236 Nampenda Mungu Zaidi Baada ya Kupitia Hukumu Yake

1 Katika miaka mingi ya kumwamini Bwana nilisoma Biblia mara nyingi lakini sikuwahi kuelewa ukweli. Nilidhani kuacha kila kitu na kutia bidii kulimaanisha mtu anampenda Mungu. Kupitia hukumu ya maneno ya Mungu hatimaye niliona unafiki wangu mwenyewe. Nilifanya kazi na kuhubiri ili kupata tu baraka ya kunyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni. Ingawa niliteseka na nikajitumia kijuujuu, nilikuwa nikihesabu thawabu zangu kwa siri. Kulalamika wakati wa majaribio kulinifichua kama mbinafsi na wa kustahili kudharauliwa. Nilikuwa mpotovu sana, lakini niliamini kuwa nilimpenda Mungu na sikuwa na aibu. Nikiwa na nia na tamaa nyingi, ningewezaje kupata idhini ya Mungu? Hatimaye niliona kwamba kupitia miaka yangu ya kumwamini Bwana kamwe sikuwa nimemjua Mungu hata kidogo. Nasujudu na kutubu kikamilifu, natamani kukubali hukumu na utakaso.

2 Kwa kupitia hukumu ya Mungu, nimeona kuwa tabia ya Mungu ni ya haki na haivumilii kosa lolote. Siku zote nikitenda dhambi na kukiri, bado nikiishi katika dhambi, ningewezaje kustahili kuona uso wa Mungu? Majaribio na usafishaji vinafichua upotovu wangu mkubwa, namiliki ubinadamu mdogo. Nimejawa na tabia ya kishetani, bila toba ya kweli bado nina ndoto ya kuingia katika ufalme wa mbinguni. Huku nikipogolewa na kushughulikiwa, najawa na mateso, aibu na hatia. Natamani kuacha tamaa zote za kupita kiasi, kufuatilia ukweli na kujifanya kuwa mpya. Nimeazimia kutafuta kumpenda Mungu, kupitia maumivu yoyote ili kumridhisha Mungu. Sitaki hadhi au thawabu, ninaomba tu kutekeleza wajibu wangu ili moyo wangu uweze kupumzika. Bila kujali dhiki ni kuu kiasi gani, hata ikimaanisha kutoa maisha yangu, nitakuwa mwaminifu hadi mwisho kabisa. Kupitia hukumu, natakaswa, nampenda Mungu hata zaidi.

Iliyotangulia: 235 Nimeona Jinsi Ukweli Ulivyo wa Thamani

Inayofuata: 237 Sasa Nimeamka

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki