Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

786 Kazi ya Mwisho Afanyayo Mungu kwa Mwanadamu

1 Nchi ziko katika machafuko makubwa, kwa sababu fimbo ya Mungu imeanza kutimiza wajibu wake duniani. Kazi ya Mungu inaweza kuonekana katika hali ya dunia. Mungu anaposema “maji yatanguruma, milima itaanguka, mito mikuu itatawanyika,” hii ni kazi ya kwanza ya fimbo duniani, na matokeo yake ni kwamba “Nyumba zote duniani zitasambaratishwa, na mataifa yote duniani yatagawanywa; siku za marudiano kati ya mke na mume zitapita, mama na mwanawe hawatakutana tena, hakutakuwa tena na kuja pamoja kwa baba na bintiye. Nitayaharibu yote yaliyokuwa duniani.” Hiyo ndiyo itakuwa hali ya jumla ya familia duniani. Kwa kawaida, haingeweza kuwa hasa hali ya wote, lakini ni hali ya wengi wao.

2 Kwa upande mwingine, inahusu hali ambazo watu wa mkondo huu wamepitia katika siku za baadaye. Inatabiri kwamba, mara wakishapitia kuadibu kwa maneno na wasioamini wamepatwa na msiba, hakutakuwa tena na mahusiano ya familia miongoni mwa watu duniani; wote watakuwa watu wa Sinim, na wote watakuwa waaminifu katika ufalme wa Mungu. Hivyo, siku za marudiano kati ya mke na mume zitapita, mama na mwanawe hawatakutana tena, hakutakuwa tena na kuja pamoja kwa baba na bintiye. Familia za watu duniani zitatenganishwa, zitapasuliwa vipande vipande, na hii itakuwa kazi ya mwisho ambayo Mungu anafanya katika mwanadamu.

3 Na kwa sababu Mungu ataeneza kazi hii kotekote ulimwenguni, Anachukua fursa ya kuwafafanulia watu neno “hisia,” hivyo Akiwawezesha kuona kwamba mapenzi ya Mungu ni kuzitenganisha familia zote za watu, na kuonyesha kwamba Mungu hutumia kuadibu ili kutatua migogoro yote ya familia miongoni mwa wanadamu. La sivyo, hapangekuwa na njia ya kuimaliza sehemu ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani. Kwa nini ni vigumu sana kwa watu kujitenga na hisia? Je, ni muhimu zaidi kuliko viwango vya dhamiri? Je, dhamiri inaweza kufanikisha mapenzi ya Mungu? Je, hisia inaweza kuwasaidia watu kupitia shida? Machoni pa Mungu, hisia ni adui Yake—hili halijanenwa wazi katika maneno ya Mungu?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 28” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia:Jinsi ya Kumshuhudia Mungu Katika Imani Yako

Inayofuata:Mungu Amsihi Mwanadamu Amshuhudie Tu

Maudhui Yanayohusiana

 • Nimeuona Upendo wa Mungu

  1 Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda. Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi! Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako, nikiishi maish…

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  1 Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…

 • Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

  Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena, hawamwiti baba tena. 1 …

 • Upendo wa Kweli

  1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha kutoka kwa ne…