237 Sasa Nimeamka

1 Miaka hiyo yote ya kumwamini Bwana, nilifikiria wokovu ulikuwa rahisi sana. Kufikiria kumtambua Bwana kwa kinywa chako na kumwamini moyoni mwako, dhambi zako zingesamehewa. Nililenga tu kufanya kazi kwa bidii lakini kamwe sikuweka maneno ya Bwana kwenye vitendo. Nilidhani mimi ni mtu anayependa Bwana na aliye mwaminifu kwa Bwana. Nilikiri dhambi zangu mara nyingi kwa Bwana lakini sikuwahi kujijua. Katika mikusanyiko nilizungumza juu ya maarifa ya Bibilia lakini sikuwa na maarifa ya Bwana. Katika ugumu na majaribio nilimwelewa vibaya na kumlaumu Bwana. Nilikuwa mwasi na mpinzani sana, lakini nilifikiria ningenyakuliwa hadi katika ufalme wa mbinguni.

2 Kupitia maneno ya Mwenyezi Mungu ya hukumu, nimeamka hatimaye. Licha ya muonekano wangu wa mwenendo mzuri, haimaanishi kuwa tabia yangu imebadilika. Kuzungumza juu ya mafundisho hakuwakilishi kuelewa ukweli au kuwa na uhalisi. Bila kumjua Mungu, bado ninakosa ukweli na uzima. Katika imani yangu bado ninafanya mapatano na Mungu, nikimpinga, nikijaribu kumdanganya. Nina tofauti gani na Mafarisayo wanafiki? Isingekuwa wokovu wa hukumu ya Mungu ningeangamia. Kupokea hukumu na kuadibu kwa Mungu ni neema ya pekee sana.

3 Kupitia hukumu ya Mungu nimeona tabia yangu ni ya ubinafsi na ya kustahili kudharauliwa sana. Nimejawa sana na majuto, nasujudu mbele za Mungu. Kwa kukubali hukumu nimetakaswa na kupata wokovu. Nimeona kuwa hukumu ya Mungu ni wokovu, kwamba ni upendo. Natamani kupitia hukumu na kuadibu zaidi, majaribio na usafishaji zaidi. Kufanya kila niwezalo ili kufuatilia ukweli, kuwa mtu anayemwogopa Mungu na kuepukana na uovu. Tabia ya Mungu ya haki na takatifu inastahili sifa za wanadamu. Natamani kumsifu na kumwabudu Mungu hata milele!

Iliyotangulia: 236 Nampenda Mungu Zaidi Baada ya Kupitia Hukumu Yake

Inayofuata: 238 Ni Watu Waaminifu Pekee Walio na Mfano wa Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

47 Furaha Katika Nchi ya Kanaani

1 Kurudi nyumbani kwa Mungu, nahisi furaha na msisimko. Nina bahati kuona hatimaye Mwenyezi Mungu wa vitendo. Maneno Yake huwaongoza watu...

263 Njia Yote Pamoja na Wewe

1 Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani. Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga....

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki