459 Mungu Aliamua Kabla Kuwa Tufuate Njia Hii

1 Sote tunaweza kuona katika uzoefu wetu wa utendaji kwamba kuna nyakati nyingi ambazo Mungu binafsi ametufungulia njia ili tuwe tunakanyaga njia iliyo imara zaidi, ya kweli zaidi. Hii ni kwa sababu hii ndiyo njia ambayo Mungu alitufungulia tangu mwanzo wa wakati na imepitishwa kwa kizazi chetu baada ya makumi ya maelfu ya miaka. Kwa hiyo tunarithi watangulizi wetu ambao hawakutembea njia hii mpaka mwisho wake; sisi ndio tumechaguliwa na Mungu kutembea sehemu ya mwisho ya njia hii.

2 Imetayarishiwa hasa sisi, na haijalishi ikiwa tutapokea baraka au kupata taabu, hakuna mwingine anayeweza kutembea njia hii. Usifanye mipango ya kutorokea mahali pengine au kupata njia nyingine, ukitamani hadhi, au kuanzisha ufalme wako mwenyewe; haya yote ni uongo. Ufalme wa Mungu ukija Atavunjavunja mataifa ya dunia, na wakati huo utaona kwamba mipango yako wewe pia imefutiliwa mbali na wale ambao wameadibiwa ni wale ambao wamevunjwa. Wakati huo Mungu atafichua kabisa tabia Yake.

3 Kwamba tumeweza kutembea njia hii mpaka leo iliamriwa na Mungu, kwa hiyo usifikirie kwamba wewe ni kitu cha kipekee au kwamba huna bahati—mtu yeyote asifanye madai kuhusu kazi ya sasa ya Mungu usije ukavunjwavunjwa kwa vipande. Nuru imenijia kupitia kazi ya Mungu, na lolote litokealo, Mungu atafanya kuwa kamili kundi hili la watu na kazi Yake haiwezi kubadilishwa—Atawafikisha watu hawa mwisho wa njia na kukamilisha kazi Yake duniani. Hiki ni kitu ambacho sote tunapaswa kuelewa.

Umetoholewa kutoka katika “Njia … (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 458 Kubali Hukumu ya Kristo wa Siku za Mwisho ili Utakaswe

Inayofuata: 461 Mungu Ameamulia Kabla Njia Ambazo Mwanadamu Lazima Atembelee

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki