Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

39. Zawadi ya Kupendeza Zaidi Ambayo Mungu Amenipa

Yixin Jiji la Shijiazhuang, Mkoa wa Hebei

Kabla, ningewasikia mara kwa mara ndugu zangu wa kiume na wa kike wakisema, “Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya matokeo mazuri; ndiyo yote wanayohitaji watu.” Nilikubali hili na kukubaliana nalo, lakini sikuwa na ufahamu wowote kupitia uzoefu wangu mwenyewe. Baadaye nilipata ufahamu kiasi kwa njia ya mazingira ambayo Mungu aliniumbia.

Nilikuwa na hamu kubwa hasa ya hadhi katika moyo wangu. Daima nilikuwa na matumaini kwamba kiongozi angenisikiliza na kwamba ndugu zangu wa kiume na wa kike wangeniheshimu, lakini uhalisi haukuwa kamwe kama nilivyotarajia ungekuwa. Kwa kipindi cha miaka kadhaa, bila kujali ni nani niliyeshirikiana naye wakati wa kutimiza wajibu wangu, nilikuwa “msaidizi” daima. Bila kujali ni nini kilichokuwa kikiendelea, kiongozi angekijadili na mshirika wangu daima na kumpangia kushughulikia mambo. Ilionekana kuwa katika macho ya kiongozi, nilikuwa mtu asiye na thamani, mtu asiye na maana. Hili kweli lilinikanganya. Niliwaza: “Mimi hutimiza aina sawa za kazi na si mbaya kuliko wengine. Kwa nini mimi daima ni ‘msaidizi’? Kwa nini mimi daima niko chini ya mtu mwingine?” Nilipata uzoefu kidogo hasa wa mateso ya usafishwaji kwa sababu matakwa yangu hayakuweza kamwe kuridhishwa, na daima nilikuwa nikiishi katikati ya kutokuelewa kwangu kwa Mungu. Sikuweza kuliponyoka. Siku moja, kiongozi alimfanya mshirika wangu akusanye maandiko fulani, lakini hakuniomba nisaidie. Hilo lilinikasirisha. Ingawa nilijua kwamba sikupaswa kufuata kitu duni kama hicho, sikuweza tu kukiachilia, na kwa mara nyingine nikaingia katika maumivu. Niliwaza: Kwa nini hali ya aina hii daima hunipata? Kwa nini hali hizi wakati wowote sizo ninazozitaka? Kwa nini Mungu hufanya mambo jinsi hii? Sikuweza kuelewa hili kabisa.

Baadaye, nilipokuwa nikila na kunywa neno la Mungu, niliona maneno yafuatayo kutoka kwa Mungu: “Hata hivyo, upotovu ndani ya asili ya binadamu ni lazima uondolewe kupitia majaribu. Katika hali yoyote usiyoipita, ni katika hizi hali ambamo ni lazima usafishwe—huu ni mpango wa Mungu. Mungu anakutengenezea mazingira, Akikulazimisha usafishwe hapo ili ujue upotovu wako mwenyewe. Hatimaye unafika hatua ambapo unaona heri kufa na kuziacha njama na tamaa zako, na kutii mamlaka na mipango ya Mungu. Hivyo ikiwa kuna yeyote ambaye hana miaka kadhaa ya usafishaji na ikiwa hana kiwango fulani cha mateso, hataweza kuwacha utumwa wa upotovu wa mwili katika mawazo na mioyo yao. Katika hali zozote zile bado ungali mtumwa wa Shetani, katika hali zozote bado ungali na tamaa zako mwenyewe, matakwa yako mwenyewe—ni katika hali hizi ambamo unapaswa kuteseka. Mafunzo yanaweza kupatikana tu katika mateso, yaani, kuweza kupata ukweli, na kuelewa mapenzi ya Mungu” (“Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo). Nilihisi wimbi la joto ndani ya moyo wangu kutoka kwa maneno ya Mungu, kana kwamba Mungu alikuwa akinipa nuru uso kwa uso, akiniambia ni kwa nini alikuwa akifanya mambo kwa njia hii, lengo lilikuwa nini, na kuniruhusu kuelewa nia Zake nzuri. Kwa kupata nuru huko kutoka kwa Mungu, sikuweza kujizuia kugeuka na kuchukua mtazamo mpya wa mazingira ambayo Alikuwa amenitengenezea. Niliona wakati huo kwamba Mungu alinijua vizuri kabisa; Alijua vipengele ambavyo kwavyo vifungo vya kero za ushawishi wa Shetani kwangu vilikuwa vibaya zaidi. Pia Alikuwa wazi kiasi kwamba upotovu wangu kutoka kwa Shetani ulikuwa mkali sana katika uwanja wa hadhi. Mungu hakuweza kuvumilia kuniona nikiishi chini ya utawala wa Shetani na kupotoshwa, kudhulumiwa, kuteswa na kuvyogwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu alilenga asili yangu, na kwa mujibu wa kile nilichohitaji, alinitakasa mara kwa mara mahali ambapo nilipotoshwa kwa kina na Shetani. Ufunuo huo, kuadibu huko, usafishaji huo—vyote vilikuwa wokovu wa upendo wa Mungu kwangu. Lakini kwa miaka mingi sana, sikuwahi kuelewa kamwe nia njema za Mungu. Sikuwa tayari kuikubali kazi ya Mungu ya “kunyang’anywa madaraka” kwangu. Ndiyo maana daima sikuuelewa ukarimu Wake na daima nilihisi kuwa Alikuwa mkali kwangu, akinikandamiza, na hangeniruhusu kwa kweli nijidhihirishe. Ninapolifikiria sasa, ikiwa mimi, kama mtu aliyeona hadhi kama uhai wenyewe, kwa kweli nilikuwa na njia yangu mwenyewe katika kila uwanja, tamaa zangu za ndani zingekuwa zimekua tu na kukua, na hatimaye ningeweza kuangamizwa tu. Ni hapo tu nilipoelewa kazi ngumu ambayo Mungu alikuwa amefanya kwangu kwa miaka mingi; ni hapo tu nilipoona kwamba mazingira ambayo Mungu alikuwa amenitengenezea yalikuwa ni ya kuniokoa. Huu ni upendo ambao hauwezi kuonyeshwa kwa maneno. Moyo wangu uliguswa na upendo wa kweli wa Mungu na kutokuelewana kwangu kwa Mungu kulipotea kutoka kwa moyo wangu. Nilikuwa tayari kwa hamu kuwa mtiifu ndani ya mazingira ambayo Mungu alinitengenezea.

Ilikuwa tu ni kupitia uzoefu huu ambapo nilitambua kwa kweli kwamba Mungu hutengeneza mazingira ili kujaribu na kusafisha wanadamu. Kuna maana ya kina na vile vile upendo mkubwa ndani ya hili! Ukweli ni kwamba, kwangu, wakati hali hizo ambazo hazikufanana na mawazo yangu zilikuwa kwangu, ndizo nilizohitaji kabisa katika maisha. Ilikuwa ni njia muhimu ya Mungu kunifanya nimtambue na kumtii ili aniokoe. Kama vile mama anavyoielewa afya ya watoto wake—ni mtoto yupi anayehitaji nini, ni lishe gani wanayohitaji iongezwe—mama anaelewa hayo vizuri. Leo, kile Mungu anachofanya katika maisha ya watu ni vivyo hivyo. Mungu hutengeneza mazingira kwa watu na kila kitu anachofanya katika maisha yao ni kulingana tu na kile wanachohitaji. Yote ni chochote kilicho cha manufaa zaidi kwa maisha yao na ni ili kuwaruhusu kupata ukweli, kufanikisha utii kwa Mungu, na kujikomboa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kama watu wanaweza kuwa watiifu ndani ya mazingira ambayo Mungu amewatengenezea, wanaweza kupata ukweli, kupata uzima. Kama watu wataupa uhuru mwenendo wao wenyewe na upendeleo wao na kumfanya Mungu awaridhishe, basi hawatakosa tu kupata chochote hata kidogo, lakini watamchukiza Mungu, na hatimaye wanaweza tu kujiumiza na kujiangamiza wenyewe. Hii ni kwa sababu kile ambacho watu hupenda hakiwafai, na hata ni cha manufaa ya chini kwa wokovu wa Mungu na ukamilifu wao. Ni kile tu ambacho Mungu huwapa wanadamu kilicho bora; ni hicho tu ambacho watu wanahitaji zaidi. Ni wakati huo ambapo hatimaye nilikuwa na ufahamu wa vitendo kiasi wa kile ambacho Mungu alisema: “Njia ya leo huenda sambamba na hukumu na laana, lakini nyote mnapaswa kujua kwamba kile Niliyowapa, iwe ni hukumu au kuadibu, zote ni zawadi bora kabisa Ninazoweza kuwapa, na vyote ni vitu ambavyo mnahitaji kwa dharura” (“Tabia Yako Ni Duni Sana!” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Ninakushukuru kupata nuru kwa Mungu ambako kumeniwezesha kupata maarifa fulani na kuelewa kwa kazi ya Mungu kwangu, na kuona kwamba jinsi ninavyozidi kutokuwa radhi kukubali kitu, ndivyo ninavyozidi kukihitaji, na ndivyo ninavyopaswa kukikubali. Ni kwa njia hii pekee ninavyoweza kupata kile ambacho Mungu ananipa. Ninatambua pia kwamba asili ya Mungu ni nzuri, na kile Anachowafanyia wanadamu wote ni upendo. Ni yote ambayo ina manufaa zaidi kwa maisha ya watu; ni riziki inayohitajika zaidi katika maisha ya watu, na ndiyo zawadi bora zaidi inayopewa mwanadamu na Mungu. Kuanzia leo kwendelea, niko tayari kujiweka kikamilifu mikononi mwa Mungu, kuitii na kuikubali kazi yote ambayo Mungu anakamilisha kwangu. Niko tayari kutafuta kuujua ukweli, kupata ukweli, na kufanikisha mabadiliko katika tabia hivi punde ndani ya mazingira ambayo Mungu hunitengenezea.

Iliyotangulia:Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu

Inayofuata:Nilijifunza Kufanya Kazi na Wengine

Maudhui Yanayohusiana

 • Huku Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo

  Kupitia uzoefu huu, nimepata kuelewa kwamba kuweka ukweli katika vitendo lazima kuwekwe kwa msingi wa neno la Mungu na lazima kuanzishwe kwa kanuni za kweli. Mtu akiacha neno la Mungu, basi kila kitu kinakuwa kitendo cha nje, yaani, kuweka ukweli wa mawazo yao wenyewe katika matendo. Hata ikiwa ningefanya mambo vizuri na kwa usahihi, bado haingechukuliwa kama kuweka ukweli katika vitendo, na hata zaidi haingeleta mabadiliko kwa tabia ya maisha yangu.

 • Utajiri wa Maisha

  Wang Jun Mkoa wa Shandong Kwa miaka mingi tangu kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, mke wangu na mimi tumepitia hili pamoja chini…

 • Jitiishe Mwenyewe ili Kufundisha Wengine Nidhamu

  Xiaoyan Jiji la Xinyang, Mkoa wa Henan Nilikuwa na ubia wa kazi wa karibu na dada mmoja mzee katika masuala ya jumla. Baada ya kufanya kazi naye kw…

 • Ubia wa Kweli

  Fang Li Jiji la Anyang, Mkoa wa Henan Hivi karibuni nilidhani nilikuwa nimeingia katika ubia wenye kuridhisha. Mshirika wangu na mimi tuliweza kujad…