32. Kwaheri, Ndoto Yangu ya Kuwa Maarufu

Mwenyezi Mungu anasema: “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kusoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu kunanigusa sana. Kunafanya nikumbuke matukio fulani ambayo nimeyapitia.

Nilipenda sanaa za uigizaji tangu nilipokuwa mdogo na niliwastahi sana watu mashuhuri na waigizaji maarufu. Nilivutiwa sana na jinsi walivyokwenda jukwaani ili kila mtu awaheshimu mno na kuwashangilia. Hata kabla ya kumaliza shule ya upili nilijiandikisha na shule ya sanaa ya maonyesho, na miaka mitatu baadaye nikawa mwigizaji. Katika kila onyesho, niliridhika sana nilipowaona hao watu wote kwenye hadhira, wakitutazama tulipoigiza. Baada ya kumwamini Mungu nilifanya wajibu wangu kama mwigizaji, nikiigiza nafasi kadhaa katika filamu zilizobuniwa na kanisa. Nilifurahi sana ndugu waliposema kwamba nilikuwa mwigizaji mzuri sana, na nikawaza, “Nikiweza kuwa mhusika mkuu katika filamu, wote wataniona, na nina hakika watanistahi. Hiyo itakuwa vizuri sana!”

Kanisa lilipokuwa likiandaa kuchukua picha za filamu nyingine baadaye, ndugu mmoja aliniambia nifanye jaribio la uigizaji wa nafasi fulani. Nilifikiri kwamba kwa kuwa tayari nilikuwa mwigizaji na nilikuwa na tajiriba kiasi, hakika nitapata nafasi hiyo. Baadaye, nilisubiri kwa furaha kiongozi huyo aniarifu nishiriki katika uchukuaji picha wa filamu hiyo. Kwa siku hizo chache, nilifikiria mandhari hayo ambapo kila mtu angeniangalia kwa kustaajabu. Wazo hili lilinifurahisha sana. Lakini siku chache baadaye kiongozi aliniambia kwamba sikuwa nimepita jaribio lile la uigizaji na kwamba ni bora nijiunge na timu ya injili, kwa sababu hawakuwa na usaidizi wa kutosha Nilishtuka na nikahisi mwenye upinzani sana, huku nikijiuliza, “Kwa nini hawakunichagua? Nimeigiza nafasi muhimu hapo awali, na wengine wote walisema kuwa nilifanya kazi nzuri. Kwa nini hawakunichagua? Je, walikosea? Siwezi kujitokeza au kujionyesha katika kazi ya injili. Hakuna fahari ndani yake kama kuwa mwigizaji.” Kadiri nilivyozidi kufikiri hilo, ndivyo nilivyozidi kuhisi upinzani, na sikuweza kabisa kukubali matokeo hayo. Lakini nilifikiria jinsi ambavyo kushiriki injili ni mapenzi ya Mungu, kwamba ni jukumu ambalo ninapaswa kukubali. Nilipaswa kuwa na dhamiri na mantiki, nilipaswa kutii, kwa hivyo nilikubali shingo upande. Hata ingawa nilikuwa nikishiriki injili, nilifikiria kila mara jinsi ndugu walivyokuwa wamenistahi nilipokuwa nikiigiza, na hasa nilipowaona wengine ambao nilikuwa nimeigiza nao katika filamu, niliona gere sana. Niliwaza, “Itakuwa vizuri sana nikifanya wajibu wa kuigiza tena. Kisha nitakuwa tu kama wao, na kuigiza katika filamu wakati wote. Ndugu ambao wananijua wataniona na kunistahi. Kwa nini hawakunichagua?” Kadiri nilivyozidi kufikiria hilo, ndivyo nilivyozidi kuteseka. Sikuwa nikiwajibikia wajibu wangu, na sikulenga kujiandaa kwa ukweli kwa ajili ya kazi ya injili. Mtu aliyekuwa akitafuta na kuchunguza kazi ya Mungu ya siku za mwisho alipo uliza swali, sikujua nishiriki kuhusu ukweli upi ili kulijibu. Nilikuja kuhisi polepole kwamba nilizidi kuwa mbali na Mungu, na niliposoma maneno ya Mungu, nilikosa nuru ya Roho Mtakatifu. Sikuweza pia kuhisi kuwepo kwa Mungu nilipoomba, na nilizongwa na mawazo kila wakati. Katika mateso yangu, nilimwomba Mungu, nikisema, “Ee Mungu, nina uchungu sana sasa. Nataka tu kufanya wajibu wangu kama mwigizaji, kuonyesha kile ninachoweza kufanya, na siwezi kutii yale Uliyopanga. Tafadhali niongoze ili nijijue na nielewe mapenzi Yako.”

Nilisoma vifungu hivi viwili vya maneno ya Mungu baada ya kuomba: “Kutii kwa kweli ni nini? Wakati wowote ambapo Mungu anafanya jambo lolote linalokuendea vizuri, na kukuruhusu uhisi kwamba kila kitu ni cha kiridhisha na kinachostahili, na umeruhusiwa kutokeza, unahisi kwamba hili ni jambo la fahari mno, na unasema, ‘Shukrani kwa Mungu’ na unaweza kutii utaratibu na mipango Yake. Hata hivyo, kila unapotumwa mahali pasiposifika ambapo huwezi kutokezea, na ambapo hakuna anayekutambua, basi unaacha kuhisi furaha na unaona vigumu kutii. … Kutii wakati hali zinafaa kwa kawaida huwa rahisi. Ikiwa unaweza pia kutii katika hali ngumu— zile ambazo mambo hayakwendei vizuri na unasononeshwa, ambazo hukufanya uwe dhaifu, ambazo zinakufanya uteseke kimwili na sifa yako iharibike, ambazo haziwezi kuridhisha majivuno na majisifu yako, na zinazokufanya uteseke kisaikolojia—basi kweli una kimo” (kwa ushirika wa Mungu). “Mara tu inapogusia cheo, sura au sifa, moyo wa kila mtu huruka kwa matazamio, na kila mmoja wenu daima hutaka kujitokeza, kuwa maarufu, na kutambuliwa. Watu wote hawataki kushindwa, bali daima wanataka kushindana—hata ingawa kushindana kunaleta fedheha na hakukubaliwi katika nyumba ya Mungu. Hata hivyo, bila kupinga, bado huridhiki. Unapomwona mtu fulani akitokeza, unahisi wivu, chuki, na kuwa hiyo si haki. ‘Mbona nisitokeze? Mbona kila mara ni mtu huyo anayetokeza, na hauwi wakati wangu kamwe?’ Kisha unahisi chuki fulani. Unajaribu kuizuia, lakini huwezi. Unamwomba Mungu na unahisi nafuu kwa muda, lakini punde unapokumbana na hali ya aina hii tena, huwezi kulishinda. Je, hii haionyeshi kimo kisicho komavu? Je, si mtu kuanguka katika hali hizi ni mtego? Hizi ndizo pingu za asili potovu ya Shetani ambazo huwafunga wanadamu” (“Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma maneno ya Mungu, niligundua kwamba sikuweza kutii mipango ya Mungu kwa sababu tamaa yangu ya sifa na hadhi ilikuwa kubwa sana na kila wakati nilitaka kuwa maarufu. Kanisa liliponipangia niwe mwigizaji, niliweza kuwa kwenye kamera na kujionyesha, kwa hivyo nilikubali hilo na kutii kwa furaha. Lakini sasa kwa kuwa nilitakiwa kueneza injili, wazo la kutoweza kujitokeza au kujionyesha katika wajibu wangu na kwamba bila kujali nitafanya kazi kiasi gani hakuna atakayeiona, lilinifanya nipinge na nisiweze kutii. Ingawa nilionekana kushiriki injili, kichwa changu kilijawa na mawazo ya siku zangu adhimu nilipokuwa mwigizaji, na kila nilipofikiria jinsi ambavyo sikuweza kufanya hivyo tena, nilifadhaika na nikahisi kwamba nilikosewa. Nilikuwa nikifanya wajibu wangu wa injili kwa namna isiyo ya dhati, nikiwa hasi na mzembe, na bila kufanikisha chochote. Nilijua vyema kwamba kueneza injili kulikuwa mapenzi ya Mungu yenye shauku, na bila kujali iwapo nilikuwa nikiigiza au kueneza injili, yote yalikuwa yakishuhudia kazi ya Mungu kwa njia tofauti. Sikufaa kabisa nafasi hiyo ya uigizaji, kwa hivyo kiongozi alinipangia nifanye kazi ya injili. Huo ulikuwa wajibu wangu pia, kwa hivyo nilipaswa kuukubali na kutia bidii katika kuufanya vizuri. Lakini sikuzingatia mapenzi ya Mungu. Nilitaka chaguo langu mwenyewe katika wajibu wangu, na nikazingatia tu iwapo nitaweza kujionyesha na kuwafanya wengine wanistahi. Nilifikiri tu kuhusu kutosheleza malengo na tamaa zangu mwenyewe. Nilikuwa nikifanya wajibu wangu kwa jina, lakini katika hali halisi, nilikuwa nikifuatilia sifa na hadhi yangu bila kumtii Mungu hata kidogo. Je, huko hakukuwa kumpinga Mungu na kujaribu kumdanganya? Je, hilo lingekosaje kuchochea maudhi na chuki ndani ya Mungu? Baada ya hapo, nilimwomba Mungu na nikapata njia ya kutenda katika maneno Yake.

Hivi ndivyo maneno ya Mungu yasemavyo: “Ikiwa unataka kujitolea kuyaridhisha mapenzi ya Mungu katika kila kitu unachofanya, huwezi kutekeleza wajibu mmoja tu; lazima ukubali agizo lolote akupealo Mungu. Liwe linalingana na upendeleo wako au halilingani na lipo ndani ya maslahi yako, ni kitu ambacho hufurahii au hujawahi kukifanya hapo awali, au ni ki kigumu, bado unapaswa kulikubali na kutii. Sio tu kwamba lazima ulikubali tu, lakini pia lazima ushirikiane kwa bidii, na ujifunze kulihusu na ufikie uingiaji. Hata ukiteseka na hujaweza kuonekana na kung’aa, bado lazima utende kujitolea kwako. Lazima ulione kama wajibu wako wa kutimiza; si kama kazi yako binafsi, lakini kama wajibu wako. Je, watu wanapaswa kuelewaje wajibu wao? Ni wakati ambapo Muumbaji—Mungu—anampa mtu kazi ya kufanya, na wakati huo, wajibu wa mtu huyo unatokea. Kazi ambayo Mungu anakupa, agizo ambalo Mungu anakupa—huu ni wajibu wako. Unapoyafuatilia kama malengo yako, na kwa kweli una moyo wa kumpenda Mungu, je, bado unaweza kukataa agizo la Mungu? Hupaswi kukataa. Unapaswa kulikubali, sivyo? Hii ndiyo njia ya kutenda” (“Ni kwa Kuwa Mtu Mwaminifu tu Ndiyo Mtu Anaweza Kuwa na Furaha Kweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Niliona kutoka kwa maneno ya Mungu kwamba wajibu ni agizo la Mungu kwa mtu, na kwamba ni jukumu ambalo haliwezi kukwepwa. Tupende au tusipende, ikiwa tunaweza kujionyesha au la, tunapaswa kuukubali na kutii, na kuufanya kwa bidii. Sikupaswa kuchukulia wajibu wangu kama biashara yangu mwenyewe ili kuridhisha tamaa yangu kuu ya kujitokeza. Nilipaswa kupa kipaumbele masilahi ya nyumba ya Mungu na majukumu yangu, kuchukua nafasi ya kiumbe na kutii mipango ya Mungu. Baada ya hapo, nilijiandaa kwa bidii kwa kanuni za ukweli za kazi ya injili, na nikamwomba Mungu nilipokumbana na shida. Niliwaendea kina ndugu ili kutafuta na kufanya ushirika wakati ambapo sikuelewa kitu. Kufumba na kufumbua, hali yangu ilianza kuboreka, na nikaona mwongozo na baraka za Mungu katika wajibu wangu. Nilianza kuona matokeo. Baada ya kupitia haya, nilihisi kwamba niliweza kutenda ukweli kidogo, na kwamba niliweza kuacha kutaka kuwa mwigizaji na kujitokeza. Pia nilihisi kuwa nilikuwa nimeanza kumtii Mungu. Lakini baadaye kitu kingine kilitokea, na tamaa yangu ya sifa na hadhi ikajitokeza tena.

Siku moja, kiongozi aliniambia kwamba walinihitaji kwa ajili ya sehemu fulani ya video ya muziki. Nilifurahi sana niliposikia haya, na nikawaza, “Nikichaguliwa kuigiza nafasi ya mhusika mkuu wakati huu, basi ndugu wengi wataniona tutakapomaliza kurekodi wimbo huo na upakiwe mtandaoni. Jambo la kupendeza sana! Ni nafasi nzuri sana ya kujionyesha! Ni vigumu kupata fursa ya aina hii. Lazima nifanye kila niwezalo.” Kadiri nilivyozidi kufikiria hili, ndivyo nilivyozidi kufurahi, na nikaelekea katika eneo la kurekodi kwa furaha. Hata hivyo, ajabu ni kwamba, sehemu niliyoshiriki ilikuwa sekunde chache tu za filamu nzima, na sehemu yangu ilikuwa ya mfanyakazi mwenza wa dini anayemripoti dada mmoja ambaye anashiriki injili ya siku za mwisho. Nilivujika moyo. Nikiigiza nafasi kama hiyo katika filamu kwa sekunde chache tu na nionekane kuwa mkali sana, nilijiuliza ndugu watanionaje watakapoiona. Niliwalalamikia ndugu kadhaa wakati wa kurekodi, “Kwa nini wanatulazimisha tuigize nafasi kama hizo zisizopendeza? ...” Hata sikuwa nimemaliza kuzungumza wakati mmoja wao alisema, "Dada, aina zote za nafasi zinahitajika katika video hii ya muziki. Kuna mhusika mkuu, na lazima kuwe na wahusika wasaidizi. Watu huchaguliwa kwa ajili ya nafasi zinazowafaa, na lazima tutii. Aidha, sisi kuwa waigizaji na kufanya wajibu wetu kwa ajili ya kazi ya injili ya nyumba ya Mungu ni kuinuliwa kwetu, bila kujali tunaigiza nafasi gani!” Uso wangu ulianza kuwaka nilipomsikia akisema hivyo. Tulikuwa tukifanya wajibu sawa kabisa, lakini yeye ndiye aliyekuwa na mtazamo sahihi. Kwa nini sikuweza kutii kabisa? Lakini bado nilihisi upinzani kwa kiasi fulani, nikifikiri, “Hamjawahi kuwa waigizaji hapo awali, kwa hivyo mnafurahia kuigiza nafasi yoyote, lakini mimi ni tofauti. Nilikuwa mwigizaji katika kundi la wachezaji hapo awali na niliigiza nafasi nzuri kila wakati, na nimefanya wajibu wa maana katika nyumba ya Mungu, lakini sasa lazima niwe mhusika huyu mbaya sana na mkatili. Ni aibu sana!” Kila mtu alifurahi sana video ya muziki ilipopakiwa, lakini sikuweza kabisa kukusanya shauku yoyote. Kujiona nikiigiza nafasi hiyo mbaya kulinifadhaisha kwa namna ambayo sikuweza kueleza. Je, watu ambao niliwajua watanionaje baada ya kuigiza kwa namna hiyo? Nilijua kwamba nilikuwa katika hali mbaya, kwa hivyo nilimwomba Mungu, “Ee Mungu! Nimefadhaika na kuhuzunika kwa sababu tu nililazimika kuigiza nafasi ya mhusika msaidizi na mhalifu, na sijaweza kutii. Tafadhali niongoze ili nijijue na nitii utaratibu na mipango Yako.”

Nilisoma maneno haya ya Mungu baada ya kuomba: “Tabia potovu ya kishetani imekita mizizi kabisa ndani ya watu; inageuka kuwa maisha yao. Je, ni nini hasa ambacho watu hutafuta na wanachotamani kupata? Huku wakidhibitiwa na tabia potovu ya kishetani, maadili, matumaini, matarajio, na malengo na mielekeo ya maisha ya watu ni yapi? Je, haviendi kinyume na mambo chanya? Kwanza, watu daima hutaka kuwa na sifa au kuwa watu mashuhuri; wanataka kupata umaarufu mkubwa na ufahari, na kuwaletea mababu zao heshima. Je, haya ni mambo chanya? Haya hayalingani hata kidogo na mambo chanya; zaidi ya hayo, yanapingana na sheria ya Mungu ya kutawala majaliwa ya wanadamu. Kwa nini niseme hivyo? Je, Mungu anamtaka mtu wa aina gani? Je, Anamtaka mtu mwenye ukuu, mtu mashuhuri, mtu mwenye cheo kikufu, au mtu muhimu sana? Kwa hivyo basi, Mungu anamtaka mtu wa aina gani? Anamtaka mtu aliye thabiti ambaye anatafuta kuwa kiumbe wa Mungu anayestahili, anayeweza kutimiza wajibu wa kiumbe, na anayeweza kusalia katika nafasi ya binadamu. … Hivyo basi, tabia potovu ya kishetani huwaletea watu nini? (Upinzani kwa Mungu.) Ni nini hutokana na watu kumpinga Mungu? (Uchungu.) Uchungu? Ni maangamizo! Uchungu sio hata nusu yake. Kile unachoona kwa dhahiri sasa ni uchungu, uhasi, na udhaifu, na ni upinzani na malalamiko— vitu hivi vitaleta matokeo yapi? Maangamizo! Hili silo jambo dogo na sio mchezo” (“Ni Kutafuta Ukweli na Kumtegemea Mungu Pekee Ndiko Kunakoweza Kutatua Tabia Potovu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo). Baada ya kusoma haya, nilitafakari kuhusu sababu ya mimi kutaka kila wakati kuwa mhusika mkuu. Ilikuwa ni kwa sababu ningeweza kufanya wengine wanistahi na kunipenda mno kwa kuigiza kama mhusika mkuu, kama wale makafiri maarufu ambao huwa na msafara mkuu kila mahali wanapokwenda, na matendo yao yote hufuatwa na kuigwa. Nilidhani kwamba hiyo ilikuwa namna ya pekee ya kuishi inayofaa na kupendeza, wakati ambapo kuigiza nafasi ndogo, nafasi ya mhusika msaidizi, kulikuwa aibu. Sikuweza kuwa maarufu au kujionyesha. Hiyo ndiyo sababu nilikuwa nikiteseka na sikuweza kutii mazingira yaliyopangwa na Mungu. Kupitia kutafakari, niligundua kwamba ufuatiliaji wangu ulitokana hasa na kwamba nilikuwa nimeathiriwa na sumu za kishetani kama vile “Mtu anapaswa kuleta heshima kwa wahenga wake,” “Kama vile mti huishi kwa sababu ya ganda lake, mtu huishi kwa sababu ya uso wake,” na “Mtu huacha nyuma urithi wake kama vile bata bukini huacha mwangwi wa kilio chake.” Nilizichukulia hizi kama ufuatiliaji mzuri, na nikahisi kwamba nilipaswa kujaribu kujitokeza na kupendwa, na nikifikiri kwamba huko kulikuwa kuwa na malengo na maadili bora. Hasa nilipowaona waigizaji hao maarufu jukwaani wakisifiwa mno na watu hao wote, nilihisi kwamba hakika hiyo ni ajabu sana, na niliwaonea gere sana. Nilitamani kuwa tu kama wao. Hiyo ndiyo sababu nilitaka kuwa mwigizaji, kuwa maarufu tangu nilipokuwa mdogo, na nilijiandikisha na shule ya maonyesho hata kabla ya kumaliza shule ya upili. Niliamka mapema na kuchelewa kwenda kulala ili niweze kufanyisha ustadi wangu mazoezi na kujifunza kazi hiyo. Nilipokuwa jukwaani nikishangiliwa kwa sauti kubwa na hadhira, nilifurahia sana, na kuhisi kwamba kuteseka kokote kulistahili. Baada ya kuwa muumini, bado sikuweza kujizuia kufuatilia sifa na hadhi. Mara nilipopata wajibu kama mwigizaji nilitamani sana kuwa mhusika mkuu na kuigiza katika filamu kadhaa nzuri ili watu zaidi wanitambue na kuniheshimu. Katika video hii ya mwisho ya muziki, mwelekezi alinifanya niigize kama mhalifu mkatili kwa sababu hiyo ndiyo ilihitajika. Nilihisi kwamba ingeharibu picha yangu na kuwapa watu fikira mbaya, kwa hivyo sikuweza kutii, na nikatoa malalamiko yangu kichinichini. Nilikuwa na kiburi sana, na tamaa yangu ya sifa na hadhi ilikuwa kuu sana! Mungu anataka tuwe viumbe wenye sifa zinazostahili, kwamba tuwe imara katika ufuatiliaji wetu wa ukweli na tufanye wajibu wetu vizuri kama viumbe Wake tuache tabia zetu za kishetani na tuishi kwa kudhihirisha mfano wa kweli wa binadamu. Lakini sikufuatilia ukweli. Nilitaka kila mara kuwa kiongozi, kuwa maarufu, na kuwafanya wengine waniheshimu sana. Nilitaka kila mtu anizingire na nifurahie uzuri wa kuigiza kama mhusika mkuu. Ufuatiliaji wangu ulikuwa kinyume kabisa cha kile ambacho Mungu anataka. Ulikuwa dhidi ya mapenzi ya Mungu. Ilikuwa tu kama wale watu mashuhuri ambao hupenda kufuatwa kila mahali na kuigwa na wengine, ambao hutaka kuonekana kama mungu au mungu wa kike, na kupendwa mno. Njia wanayoitembea ni mbaya. Mungu ndiye Muumba—wanadamu wanapaswa kumwabudu Mungu na kumwona Yeye kama mkuu. Hii ni kanuni isiyobadilika. Lakini licha ya kuwa muumini, sikuwa nikimwabudu Mungu au kufanya wajibu wangu kama kiumbe. Nilikuwa tu kama kafiri, nikitamani kila wakati kuwa maarufu ili watu waniheshimu sana na kunifuata. Je, sikuwa nikijaribu kusimama katika nafasi ya Mungu, ili kuchukua nafasi Yake mioyoni mwa watu? Je, sikuwa adui wa Mungu? Hilo ni jambo ambalo hukosea sana tabia ya Mungu, na nilijua kwamba nisipotubu hakika nitapata adhabu ya Mungu ya haki! Wakati huo mwishowe niligundua jinsi ufuatiliaji wangu wa kila wakati wa kujitokeza na kuwa maarufu ulivyokuwa mwovu na wa kutisha sana. Niliona pia kuwa vipingamizi vyangu, kutopata nafasi yoyote ya mhusika mkuu, kutofanikisha malengo na tamaa zangu, yote yalikuwa ulinzi mkubwa wa Mungu kwangu. Niliguswa sana mara nilipoelewa haya, na nilimwomba Mungu sala hii, “Ee Mungu! Sitaki kukupinga na kukuasi tena. na sijali kuhusu kuwa maarufu tena au kuhusu kuwafanya wengine waniheshimu sana. Ninataka tu kutii utaratibu na mipango Yako, kuwa imara katika ufuatiliaji wangu wa ukweli, na kufanya wajibu wangu kama kiumbe.”

Kisha nikasoma kifungu hiki cha maneno ya Mungu: “Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinionyesha njia ya utendaji. Nilipaswa kuwa imara na kufanya wajibu wangu vizuri, na bila kujali agizo ambalo Mungu alinipa ni lipi, napaswa kulikubali na kutii, na kufanya kila niwezalo kulikamilisha. Kanisa hurekodi video za muziki ili kumshuhudia Mungu, na ikiwa ninaigiza kama shujaa au mhalifu, mhusika mkuu au mhusika msaidizi, ni kile ambacho nyumba ya Mungu inahitaji. Kina ndugu hupanga wajibu unaofaa kulingana na sura na tabia ya kila mwigizaji. Yote hufanywa kwa idhini ya Mungu, kwa hivyo ninapaswa kutii na kufanya yote niwezalo katika wajibu wowote ule. Mungu hajali ikiwa mimi ni mhusika mkuu au mhusika msaidizi, au jinsi mhusika ninayeigiza anavyopendeza. Anachojali ni ikiwa ninamtii moyoni mwangu, na ikiwa ninafanya wajibu wa kiumbe. Nilihisi kana kwamba niliondolewa uzito fulani nilipoelewa haya.

Nilishiriki katika filamu nyingine zaidi baadaye, na niliigiza kama mhusika msaidizi kila wakati. Wakati mwingine nilifadhaika kwa sababu tamaa yangu ya sifa na hadhi haikuwa ikitimizwa. lakini nilimwomba Mungu kwa makusudi na nikaacha nia zangu zisizo sahihi, na niliweza kutii na kufanya wajibu wangu kwa bidii. Niliacha kutafuta kwa uthabiti kujitokeza na kuwa maarufu, na badala yake nilifanya wajibu wangu kwa uthabiti. Haya yote yalifanikishwa kupitia kuhukumiwa na kuadibiwa na maneno ya Mungu, Kutenda ukweli ni vizuri sana!

Iliyotangulia: 29. Kiburi Huja Kabla ya Kuanguka

Inayofuata: 33. Baada ya Uwongo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki