Sura ya 47. Wale Ambao Wamepoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi

Katika kazi ya kueneza injili ya Mungu ya siku za mwisho, watu walio wachache tu ndio wanaweza kuacha kila kitu na kuziacha familia zao, kufikia kiwango ambacho wanahisi hawatarudi nyumbani kwa miaka kumi au kwa maisha yao yote, na hawahisi mateso yoyote kwa sababu ya kufanya hivyo; hii ndiyo nguvu inayopewa watu na Roho Mtakatifu. Lakini kiwango hiki hakiwezi kufikiwa kupitia kwa kimo cha mtu, kwa sababu watu hawaumiliki ukweli, uaminifu fulani tu wa kutumia kwa ajili ya Mungu. Kama watu wanao uamuzi fulani wa kuutafuta ukweli, na Roho Mtakatifu kisha awape neema fulani, basi watahisi hasa kuwa na shukrani na watakuwa na nguvu za aina fulani, na hivyo wataweza kujitokeza na kutumia kwa ajili ya Mungu—hii ndiyo neema ya Mungu. Lakini wapo baadhi ya watu wasioifuata njia sahihi wakati wanapoutekeleza wajibu wao, hawautafuti ukweli hata kidogo na hata wanakosa adabu, na katika hali kama hiyo Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yao. Yaani, mtu huyo hayuko sahihi, na hata kama Roho Mtakatifu aliwahi kufanya kazi ndani yake, kazi hiyo itaharibiwa na wao watafuata bila kukusudia njia ya kwenda chini. Kama unao uamuzi wa kuutafuta ukweli, basi Roho Mtakatifu atakupa neema ya kufurahiwa, na unaweza kusonga mbele ukifuata ya njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu; ukweli utakuwa wazi zaidi na zaidi kwako wewe, uamuzi wako utakuwa thabiti zaidi na zaidi, na kazi ya Roho Mtakatifu inayofanya kazi ndani yako itakuwa rahisi zaidi na zaidi. Kama watu hawaitembelei njia sahihi basi Roho Mtakatifu, mwishowe, atawaondoa, na baada ya kuondolewa, uamuzi wao wa mwanzo, mapenzi ya mwanzo, na nguvu zao za kuacha na kutumia vyote vitatoweka, na hawataweza kujizuia dhidi ya kusema, "Kwa nini sikuwahi kumsadiki Mungu? Kama sikuwa nimemsadiki Mungu, ningekuwa ninakumbana na haya sasa?" Wakati majuto haya, malalamiko haya, na ubaya huu yanapojitokeza, Roho Mtakatifu atakuwa tayari ameacha kufanya kazi. Ingawa watu hawa wanaweza bado kutumika kuihubiri injili au kufanya kazi nyingine, kile watakachokuwa wakifanya hakitakuwa kazi ya Roho Mtakatifu, wala hakitapewa nuru au kuongozwa na Roho Mtakatifu. Kitafanywa tu kwa kutegemea akili kidogo na elimu waliyonayo. Ingawa wataweza kufanya mambo haya yote ya nje ambayo yanaweza kutimizwa kwa mwili, hayatawakilisha mwongozo wa Roho Mtakatifu, wala kuwakilisha akili ya Roho Mtakatifu. Kama tu mtoaji huduma, hata kama Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yake, mtu anaweza bado kuitoa huduma kwa kipindi fulani. Hata hivyo, anayo mawazo ya mtu, ubongo wa mtu, kufikiria kwa mtu; yeye ni tofauti na ng’ombe, farasi, au punda—anako kufikiria kwa binadamu na ni wa kiwango cha juu zaidi cha mnyama, na anaweza angaa kufanya baadhi ya mambo ambayo mtu wa kawaida anaweza kufanya. Amefuata tu njia mbaya; hauutafuti ukweli, au wokovu au kuulipiza upendo wa Mungu, hivyo anapotembea, anagundua kwamba njia hii yaishia hapo, na hana chaguo ila kuenda nyumbani na kuishi maisha ya kawaida ya familia. Kwa sasa, watu wengi wanasema haya: "Najua kwamba Mimi ni mbaya kwa kawaida! Mimi ni mwepesi sana wa kuvutwa na huruma na nimeasi mno." Haijalishi ni nini wanachosema, hawajui asili yao binafsi, wala hawafahamu hali yoyote ya ukweli; haijalishi wanaweza kuongea vyema kwa njia gani kuhusu mafundisho na wanaonekana kufahamu kila kitu, hawawezi kuweka chochote katika vitendo, na haya yanatosha kuthibitisha kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ndani yao tayari imetoweka. Hivyo basi, haijalishi ubinadamu wako uko vipi au unafahamu kiasi kipi cha mafundisho, umevumilia mateso kiasi kipi au ni mangapi ambayo umetelekeza, kama Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yako basi kila kitu kitasitishwa. Bila kazi ya Roho Mtakatifu mtu ni mpumbavu; mtu anaweza kuwa na nguvu kiasi kipi basi? Imani kiasi kipi? Maarifa ya mtu yatakuwa na manufaa yapi? Chukulia kuwa gerezani kwa mfano: Tangu wakati ambapo watu walianza kumsadiki Mungu, watu wamekumbana na haya; mara nyingi wanateswa na kusakwa, wakitorokea kila pahali. Matukio haya yote yakitiwa, ndani ya fikira na moyo wa kila mmoja, mawazo yasiyofutika: "Siwezi kuwa Yuda, siwezi kuongea kabisa kuhusu masuala ya kanisa." Je, watu wengi zaidi hawajajitayarishia haya? Lakini wakati bahati mbaya inapokupata, unaweza kuchukua hatua bila kujua. Mtu hawi Yuda pindi mkanganyo unapompata. Imesemekana awali kwamba vile utakavyokuwa hatimaye lazima iamuliwe na kama umeidhinishwa na Mungu. Kuona kama unayo idhini ya Mungu ni kimsingi kuangalia mambo kama vile iwapo unaye Roho Mtakatifu akifanya kazi ndani yako, kama Roho Mtakatifu anakupa nuru na kukuongoza, na kama unaandamana na neema fulani.

Wakati baadhi ya watu walipotenda kwanza wajibu wao, walijaa nguvu, ni kana kwamba hawangewahi kuishiwa na nguvu hizo. Lakini inakuwaje kwa kadri wanapoendelea ndipo wanapoonekana kupoteza nguvu hizo? Mtu waliokuwa wakati huo na mtu waliye sasa ni sawa na watu wawili tofauti. Kwa nini walibadilika? Sababu ilikuwa gani? Ni kwa sababu imani yao kwa Mungu ilienda njia mbaya kabla ya kufikia njia sahihi. Waliichagua njia mbaya. Kulikuwa na jambo lililokuwa limefichwa ndani ya kufuatilia kwao kwa kwanza, na kwa wakati mwafaka jambo hilo likaibuka. Nini kilikuwa kimefichwa? Ni matarajio yanayokuwa ndani ya mioyo yao wakati wakimsadiki Mungu, matarajio kwamba siku ya Mungu inawadia hivi karibuni ili taabu yao itafika mwisho; matarajio kwamba Mungu atabadilika na kwamba mateso yao yote yataisha. Wote wanatarajia siku wanayoweza kurudi nyumbani ili kuungana tena na familia zao, wakati hakutakuwa na mateso tena, wakati watakuwa huru kabisa, wakati wanaweza kumsadiki Mungu kabisa bila ya vizuizi vyovyote kutoka kwa wengine, na kila mmoja anaweza kuishi katika mazingira mazuri pale wanapoweza kuvalia vizuri na kula vizuri. Je, hawana tumaini hili lote? Fikira hizi zipo katika kina cha mioyo yao kwa sababu mwili wa binadamu hauko radhi kuteseka na unatazamia siku bora zaidi kila unapopitia mateso. Mambo haya hayatafichuliwa bila ya hali sahihi[a]. Wakati hakuna hali yoyote kama hiyo, kila mmoja ataonekana kuwa sawa hasa, ataonekana hasa kuwa na kimo, kuufahamu ukweli kwa kiasi fulani, na kuonekana mwenye nguvu za kipekee. Siku moja, wakati hali fulani itakapoibuka, fikira hizi zote zitajitokeza. Akili zao zitaanza kung’ang’ana, na baadhi yao wataanza kuharibikiwa. Si kwamba Mungu haifungui njia kwa ajili yako, au kwamba Mungu hakupatii neema yake, na bila shaka si kwamba Mungu hakufikirii katika ugumu wako. Ni kwamba kuyavumilia maumivu haya sasa ndiyo baraka yako, kwa sababu lazima ustahimili mateso kama haya ili kuokolewa na kunusurika, na yote haya yamepangiliwa awali. Hivyo kwa mateso haya kukukumba wewe ni baraka kwako. Usifikirie kwamba jambo hili ni rahisi; hili si jambo tu la kuchezea watu na kuwafanya kuteseka; maana yake fiche ni ya kina sana, muhimu sana. Kama hutawahi kuoa katika maisha yako, au kutowahi kurudi nyumbani katika maisha yako yote, hayo yatakuwa mambo muhimu. Kama njia unayoifuata ni sahihi, kama kile unachotafuta ni sahihi, basi mwishowe kile utakachopata kitakuwa zaidi ya kile ambacho watakatifu wa enzi, na ahadi utakazorithi zitakuwa kubwa zaidi. Kwa sasa baadhi ya watu siku zote wanafikiria: "Kwa kweli Mungu atakumbuka mateso haya yote ninayoyavumilia? Kama kwa bahati yoyote hakuna mtu wa kunisaidia mwishowe, nitafanya nini? Ni nani atakayenitunza kama nitakuwa mgonjwa? Je, Mungu ana habari? Je, mateso haya yataisha lini? Je, mwangaza wa siku utawasili lini?" Siku zote watu wanayatarajia mambo haya ilhali hawafikirii ni nini umuhimu wa mateso yao. Siku zote wanatamani Mungu kuweza kubadilika ili waweze kujiondolea mateso. Kila mmoja anayo mipango yake ya kibinafsi, na mwishowe ni katika asili ya binadamu kumsaliti Mungu; hakuna watu ambao kwa kweli wanampenda Mungu, hakuna mtu anayemtamani Mungu, anayetaka kuishi pamoja na Mungu; hawawezi kumsubiri Mungu kuondoka ulimwenguni. "Haijalishi ni kwa kiasi kipi ambacho Mungu ameteseka, mradi tu Anaondoka na tunaweza kuyaondoa mateso haya, basi itakuwa sawa." Kwa nini watu husema hivyo? Siku hizi watu wengi wanalo tarajio hili: "Kama Mungu ataondoka, basi tutatawala kama wafalme na hatutawahi kupitia mateso haya; Joka Kuu Jekundu atakuwa pia amemalizika, na tunafaa kutumia fimbo ya chuma ili kuyatawala mataifa yote na watu wote, je, hatutauona basi mwangaza wa siku?" Baadhi ya watu hata hujifikiria: "Mume, watoto, jamaa, marafiki—nyinyi nyote ni mashetani mnaonitesa. Siku moja Mungu wetu atajitokeza hadharani na kuwaadhibu. Mtaona kwamba njia tu tunayoifuata ndiyo njia sahihi." Ingawa tumaini hili sio haki, kuna kitu kibaya na baadhi ya hali ndani ya watu. Hakuna anayepangilia kuifuata barabara hii kwa maisha yake yote, akiutafuta ukweli ili kuyapata maisha na kumfahamu Mungu, na kuishi maisha yenye maana kama Petero mwishowe. Hivyo basi, watu hupotoka katika njia yao, hawana nafasi ya Mungu mioyoni mwao wakiwa njiani, na Roho Mtakatifu hafanyi kazi tena ndani yao, na wanatembea kinyumenyume; bidii yao yote inayotokana na kusadiki katika kipindi cha miaka minane au tisa ya awali kunaharibika kabisa—hili ni jambo hatari sana! Kuteseka sana, kusikiliza mahubiri mengi sana, kuendelea vivyo hivyo kwa miaka mingi sana, yote haya ni bure; hii ni hatari sana! Ni rahisi kuuteremka mlima lakini ni vigumu kuupanda mlima na kuchagua barabara sahihi ambayo mtu anafaa kutembelea. Vichwa vya watu wengi havifikirii vizuri! Hawawezi kuchagua kwa usahihi ni barabara gani sahihi na ipi ni ya kupotosha. Baada ya kuyasikiliza mahubiri mengi na kuyasoma maneno mengi ya Mungu, wanajua kwamba Yeye ni Mungu, lakini bado hawaamini; wanajua ni njia ya kweli, lakini bado hawawezi kuitembelea; ni vigumu vipi kuwaokoa watu! Je, unawezaje kujua kwamba Yeye ni Mungu lakini kutoweza kumsadiki Yeye? Je, wewe si Shetani? Hatutaizungumzia asili yako, lakini wewe ni kitu cha aina gani, kwa nini wewe ni mjinga hivyo? Unajua kwamba ndiyo njia ya kweli ilhali huitafuti, unaufahamu ukweli lakini umeshindwa kuutenda hivyo, hivyo wewe si Shetani? Akilini mwako hakuna madhumuni ya maisha, mwelekeo wa maisha, wala mambo yoyote yale ya binadamu wa kweli; wewe ni sawa tu na mnyama. Hivyo basi, kwa baadhi ya watu, si kwamba Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yao au kwa makusudi au huwafichua kwa makusudi, ni kwamba hakuna njia yake Yeye kufanya kazi ndani yao. Watu ni wapotovu sana, wagumu sana wa kuwashughulikia, na hawachagui njia sahihi, hivyo ni vipi Roho Mtakatifu atakavyofanya kazi ndani yao? Kila wakati Roho Mtakatifu anapofanya kazi anawapa watu nafasi ya kufanya uchaguzi wao binafsi na halazimishi kamwe yeyote. Lakini moyo wa binadamu ni mjinga sana; hawaupendi ukweli, hawako radhi kutembea njia ya mateso, na hawako radhi kuzitumia jitihada yoyote au kulipa gharama yoyote. Watu wanajali tu kile kilicho mbele yao, na ni wachoyo sana. Kama kuna kitu mbele yao ambacho wanaweza kuona na kufurahia, basi watakitafuta, kukifikia, na watapuuza yale mambo ambayo hawawezi kuyaona au yale wanayoyaona hayana maana; hii ndio hali ya watu wengi zaidi, na karibu hakuna nafasi yoyote kwa Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yao. Watu wengine husema: "Ninawezaje kuutatua ugumu huu? Pengine itakuwa vyema kama nitapata mtu anayefahamu namna ya kuzungumza nami." Baada ya mtu mwingine kumaliza kuzungumza nao, wanakubali kwamba hali iko hivyo, na wanafahamu kwa kiwango cha kimafunzo, lakini wanasema kwamba hawawezi kuweka hilo katika matendo. Kama huwezi kuliweka katika matendo, basi ni nini haja ya Mimi kukuambia kulihusu? Unafaa kukaa pembeni! Hustahili kuusikia ukweli! Hustahili kumsadiki Mungu! Unafaa kusubiri tu kuangamia! Kwa vile kile ulichochagua ni njia mbaya, inayostahili dharau, ya kishetani, haijalishi ni ukweli kiwango kipi utakaozungumziwa, hautaupenda, hivyo unafaa tu kukaa pembeni! Hakuna haja ya kusema chochote kwa mtu aina hii. Siku hizi mara nyingi kunasemekana: "Ninaelewa kila kitu, siwezi tu kukiweka katika matendo." Maneno haya ni ithibati kwamba mtu huyo ni Shetani na yeye ni wa namna ya Shetani kabisa. Mtu asiyeupenda ukweli ni mtu mwovu kwa kweli; kile ambacho mtu anapenda, anatumainia, anatamani na ana kiu nacho ni uwakilishi kamili wa asili ya mtu huyo. Kama huupendi ukweli basi wewe ni wa Shetani, wewe ni kitu cha maangamizo; kama unaupenda ukweli basi wewe ni mmojawapo wa wale waliopangiliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu; je, haya si wazi?

Njia anayochagua mtu ni muhimu. Unaweza kutafakari kwa utulivu na makini, na hujachelewa kutubu. Kama unao uamuzi, basi hilo ni jambo zuri; wale wasiokuwa na uamuzi ndio wa chini zaidi ya wote. Angalau kabisa unahitaji kuwa na uamuzi; kuhusiana na namna ya kufikia kile ulichoamua kufanya, namna unavyoweza kukikamilisha kile ulichoamua kufanya, lazima kuwepo na njia kwa hili. Kwanza kabisa, lazima uuelewe ukweli, ujue hatima itakayofuata kwa wanadamu, ujue njia ambayo wanadamu wanafaa kutembelea na shabaha wanazofaa kufikia. Imesemekana, "Mambo na masuala yote yamo mikononi mwa Mungu." Unaweza kuyapitia maneno haya na kuyapima mambo yote dhidi yao. Kwa vile sasa unamsadiki Mungu, unafaa kuwa mtiifu kwa Mungu? Umuhimu wa imani kwa Mungu ni upi?? Je, imani kwa Mungu ni kuzipokea baraka tu? Unatembelea sasa katika njia hii, lakini utaweza kuvumilia mpaka mwisho? Utawezaje kuitembea katika siku za usoni? Wakati unapokumbana na ugumu, unafaa kuwa na baadhi ya kanuni za ukweli ili kujihimiza, ili usisite, kuwa mnyonge, usiwe mwenye mawazo mabaya, usilalamike kuhusu Mungu, na usitende dhambi dhidi ya Mungu—lazima uelewe na uwe wazi kuhusu mambo haya yote.

