Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

606 Watu Hawampi Mungu Mioyo Yao

1 Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata uzoefu wa maisha ya binadamu, Nikichunguza kwa karibu matendo yote ya mwanadamu. Hakuna aliyewahi kujitolea Kwangu kwa kweli. Hakuna aliyewahi kufuata ukweli. Hakuna aliyewahi kuwa mwangalifu Kwangu. Hakuna aliyewahi kufanya maazimio mbele Yangu na kufanya wajibu wake. Hakuna aliyewahi kuniruhusu kuishi ndani yake. Hakuna aliyewahi kunithamini kama afanyavyo maisha yake. Hakuna aliyewahi kuona kwa vitendo vya ukweli uzima wote wa uungu Wangu. Hakuna aliyewahi kutamani kuwasiliana na Mungu wa vitendo Mwenyewe.

2 Kwa sababu katika uchafu wake mwanadamu hafai kutazama utukufu Wangu, kwa maelfu ya miaka Sijawahi kujitokeza hadharani, lakini Nimebakia mafichoni; kwa sababu hii utukufu Wangu hujawahi kuwa wazi mbele ya mwanadamu, na mwanadamu daima amezama kwa shimo la kina la dhambi. Nimeusamehe udhalimu wa binadamu, lakini wanadamu hawajui jinsi ya kujihifadhi, na badala yake daima wanajiweka wazi kwa dhambi, kuruhusu dhambi kuwajeruhi. Huu si ukosefu wa mwanadamu wa kujiheshimu na kujipenda? Katikati ya binadamu, kuna kweli yeyote anayeweza kupenda? Ibada ya mwanadamu inaweza kuwa na uzito wa wakia ngapi? Hakuna bidhaa safi zilizochanganywa na kinachoitwa uhalisi wake? Si ibada yake imeungana kabisa na mkanganyiko? Ninachohitaji ni upendo wa mwanadamu usiogawanyika. Mwanadamu hanijui, na ingawa anaweza kupata kunijua, hatanipa moyo wake wa ukweli na dhati.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 19” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Mungu Atumai Kwamba Mwanadamu Anaweza Kuwa Mwaminifu kwa Maneno Yake

Inayofuata:Nani Awezaye Kuepuka Kuja kwa Nuru ya Mungu?

Maudhui Yanayohusiana