Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Maneno Bora zaidi ya Mungu Kuhusu Injili ya Ufalme

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu? Iwapo ni hivyo, basi utakaribishaje, kurudi kwa Yesu? Je, uko tayari kabisa? Utakaribisha kurudi kwa Yesu kwa namna gani? Nafikiri kuwa kila ndugu na dada wanaomfuata Yesu wangependa kumpa Yesu makaribisho mazuri. Lakini Je, mmewaza iwapo utamjua Yesu Atakaporejea? Je, mtaelewa kila kitu Atakachosema? Je, mtakubali bila masharti, kila kazi ambayo Anafanya? Wale wote ambao wamesoma Biblia wanajua kuhusu kurudi kwa Yesu, na wale wote ambao wamesoma Biblia wanangoja kwa makini kuja Kwake. Nyote mmetazamia wakati wa kurudi, na uaminifu wenu ni wa kusifika, na imani yenu kweli ni ya kuleta wivu, lakini mnatambua kuwa mmefanya kosa kuu? Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: wingu hili jeupe linaashiria nini? Na kwa kuwa wafuasi wengi wa Yesu wanangoja kurejea Kwake, Atashuka miongoni mwa watu wapi? Iwapo mtakuwa wa kwanza kati ya wale ambao Yesu Atawashukia, Je, wengine hawataona jambo hili kama lisilo la haki? Najua kuwa nyinyi mna ukweli mkubwa na utiifu kwa Yesu, lakini mmewahi kukutana na Yesu? Mnajua tabia Yake? Mmewahi kuishi na Yeye? Mnaelewa kiasi gani kumhusu kwa kweli? Wengine wanasema kuwa maneno haya yanawaweka katika tatizo gumu. Watasema, “Nimesoma Biblia kuanzia mwanzo hadi mwisho mara nyingi sana. Nitakosaje, kumwelewa Yesu? Usijali kuhusu tabia ya Yesu—najua hata rangi ya nguo Alizopenda kuvaa. Je, haushushi hadhi yangu ukisema simwelewi?” Napendekeza kuwa msiyapinge masuala haya; ni vizuri mtulie na kufanya ushirika juu ya maswali yafuatayo: Kwanza, unajua uhalisi ni nini, na nadharia ni nini? Pili, unajua dhana ni nini, na ukweli ni nini? Tatu, unajua kile kinachowazwa na kile kilicho halisi?

Watu wengine wanakataa ukweli kuwa hawamwelewi Yesu. Ilhali Nasema hammwelewi hata kidogo, na hamelewi hata neno moja la Yesu. Hii ni kwa sababu kila mmoja wenu anamfuata kwa sababu ya matukio ya Biblia, kwa sababu ya yale yaliyosemwa na wengine. Hamjawahi kumwona Yesu, wala kuishi na Yeye, na hata hamjapata kushinda na Yeye hata kwa muda mfupi. Hivyo, Je, kuelewa kwenu kuhusu Yesu sio nadharia pekee? Je, si kuelewa kwenu kunakosa uhakika? Labda watu wengine wameiona picha ya Yesu, ama wengine wametembea nyumbani kwa Yesu. Labda wengine wameguza mavazi ya Yesu. Ilhali kuelewa kwako kumhusu bado ni nadharia ila si wa vitendo, hata kama umeonja chakula kilicholiwa na Yesu. Haijalishi ni hali ipi, hujawahi kumwona Yesu, na hujawahi kuwa pamoja na Yeye katika hali ya kimwili, na hivyo, kuelewa kwako kumhusu Yesu kutabaki kuwa nadharia tupu ambayo haina ukweli. Pengine maneno Yangu yana uvutio mdogo kwako, lakini Nakuuliza hivi: Ingawa labda umesoma maandishi mengi yaliyoandikwa na mwandishi unayempenda, Je, unaweza kumwelewa bila kuwahi kukaa na yeye kwa muda? Je, unajua utu wake ulivyo? Je, unajua ni maisha ya aina gani anayoishi? Unajua chochote kuhusu hali ya hisia zake? Huwezi hata kumwelewa kikamilifu mwanadamu unayempenda, sasa utawezaje, kumwelewa Yesu Kristo? Kila kitu unachoelewa kumhusu Yesu kimejaa mawazo na dhana, na hakina ukweli wowote wala uhalisi. Kila kitu kinanuka, na kimejaa mwili. Kuelewa kwa aina hii kutakuwezesha vipi kuwa tayari kukaribisha kurejea kwa Yesu? Yesu hatawakaribisha wale waliojawa na mawazo na dhana za mwili. Wale wasiomwelewa watafaa vipi kuwa waumini Wake?

Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu kama hawa, wakaidi na washenzi wanaweza kupata baraka za Mungu? Watawezaje, kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya kweli iliyozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha, na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuonyesha heshima tupu kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa mbeleni, ikiwa kwamba hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kuwa huwezi kumpinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale ambao hawakumfahamu Masiha wote walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, kumkataa Yesu, kumpaka Yeye tope. Watu wasiomwelewa Yesu wote wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kuwa uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliye kurudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje, kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni asili ya watu ambayo itaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia raha ya ulimwengu wa mbinguni, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupata ukweli utakaoonyeshwa na Yesu atakaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, kisha mnazikiri, wakati baada ya mwingine? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?

Uaminifu wenu uko kwa maneno pekee, maarifa yenu ni ya kiakili tu na ya dhana, utumishi wenu ni kwa sababu ya kupata baraka za mbinguni, na kwa hivyo imani yenu inafaa kuwa vipi? Hata leo, bado mnapuuza kila neno la ukweli. Hamjui Mungu ni nini, hamjui Kristo ni nini, hamjui jinsi ya kumcha Yehova, hamjui jinsi ya kuingia katika kazi ya Roho Mtakatifu, na hamjui jinsi ya kutofautisha kati ya kazi ya Mungu Mwenyewe na uongo wa mwanadamu. Unajua tu kukashifu neno lolote la ukweli linayoelezwa na Mungu lisilolingana na mawazo yako. Unyenyekevu wako uko wapi? Utiifu wako u wapi? Uaminifu wako uko wapi? Tamaa yako ya kupata ukweli iko wapi? Uchaji Mungu wako uko wapi? Nawaambieni, wale wanaoamini katika Mungu kwa sababu ya ishara hakika ni kiwango ambacho kitapata kuangamizwa. Wale wasio na uwezo wa kukubali maneno ya Yesu Ambaye Amerudi kwa mwili kwa hakika ni vizazi vya kuzimu, kizazi cha malaika mkuu, kiwango ambacho kitakabiliwa na kuangamizwa kwa milele. Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeitwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Itaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna uashirio wa ukweli tu. Wale wanaokubali ukweli na hawatafuti ishara, na hivyo kutakaswa, watakuwa wamerudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu na kuingia katika kumbatiao la Muumba. Ni wale tu ambao wanashikilia imani kwamba “Yesu Asiyeshuka juu ya wingu jeupe ni Kristo wa uongo” watakabiliwa na adhabu ya milele, kwani wanaamini tu katika Yesu ambaye Anaonyesha ishara lakini hawamkubali Yesu Anayetangaza hukumu kali na Anatoa njia ya kweli ya uzima. Na hivyo itakuwa tu kuwa Yesu Anashughulika nao tu Atakaporejea wazi wazi juu ya wingu jeupe. Ni wakaidi sana, wanajiamini sana, wamejaa kiburi. Wapotovu kama hawa watatunukiwa vipi na Yesu? Kurejea kwa Yesu ni wokovu mkuu kwa wale ambao wana uwezo wa kuukubali ukweli, lakini kwa wale wasioweza kuukubali ukweli ni ishara ya kuhukumiwa. Mnafaa kuchagua njia yenu wenyewe, na msimkufuru Roho Mtakatifu na kuukataa ukweli. Hampaswi kuwa wajinga wala watu walio na kiburi, lakini watu ambao wanatii uongozi wa Roho Mtakatifu na wanangoja kwa hamu na kuutafuta ukweli; kwa njia hii tu ndio mtapata kufaidika. Nawashauri mtembee katika njia ya kuamini katika Mungu kwa uangalifu. Msiwe wepesi wa kuamua bila kuzingatia suala nzima; kilicho zaidi, msiwe kawaida na wenye kutojali katika imani yenu kwa Mungu. Mnafaa kujua kwamba, kwa kiwango cha chini zaidi, wale wanaoamini Mungu wanafaa kuwa wanyenyekevu na wenye kumcha. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali wanaudharau ni wajinga na wapumbavu. Wale ambao wamesikia ukweli ilhali bila kujali wanaamua mambo bila kuzingatia kila kitu ama kuukashifu wamejawa na kiburi. Hakuna anayeamini katika Yesu anayeruhusiwa kuwalaani au kuwahukumu wengine. Nyote mnafaa kuwa mtu aliye mantiki na anayekubali ukweli. Pengine, baada ya kusikia njia ya kweli na kusoma neno la uzima, unaamini kuwa neno moja tu kati ya maneno elfu kumi ndiyo yanayolingana na dhana zako na Biblia, kisha unafaa kuendelea kutafuta katika moja kati ya elfu kumi ya maneno haya. Bado Nawashauri muwe wanyenyekevu, msijiamini sana, na msijiinue juu sana. Moyo wako ukiwa na uchaji mdogo kama huu kwa Mungu, utapata mwanga mkuu. Ukichunguza kwa makini na kurudia kutafakari maneno haya, utapata kuelewa iwapo ni ya kweli au la, na iwapo ni ya uzima au la. Pengine, baada ya kusoma tu sentensi chache, watu wengine watakashifu kwa upofu maneno haya, wakisema, “Hiki sio chochote ila kupata nuru kwa Roho Mtakatifu,” ama, “Huyu ni Kristo wa uongo ambaye amekuja kuwadanganya watu.” Wale wanaosema vitu kama hivyo wamepofushwa na ujinga! Unaelewa kiasi kidogo sana kuhusu kazi na hekima ya Mungu, na Nakushauri uanze tena kutoka mwanzo! Hamfai kuyakashifu tu kwa upofu maneno yaliyonenwa na Mungu kwa sababu ya kutokea kwa Makristo wa uongo katika siku za mwisho, na msiwe watu wanaokufuru Roho Mtakatifu kwa sababu mnaogopa kudanganywa. Je, hiyo haitakuwa hali kubwa ya kuhuzunisha? Iwapo baada ya uchunguzi mwingi, bado unaamini kuwa maneno haya si ukweli, sio njia, na sio maonyesho ya Mungu, basi utaadhibiwa hatimaye, na kuwa bila baraka. Iwapo huwezi kukubali ukweli kama huu ulionenwa wazi na bila kufichika, basi wewe si ni asiyefaa kwa wokovu wa Mungu? Je, wewe si mtu ambaye hana bahati zaidi kurejea mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Waza kuhusu hili! Usiwe na pupa wala mwenye kutenda bila kufikiria, na usiichukulie imani kwa Mungu kama mchezo. Fikiria kwa ajili ya hatima yako, kwa ajili ya matarajio yako, kwa ajili ya maisha yako, na usifanye mchezo na nafsi yako. Je, unaweza kuyakubali maneno haya?

Iliyotangulia:Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Inayofuata:Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu

Unaweza Pia Kupenda