Watu wanapofurahi, wanasema: "Niko radhi kuitumia jitihada kwa ajili ya Mungu, nitaitumia kwa ajili ya Mungu kwa maisha yangu yote." Lakini pengine kwa wakati fulani wakati watakapokumbana na changamoto, watakuwa na mawazo mabaya na kujisemea wenyewe: "Mungu yupi? Mimi siwezi kumsadiki Yeye. Barabara hii ni ngumu sana!" Baada ya kuomba, kuna lawama: "Mimi napaswa kumshukuru Mungu!" Kujua kuwa unapaswa kumshukuru Mungu, hufai tena kutenda namna hivyo. Basi pengine siku moja itafika utakapokumbana na tukio baya na tena kuwa mwenye fikira mbaya, tena kulalamika kuhusu Mungu: "Mbona Mungu amepangilia hali hizi kwangu Mimi, kwa nini Yeye siku zote hunifanya Mimi kuteseka? Kwa nini hawezi kunizuia dhidi ya kuteseka?” Watu siku zote hulalamika, na pia husema kwamba wao wanapaswa kumshukuru Mungu. Siku zote hawabadiliki katu. Wakati wanapokumbana na changamoto au hata kitu kisichowapendeza kutakuwa na chuki na maudhi, na mbaya zaidi kutakuwa hata na baadhi ya watu wanaosema maneno ya kukufuru na hukumu; baadaye watahisi haikuwa vyema kuongea kwa njia hiyo, na watahisi vibaya kuhusu kufanya hivyo, na kujaribu haraka kutenda baadhi ya wajibu na kufanya baadhi ya mambo mazuri ili kuweza kufidia. Haya yote yanaonyesha nini? Asili ya binadamu ni mbaya, wao hawana akili na hisi. Sawa tu na kujihusisha katika mipango ya biashara, wakati wanapomhitaji Mungu watamvuta Yeye karibu, na wakati hawamhitaji Yeye watasonga mbali na Yeye na kumpinga Yeye, wakifanya kile kinachowafanya kufurahi. Binadamu ana kiburi na ni mwenye kujiamini mno, na hana uoga. Hana chuki ya kweli wala upendo wowote wa kweli ndani ya moyo wake, hakuna tofauti kati ya uhaki na kutokuwa na uhaki; hana mipaka. Hana shabaha, sembuse kuwa na kanuni zozote au ufahamu wa adabu anapofanya chochote. Moyo wa binadamu ni mbaya sana. Katika hali hii, watu wangali wanatazamia ahadi kuu wanazoweza kupokea, baraka nyingi wanazoweza kupata, namna watakavyopata umaarufu au anasa watakayopitia. Wanapofikiria tu kuhusu mambo haya ndipo wanapofikiri: "Namna Mungu alivyo mzuri! Lazima niufidie upendo wa Mungu!" Kwa nini wanasema "mzuri"? Wanatoa wapi msemo wa "fidia"? Unasemwa kwa nia? Hayo ni maneno ya wepesi wa kuvutwa na huruma yanayotamkwa katika hali ya kivutio na furaha ya mara moja, lakini je, yanachukuliwa kama ufahamu wa kweli? Huu ni upendo wa kweli? Je, unatoka ndani ya kina cha moyo wako? Kama una ufahamu huu kwa kweli, basi kwa nini bado unalalamika? Kama kweli unahisi unapaswa kumshukuru Mungu basi kwa nini unalalamika? "Mungu, Hujawa mwema kwangu Mimi, Umenipuuza, Hujawa mzuri kwangu Mimi, hivyo sitakumakinikia Wewe kwa vyovyote vile! Hunihitaji Mimi, hivyo sitakufanyia kazi Wewe tena!" Watu wanayo chuki nyingi sana ndani yao! Hatimaye, wangali wanafikiria: "Ninampenda Mungu! Ninampenda Mungu zaidi ya wengine wanavyompenda." Je, huu ni upendo wa kimatendo vipi kwa Mungu? Kwamba watu wanaweza kusema hivi kunathibitisha kwamba hawaijui asili yao binafsi, hawajui kile walicho wao, wameundwa na nini, na kwamba hawawezi kujikadiria wao binafsi. Kwa hakika ni katika asili ya kila mmoja kupinga na kumsaliti Mungu; hili ni jambo ambalo kila mmoja analo kwa pamoja na wote wanavyo vitu hivi ndani yao. Hakuna mtu anayependa kwa kweli kile ambacho kinastahili kupendwa, na hata zaidi hakuna mtu anayechukia kile kinachofaa kuchukiwa; hana mipaka yoyote sembuse maono yoyote, ndani yake hakuna tofauti kati ya haki na kutokuwa na haki, hakuna tofauti kati ya nyeusi na nyeupe, sembuse tofauti wowote kati ya ukweli na mafundisho au uvumi; hawezi kutambua kati ya mambo yoyote haya. Watu hawaelewi kuhusu kile kinachostahili upendo, kile kinachostahili kutafutwa, na kile kinachofaa kuchukiwa, na hawawezi kuchukuliwa kama wana utambuzi. Wakati watu wa ulimwengu wanapouimba wimbo, "Rudi Nyumbani Mara kwa Mara," baadhi ya watu wanashawishika kuwa mbali. Watu wana nini ndani yao? Wanao ukweli wowote? Baadhi ya watu hufikiri kwamba wanaweza kufanya kazi fulani, kwamba wana baadhi ya sifa zinazostahili, na wanaonekana kuwa na ukweli fulani. Kwa hakika, huna chochote, na wewe si chochote! Ingawa unaweza kuzungumzia mafundisho fulani kwa wengine sasa, pengine siku moja katika siku za usoni utaweza kubembelezwa na wengine, na utatetereka vibaya zaidi kuliko mtu yeyote mwingine, na utaathirika vikali zaidi na ubaya kuliko mtu mwingine yeyote. Je, unayaamini haya? Je, umeshawishika na suala hili? Pengine ungali bado hujapitia kuwa mbaya sana au kuanguka vibaya na kufikiria kuwa wewe ni mwenye nguvu sana. Bila ya uzoefu huo unafikiria kwamba unacho kimo kikuu, lakini pengine siku moja unapofichuliwa, utalia na kusema, "Nimepatikana, nimepatikana tu." Unaanza kusonga kutoka katika kipeo kimoja hadi kingine. Watu wengi walikuwa wamejaa nguvu walipomwamini Mungu mara ya kwanza, lakini pengine walikuja kukumbana na kitu kilichowafanya kuwa wanyonge ghafla, na hawakuweza katu kuinuka tena. Je, umewahi kugundua matatizo yoyote na watu hawa? Nguvu au unyonge wa kila mtu si jambo ambalo wanaweza kudhibiti wenyewe. Mambo yaliyofichwa ndani ya watu yanaweza kujitokeza wakati wowote na mahali popote. Hakuna kiwango chochote kidogo cha uchafu mbaya kilichoko ndani ya watu, na kinajitokeza kwa mtiririko usioisha! Hivyo basi, asili ya watu ni asili ya Shetani—hakuna tofauti kamwe—na ni tofauti kabisa na kiini cha Mungu.

Kitambo, Mungu alisema: "Ninaweza kumpenda binadamu milele, na ninaweza pia kumchukia binadamu milele." Yaani, Anavyo viwango, Anafikia hitimisho Zake mwenyewe, na anao msingi ambao Anafikia hitimisho hizo. Anazo hukumu Zake, vipimo na viwango vya kile Anachopenda na kuchukia, kinachomfanya Yeye kuwa na furaha na kile Anachochukia. Watu hawana vitu hivi hivyo watapotoka wakati wanapotembea, watakuwa vigeugeu na, bila mtu yeyote wa kuwaongoza, siku zote wataelekea upande usiofaa.

Baadhi ya watu wangali bado siku zote wanatumai: "Mungu anaondoka duniani lini? Harakisha na kuondoka. Baada ya kuipitia kazi Yake miaka hii michache, nafaa kuolewa lakini nagundua kuwa siwezi; waona, hili ndilo ninalopata kwa kumsadiki Mungu miaka yote hii!" Jukumu lote sasa linawekwa kwa Mungu. Hawajui kabisa kuhusu kile walichopata kwenye miaka hiyo, na thamani yake. Kama si kazi ya Mungu mwenye mwili, basi watu wa Kichina wangekuwa wametoweka kitambo; pengine hili ni jambo ambalo baadhi hawatasadiki. Kama hulisadiki, basi yamaanisha kwamba wewe huyaelewi mambo kabisa, lakini huu ndio ukweli. Watu hata hufikiria: "Bila ya Mungu kutuongoza, tunaweza bado kutembelea njia. Tumekisoma kitabu cha Neno Laonekana katika Mwili mara nyingi sana, kimeelezwa kwa muhtasari akilini mwetu, na tunazifahamu kanuni, ili tuweze kuichukua hatamu." Je, unaweza kweli kuichukua hatamu? Huwezi kuitembelea njia sahihi, na unapotoka baada ya kuitembelea kidogo, hivyo unaweza bado kuingia kuhalisia? Ungali wewe hujashawishika. Yaweza kusemekana kwamba yeyote atapotoka kama hana mwongozo wa aina hii kutoka kwa Mungu? Je, Roho Mtakatifu alikuwa akifanya katika Enzi ya Neema? Je, Roho Mtakatifu alifanya kazi? Ni madhehebu mangapi yalitenganishwa baadaye? Kulikuwepo na madhehebu yasiyofikirika ya kila aina, hata yale ambayo majina yao hayawezi kufikiriwa au kukumbukwa. Ni nini tatizo na hali hii? Mambo ya asili ya watu yaliyo ndani yao lazima yaeleweke kabisa, na lazima pia kuwepo na ufahamu wa kiini cha watu. Kufahamu na kuona kabisa hakumaanishi unafaa siku zote kukwama pale, lakini badala yake kunamaanisha kwamba kutoka pale, lazima uinuke na uutafute ukweli, yasome maneno ya Mungu uijue asili ya binadamu, ili kukifahamu kiini cha binadamu, na kutia jitihada na ukweli; kwa njia hii tu ndipo utakapotembea katika njia sahihi. Neno la Mungu lafunua na kuifichua asili ya binadamu, na kuwaruhusu watu kujua kiini chao ni kipi. Ni muhimu sana kuelewa kiini potovu cha binadamu. Waona, Shetani ni msiri kweli. Mungu alimwuliza: "Wewe watokea wapi?" naye Shetani akajibu: "Natoka katika kuzunguka huku na kule duniani, na katika kutembea huku na huku humo." Ukisikiza kwa makini kwa kauli hii ya Shetani, "Kutembea huku na kule duniani," utashangaa, alikuwa akienda au akitoka? Hivyo basi, kauli hii ni kauli ya siri, na kutoka katika kauli hii Shetani anaweza kuchukuliwa kuwa kiumbe cha siri. Baada ya watu kupotoshwa na Shetani wao pia huwa wasiri ndani yao; wakati wanapoyafanya mambo hawana kigezo, viwango, na kanuni, na hivyo basi kila mmoja anapotoshwa kwa urahisi. Wakati Shetani alipomjaribu Hawa, alisema: "Kwa nini usile tunda la mti ule?" Hawa akajibu, "Mungu alisema kwamba kama nitakula tunda la mti ule, nitakufa." Shetani kisha akasema, "Si lazima ufe kama utalila tunda la mti ule." Nia ya kauli hii ya Shetani ilikuwa ni kumjaribu; hakusema kwa hakika kwamba kwa kulila tunda lile kutoka katika mti binadamu asingekufa, alisema tu kwamba binadamu si lazima afe, na hivyo binadamu akafanywa kufikiria: "Kama si lazima nife, ni sawa nikilila." Binadamu hakuweza kulipinga jaribio la kulila tunda. Kwa njia hii, Shetani aliifikia shabaha yake ya kumjaribu binadamu hadi aitende dhambi; hakuchukua jukumu la hayo, kwa sababu hakulazimisha yeyote kulila. Sasa watu wote wanazo sumu za Shetani ndani yao ambazo humjaribu Mungu na kumjaribu binadamu. Wakati mwingine wakati watu wanapoongea wanaongea kwa sauti ya Shetani, kwa nia ya kupima na kujaribu. Fikira na mawazo yote yanayojaa ndani ya watu ni sumu za Shetani, tabia waliyo nayo ni jambo la Shetani, na wakati mwingine konyezo au ishara ya mkono huwa na dalili ya kupima na majaribu. Watu wengine husema: "Ninamsadiki Mungu na nafuata kwa njia hii, hivyo lazima kupata kitu. Siutafuti ukweli lakini ninaufuata hadi mwisho, na ninatumia nguvu zangu zote ili kuitumia jitihada na kuyaacha mambo yaliyo katika mkondo wa wajibu wangu. Hata kama nitatenda baadhi ya makosa, ninaweza bado kupata jambo." Hawajui kile wanachosema. Huku kukiwa na upotovu mwingi sana ndani ya watu, wanawezaje kubadilika kama hawautafuti ukweli? Kwa kiwango cha upotovu ambacho binadamu anacho, kama hakuna ulinzi kutoka kwa Mungu, basi mtu anaweza kutetereka na kumsaliti Mungu wakati wowote. Je, unayasadiki hayo? Hata kama utajilazimisha, huwezi bado kufaulu hadi mwisho kwa sababu hatua ya mwisho ni kuunda kundi la washindi; je, inaweza kuwa rahisi kama unavyofikiria? Mwishowe haihitajiki kwa watu kubadilika asilimia 100 au asilimia 80, lakini angaa kunafaa kuwa na badiliko la asilimia 30 au 40; angalau kabisa lazima uyachimbue mambo ambayo yamepachikwa ndani yako kabisa na kuyabadilisha; na unaweza kufikia hitaji la Mungu la asilimia 30 hadi 40, au bora zaidi kufikia badiliko la asilimia 60 hadi 70, kumaanisha kwamba unaumiliki ukweli fulani ndani yako, kwamba unayo mambo ambayo yanalingana na ya Mungu ndani yako, na kwamba unapokumbana na baadhi ya masuala haitakuwa rahisi kwako wewe kumpinga Mungu, na haitakuwa rahisi kuikosea tabia ya Mungu. Kwa njia hii, mwishowe, utafanywa kuwa mtimilifu, na kupongezwa.

Baadhi ya watu siku zote hufikiria: "Je, kumwamini Mungu ni kuhudhuria tu mikutano, kuimba nyimbo, kulisikiliza neno la Mungu, kuomba, kufanya baadhi ya wajibu? Je, hali haiko hivyo?" Haijalishi ni kwa muda gani mmekuwa waumini wa Mungu bado hamjaelewa kabisa umuhimu wa imani kwa Mungu. Kwa hakika, umuhimu wa imani kwa Mungu ni wa kina sana, na watu hawajaifikiria kabisa kuihusu. Mwishowe, mambo yaliyo ndani ya watu ambayo ni ya Shetani, na mambo ya asili yao lazima yabadilike, na lazima yalingane na mahitaji ya ukweli; kufanya hivi tu ndiko kuutimiza kwa kweli wokovu. Kama upo vile ulivyokuwa kwenye dini—kupiga kelele ukitaja baadhi ya maneno ya mafundisho tu au kupiga kelele ukitaja kaulimbiu fulani na kisha kutenda baadhi ya vitendo na tabia njema na kutotenda dhambi fulani, kutotenda dhambi za waziwazi—hii bado haimaanishi kwamba umeingia katika njia sahihi ya kumsadiki Mungu. Kwa sababu tu unaweza kuzitii sheria, hiyo inamaanisha kwamba unaitembelea njia sahihi? Je, inamaanisha kuwa umechagua kwa usahihi? Kama mambo ndani ya asili yako hayajabadilika na mwishowe ungali unampinga Mungu na kumkosea Mungu, basi haya ndiyo matatizo makubwa zaidi. Kama unamwamini Mungu lakini hulitatui tatizo hili, basi unaweza kuchukuliwa kuwa umeokolewa? Mimi kuyasema haya, kunamaanisha nini? Ni kuwafanya nyote kufahamu ndani ya mioyo yenu kwamba imani kwa Mungu haiwezi kutenganishwa na maneno ya Mungu, na Mungu au na ukweli. Lazima uichague njia yako vyema, utie jitihada katika ukweli na kutia jitihada ndani ya maneno ya Mungu. Usiwe tu na maarifa kiasi ya kijinga na kisha kujiona kuwa umemaliza, au kuyafahamu tu. Ukiyafanya mambo kwa njia ya haraka, utajidhuru tu mwenyewe. Mtu hafai kupotoka katika imani yake kwa Mungu; kama mwishowe hakuna Mungu ndani ya moyo wake, na anashikilia tu kitabu akikiangalia kidogo kana kwamba anatazama maua huku akienda shoti akiwa juu ya mgongo wa farasi, bila ya kuwa na nafasi ya Mungu ndani ya moyo wake, basi amepatikana. Je, "Imani ya binadamu kwa Mungu haiwezi kutenganishwa na maneno ya Mungu" inamaanisha nini? Unaelewa? Je, inakinzana na, "Imani katika Mungu haiwezi kutenganishwa na Mungu"? Unawezaje kuwa na Mungu ndani ya moyo wako kama maneno ya Mungu hayamo ndani ya moyo wako? Kama unamsadiki Mungu lakini Mungu hayumo ndani ya moyo wako, wala maneno ya Mungu hayako, wala mwongozo wa Mungu, basi umepatikana kabisa. Kama huwezi kufanya jambo dogo kulingana na hitaji la Mungu, basi ukikumbana na suala kubwa la kanuni utakuwa hata na uwezo mdogo zaidi kulitimiza hitaji la Mungu. Hii inamaanisha huna ushuhuda, na kwa hivyo kuna matatizo, na hivyo kuthibitisha kwamba huna chochote. Kunayo mambo mengi ambayo hayawezi kuelezewa kwa undani, na siku moja tu wakati Roho Mtakatifu atakupa nuru ndipo utakapofahamu kabisa. Sasa hivi ninaweza tu kutumia kauli kwamba watu watafikiria kuwa ni kawaida kabisa na pia haina mantiki sana kuonyesha. Je, wajua kwamba katika nchi hii, wakati unaweza kupitia mateso haya na kuifurahia kazi ya Mungu, wageni huwa wanawaonea wivu kabisa nyinyi wote? Matamanio ya wageni ni: Tunataka pia kupitia kazi ya Mungu, tutateseka kwa vyovyote vile kwa sababu ya hilo. Tunataka kuupata ukweli pia! Tunataka pia kupata umaizi fulani, kupata kimo fulani, lakini kwa bahati mbaya hatuna yale mazingira. Wanafikiria kwamba watu wa Kichina wamebarikiwa sana, lakini wewe unafikiria kwamba wao ndio waliobarikiwa, na unawaonea wivu; hii kwa kweli ni maana ya kuishi katika baraka lakini kutoweza kuihisi. Kulifanya kundi hili la watu kuwa kamili katika nchi ya joka kuu jekundu, kuwafanya kuvumilia mateso haya, kunaweza kusemekana kuwa utukuzaji mkubwa zaidi. Iliwahi kusemwa: "Nimeuleta utukufu Wangu kutoka Israeli hadi Mashariki kitambo." Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya kauli hii sasa? Mnafaa kuitembelea vipi njia iliyo mbele? Mnafaa kuutafuta vipi ukweli? Kama hamtautafuta ukweli basi mnawezaje kuipata kazi ya Roho Mtakatifu? Pindi utakapopoteza kazi ya Roho Mtakatifu, basi utakuwa katika hatari kubwa zaidi. Mateso ya sasa si muhimu. Je, wajua yatakufanyia nini?

Tanbihi:

a. Maandiko ya awali yameondoa "sahihi."

Iliyotangulia: Sura ya 46. Ni Kwa Kuujua Uweza wa Mungu Pekee Ndipo Unaweza Kuwa na Imani ya Kweli

Inayofuata: Sura ya 48. Ni kwa Kuzielewa Hali Zako tu Ndipo Utakapoweza Kutembea Katika Njia Sawa

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki