Dibaji

Mwaka wa 1991 ulikuwa mwaka wenye umuhimu mkubwa mno na wenye athari nyingi kwa wanadamu wote, licha ya wao kuwa wapotovu sana. Huo ulikuwa mwaka ambapo Mwokozi wetu Yesu alionekana, baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu na wale wote waliomwamini Bwana kwa uchaji na kutamani ukweli, na Alikuwa amerudi kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho. Kuja kwa Mwenyezi Mungu kulienda kinyume na fikira za watu wote, kwa kuwa hakuwa Ameshuka huko Israeli juu ya wingu jeupe, wala hakuonekana wazi kwa mataifa yote na watu wote; badala yake, Alikuja kwa siri ndani ya ngome ngumu ya ukanaji Mungu—China—na katika nchi ambayo joka kubwa jekundu limelala likiwa limejiviringisha, Alianza kazi ya hukumu Akianza katika nyumba ya Mungu. Kwa sababu China ni taifa bovu, potovu, na linalompinga Mungu zaidi ulimwenguni, na kwa sababu ni nchi ambamo joka kubwa jekundu na kila aina ya roho waovu wameifanya kuwa maskani yao, ni hapa ambapo Mungu ananena maneno Yake, na ni hapa ambapo Mungu huwahukumu, huwaadhibu, kuwatakasa na kuwaokoa wale ambao wamedanganywa sana na kupotoshwa kwa kina na joka kubwa jekundu. Kupitia kazi hii, Mungu amepata kundi la washindi Mashariki ya dunia ambao wamekuwa ushuhuda wa ushindi wa Mungu juu ya Shetani, na kwa hivyo hekima na uweza wa Mungu vinafunuliwa waziwazi zaidi. Kama Mwenyezi Mungu asemavyo: “Katika maeneo mengi, Mungu Alitabiri kupata kundi la washindi katika nchi ya Sinimu. Ni katika Mashariki mwa ulimwengu ambapo washindi watapatwa, hivyo nchi ambapo Mungu anashukia katika kupata mwili Kwake mara ya pili bila shaka ni nchi ya Sinimu, mahali ambapo joka jekundu linaishi. Hapo Mungu Atawapata warithi wa joka kuu jekundu na litashindwa na kuaibishwa. Mungu Anataka kuwaamsha watu hawa walioteseka sana, kuwaamsha kabisa, na kuwafanya waondoke katika ukungu na kulikataa joka kuu jekundu. Mungu Anataka Awaamshe kutoka katika ndoto zao, kuwafanya waelewe tabia ya joka kuu jekundu, kuutoa moyo wao wote kwa Mungu, kuinuka kutoka katika nguvu kandamizi za giza, kusimama Mashariki mwa dunia, na kuwa uthibitisho wa ushindi wa Mungu. Baada ya hapo Mungu Atakuwa Amepata utukufu” (“Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kwa sababu ya kazi na maneno ya Kristo ya siku za mwisho, wateule wa Mungu huko China, ambao wamedanganywa sana na joka kubwa jekundu wanapoishi chini ya utawala wake mwovu, wote wameshindwa na maneno ya Mwenyezi Mungu. Mmoja baada ya mwingine, wanakombolewa kutoka katika utumwa na udhibiti wa joka kubwa jekundu na kurudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kupokea unyunyiziaji na riziki, upogoaji na ushughulikiaji, na hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mwenyezi Mungu, na vilevile aina zote za majaribio na usafishaji. Hatimaye, katikati ya njia nyingi ambazo utawala wa joka kuu jekundu hutumia kuwasaka na kuwatesa, wateule wa Mungu wanakuwa mashahidi, na hivyo kuwa vielelezo na mifano ya kazi ya Mungu katika siku za mwisho ambao Mungu anawakamilisha nchini China, na pia wanakuwa ushuhuda wenye nguvu kwa ushindi wa Mungu juu ya nguvu ovu za Shetani.

Tangu kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ilipoanza barani China, joka kubwa jekundu halijawahi kuacha kulitesa Kanisa la Mwenyezi Mungu. Ili kukomesha kazi ya Mungu katika siku za mwisho, kuigeuza China kuwa eneo lisilomtambua Mungu, na kufikia lengo lake la kuwadhibiti wanadamu milele, linafanya kile kinachofanya vyema kabisa: kuvuruga, kuharibu, na kufanya yote liwezayo kupinga kazi ya Mungu. Si tu kwamba linasambaza kila aina ya uvumi na uwongo ili kuwashambulia na kuwashtaki wateule wa Mungu kwa uongo, lakini pia hutumia kila aina za njia zinazostahili dharau kuwatesa: Linachunguza watu kwa wazi na sirini, linafuatia mazungumzo ya simu, linawafuata watu kwa siri, kuwakamata watu kwa siri, kupekua maskani na kutoza faini, linapata uungamo kwa nguvu kupitia mateso, linatishia na kushawishi, na linawaacha watu wakiwa wameharibika kimwili na kiakili. Njia hizi zimesababisha wateule wengi sana wa Mungu kukamatwa, kupigwa kikatili, na kulazimishwa kuadilishwa tena kupitia kazi, huku wengine wao wameachwa wakiwa vilema au kupoteza maisha yao. Joka kubwa jekundu hutumia njia hizi katika jaribio la kuwalazimisha wateule wa Mungu kumkataa na kumsaliti Mungu, ili wakubali mamlaka yake, utawala wake juu yao, na ukandamizaji na unyonyaji wake milele. Lakini Mungu ni Mungu mwenye uweza, na hekima Yake hutumiwa daima kwa msingi wa hila danganyifu za Shetani. Katikati ya mateso maharibifu waliyopata kutoka joka kubwa jekundu, ingawa wateule wa Mungu wanapitia uchungu na mateso nyingi na kukabili dhiki kukiwa na nafasi ndogo zaidi ya kuendelea kuishi, bado wanakuja kuona waziwazi asili mbovu na ya kupinga maendeleo ya joka kuu jekundu, ambayo ni potovu sana na ambayo huenda kinyume kabisa na Mbingu, na pia wanakuja kuona sura yake ya kishetani. Katika mioyo yao kunaibuka chuki kali kwa joka kubwa jekundu, na ndani yao kunatokea azimio la kuwa shahidi kwa Mungu hata wakipoteza maisha yao wenyewe. Mwishowe, wanategemea mwangaza na mwongozo wa maneno ya Mungu na nguvu ambayo Mungu huwapa, hadi hatimaye wanashinda udhaifu wa miili yao, wanajiondoa katika mshiko ambao kifo kinao juu yao na, wakiwa na imani ya kweli na moyo uliojawa upendo kwa Mungu, wanatoa ushuhuda mkuu zaidi kwa Mungu mbele ya joka kubwa jekundu, na kumsababisha Shetani kuaibishwa na kushindwa kabisa. Kama vile Mwenyezi Mungu asemavyo: “Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi” (“Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kwa hivyo, washindi hawa ni kundi la watu ambao huadilishwa na kukamilishwa na maneno ya Mungu katikati ya ukandamizaji mwovu wa joka kubwa jekundu.

Kwa wengine, wanaonekana tu kama watu wengine wowote, lakini chini ya unyunyiziaji na riziki ya maneno ya Mwenyezi Mungu, wanakuja kuelewa ukweli kiasi, na wanapata imani na azimio la kutupilia mbali ushawishi mbaya wa Shetani, kumfuata Mungu, na kutembea kwenye njia sahihi maishani. Kwa hivyo bado wanamwomba Mungu, wanamtegemea Mungu, wanasalia kuwa wenye haki kwa kutegemea nguvu iliyotolewa na maneno ya Mungu, na kamwe hawajisalimishi au kusalimu amri chini ya mateso yote ya kikatili na maharibifu yaliyotolewa kwao na joka kubwa jekundu na katika siku zao zote walizoshinda wakidhoofika katika seli za gereza zenye giza. Ingawa baadhi yao wanaweza kuteswa kinyama hadi kuchungulia kaburi, azimio lao la kufuatilia ukweli huimarishwa; ingawa baadhi yao wanaweza kuwa katika upeo wa ujana wao, wanapokabiliwa na mateso ya kikatili na kufungwa jela mikononi mwa pepo wa joka kubwa jekundu, bado wanaonyesha hali inayoashiria upendo na huishi ujana wao bila majuto; ingawa baadhi yao wanaweza kupitia mateso na dhiki na kushambuliwa kikatili na pepo, hata hivyo wanahisi hata zaidi jinsi ambavyo neema ya Mungu ni ya thamani, na upendo wao kwa Mungu unaimarishwa hata zaidi; wanaposafiri kwenye barabara ngumu, wakinywea kikombe kichungu cha ukatili, wengine wanapata mwangaza, msukumo na mwongozo wa maneno ya Mungu, roho zao zinazinduliwa, na wanatunga nyimbo za sifa za maisha; wengine wanapambana dhidi ya uovu na ukandamizaji, na wakati wa hatari, wanapitia upitaji mipaka na ukuu wa nishati uhai ya Mungu; wengine wanamtegemea Mungu na wanaokolewa kutokana na kifo wakati wa mwisho, wanaona ukuu usio na kifani wa upendo wa Mungu, na kupata nguzo katika maneno ya Mungu ambayo huwafanya waendelee kushikilia uzima. Kwa hivyo, ni dhahiri kwamba ingawa kikundi hiki cha wateule wa Mungu ambao hushinda Shetani chini ya mwongozo wa Mungu hupoteza raha za mwili, lakini wanapata ukweli, wanapata ukombozi wa kiroho, na wanaishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Ingawa wanapitia dhoruba za upepo na mvua na kupitia shida nyingi, wanatoa ushuhuda wenye nguvu na mkuu sana kwa Mungu mbele ya Shetani, na kuwa washindi ambao wanaadilishwa na kukamilishwa na Mungu katikati ya shida. Hii inatimiza kabisa maneno ya Mwenyezi Mungu: “Nimesema hapo awali kuwa kikundi cha washindi wanapatwa kutoka Mashariki, washindi ambao wanatoka katika mashaka makubwa” (“Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Unaposoma kitabu hiki, wazo hili linaweza kuibuka akilini mwako: Je, si Mungu ni mwenye uweza? Kwa nini Aruhusu mfumo wa utawala wa joka kubwa jekundu uwaumize watu Wake wateule jinsi hiyo? Ikiwa unafikiria hivi, basi inaonyesha kuwa bado huelewi kikamilifu uweza na hekima ya Mungu, kwa kuwa ni wale tu ambao hawajui kazi ya Mungu ndiyo huhukumu mambo kadiri yaonekanavyo kwa nje, na kuhukumu vitu kwa fikira na mawazo yao wenyewe—hivi sivyo jinsi ya kutambua matunda ya kweli ya kazi ya Mungu. Mwenyezi Mungu asema: “Ninapoanza kirasmi Kazi Yangu, watu wote wanatembea kama Mimi hatua kwa hatua, kiasi kwamba watu katika ulimwengu wote wanakuwa katika hatua na Mimi, kuna ‘shangwe’ ulimwengu mzima, na mwanadamu anaendelezwa mbele na Mimi. Kwa sababu hii, joka kubwa jekundu mwenyewe anachapwa na Mimi mpaka anakuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na wazimu, na anahudumia Kazi Yangu, na, licha ya kutokuwa na nia, anashindwa kufuata tamaa zake mwenyewe, na kukosa njia nyingine ila kujiwasilisha kwa udhibiti Wangu. Katika mipango Yangu yote, joka kubwa jekundu ni foili[a] Yangu, adui Wangu, na pia mtumishi Wangu; kwa hivyo, Sijawahi kushusha ‘mahitaji’ Yangu kwake. Kwa hivyo, hatua ya mwisho ya kazi Yangu katika mwili inakamilika katika nyumba ya joka huyu. Kwa njia hii, joka kubwa jekundu anapata uwezo zaidi wa kunitumikia Mimi vizuri, kwa njia ambayo Mimi Nitamshinda na kukamilisha Mpango Wangu” (“Sura ya 29” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). “Mungu anakusudia kutumia sehemu ya kazi ya pepo wachafu ili kuikamilisha sehemu ya mwanadamu, ili watu hawa waweze kufahamu matendo ya mapepo, na kuwawezesha watu wote wawafahamu kwa kweli mababu zao. Ni kwa njia hii pekee wanadamu wanaweza kujinasua kabisa, sio tu kutoroka kizazi cha mapepo, lakini hata zaidi mababu wao. Hili ndilo kusudi la asili la Mungu kulishinda kabisa joka kubwa jekundu, kufanya hivyo ili wanadamu wote wajue umbo halisi la joka kubwa jekundu, Aambue kinyago chake kabisa, na kuona umbo lake halisi. Hili ndilo Mungu anataka kutimiza, nalo ni lengo Lake la mwisho duniani ambalo Amefanyia kazi nyingi sana; Ananuia kulifanikisha hili ndani ya watu wote. Hili linajulikana kama ushawishi wa vitu vyote kwa ajili ya kusudi la Mungu” (“Sura ya 41” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Katika kila hatua ya kazi Yake, Mungu huhamasisha vitu vyote kumfanyia kazi na kumhudumia, na hii hasa ndiyo hufanyika katika kazi ya Mungu ya siku za mwisho ambayo Ameonyesha nchini kote China. Joka kubwa jekundu halijaachwa, kwani limekuwa foili[a] na chombo cha huduma ndani ya kazi ya Mungu. Kupitia upinzani na vurugu ya joka kubwa jekundu kwa kazi ya Mungu, Mungu humwezesha kila mtu kutambua tabia yake halisi, na hivyo kuvunja uhusiano wote nalo na kujikomboa kutokana na pingu zake. Lakini je, Mungu kuwataka watu wabainishe vitendo vya pepo na kulitelekeza joka kubwa jekundu kabisa kunahusianaje na wao kupata wokovu kamili? Kama sote tunavyojua, joka kubwa jekundu hutenda kwa upotovu, hufanya kinyume na mbingu, na hupinga mabadiliko mno. Ili kuibadilisha China kuwa eneo lisilomtambua Mungu na kuwadhibiti watu wa China kabisa chini ya utawala wake mbaya, linaubadilisha ukweli kuwa uwongo siku zote, hueneza ukanaji Mungu na tamaa ya vitu kwa utukutu, na kusambaza kila aina ya uwongo na uzushi ili kuharibu akili za watu, kudanganya roho zao, na kuwazuia watu kuja mbele za Mungu kukubali wokovu Wake. Kwa hivyo linafikia lengo lake la kudhibiti na kuwateketeza watu milele. Iwapo watu wangependa kuzinduka kutoka kwa udanganyifu wa joka kubwa jekundu, wajiondolee udhalimu na ukandamizaji wake, na kumgeukia Mungu kabisa, basi ni kwa kupitia tu mateso na uonevu mikononi mwa joka kubwa jekundu ndiyo wataweza kuona waziwazi sura yake ya kishetani iliyo mbaya, mbovu, na ya kustahili dharau na isiyo na aibu, na ndipo tu watakapolichukia na kulilaani kwa dhati. Kisha wao wanaahidi maisha yao kukatiza uhusiano wote na joka kubwa jekundu, wanaondoa ushawishi wa Shetani kabisa, na wanamfuata Mungu, wanamtii Mungu, na kutembea kwenye njia ya nuru maishani ambapo wanafuatilia ukweli na kupata wokovu kamili. Kwa hivyo ni dhahiri kuwa Mungu hutumia joka kubwa jekundu kama foili[a] na chombo cha huduma ili kuwezesha watu Wake walioteuliwa kuelewa ukweli, kukuza utambuzi, kuwa mashahidi kwa Mungu, na mwishowe kukamilishwa na kupata wokovu kamili. Jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi ni adhimu! Mungu hutumia uonevu wenye mhemuko wa joka kubwa jekundu ili limhudumie kwa ajili ya kuwakamilisha watu Wake walioteuliwa, kuwawezesha kujua tabia Yake ya haki, hekima na uweza Wake, na kuona jinsi kazi ya Mungu ilivyo ya vitendo, ili wote waweze kuonyesha kwa dhati sifa ya kweli kwa Mungu! Kama vile maneno ya Mwenyezi Mungu yasemavyo: “Katika mpango Wangu, Shetani amewahi kushindana na kila hatua, na, kama foili[a] ya hekima Yangu, amejaribu siku zote kutafuta njia na namna za kuvuruga mpango Wangu wa awali. Lakini Ningeweza kushindwa na njama zake danganyifu? Vyote mbinguni na duniani vinanitumikia—njama danganyifu za Shetani zingeweza kuwa tofauti? Huku ndiko hasa kukutana kwa hekima Yangu, ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu matendo Yangu, na ni kanuni ya utendaji ya mpango Wangu mzima wa usimamizi. Katika enzi ya ujenzi wa ufalme, bado Mimi siepuki njama danganyifu za Shetani, ila Naendelea kufanya kazi ambayo lazima Nifanye. Kati ya ulimwengu na vitu vyote, Nimechagua matendo ya Shetani kama foili Yangu. Je, hii si hekima Yangu? Je, si haya ndiyo hasa yaliyo ya ajabu kuhusu kazi Yangu? Wakati wa kuingia katika Enzi ya Ufalme, mabadiliko makubwa mno hutokea katika vitu vyote mbinguni na duniani, na wao husherehekea na kufurahia. Je, nyinyi mna tofauti yoyote? Ni nani asiyejisikia mtamu kama asali katika moyo wake? Ni nani asiyebubujikwa na furaha katika moyo wake? Ni nani asiyecheza kwa furaha? Ni nani asiyesema maneno ya sifa?” (“Sura ya 8” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili).

Maelezo yote yaliyokusanywa katika kitabu hiki, Ushuhuda wa Washindi, ni ushuhuda wa ushindi wa wateule wa Mungu nchini China, ambao wanakamilishwa na maneno ya Mungu katikati ya mateso yenye mhemuko ya joka kubwa jekundu. Kama ukweli unavyoonyesha, Mungu hutumia upinzani na mateso makali ya joka kubwa jekundu kuwaadilisha na kuwakamilisha watu Wake wateule na kuwezesha maisha yao kukua na kukomaa. Wakati huo huo, Mungu hutumia upinzani na mateso haya kuwafunua na kuwaondoa watu wote waovu ambao hawamwamini kwa kweli na ambao hawaupendi ukweli. Hii ni ya kufaa kuonyesha kuwa hekima ya Mungu inatumiwa kwa kutegemea hila danganyifu za Shetani, kwamba Mungu tayari amelishinda joka kubwa jekundu kabisa, na kwamba Amepata utukufu wote!

Maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema: “Po pote ambapo Aliyepata mwili huonekana, adui anaangamiziwa mahali hapo. Uchina ni ya kwanza kuangamizwa, kuharibiwa kabisa kwa mkono wa Mungu. Mungu haipi Uchina upande wowote kabisa. Thibitisho la kuendelea kuanguka kwa joka kubwa jekundu linaweza kuonekana katika ukomavu wa watu unaoendelea. Hili linaweza kuonekana wazi na mtu yeyote. Ukomavu wa watu ni ishara ya kifo cha adui” (“Sura ya 10” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili). Wateule wa Mungu wanaomshuhudia ndio kundi linalomshuhudia Mungu wakati ule ule wa kuanguka kwa taifa la joka kubwa jekundu; wao ndio ushuhuda wa ushindi wa Mungu katika vita Vyake dhidi ya Shetani, na uthibitisho dhahiri wa kushindwa na kufedheheshwa kwa Shetani. Upevu wa watu wa Mungu ni ishara ya kuanguka kwa taifa la joka kubwa jekundu. Kazi ya Mungu barani China itaisha kwa utukufu: Amefanya kundi la watu kuwa washindi na Amepata utukufu Wake! Watu wateule wa Mungu sasa wamekubali misheni takatifu, kushuhudia kazi ya Mungu katika kila pembe ya ulimwengu na kueneza jina takatifu la Mungu. Jina la Mungu litatukuzwa katika ulimwengu wote, wanadamu wote watanyenyekea mbele za Mungu na kumwabudu Mwenyezi Mungu mwenye mwili, na mataifa yote ya ulimwengu yatakuwa taifa la Kristo—hili litafanywa na Mungu hivi karibuni!

Agosti 16, 2014

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Inayofuata: 1. Siku Baada Ya Nyingine Katika Jela Ya Chama Cha Kikomunisti

Ikiwa una matatizo au maswali yoyote katika imani yako, tafadhali wasiliana nasi wakati wowote.

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp