya Mungu, na kupata wokovu wa Mungu. Nikikumbuka miaka hiyo miwili mirefu sana ya kufungwa, najua kwamba Shetani alijaribu bure kutumia dhuluma yake ya kidikteta kunilazimisha nimsaliti Mungu. Hata hivyo, Mungu alitumia mazingira hayo mabaya kuongeza imani, uaminifu, na utiifu wangu Kwake, Akitakasa hisia zangu zilizokanganywa za upendo Kwake, na kuniruhusu nitambue hekima na uweza wa Mungu na kupata ufahamu wa kina wa ukweli kwamba Mungu ndiye wokovu wa wanadamu na kwamba Yeye ni upendo! Kutoka moyoni mwangu nilitoa ibada na sifa isiyo na kifani kwa Mungu!

Iliyotangulia: 6. Baada ya Kuvumilia Shida, Upendo Wangu kwa Mungu Ni Thabiti Hata Zaidi

Inayofuata: 8. Mateso na Majaribio—Baraka za Kufadhiliwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

3. Ujana Usio na Majuto Yoyote

Hata kama miaka bora zaidi ya ujana wangu ilitumika gerezani; katika miaka hii saba na miezi minne nilipopitia shida kwa sababu ya imani yangu katika Mungu, sina malalamiko na sina majuto, kwa sababu ninaelewa ukweli fulani na nimepitia upendo wa Mungu. Nahisi kuwa kuna maana na thamani kwa mateso yangu; hili ni jambo la pekee la utukufu na neema ambazo Mungu alinitengenezea, hili ni pendeleo langu!

24. Kuinuka Kupitia Ukandamizaji wa Giza

Maneno ya Mungu yalinipa kitu imara cha kutegemea! Kiliniruhusu kufurahia nuru na mwongozo wa maneno ya Mungu wakati wa maumivu yangu ya kuzidi kiasi na udhaifu, ambayo ndiyo iliyokuwa njia ya pekee ambayo ningeweza kupita kipindi hiki cha giza na kilichorefuka kupita kiasi Ingawa nimepata uzoefu wa kukamatwa na kuteswa mara nyingi na serikali ya CCP, na mwili wangu umepitia ukatili usio na huruma na mateso, kwa kweli naelewa ukweli mwingi ambao sikuufahamu katika siku za nyuma na ninaona kwa dhahiri tabia ya kishetani ya uovu unaopinga maendeleo wa serikali China. Nimepata uzoefu pia wa upendo wa kweli wa Mwenyezi Mungu kwangu na nimeonja hekima inayoweza ya Mwenyezi Mungu na matendo ya ajabu. Huniamsha kutafuta kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu. Leo, bado ninatimiza wajibu wangu katika kanisa kama nilivyofanya zamani; mimi humfuata Mungu katika njia sahihi ya uzima, mimi hutafuta ukweli na hutafuta kuishi maisha ya maana.

1. Upendo wa Mungu Ulikuwa Nami Katika Gereza la Giza la Ibilisi

Wakati huo, licha ya mimi kuteswa na kukandamizwa na ibilisi waovu, na kuwa ukingoni mwa kifo mara kadhaa, Mwenyezi Mungu alitumia mkono Wake wa nguvu kuniongoza na kunilinda, kunirudisha kwa uhai, na kunipeleka kwa usalama…. Kupitia hili, kwa kweli nilipitia uvukaji mipaka na ukuu wa nguvu ya uhai wa Mungu, na kupata utajiri wa thamani wa maisha niliyotunikiwa na Mungu.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki