1. Maana ya Ukweli

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1).

“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu … aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).

“Mimi ndiye njia, ukweli, na uzima” (Yohana 14:6).

“Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli” (Yohana 17:17).

Maneno Husika ya Mungu:

Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ukweli na maisha. Ukweli kwa mwanadamu ni kitu ambacho hawawezi kukosa katika maisha yao, kitu ambacho hawawezi kuishi bila; unaweza pia kusema kwamba ndicho kitu kikuu zaidi. Ingawa huwezi kukiangalia au kukigusa, umuhimu wake kwako hauwezi kupuuzwa; ndicho kitu cha pekee kinachoweza kukuletea pumziko moyoni mwako.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Haijalishi kama maneno yanayonenwa na Mungu ni makavu au makubwa katika mwonekano wa nje, yote ni ukweli ulio lazima kwa mwanadamu anapoingia katika uzima; ni chemichemi ya maji ya uzima yanayomwezesha kuishi katika roho na mwili. Yanatosheleza kile ambacho mwanadamu anahitaji ili awe hai; kanuni na imani ya kufanya maisha yake ya kila siku; njia, lengo, na mwelekeo ambao lazima apitie ili kupokea wokovu; kila ukweli ambao anapaswa awe nao kama kiumbe aliyeumbwa mbele za Mungu; na kila ukweli jinsi mwanadamu anavyotii na kumwabudu Mungu. Ni uhakika ambao unahakikisha kuishi kwa mwanadamu, ni mkate wa kila siku wa mwanadamu, na pia ni nguzo ya msaada inayowezesha mwanadamu kuwa na nguvu na kusimama. Yamejaa utajiri wa ukweli wa ubinadamu wa kawaida anavyoishi binadamu aliyeumbwa, yamejaa ukweli ambao mwanadamu anatumia kutoka kwa upotovu na kuepuka mitego ya Shetani, yamejaa mafunzo bila kuchoka, kuonya, kuhamasisha na furaha ambayo Muumba anampa binadamu aliyeumbwa. Ni ishara ambayo inawaongoza na kuwaelimisha wanadamu kuelewa yale yote yaliyo mazuri, hakika inayohakikisha kuwa wanadamu wataishi kwa kudhihirisha na kumiliki yale yote yaliyo ya haki na mema, kigezo ambacho watu, matukio, na vitu vyote vinapimwa, na pia alama ya usafiri inayowaongoza wanadamu kuelekea wokovu na njia ya mwanga.

Kimetoholewa kutoka katika “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ukweli si wa kifomyula, wala si sheria. Haujakufa—ni uzima wenyewe, ni kitu ambacho kina uhai, na ni kanuni ambayo lazima kilichoumbwa kifuate katika Maisha na kanuni ambayo lazima mwanadamu awe nayo katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho lazima, kwa vyoyote vile, uelewe kupitia uzoefu. Haijalishi ni katika awamu gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho ni vitu ambavyo vimeonyeshwa vyote katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho mwenyewe ni ukweli kwa njia yake; ukweli ni dhihirisho halisi la tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Unafanya kile Mungu Alicho nacho kuonyesha waziwazi kile Mungu alisema; unakuonyesha moja kwa moja kile ambacho Mungu hapendi, kile ambacho Hapendi, kile Anachokutaka ufanye na kile ambacho Hakuruhusu ufanye, watu ambao Anawachukia na watu ambao Anawafurahia. Katika ule ukweli ambao Mungu anaonyesha watu wanaweza kuona furaha, hasira, huzuni, na shangwe Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake.

Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake. Ukisema kwamba kuwa na uzoefu fulani kunamaanisha kuwa una ukweli, basi unaweza kuwakilisha tabia ya Mungu? Huwezi. Mtu anaweza kuwa na uzoefu fulani ama mwanga kuhusu kipengele fulani ama upande wa ukweli, lakini hawezi kuwatolea wengine milele, kwa hivyo mwanga wake sio ukweli; ni kiwango tu ambacho kinaweza kufikiwa na mtu. Ni uzoefu unaofaa tu na ufahamu unaofaa ambao mtu anapaswa kuwa nao, ambao ni uzoefu na ufahamu wake halisi wa ukweli. Mwanga huu, nuru na uelewa kwa msingi wa uzoefu hayatawahi kuwa mbadala wa ukweli; hata kama watu wote wamepata uzoefu wa ukweli huu kabisa, na wakiweka pamoja uzoefu na ufahamu wao wote, hilo bado halilingani na ukweli huo mmoja. Kama ilivyosemwa zamani, “Nilifupisha hili kwa ajili ya dunia ya binadamu kwa kanuni: Miongoni mwa wanadamu hakuna yule anayenipenda Mimi.” Hii ni kauli ya ukweli, ni asili ya kweli ya maisha, ni kitu chenye cha maana sana, ni udhihirisho wa Mungu binafsi. Unaweza kuipitia. Ukiipitia kwa miaka mitatu utakuwa na uelewa usio na kina, ukiipitia kwa miaka minane utapata uelewa zaidi, lakini uelewa wako hautaweza kuwa mbadala wa kauli ya ukweli. Mtu mwingine akipata uzoefu wake kwa miaka miwili atakuwa na uelewa mdogo; akiupitia kwa miaka kumi atakuwa na uelewa wa juu, na akipata uzoefu kwa maisha yake yote atapata uelewa mkubwa zaidi, lakini mkiuweka uelewa wenu pamoja, haijalisha uelewa wa kiwango kipi, uzoefu wa kiwango kipi, ufahamu kiasi gani, mwanga wa kiasi kipi, ama mifano mingapi ambayo ninyi wawili mnayo, hayo yote hayawezi kuwa mbadala wa kauli hiyo. Ninamaanisha nini na hili? Namaanisha kwamba maisha ya mwanadamu daima yatakuwa maisha ya mwanadamu, na haijalishi uelewa wako unalingana vipi na ukweli, kulingana na maana ya Mungu, kulingana na nia za Mungu, hayataweza kamwe kuwa mbadala wa ukweli. Kusema kuwa watu wana ukweli kunamaanisha kuwa wana uhalisi fulani, kuwa wana uelewa fulani wa ukweli wa Mungu, kuwa wana kuingia wa kweli katika maneno ya Mungu, kuwa wana uzoefu fulani wa kweli na maneno ya Mungu, na kuwa wako katika njia sahihi katika imani yao kwa Mungu. Kauli moja tu ya Mungu inatosha mtu kupata uzoefu kwa maisha yake yote; hata kama watu wangekuwa na uzoefu wa maisha kadhaa ama wa milenia kadhaa, bado hawangeweza kuupitia ukweli kabisa. Kama umeelewa tu maneno ya juu juu kisha useme kuwa una ukweli, je si hilo halina msingi?

Kimetoholewa kutoka katika “Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Katika kuonyesha Kwake ukweli, Mungu huonyesha tabia na kiini Chake; havionyeshwi kulingana na mihutasari ya wanadamu ya mambo mbalimbali chanya na njia za kuzungumza ambazo wanadamu wanatambua. Maneno ya Mungu ni maneno ya Mungu; maneno ya Mungu ni ukweli. Hayo ndiyo msingi na sheria ambayo kwayo wanadamu wanapaswa kuishi, na hizo zinazodaiwa kuwa kanuni zinazotokana na binadamu zimelaaniwa na Mungu. Hazikubaliwi na Yeye, sembuse kuwa asili au msingi wa matamshi Yake. Mungu huonyesha tabia Yake na kiini Chake kupitia maneno Yake. Maneno yote yaliyotolewa na maonyesho ya Mungu ni ukweli, kwa maana Yeye anacho kiini cha Mungu, na Yeye ndiye uhalisi wa mambo yote chanya. Ukweli kwamba maneno ya Mungu ni ukweli haubadiliki kamwe, bila kujali jinsi wanadamu hawa wapotovu wanavyoyachukulia au kuyafafanua, wala jinsi wanavyoyaona au kuyaelewa. Haijalishi ni maneno mangapi ya Mungu ambayo yamezungumzwa, na bila kujali jinsi binadamu hawa wapotovu na wenye dhambi wanavyoyashutumu kwa kiasi kipi, hata kiasi kwamba hawayasambazi, na hata kufikia kiwango ambacho yanadharauliwa na wanadamu wapotovu—hata katika hali hizi, bado kuna ukweli ambao hauwezi kubadilishwa: Hizi zinazodaiwa kuwa mila na desturi ambazo wanadamu huthamini haziwezi kuwa vitu chanya na haziwezi kuwa ukweli, hata sababu zilizopo hapo juu zikizingatiwa. Hili haliwezi kubadilika.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Ukweli ni Nini” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Tamaduni za jadi za wanadamu na njia za kuishi hazitakuwa ukweli kwa sababu ya mabadiliko au kupita kwa wakati, na wala maneno ya Mungu hayatakuwa maneno ya mwanadamu kwa sababu ya shutuma na kusahau kwa wanadamu. Kiini hiki hakitabadilika kamwe; ukweli ni ukweli kila wakati. Kuna ukweli ndani ya hili: Hiyo misemo yote inayofupishwa na wanadamu inatoka kwa Shetani—ni fikira na mawazo ya wanadamu, hata inatokana na hamaki ya binadamu, na haihusiani hata kidogo na mambo chanya. Maneno ya Mungu, kwa upande mwingine, ni maonyesho ya kiini na hadhi ya Mungu. Yeye huyaonyesha maneno haya kwa sababu gani? Kwa nini Ninasema maneno hayo ni ukweli? Sababu ni kwamba Mungu anatawala juu ya sheria, kanuni, vyanzo, viini, uhalisi na siri zote za vitu vyote, na vimefumbatwa mkononi Mwake, na ni Mungu pekee Anayejua kanuni, uhalisi, ukweli, na siri zote za vitu vyote; Anajua asili ya vitu hivyo na vyanzo vyao ni nini hasa. Kwa hivyo, ni ufafanuzi wa vitu vyote uliotajwa katika maneno ya Mungu pekee ndio sahihi kabisa, na mahitaji kwa wanadamu yaliyo ndani ya maneno ya Mungu ndicho kiwango pekee kwa wanadamu—kigezo pekee ambacho mwanadamu anapaswa kuishi kwa kufuata.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Ukweli ni Nini” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 3. Ufafanuzi wa Mungu mmoja wa kweli kama Mungu wa utatu ni upinzani na kumkufuru Mungu

Inayofuata: 2. Ukweli ni nini, na maarifa ya Biblia na mafundisho ni nini

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

8. Jinsi ambavyo Mungu anatamatisha enzi ya giza ya utawala wa Shetani katika siku za mwisho

Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa maelfu ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu, Atabadilisha namna wanavyomfahamu na mitazamo yao Kwake, ili kwamba maarifa yao juu ya Mungu, yaweze kuanza katika rekodi safi, na mioyo yao itakuwa imesafishwa upya na kubadilishwa.

5. Jinsi ambavyo Mungu aliwaongoza na kuwaruzuku wanadamu hadi leo

Kazi ya usimamizi wa Mungu ilianza Alipoumba ulimwengu, na mwanadamu ni kiini cha kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa kila kitu, unaweza kusemwa, ni kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu Kazi ya usimamizi Wake imesambaa katika maelfu ya miaka, na haijatekelezwa katika dakika na sekunde tu, ama kufumba na kufumbua, ama katika mwaka mmoja au miwili, ilimbidi Aumbe vitu vingine zaidi kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, kama vile jua, mwezi, na aina zote za viumbe walio hai, na chakula na mazingira kwa ajili ya wanadamu. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa usimamizi wa Mungu.

20. Asiyeamini ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii...

2. Kwa nini inasemekana kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote wanaitembea njia ya Mafarisayo na kiini chao ni kipi

Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki