Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda wa Uzoefu Mbele ya Kiti cha Hukumu cha Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

40. Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu

Xiaowei Mji wa Shanghai

Wakati fulani kitambo, hata kama daima nilipata msukumo kiasi na fadhila wakati dada mmoja aliyeshiriki nami alishiriki nuru aliyokuwa amepata wakati alipokula na kunywa neno la Mungu, pia kila wakati nilikuwa na hisia ya muda mrefu kuwa alikuwa anajionyesha. Ningejiuliza, “Nikimjibu sasa hivi, sitakuwa nikimtia moyo? Kwa namna hiyo, sitaonekana basi kuwa duni kuliko yeye?” Matokeo yake yakawa, nilikataa kutaja maoni yangu mwenyewe katika ushirika au kutoa maoni kuhusu mawazo yoyote aliyoshirikisha. Wakati mmoja, dada yangu, alipopata utambuzi fulani kutoka kwa kula na kunywa fungu fulani la neno la Mungu, alihisi kuwa kulikuwa na kasoro fulani na hali yetu na kuniuliza kama ningekuwa radhi kuwasiliana naye kuhusu fungu hilo la neno la Mungu. Mara tu alipouliza, mawazo haya yote na hisia za chuki zilitanda juujuu: “Unataka tu kujishuhudia mwenyewe, kuwa na wasikilizaji wa kuhubiria. Kwa nini niwasiliane na wewe?” Hata nilifika kiwango cha kuhepa mkutano ili isinibidi kumsikiliza. Baada ya muda, nilihisi uzito mkubwa moyoni mwangu, nilijua kitu fulani kilikuwa kibaya na hali yangu, lakini sikuweza kufikiria njia nzuri ya kutatua mgogoro wangu wa ndani. Kile nilichoweza kufanya tu ni kujishughulisha kikamilifu katika wajibu wangu, kula na kunywa neno la Mungu, na kuimba nyimbo za injili ili kujizuia kutokana na hisia hizi hasi. Hata hivyo, kila mara nililazimika kukabiliana na hali ya sasa, uharibifu huo huo ungeinuka katika moyo wangu—mambo yalikuwa yanazidi kuwa mabaya, sio mazuri—na sikuwa na dokezo la nini kufanya kuhusu hayo.

Siku chache baadaye, Nilikuwa na mkabala na dada wakati wa ushirikiano. Dada huyo alisema: “Siku hizi umekuwa mnyamavu sana wakati wa ushirikiano, kuna jambo linaloonekana kuwa si la kawaida na wewe karibuni.” Niliyahisi maneno hayo kama ngumi tumboni, lakini ili kujiepusha na haya nilikana kuwa kulikuwa na shida yoyote. Wakati huo ilionekana kwamba dada huyo alikuwa na kiburi sana: Alionekana kuzungumza bila kujali heshima yangu mwenyewe na nilihisi kuwa alikuwa ananidharau. Zile fikira zote potovu zilinirudia kwa upesi. Kadri nilivyong’ang’ana zaidi, ndivyo roho yangu ilivyozidi kuwa yenye giza; nilikuwa nimekoma kuwasiliana na Mungu. Nikiwa nahisi asiyejiweza kabisa, nilipiga magoti mbele ya Mungu na kumwomba Anifumbulie hali yangu halisi. Katikati ya maombi, neno la Mungu lilinijia: “Wale wanaoona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo ni wenye upuzi!” (“Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Baadaye, pia nilipatana na kifungu kifuatacho: “Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi ndani ya mtu mwingine ajaye. Fanya hima ufuate; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndivyo maisha yako yanaweza kuzidi kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Kwa kufanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu kwa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui ni kupitia kwa mtu wa aina gani ndiyo Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo ndiyo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani. Ukiweza kutembea kwenye njia hii sawa, hii inaonyesha kwamba kuna matumaini makubwa kwako kukamilishwa na Mungu. Kama huwezi kufanya hivyo, inaonyesha kwamba maisha yako ya baadaye ni ya dhalili na giza” (“Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nikiwa nasoma kifungu hiki, nilitambua ghafla: Wakati huu wote nimekuwa nikipinga kazi ya Roho Mtakatifu! Siku hizi, dadangu mara nyingi amepata nuru kutoka kwa kula na kunywa neno la Mungu, ana mzigo kiasi wa wajibu wake na maisha ya wengine, na ana furaha kuwakimu na kuwasaidia wengine; bila shaka Roho Mtakatifu anafanya kazi kupitia kwake. Natakiwa kuwa mtiifu kwa kazi ya Roho Mtakatifu na nikubali msaada wake, lakini badala yake nilimchukulia huyo dada kuwa mwenye maringo, nikifikiri alikuwa akitaka tu kuthibitisha jinsi alivyokuwa bora zaidi kuliko watu wengine wote. Kwa hiyo, nilikataa umaizi wake, na kukataa kushiriki naye. Mungu alikuwa Anafanya kazi kupitia dada huyo ili kunionyesha hali yangu na kunisaidia na nami nilimchukia na kumbagua tu na kumchukulia kama adui yangu. Kwa juujuu, inaonekana kana kwamba huu ulikuwa tu ugomvi kati yangu na huyo dada, lakini kwa kweli nimekuwa nikijipambanisha naye Mungu! Sikuwa nakana na kupinga kazi yake Roho Mtakatifu? Nimekuwa fidhuli na mkaidi kweli! Kujiepusha na haya na kulinda heshima yangu, nilikataa kutojifikiria ili kupokea usaidizi wake na pia nikakataa, nikaepuka na kuhukumu ushirikiano wake! Sikuwa na akili au ubinadamu hata kidogo! Wakati huu, nilibashiri kuwa kwa kweli sikuwa nikiishi katika utiifu na hofu ya Mungu, sikuupenda ukweli nami nilikuwa kipofu kwa kazi ya thamani ya Roho Mtakatifu ndani ya dada yangu. Badala yake, niliweka hadhi na majivuno yangu mwenyewe mbele ya chochote kingine. Niliona heri kuacha kazi ya Roho Mtakatifu kuliko kupata haya. Matendo yangu yalikuwa tofauti vipi na wale viongozi wa kidini, ambao, ili waweze kuhifadhi umaarufu na hadhi yao, walimpinga na kumshutumu Mungu hata wakijua kuwa hii ndiyo njia ya ukweli? Je, sikuwa tu mtu mpuuzi mwingine ambaye, kama alivyosema Mungu, huona kazi ya Roho Mtakatifu kama mchezo? Nikitazama nyuma, natambua kuwa Roho Mtakatifu hakuwa Anafanya kazi tu ndani ya dada, Alikuwa pia Akijaribu kuniendeleza, kunifungua macho na kupata kitu kutokana na mchakato huo. Nilifanya nini kama malipo? Nilikuwa mwenye kiburi na mwenye majivuno na nilikataa neema yake Mungu kila wakati. Ni nafasi ngapi nilikosa kukamilishwa, kupatiwa nuru na kupata umaizi zaidi katika ukweli! Nimekuwa mpumbavu vipi, mjinga vipi!

Wakati huo, nilihisi hata uchungu zaidi na hatia kwa yote mbayo nimetenda, kwa hiyo nikamwomba Mungu, “Mungu, nimekuwa mjinga, mpumbavu, na mwenye kiburi, na sistahili hata kidogo kazi Umetekeleza ndani yangu au kuokolewa na Wewe. Mungu, asante kwa mwongozo Wako na nuru, kwa kunionyesha ujinga wangu mwenyewe na upumbavu. Ninakuahidi, tangu sasa kuendelea, bila kujali ni ndugu yangu yupi anayewasiliana, almuradi azungumze kulingana na neno la Mungu au na mapenzi ya Mungu, nitafuata, nitatii na kukubali, kwa sababu hii ndiyo njia ya kuelekea katika ukuaji maishani mwangu na alama ya baraka Yako. Mimi si mtiifu kwa mtu yeyote yule, ila badala yake kwa mambo yote mazuri yanayotoka Kwako. Ni fursa ya kukubali wokovu Wako. Nikiwahi kukaidi au kuasi dhidi Yako tena, naomba kwamba Urushe adhabu kwangu.”

Iliyotangulia:Kutumia Neno la Mungu Kama Kioo

Inayofuata:Zawadi ya Kupendeza Zaidi Ambayo Mungu Amenipa

Maudhui Yanayohusiana

 • Kuibuka Kutoka Kwenye Ukungu

  Asante, Mwenyezi Mungu! Ni Wewe uliyenitunza na kunipa nuru na kuniongoza kujitoa katika pingu ambazo zilikuwa zimenidhibiti kwa miaka mingi sana, kuniruhusu kutoka katika ukungu. Zamani, sikukujua Wewe na mara nyingi niliishi katika kutoelewa, nisiweze kuamini neno Lako na kulichukulia kama tu la kuliwaza na kuwatia watu moyo. Sikulichukulia neno Lako kama ukweli na uzima, na zaidi sikukuchukulia wewe kama Mungu. Lakini Ulinivumilia, na Ulikuwa mwenye subira kwangu. Ulinipa nuru na kuangaza mwanga Wako kwangu, ili kwamba niwe na ufahamu kidogo wa kiini Chako cha haki na uaminifu. Hii hasa ni mfano kamili wa upendo Wako kwa mwanadamu.

 • Hatimaye Naishi kwa Kudhihirisha Kiasi Kama Mwanadamu

  Ninawaza jinsi sikuutafuta ukweli, jinsi katika kutimiza wajibu wangu nilishindana na wenzangu kazini tena na tena, jinsi kwa ajili ya sifa na faida yangu ningekandamiza au kukana yule mwingine—jinsi nilisababisha hasara kwa maisha yangu na pia kwa kazi ya familia ya Mungu. Lakini Mungu aliendelea kunihurumia, kuniokoa, na ni baada tu ya kuadibu na kuhukumu tena na tena ndipo nilizinduka na kuelewa tamanio la Mungu kutuokoa, nikaweka kando kufukuzia kwangu sifa na hadhi na kuanza kutenda kidogo kama mwanadamu.

 • Roho Mtakatifu Hufanya Kazi kwa Njia Yenye Maadili

  Ee Mungu! Ninatoa shukrani kwa sababu ya kutoa nuru Kwako kwa muda ufaao ambako kuliniruhusu kuona mkengeuko katika uzoefu wangu mwenyewe.

 • Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

  Maneno ya Mungu tena yalinileta kwa ufahamu wa jinsi huduma yangu kwa Mungu kwa kweli ilikuwa ni kujishuhudia mwenyewe na kujiinua na yalinisaidia kuona matokeo mabaya ya tabia hii. Maneno ya Mungu yalinisaidia kuona kwamba asili yangu, kama ile ya malaika mkuu, ingeweza kuniongoza kuwa gaidi dhalimu, na kwamba ningeweza kusababisha maangamizi makubwa. Nilifikiria kuhusu jinsi huduma yangu kwa Mungu haikutimizwa kulingana na kanuni sahihi za huduma; haikuwa ikimwinua Mungu na kumshuhudia Mungu, si kufanya wajibu wangu. Badala yake, siku zangu zilitumiwa kujionyeshwa mwenyewe, kujishuhudia mwenyewe, kuwavuta ndugu zangu wa kiume na wa kike mbele yangu. Je, si aina hii ya huduma ni ya kudharauliwa?