9. Mtu anafaaje kutenda kuingia kuwa mtu mwaminifu?

Maneno Husika ya Mungu:

Kufuatilia ukweli ndilo jambo la muhimu zaidi, na kuutenda kwa kweli ni rahisi sana. Unapaswa kuanza kwa kuwa mtu mwaminifu na kuzungumza ukweli, na kuufungua moyo wako kwa Mungu. Ikiwa kuna kitu ambacho unahisi aibu sana kukizungumzia na ndugu zako, basi unapaswa kupiga magoti na kumwambia Mungu kukihusu kupitia sala. Unapaswa kumwambia Mungu nini? Mwambie Mungu kile kilicho moyoni mwako; usimwambie maneno matupu ya bure au kujaribu kumdanganya. Anza na kuwa mwaminifu. Ikiwa umekuwa dhaifu, basi sema umekuwa dhaifu; kama umekuwa mwovu, basi sema umekuwa mwovu; ikiwa umekuwa madanganyifu, basi sema umekuwa mdanganyifu; iwapo umekuwa na mawazo maovu na ya kudhuru kwa siri, mwambie Mungu kuyahusu. Ikiwa kila wakati wewe hushindana kwa ajili ya cheo, mwambie jambo hili pia. Mwache Mungu akufundishe nidhamu; mwache Akupangie mazingira. Mruhusu Mungu akusaidie kushinda dhiki zako na kutatua matatizo yote yako. Unapaswa kuufungua moyo wako; usiufunge. Hata ukimzuia, bado Anaweza kuona ndani yako. Hata hivyo, lakini ukimfungulia moyo, unaweza kupata ukweli. Ni njia gani ambayo unaweza kusema kuwa unapaswa kuchagua? Anza kwa kuwa mwaminifu, na hakika wasijifanye. … Moyo wako unaweza tu kufunguka ukitenda uaminifu, na mara tu moyo wako unapofunguka ndipo ukweli unaweza kuingia ndani yako, kwa hiyo, utaweza kuuelewa na kuupata. Ikiwa moyo wako daima hufungwa, na kamwe huzungumzi ukweli kwa mtu yeyote, na wewe hukwepa na asiyeshikika kila mara, basi ni nini kitakachotoka katika kukwepa kwako? Hatimaye utajiangamiza, na hutakuwa na uwezo wa kufahamu au kupata ukweli wowote.

Umetoholewa kutoka katika “Ishara Sita za Ukuaji katika Maisha” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Kuwa mwaminifu, lazima kwanza uuweke wazi moyo wako ili kila mtu aweze kuuona moyo wako, kuona vyote unavyofikiri, na kuuona uso wako wa kweli; hupaswi kujifanya ama kujaribu kujificha. Hapo tu ndipo watu watakuamini na kukuchukua kuwa mwaminifu. Hili ndilo tendo la msingi kabisa, na sharti, la kuwa mwaminifu. Daima unajifanya, daima unasingizia utakatifu, uadilifu, ukubwa na kusingizia sifa za juu za maadili. Huwaruhusu watu kuona upotovu na kushindwa kwako. Unaonyesha taswira ya uongo kwa watu, ili waamini kwamba wewe ni mwadilifu, mkuu, anayejitolea, asiyependelea na asiye na ubinafsi. Huu ni udanganyifu. Usijifanye na usijionyeshe usivyo; badala yake, jiweke wazi na uweke wazi moyo wako ili wengine waone. Iwapo unaweza kuweka wazi moyo wako ili wengine waone, yaani, ikiwa unaweza kuweka wazi yote unayofikiri na kupanga kufanya ndani ya moyo wako—bila kujali iwapo ni nzuri ama mbaya—basi wewe huwi mwaminifu? Iwapo unaweza kujiweka wazi kwa wengine waone, Mungu pia atakuona, na kusema: “Umejiweka wazi kwa wengine wakuone, na hivyo mbele Yangu bila shaka wewe ni mwaminifu pia.” Iwapo unajiweka wazi kwa Mungu wakati wengine hawaoni pekee, na daima unajifanya kuwa mkuu na mwadilifu ama mwenye haki na asiye na ubinafsi mbele yao, basi Mungu atafikiri nini na Mungu atasema nini? Mungu atasema: “Kwa kweli wewe ni mdanganyifu, wewe ni nafiki kabisa na anayejishughulisha na mambo madogo madogo, na wewe si mwaminifu.” Mungu atakuhukumu hivi. Iwapo unataka kuwa mwaminifu, basi bila kujali kile unachofanya mbele ya Mungu ama watu, unapaswa kuweza kuufungua moyo wako na kujiweka wazi.

Umetoholewa kutoka katika “Vitendo vya Msingi Kabisa vya Kuwa Mtu Mwaminifu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Leo, watu wengi wanaogopa sana kuyaleta matendo yao mbele za Mungu, na ingawa unaweza kuudanganya mwili wa Mungu, huwezi kumdanganya Roho wa Mungu. Yale yote ambayo hayawezi kustahimili uchunguzi wa Mungu hayakubaliani na ukweli nayo lazima yawekwe kando, ama unatenda dhambi dhidi ya Mungu. Kwa hivyo, haijalishi kama ni wakati unaomba, unaponena na kushiriki na ndugu na dada zako, ama unapofanya wajibu wako na kufanya biashara yako, lazima uuweke moyo wako mbele za Mungu. Unapoitimiza kazi yako, Mungu yuko nawe, na bora nia yako iwe sawa, nayo iko kwa ajili ya kazi ya nyumba ya Mungu, Mungu atakubali kila kitu ufanyacho, kwa hivyo ni lazima uweke bidii kwa dhati kujishughulisha na kuitimiza kazi yako. Unapoomba, kama una upendo kwa Mungu katika moyo wako, na kama unatafuta utunzaji wa Mungu, ulinzi, na uchunguzi, kama haya ndio nia yako, maombi yako yatafaulu. Unapoomba katika mikutano, ndivyo unafaa kufungua moyo wako na kuomba Mungu, ambia Mungu kile kilicho moyoni mwako, na bila kuongea uongo, basi maombi yako yatafaulu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Anakamilisha Wale Wanaoufuata Moyo Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Leo, hakuna asiyekubali uchunguzi wa Mungu anaweza kupokea idhini ya Mungu, na yeyote asiyemjua Mungu mwenye mwili hawezi kukamilishwa. Jiangalie nawe ujiulize kama kila kitu unachofanya kinaweza kuletwa mbele ya Mungu. Iwapo huwezi kuleta kila kitu unachofanya mbele za Mungu, hii inaonyesha kuwa wewe ni mtenda maovu. Je, watenda maovu wanaweza kufanywa wakamilifu? Kila kitu unachofanya, kila tendo, kila nia, na kila jibu lazima kiletwe mbele za Mungu. Hiyo ni, maisha yako ya kawaida ya kiroho, maombi yako, ukaribu wako na Mungu, kula na kunywa neno la Mungu, ushirika na ndugu na dada zako, kuishi maisha yako katika kanisa, na hata huduma yako katika ushirikiano wako ni vitu vyote ambavyo lazima viletwe mbele za Mungu na kuchunguzwa na Yeye. Ni matendo kama hayo ndiyo yatakayokusaidia kustawi katika maisha. Mchakato wa kukubali uchunguzi wa Mungu ni mchakato wa kutakaswa. Kadri unavyoukubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyotakaswa zaidi, kadri unavyokuwa katika uwiano na matakwa ya Mungu, ili kwamba hutasikia wito wa uasherati na ubadhirifu, na moyo wako utaishi katika uwepo wa Mungu; kadri unavyokubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyomuaibisha Shetani na kuutelekeza mwili. Kwa hivyo, kukubali uchunguzi wa Mungu ni njia ambayo watu wanafaa kutenda. Haijalishi kile unachokifanya, hata katika ushirika na ndugu na dada zako, ukiyaleta matendo yako mbele za Mungu na kutafuta uchunguzi wa Mungu, na kama nia yako ni kumtii Mungu Mwenyewe, unachotenda ni sahihi zaidi. Kama tu wewe ni mtu anayeleta kila kitu anachofanya mbele za Mungu na kukubali uchunguzi wa Mungu ndipo utakapokuwa mtu anayeishi kwa hakika katika uwepo wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Anakamilisha Wale Wanaoufuata Moyo Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu. … Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme.

Umetoholewa kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Ukitaka kuwa na uwezo katika kuutimiza wajibu wako—na sio tu kufanya kitu kwa njia isiyokuwa ya dhati na kumdanganya Mungu—basi lazima ulitatue suala la kuwa mtu mwaminifu. Wakati wa kutimiza wajibu wako lazima ukubali upogoaji na ushughulikiaji, uchunguzaji wa Roho Mtakatifu, na lazima uyatende mambo haya hasa kwa mujibu wa matakwa ya Mungu. Ukigundua kwamba u mzembe, mwombe Mungu. Ukijigundua kuwa mwenye kujaribu kumdanganya Mungu, lazima ulikiri kosa hili. Huwezi kulificha hili, kujisingizia, sembuse kupotosha ukweli ili kuwalaumu mwingine. Unahitaji kuwa makini jinsi hii kuhusu mambo unayoyatenda, na kushughulikia kila neno na tendo lako kwa moyo. Fanya maneno yako yafae uhalisi, tafuta ukweli kutoka kwa ukweli, na usiyatumie maneno ya kuongezea utamu kwa kujisingizia. Ukiligundua kosa, licha ya kumwomba Mungu, lazima pia ulikiri waziwazi kwa wengine. Usijitanibu kwa kuijali sifa yako. Unapaswa kusema ukweli kwa ujasiri. Utendaji kama huu ni wenye maana, na unaahidiwa kuwa wenye manufaa kwako. Kwanza, unaweza kuzidisha imani yako katika kuwa mtu mwaminifu. Pili, unaweza kukufundisha usiogope fedheha, na kuacha majisifu na kutojiona kuwa bora kwako. Tatu, unaweza kukupa ujasiri kusema na kuheshimu kweli. Nne, unaweza kukuza ndani mwako nia ya kuyafikiria kwa makini mambo unayoyatenda. Baada ya kufanya mazoezi jinsi hii kwa muda watu watakuwa waaminifu zaidi katika kutimiza wajibu wao, wenye uhalisi zaidi katika kutenda mambo, na wasiokuwa wenye hila. Miaka michache karibuni watakuwa watu waaminifu ambao wanakichukulia kile wanachokitenda kwa uaminifu na kwa bidii na wanawajibika wanapoyashughulikia mambo. Watu kama hao kwa kwa kulinganisha ni wenye kutegemewa katika kutimiza wajibu na kutenda kazi yao. Nyumba ya Mungu inapowatumia watu kama hao, inaweza kuahidiwa kwamba hakuna litakaloharibika.

Umetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Sasa hivi, mko katika mchakato wa kujifunza kuwa watu waaminifu. Katika mchakato wa kujifunza, mnapaswa kuzingatia nini zaidi? Mnapaswa kuzingatia kumjua Mungu, kuzingatia kuelewa ukweli, na lazima mtimize kuingia kwa kweli kutoka kwa upande chanya. Mkiingia kutoka upande chanya, upotovu kutoka kwa upande hasi utapunguka kwa kawaida, na hili ni muhimu. Kwa mfano, ili kuwa mtu mwaminifu, kwanza unahitaji kujiandaa na uhalisi na ukweli wa kuwa mtu mwaminifu. Baada ya kufanya hivi, sehemu yako aminifu itaongezeka na uongo na ujanja utapungua kwa kawaida, siyo? Kama tu kikombe kilichojazwa maji machafu. Huwezi kuyamwaga, kwa hiyo utafanya nini? Lazima umwage maji safi mazuri kiasi ndani ya kikombe hicho, na maji mazuri kwa kawaida yataondoa maji machafu. Sasa lazima mjiandae kwa ukweli, na punde ukweli unapoingia ndani yenu, mambo hasi ndani yenu yatatoweka kwa kawaida.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kutatua Tatizo la Kudanganya Kutoka kwa Chanzo Kwenda Juu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha I

Iliyotangulia: 8. Kuna tofauti ipi kati ya mtu mwaminifu na mtu mdanganyifu?

Inayofuata: 10. Mtu kutekeleza wajibu wake ni nini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

2. Kuna tofauti ipi kati ya maneno ya watu wanaotumiwa na Mungu kote katika enzi zote ambayo yanakubaliana na ukweli na maneno ya Mungu?

Ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha.

5. Matokeo ya mtu anayemwamini Mungu katika dini na ambaye hupitia mchafuko na udhibiti wa Mafarisayo na wapinga Kristo ni yapi? Mtu anaweza kuokolewa na Mungu kama anamwamini Mungu kwa njia hii?

Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua fikira zao, sembuse kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokionyesha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambao hauambatani na uhalisi na hauwezi kabisa kuwapa watu uzima.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki