Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

490 Mtegemee Mungu Nyakati Zote ili Kumshinda Shetani

1 Kanisa linajengwa na Shetani anajaribu kwa uwezo wake kulibomoa. Anataka kubomoa ujenzi Wangu kwa njia yoyote iwezekanayo, kwa hivyo, lazima kanisa litakaswe kwa haraka. Lazima kusiwe na makapi au mabaki yoyote maovu; lazima litakaswe ili lisiwe na dosari na libaki takatifu kama awali. Lazima muwe macho na kusubiri kila wakati, na ni lazima mje mbele Yangu zaidi. Lazima mtambue mipango ya njama na hila mbalimbali za Shetani, mjue roho, mjue watu na mweze kupambanua watu wa aina zote, masuala na mambo; lazima mle na mnywe maneno Yangu zaidi na, muhimu zaidi, lazima mweze kuyala na kuyanywa nyinyi wenyewe. Jiandaeni wenyewe na ukweli wote, njooni mbele Yangu ili nifungue macho yenu ya kiroho na kuwaruhusu kuona siri zote zilizo rohoni….

2 Wakati kanisa linaingia awamu yake ya ujenzi, vita vya watakatifu dhidi ya Shetani vinaanza. Vipengele mbalimbali vya Shetani vya kutisha Vinawekwa mbele yenu; je, mnaacha na kurudi nyuma au mnainuka na kuendelea mkinitegemea Mimi? Weka hadharani vipengele vya Shetani vyenye upotovu na viovu, bila hisia wala huruma! Pambana na Shetani hadi kifo! Mimi ni msaada wenu na ni lazima muwe na roho ya mwana wa kiume! Shetani yuko katika hekaheka zake za kifo cha mwisho lakini bado hataweza kuhepa hukumu Yangu. Shetani yuko chini ya miguu Yangu na pia anakanyagwa chini ya miguu yenu—ni ukweli! Wale wapinga dini wote na wale ambao hubomoa ujenzi wa kanisa hawafai kuvumiliwa hata kidogo na nitawahukumu mara moja. Weka Shetani hadharani, mkanyagie chini ya miguu, muangamize kabisa na usimuachie pa kujificha. Kila aina ya mapepo na vizuka hakika wataonyesha maumbile yao ya kweli mbele Yangu na Nitawatupa wote kuzimu ambamo hawatawahi kuwa huru; wote wako chini ya miguu yetu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 17” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Yachukulie Maneno ya Mungu kama Msingi wa Matendo Yako

Inayofuata:Pigana Mapigano Mazuri kwa Ajili ya Ukweli

Maudhui Yanayohusiana

 • Upendo Safi Bila Dosari

  1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vizuizi au ba…

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  1 Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…

 • Nitampenda Mungu Milele

  1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na hasi, m…

 • Njia Yote Pamoja na Wewe

  1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga. Maneno Yako ya…