Dibaji

Katika mwaka wa 1991, Mwenyezi Mungu mwenye mwili alionekana na kuanza kufanya kazi nchini China. Ameonyesha maneno milioni kadhaa, na amekuwa akifanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho akianzia na nyumba ya Mungu. Amehitimisha Enzi ya Neema, akaanza Enzi ya Ufalme, na akaanzisha injili ya ufikaji wa ufalme wa mbinguni. Mwenyezi Mungu ameonyesha ukweli wote ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, akafungua kabisa ukurasa uliotiwa muhuri katika Kitabu cha Ufunuo katika Biblia, akafichua kabisa mafumbo ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita wa jinsi Mungu anavyowaokoa wanadamu, kama vile ni nini kusudi la usimamizi wa Mungu wa wanadamu, kwa nini kuna hatua tatu katika wokovu wa Mungu wa wanadamu, jinsi Mungu anavyofanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, fumbo la kupata mwili, habari halisi ya Biblia, mamlaka ya pekee ya Mungu, tabia ya haki ya Mungu, utakatifu wa Mungu, jinsi Shetani huwapotosha wanadamu, jinsi Mungu awaokoavyo wanadamu, fumbo la kunyakuliwa kabla ya maafa, jinsi washindi hutengenezwa, hatima ya mwisho na mwisho wa aina mbalimbali za watu, jinsi ufalme wa Kristo utakavyofanikishwa, nk. Kwa hakika limeifungua upeo mpya na kuyafurahisha macho ya wanadamu! Mwenyezi Mungu anasema: “Nitawaambia hili wakati ambapo Nitafungua kitabu Changu katika siku za mwisho. (Kitabu kinahusu maneno yote ambayo Nimeyanena, maneno Yangu katika siku za mwisho—haya yote yako ndani yake)” (“Sura ya 110” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili). “Kazi katika siku za mwisho inaonyesha wazi kazi ya Yehova na ile ya Yesu na mafumbo yote yasioeleweka na mwanadamu. Hii inafanywa ili kuonyesha hatima na mwisho wa binadamu na kukamilisha kazi yote ya wokovu miongoni mwa wanadamu. Hatua hii ya kazi katika siku za mwisho huleta kila kitu kufika mwisho. Mafumbo yote yasiyoeleweka na mwanadamu lazima yaelezwe ili kumpa mwanadamu ufahamu na kuweza kuelewa kwa kina katika mioyo yao. Hapo tu ndipo wanadamu wataweza kugawanywa kulinga na aina zao” (“Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno yanayoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, ni mengi, ya faida, na ya kina, yakiwaruhusu wanadamu kuona kwamba Kristo bila shaka ndiye njia, ukweli, na uzima, na kwamba Yeye huwaletea wanadamu njia ya milele ya maisha, njia ya uzima wa milele.

Bwana Yesu alisema: “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata” (Yohana 10:27). “Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa” (Ufunuo 2:7). Mwenyezi Mungu asema: “Watu Wangu wataisikiliza sauti Yangu, na kila mmoja wa wale wanaonipenda kwa kweli atarudi mbele ya kiti Changu cha enzi” (“Sura ya 1” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Tangu kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho ianze nchini China, watu kutoka kwa dini na madhehebu mbalimbali ambao kwa kweli wanamwamini Mungu, kupenda ukweli, na wanatamani kuonekana kwa Mungu, wametambua sauti ya Mungu katika maneno yaliyosemwa na Mwenyezi Mungu. Wameona kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ndiyo ukweli, na kwa kweli ni kile ambacho Roho husema kwa makanisa, na kwamba Mungu ameonekana ili kufanya kazi Yake wakati wa siku za mwisho. Watu hawa wamekusanyika mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Siku hizi watu zaidi na zaidi duniani kote wanajitahidi kuchunguza maneno na kazi ya Mwenyezi Mungu. Jamii ya binadamu imeamshwa hatua kwa hatua katika maneno ya Mungu, na imeanza kuukubali ukweli na kuujua. Maneno ya Mungu yatawaleta wanadamu katika enzi mpya—Enzi ya Ufalme. Yote yatafanikishwa kwa maneno ya Mungu, na watu wote walio na kiu ya kweli na kutafuta kuonekana kwa Mungu watarudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Huu ndio mwelekeo mkubwa; ni uhalisi ambao Mungu bila shaka atautimiza.

Kwa sasa watu wengi katika ulimwengu wote wa kidini hutaka sana na kutafuta kuonekana kwa Mungu, lakini kwa sababu hawasisitizi kutafuta kile ambacho Roho husema kwa makanisa, huwa hawasikii sauti ya Mungu na hawapokei kwa furaha kurudi kwa Mungu. Tumechukua vipengele vya ukweli wa maono yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika kazi Yake ya siku za mwisho na kuvikusanya na kuvihariri kuwa vipengele ishirini vya ukweli vya kueneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu ili watu katika nchi na sehemu zote wanaotafuta ukweli na kuonea kiu kuonekana kwa Mungu waweze kusoma na kuchunguza kazi ya siku za mwisho ya Mwenyezi Mungu, kusikia sauti ya Mungu na kuletwa katika uwepo Wake. Tumepanga maneno ya Mungu na mahubiri na ushirika kulingana na dhana za kawaida za kidini za watafutaji, ili kuwasaidia kuona kwa dhahiri upuuzi na kukosa mantiki kwa dhana za kidini kwa kuzingatia mwanga wa ukweli kutoka kwa neno la Mungu. Kwa hiyo watu wanaweza kuziacha dhana za kidini ambazo zimewafunga na kuwazuia, na kukubali wokovu wa Mungu katika siku za mwisho na kuletwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na wanaweza kufuata nyayo za Mwana Kondoo na kuingia katika enzi mpya.

Inayofuata: 1. Bwana Yesu Mwenyewe alitabiri ya kwamba Mungu angepata mwili katika siku za mwisho na kuonekana kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

4. Hakuna njia ya uzima wa milele ndani ya Biblia; mwanadamu akiishika Biblia na kuiabudu, basi hatapata uzima wa milele

Njia ya maisha si kitu ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote tu, wala hakipatikani kwa urahisi na wote. Hiyo ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote.

2. Kwa nini inasemekana kwamba “Utatu” ni kauli ya upuuzi zaidi?

Hata hivyo, wengine wanaweza kusema: “Baba ni Baba; Mwana ni Mwana; Roho Mtakatifu ni Roho Mtakatifu, na mwishowe, Watafanywa kitu kimoja.” Je, Utawafanyaje kitu kimoja? Baba na Roho Mtakatifu Wawezaje kufanywa kitu kimoja? Ikiwa Walikuwa wawili kiasili, haijalishi Wamewekwa pamoja kwa namna gani, je, Hawataendelea kuwa sehemu mbili? Unaposema kuwa kuwafanya kuwa kitu kimoja, huko si kuunganisha sehemu mbili kutengeneza kitu kamili? Je, Hawakuwa sehemu mbili kabla ya kufanywa kitu kizima? Kila Roho ana kiini kinachotofautiana, na Roho wawili Hawawezi kufanywa kuwa kitu kimoja. Roho si chombo cha kutengenezwa, si kama chombo chochote katika ulimwengu. Kulingana na mitazamo ya wanadamu, Baba ni Roho mmoja, Mwana ni mwingine, na Roho Mtakatifu tena ni mwingine, halafu Roho Hawa huchanganyika sawa na glasi tatu za maji kuunda kitu kimoja kizima. Je, hizo si sehemu tatu zimefanywa kuwa kitu kimoja? Haya bila shaka ni maelezo ya kimakosa! Je, huku si kumgawa Mungu? Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu wanawezaje kufanywa kuwa kitu kimoja? Je, Wao si sehemu tatu zenye asili tofauti?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki