2. Ukweli ni nini, na maarifa ya Biblia na mafundisho ni nini

Maneno Husika ya Mungu:

Kuwa na uwezo wa kuyaeleza maneno ya Mungu kwa uwazi haimaanishi kwamba wewe unaumiliki uhalisi—mambo si rahisi kama ulivyoweza kufikiria. Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake, inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hili tu ndilo linalochukuliwa kama uhalisi, na hili tu ndilo linachukuliwa kama wewe kumiliki uelewa na kimo cha kweli. Lazima uwe na uwezo wa kuhimili uchunguzi kwa muda mrefu, na lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kuidhihirisha sura ambayo inahitajika kwako na Mungu; isiwe mkao tu, lakini ni lazima ibubujike kwa kawaida kutoka ndani mwako. Hapo tu ndipo basi utakapokuwa na uhalisi kikweli, na ndipo tu basi utakapopata maisha. Wacha Nitumie mfano wa jaribio la watendaji huduma ambao kila mtu ana uzoefu nao. Mtu yeyote anaweza kuzungumzia nadharia zenye fahari sana kuhusu watendaji huduma, na kila mtu ana ufahamu unaofaa wa mada hii; wanazungumza juu yake na kila usemi unazidi ule wa awali, kana kwamba kuna mashindano. Hata hivyo, kama mwanadamu hajapitia jaribio kubwa, ni vigumu kusema ana ushahidi mzuri. Kwa ufupi, kuishi kwa kudhihirisha kwa mwanadamu bado kuna upungufu mwingi, na hii inatofautiana na uelewa wake. Kwa hiyo, bado hakijakuwa kimo halisi cha mwanadamu, na bado hayajakuwa maisha ya mwanadamu. Kwa sababu uelewa wa mwanadamu haujaletwa katika uhalisi, kimo chake bado ni kama ngome iliyojengwa kwenye mchanga, ikiyumbayumba na ikiwa karibu kuanguka. Mwanadamu anao uhalisi kidogo mno—ni vigumu kuupata uhalisi wowote katika mwanadamu. Kunao uhalisi kidogo mno unaobubujika kwa asili kutoka kwa mwanadamu na uhalisi wote katika maisha yake umelazimishwa, ndiyo maana nasema kwamba mwanadamu hamiliki uhalisi wowote. Usiweke hisa nyingi sana katika wanadamu wakisema kwamba upendo wao wa Mungu haubadiliki kamwe—hiki tu ndicho kile wao husema kabla ya kukabiliwa na majaribu. Mara tu wanapokabiliwa na majaribu kwa ghafla, mambo ambayo wao hunena kwa mara nyingine tena hayalingani na uhalisi, na kwa mara nyingine yatathibitisha kwamba wanadamu hawana uhalisi. Inaweza kusemwa kwamba wakati wowote unapokumbana na mambo ambayo hayalingani na dhana zako nayo yanakuhitaji kujiweka kando, haya ni majaribu yako. Kabla mapenzi ya Mungu kufichuliwa, kuna mtihani mkali kwa kila mwanadamu, jaribio kubwa kwa kila mtu—je, waweza kuliona wazi jambo hili? Wakati Mungu anapotaka kuwajaribu wanadamu, Yeye daima huwaacha kufanya maamuzi yao kabla ya ukweli wa uhalisi kufichuliwa. Yaani wakati Mungu anamweka mwanadamu katika majaribu, kamwe Yeye hatakwambia ukweli, na hivyo ndivyo wanadamu wanaweza kufichuliwa. Hii ni njia mojawapo ambayo Mungu huifanya kazi yake, ili kuona kama unamwelewa Mungu wa leo, na ili kuona kama unaumiliki uhalisi wowote. Je, kweli wewe huna shaka yoyote kuhusu kazi ya Mungu? Je, utaweza kusimama imara wakati jaribio kuu linakujia? Ni nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Nahakikisha hakutakuwa na matatizo”? Nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Wengine wanaweza kuwa na mashaka, lakini Mimi sitakuwa na shaka kamwe”? Kama vile nyakati Petro alipitia majaribu—alikuwa siku zote akizungumza maneno makubwa kabla ukweli haujafichuliwa. Huu sio udhaifu wa kibinafsi wa kipekee kwa Petro; hii ni shida kubwa zaidi inayomkabili kila mwanadamu sasa. Kama ningetembelea maeneo kadhaa, au kama ningewatembelea ndugu na dada kadhaa, kuuangalia uelewa wenu wa kazi ya Mungu ya leo, hakika mngeweza kweli kuzungumza kuhusu mengi ya uelewa wenu, nayo ingeonekana kwamba ninyi hamna mashaka yoyote. Kama ningewauliza: “Je, kweli waweza kutabainisha kwamba kazi ya leo inatekelezwa na Mungu Mwenyewe? Bila shaka yoyote”? ungejibu bila shaka: “Bila shaka yoyote, ni kazi inayotekelezwa na Roho wa Mungu.” Mara tu unapojibu kwa namna hiyo, kwa hakika usingekuwa hata na chembe cha shaka na unaweza hata kuhisi starehe kubwa—unaweza kuhisi kuwa umepata uhalisi kiasi kidogo. Wale ambao mara nyingi huelewa mambo kwa njia hii ni wale ambao wanamiliki uhalisi kidogo zaidi; kadri mtu anavyodhani kwamba amelipata, ndivyo atakavyokosa uwezo wa kusimama imara katika majaribio. Ole wao walio na kiburi na wenye maringo, na ole wao wasio na maarifa ya wao wenyewe. Watu kama hawa ni hodari katika kuzungumza ilhali huendelea vibaya zaidi katika matendo yao. Wakati kuna dalili ndogo zaidi ya matatizo, watu hawa wataanza kuwa na mashaka na mawazo ya kukata tamaa huingia akilini mwao. Hawana umiliki wa uhalisi wowote; yote waliyo nayo ni nadharia zenye fahari zaidi kuliko zile za dini, bila ya hali halisi ambazo Mungu anadai sasa. Nachukizwa zaidi na wale wanaosema kuhusu nadharia tu nao hawana uhalisi. Wao kufanya kilio kikubwa zaidi wanapoitenda kazi yao, lakini wao husambaratika punde tu wanapokabiliwa na uhalisi. Je, si inaonyesha kwamba watu hawa hawana uhalisi? Haijalishi jinsi upepo na mawimbi yalivyo kali, kama unaweza kubaki umesimama bila hata dalili ya shaka kuingia mawazoni mwako, na unaweza kusimama imara na usiwe kati hali ya kukana hata kama hakuna mtu mwingine aliyebaki, basi hili linachukuliwa kama wewe kuwa na uelewa wa kweli na wewe kuwa na umiliki wa uhalisi.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ndiko Kuwa na Uhalisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Masharti ya Mungu kwa wanadamu siyo tu kuweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Je, si hiyo itakuwa rahisi sana? Kwa nini basi Mungu anazungumza kuhusu kuingia katika maisha? Kwa nini Anaongea kuhusu mabadiliko? Kama mtu ana uwezo wa mazungumzo matupu tu kuhusu uhalisi, mabadiliko katika tabia yangeweza kupatikana? Kulifunza kundi la wanajeshi wazuri wa ufalme sio sawa na kuwafunza wanadamu ambao wanaweza tu kuongea kuhusu uhalisi au watu ambao hujigamba tu, bali ni kuwafunza wanadamu ambao wanajivunia tu, lakini wanadamu ambao wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu wakati wote, ambao ni wagumu bila kujali vikwazo wanavyokumbana navyo, na wanaoishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu wakati wote, na hawarudi kwa ulimwengu. Huu ndio uhalisi ambao Mungu anauzungumzia, nayo ni matakwa ya Mungu kwa binadamu. Kwa hiyo, usiuone uhalisi ulionenwa na Mungu kama rahisi sana. Kupata nuru tu kwa Roho Mtakatifu sio sawa na kuumiliki uhalisi: Hiki sicho kimo cha wanadamu, lakini neema ya Mungu, nayo haihusishi mafanikio yoyote ya wanadamu. Kila mwanadamu ni lazima ayavumilie mateso ya Petro, na hata zaidi aumiliki utukufu wa Petro, ambao ndio watu huishi kwa kudhihirisha baada ya kupata kazi ya Mungu. Hii tu ndiyo inaweza kuitwa uhalisi. Usidhani kwamba utamiliki uhalisi kwa sababu unaweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Huu ni uongo, huu haulingani na mapenzi ya Mungu, na hauna maana halisi. Usiseme mambo kama haya katika siku zijazo—komesha misemo kama hii! Wale wote walio na uelewa wa uongo wa maneno ya Mungu ni makafiri. Hawana maarifa yoyote halisi, sembuse kimo chochote halisi; wao ni watu wenye kujigamba bila ya uhalisi. Hiyo ni, wale wote wanaoishi nje ya dutu ya maneno ya Mungu ni makafiri. Wale wanaoonekana kuwa makafiri na wanadamu ni wanyama mbele za Mungu, na wale wanaoonekana kuwa makafiri na Mungu ni wale ambao hawana maneno ya Mungu kama maisha yao. Kwa hiyo, wale ambao hawana uhalisi wa maneno ya Mungu nao wanashindwa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ni makafiri. Nia ya Mungu ni kufanya iwe kwamba kila mmoja anaishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu. Sio tu kwamba kila mtu anaweza kuzungumza kuhusu uhalisi, lakini muhimu zaidi, kwamba kila mmoja anaweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ndiko Kuwa na Uhalisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ikiwa mmesoma maneno mengi ya Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandiko na hamna maarifa ya moja kwa moja ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu halisi, basi hutajua neno la Mungu. Kwa kadiri inavyokuhusu, neno la Mungu si uzima, bali tu nyaraka zisizovutia. Na ikiwa unaishi tu kwa kufuata nyaraka zisizovutia, basi huwezi kuelewa asili ya neno la Mungu wala hutaelewa mapenzi Yake. Ni wakati tu ambapo unapitia neno Lake katika matukio yako halisi ndipo maana ya kiroho ya neno la Mungu itafichuka kwako, na ni kupitia uzoefu tu ndiyo unaweza kuelewa maana ya kiroho ya ukweli mwingi na ufungue siri za neno la Mungu. Usipouweka katika vitendo, basi bila kujali jinsi neno Lake lilivyo dhahiri, yote uliyoelewa ni nyaraka na mafundisho matupu tu, ambayo yamekuwa kanuni za kidini kwako. Je, Mafarisayo hawakufanya hivi? Mkitenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa la utendaji kwenu; usipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwako ni hekaya ya mbinguni ya tatu tu.

Kimetoholewa kutoka katika “Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga ulivyo ufuoni, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Je, wewe hujaribu kuwapumbaza watu kwa kufanya hivi? Je, unafanya maonyesho matupu, bila dutu ya kuyasitiri? Mienendo yote kama hii ni ya madhara kwa watu! Kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisi zaidi, na ndivyo inavyokosa zaidi uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisi; kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya umuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisi, maana watu hawajazipitia wao binafsi, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kuwaongoza wengine katika njia sahihi, na watawapotosha. Je, hili halileti madhara kwa watu? Angalau kabisa, unapaswa kuweza kutatua shida za sasa za watu na kuwaruhusu kupata kuingia; hii tu ndiyo inachukuliwa kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno ya kifahari, ya ajabu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo, na kunaweza kuongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuendelea kwa namna hii kutazalisha mafundisho mengi, ambazo zitawafanya watu wakuchukie. Hivyo ndivyo ulivyo udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli unadhalilisha.

Kimetoholewa kutoka katika “Sisitiza Uhalisi Zaidi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mtu asipoutafuta ukweli, kamwe hatauelewa. Unaweza kusema maandiko na mafundisho mara elfu kumi, lakini bado yatakuwa tu maandiko na mafundisho. Baadhi ya watu husema tu, “Kristo ndiye ukweli, njia na uzima.” Hata ukirudia maneno haya mara elfu kumi, bado itakuwa ni bure; huna ufahamu wa maana yake. Kwa nini inasemwa kuwa Kristo ndiye ukweli, njia na uzima? Je, unaweza kuelezea kwa ufasaha ufahamu uliopata kuhusu haya kwa uzoefu? Je, umeingia katika uhalisi wa ukweli, njia na uzima? Mungu ametamka maneno yake ili wewe uweze kuyapata na kupata maarifa; kuongea tu maandiko na mafundisho haina maana. Unaweza tu kujijua mara unapoelewa na kuingia katika maneno ya Mungu. Ikiwa huelewi maneno ya Mungu, basi huwezi kujijua. Unaweza tu kumaizi unapokuwa na ukweli; bila ukweli huwezi kumaizi. Unaweza tu kuelewa kikamilifu jambo unapokuwa na ukweli; bila kuwa na ukweli huwezi kuelewa jambo. Unaweza tu kujijua unapokuwa na ukweli; bila kuwa naukweli huwezi kujijua. Asili yako inaweza tu kubadilika unapokuwa na ukweli; bila ukweli asili yako haiwezi kubadilika. Ni baada tu ya wewe kuwa na ukweli ndipo unaweza kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu; bila ukweli huwezi kutumiki kulingana na mapenzi ya Mungu. Ni baada tu ya kuwa na ukweli ndipo unaweza kumwabudu Mungu; bila ukweli, ibada yako itakuwa tu utendaji wa kaida za kidini. Haya yote yanategemea kupata ukweli kutoka kwa maneno ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Watu wengine hufanya kazi na kuhubiri na, ingawa kwa juu juu inaonekana kana kwamba wanashiriki kuhusu neno la Mungu, yote wanayozungumza kuhusu ni maana sisisi ya neno la Mungu, lakini hakuna kitu halisi kinachotajwa. Mahubiri yao ni kama mafundisho kutoka kwa kitabu cha kiada cha lugha, yanapangwa kitu kimoja baada ya kingine, kipengele baada ya kipengele, na baada ya wao kumaliza kila mtu huwasifu, kwa kusema: “Mtu huyu ana uhalisi. Alihubiri vizuri sana na kwa maelezo ya kina sana.” Baada ya wao kumaliza kuhubiri, wanawaambia wengine wayaweke yote pamoja na kuyatuma kwa kila mtu. Matendo yao yanakuwa kuwadanganya wengine na yote wanayohubiri ni uongo. Kwa juu juu, inaonekana kana kwamba wanahubiri neno la Mungu tu na linaonekana kulingana na ukweli. Lakini kwa utambuzi ulio makini zaidi, utaona kwamba ni maandishi na mafundisho tu na fikira za uongo pamoja na mawazo na mawazo kiasi ya binadamu na vile vile sehemu fulani zinazomwekea Mungu mipaka. Je, kuhubiri kwa namna hii hakuingilii kazi ya Mungu? Ni huduma inayompinga Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Mmekengeuka katika kufanya kwenu muhtasari wa ukweli; baada ya kufanya muhtasari wote huu, matokeo yamekuwa tu sheria. Kutoa kwenu “muhtasari kuhusu ukweli” hakufanywi ili watu wapate maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, kunawafanya watu wawe weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka katika ukweli. Wao huonekana kuelewa lengo la kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno na mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli; si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia. Unakusanya vitabu hivi au vifaa hivyo, na kisha unamiliki kipengele hiki cha mafundisho au kipengele kile cha ujuzi. Wewe ni msemaji wa kiwango cha juu wa mafundisho—lakini ni nini kinachofanyika unapomaliza kunena? Watu basi hawana uwezo wa kupitia, hawana ufahamu wa kazi ya Mungu, wala hawajifahamu. Mwishowe, yote ambayo watakuwa wamepata ni virai na kanuni, na wanaweza kuzungumza juu ya mambo hayo machache pekee. Mungu angefanya jambo jipya, je, ungeweza kulinganisha mafundisho yote unayojua na hilo? Hayo mambo yako ni kanuni tu na wewe unawafanya watu wajifunze theolojia tu, kutowaruhusu kupitia neno la Mungu au ukweli. Kwa hivyo, vitabu hivyo ambavyo mnakusanya vinaweza kuwaleta wengine katika theolojia na maarifa tu, katika virai vipya na katika kanuni na mila mpya. Haviwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu au kuwaruhusu kuuelewa ukweli au mapenzi ya Mungu. Unafikiria kwamba kwa kuuliza maswali hayo moja baada ya lingine, ambayo kisha unayajibu na ambayo unayaandikia maelezo, tabia ya aina hiyo itawafanya ndugu zako kuyaelewa. Unafikiri kwamba mbali na kuwa rahisi kukumbuka, masuala haya ni wazi mara moja, na kwamba hii ni njia nzuri sana ya kufanya vitu. Lakini kile wanachokielewa siyo maana halisi iliyokusudiwa ya ukweli na hakilingani na uhalisi—ni maneno na mafundisho tu. Hivyo ingekuwa bora zaidi kama wewe hungefanya mambo haya hata kidogo. Kufanya hivi ni kuwaongoza watu kuelewa na kuwa weledi wa maarifa. Wewe huwaleta wengine katika mafundisho, katika dini, na kuwafanya wamfuate na kumwamini Mungu ndani ya mafundisho ya dini. Je, huko si kuwa sawa tu na Paulo? Wewe hufikiri kwamba kupata weledi wa maarifa ya ukweli ni muhimu hasa, na vile vile kukariri mafungu mengi ya maneno ya Mungu. Lakini jinsi watu wanavyoelewa neno la Mungu si muhimu hata kidogo. Ninyi hudhani ni muhimu sana kwa watu kuweza kukariri mengi ya maneno ya Mungu, kuweza kuzungumza mafundisho mengi na kugundua fomyula nyingi ndani ya maneno ya Mungu. Kwa hiyo, siku zote ninyi hutaka kuweka katika mfumo vitu hivi ili watu wote washirikiane, wakisema mambo sawa, na kuzungumza kuhusu mafundisho, ili wawe na maarifa sawa na kutii kanuni sawa—hili ndilo lengo lenu. Ninyi kufanya hili kunaonekana kuwa kwa ajili ya watu kupata ufahamu, wakati kinyume chake hamjui kwamba hili linawaleta watu katikati ya kanuni ambazo ziko nje ya ukweli wa maneno ya Mungu. Ili kuwaruhusu watu wawe na ufahamu halisi wa ukweli, ni lazima uuunganishe na uhalisi na kazi, na kutatua shida za utendaji kulingana na ukweli wa maneno ya Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo watu wanaweza kuelewa ukweli na kuingia katika uhalisi, na kufanikisha matokeo kama hayo tu ndiko kuwaleta watu mbele ya Mungu kwa kweli. Ikiwa yote unayozungumzia ni nadharia za kiroho, mafundisho, na kanuni, ikiwa unaweka juhudi katika maneno sisisi tu, yote unayoweza kufanikisha ni kuwafanya watu waseme mambo sawa na kufuata kanuni, lakini hutaweza kuwaongoza watu kuelewa ukweli. Hasa hutaweza kuwafanya watu wajielewe vizuri zaidi, na kufanikisha toba na mabadiliko. Kuzungumzia nadharia za kiroho kukichukua nafasi ya kuingia katika uhalisi wa ukweli, haitahitajika wewe kuongoza kanisa.

Kimetoholewa kutoka katika “Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 1. Maana ya Ukweli

Inayofuata: 3. Matokeo ya kutegemea maarifa ya Biblia na nadharia ya theolojia katika imani ya mtu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki