3. Watu wanafaa kupitiaje hukumu na adabu ya Mungu ili kuokolewa?

Maneno Husika ya Mungu:

Kwa ufupi, kuichukua njia ya Petro katika imani ya mtu kunamaanisha kuitembea njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kupata kujijua na kubadilisha tabia yako kwa kweli. Ni kwa kuitembea njia ya Petro tu ndipo mtu atakuwa katika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe jinsi hasa ya kuitembea njia ya Petro, na vilevile jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia na vitu vyote vya mwili wake mwenyewe. Yeye lazima ajitolee kwa moyo wote; yaani, lazima ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, alenge kula na kunywa maneno ya Mungu, azingatie kutafuta ukweli na kutafuta madhumuni ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi na muhimu zaidi ya utendaji. Hilo ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu anaweza kufanikisha matokeo bora zaidi. Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu kimsingi kunajumuisha kutafuta ukweli, kutafuta nia za Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka katika maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini, sembuse kuzingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alitilia maanani kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na vile vile kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Petro pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka katika maneno ya Mungu, na vile vile asili potovu ya mwanadamu na dosari yake halisi hivyo kufikia vipengele vyote vya matakwa ya Mungu kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. petro alikuwa na vitendo vingi sahihi vilivyofuata maneno ya Mungu; hili lililingana zaidi na mapenzi ya Mungu, na ni njia bora zaidi ambayo mtu angeshirikiana huku akipitia kazi ya Mungu. Wakati ambapo alipitia mamia ya majaribio kutoka kwa Mungu, Petro alijichunguza kabisa dhidi ya kila neno la hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kila neno la ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, na kila neno la madai Yake kwa mwanadamu, na akajitahidi kuelewa maana ya maneno hayo. Alijaribu kwa bidii kutafakari na kukariri kila neno ambalo Yesu alimwambia, na alitimiza matokeo mazuri sana. Kupitia namna hii ya utendaji, aliweza kutimiza kujifahamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na hakuja tu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu, lakini pia alikuja kuelewa kiini, asili, na dosari mbalimbali za mwanadamu. Hii ndiyo maana ya kujifahamu kwa kweli. Kutoka kwa maneno ya Mungu, Petro hakutimiza tu kujifahamu kwa kweli, lakini kutokana na mambo yaliyoonyeshwa katika maneno ya Mungu—tabia ya Mungu yenye haki, kile Anacho na alicho, mapenzi ya Mungu kwa kazi Yake, mahitaji Yake kwa wanadamu—kutoka kwa maneno haya alikuja kumjua Mungu kabisa. Alikuja kujua tabia ya Mungu, na asili yake; alikuja kujua na kuelewa kile Mungu anacho na Alicho, na vilevile uzuri wa Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu. Ingawa Mungu hakuzungumza wakati huo sana kama Anavyofanya leo, matokeo katika vipengele hivi, hata havyo yalipatikanana Petro. Hili lilikuwa jambo adimu na la thamani.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Wakati ambapo tunapokea hukumu ya maneno ya Mungu, hatupaswi kuogopa mateso, wala hatupaswi kuogopa maumivu; na sembuse kuogopa kwamba maneno ya Mungu yataumiza mioyo yetu. Tunapaswa kusoma matamshi Yake zaidi kuhusu jinsi Anavyotuhukumu na kutuadibu na kufichua asili zetu potovu. Lazima tuyasome na kuyafuata na kujilinganisha kwayo mara kwa mara. Kamwe usiwalinganishe wengine nayo—tunafaa tujilinganishe wenyewe dhidi. Hatuna upungufu wowote katika vitu hivi vyote; sote tunaweza kulingana nao. Kama huamini hili, nenda ujionee mwenyewe. … Katika imani yetu, lazima tusisitize kwa uthabiti kwamba maneno ya Mungu ndiyo ukweli. Kwa kuwa kweli ndiyo ukweli, tunapaswa kuyakubali kwa busara. Bila kujali ikiwa tunaweza kutambua au kukubali au la, mtazamo wetu wa kwanza kuelekea maneno ya Mungu unapaswa kuwa ule wa kukubali kabisa. Kila mstari wa maneno ya Mungu unafungamana na hali fulani. Yaani, hakuna kati ya mistari yote ya matamshi Yake yanahusu kuonekana nje, sembuse sheria za nje au tabia ya aina rahisi ndani ya watu. Hayako hivyo. Ikiwa wewe huona kila mstari unaotamkwa na Mungu kama linahusu aina rahisi ya tabia ya mwanadamu au kama jambo linaloonekana nje, basi huna ufahamu wa kiroho na huelewi ukweli ni nini. Maneno ya Mungu ni ya maana sana. Je, ni ya maana vipi? Kila kitu ambacho Mungu husema, kila kitu ambacho hufichua kinahusu tabia potovu za watu, na vitu muhimu na vilivyokita mizizi ndani ya maisha yao. Hayo ni mambo muhimu, si mambo yanayoonekana nje, na haswa si tabia za nje.

Kimetoholewa kutoka katika “Umuhimu wa Kufuatilia Ukweli na Njia ya Kuufuatilia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Kama unaamini katika utawala wa Mungu, basi lazima uamini kuwa mambo ambayo hutokea kila siku, yawe mema au mabaya, si matukio ya kubahatisha. Sio kwamba mtu fulani ni mkali kwako au anakulenga kwa makusudi; yote kwa kweli husafidiwa na kupangwa na Mungu. Kwa nini Mungu hupanga mambo haya? Sio ili kuzifichua kasoro zako au kukukashifu; kukukashifu si lengo la mwisho. Lengo la mwisho ni kukukamilisha na kukuokoa. Mungu anafanyaje hilo? Kwanza, Anakufanya ufahamu tabia yako potovu, kufahamu asili na hali yako, kasoro zako, na kile unachokosa. Ni kwa kuelewa mambo haya yaliyomo katika moyo wako tu ndiyo utaweza kufuatilia ukweli na kuacha tabia yako potovu hatua kwa hatua. Huku ni Mungu kukupa fursa. Lazima ujue jinsi ya kuitumia fursa hii na usiwe mkaidi kwa Mungu. Hasa unapokabiliwa na watu, matukio, na mambo ambayo Mungu anapanga kando yako, usifikiri kila mara kwamba mambo hayako kama unavyotaka yawe, kila mara ukitaka kutoroka, kila mara ukimlaumu na kumwelewa Mungu visivyo. Huko si kuipitia kazi ya Mungu, na hiyo itafanya iwe vigumu sana kwako kuingia katika uhalisi wa ukweli. Lolote lile ambalo huwezi kulielewa kikamilifu, wakati ambapo una matatizo, lazima ujifunze kutii. Unapaswa kwanza kuja mbele ya Mungu na kuomba zaidi. Kwa njia hiyo, kabla ya wewe kujua kutakuwa na mabadiliko katika hali yako ya ndani na utaweza kutafuta ukweli ili kutatua tatizo lako utaweza kuipitia kazi ya Mungu. Katika kipindi hiki, uhalisi wa ukweli unahemshwa ndani yako, na hivi ndivyo jinsi utakavyoendelea mbele na jinsi mabadiliko katika hali ya maisha yako yatafanyika. Utakapokuwa umepitia mabadiliko haya na kuwa na aina hii ya uhalisi wa ukweli, basi utakuwa na kimo, na kimo huleta uzima. Ikiwa mtu huishi daima kulingana na tabia potovu ya Shetani, basi bila kujali ana shauku au bidii kiasi gani, bado hawezi kufikiriwa kuwa na kimo, au uzima. Mungu hufanya kazi ndani ya kila mtu, na bila kujali mbinu Yake ni ipi, ni watu, vitu au masuala ya aina gani ambayo Yeye hutumia kufanya huduma, au maneno Yake yana sauti ya aina gani, Ana lengo moja tu la mwisho: kukuokoa. Kabla ya kukuokoa, Anahitaji kukubadili, hivyo utakosaje kuteseka kidogo? Ni lazima upate kuteseka. Kuteseka huku kunaweza kuhusisha mambo mengi. Wakati mwingine Mungu huwainua watu, mambo, na vitu ambavyo viko karibu nawe ili kwamba uweze kujitambua, vinginevyo unaweza kushughulikiwa moja kwa moja, kukupogolewa, na kufunuliwa. Kama vile tu mtu aliye juu ya meza ya upasuaji–lazima upitie maumivu kiasi kwa ajili ya matokeo mazuri. Kama kila wakati Mungu anapokupogoa na kukushughulikia na kila wakati Anaibua watu, mambo, na vitu, hilo huchochea hisia zako na kukuongezea nguvu, basi kupitia hayo kwa njia hii ni sahihi, na utakuwa na kimo na utaingia katika uhalisi wa ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na kuwa bila kitu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake kwa Mungu. Je, huu haukuwa upendo mkamilifu kwa Mungu? Je, huku hakukuwa ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? Kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo kwa Mungu. Kama mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki, basi yeye ni kiumbe wa Mungu mwenye sifa inayostahili, na hakuna kitu kinachokidhi mapenzi ya Muumba bora zaidi ya hiki.

Kimetoholewa kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ukweli ambao mwanadamu anahitaji kuwa nao unapatikana katika neno la Mungu, na ni ukweli wenye manufaa na usaidizi zaidi kwa wanadamu. Ni dawa na ruzuku ambayo miili yenu inahitaji, kitu kinachomsaidia mwanadamu kurejesha tena ubinadamu wake wa kawaida. Ni ukweli ambao mwanadamu anapaswa kujitayarisha nao. Kadiri mnavyotenda neno la Mungu, ndivyo maisha yenu yatakavyositawi haraka zaidi, na ndivyo ukweli utakavyokuwa dhahiri zaidi. Mnapozidi kukua katika kimo, mtaona vitu vya dunia ya kiroho kwa dhahiri zaidi, na ndivyo mtakavyokuwa na nguvu zaidi kumshinda Shetani. Ukweli mwingi ambao hamwelewi utafanywa kuwa dhahiri mtakapotenda neno la Mungu. Watu wengi wanaridhishwa kuelewa tu maandiko ya neno la Mungu na hawalengi kujitayarisha kwa mafundisho badala ya kuzidisha uzoefu wao kwa vitendo, lakini, je, hiyo si njia ya Mafarisayo? Kwa hivyo msemo “Neno la Mungu ni uzima” unawezaje kuwa wa kweli kwao? Maisha ya mtu hayawezi kukua kwa kusoma neno la Mungu tu, bali ni wakati tu neno la Mungu linawekwa katika vitendo. Ikiwa unaamini kwamba kuelewa neno la Mungu ndicho kitu pekee kinachohitajika kuwa na uzima na kimo, basi ufahamu wako umepotoka. Kuelewa neno la Mungu kwa kweli hutokea unapoweka ukweli katika vitendo, na ni lazima uelewe kwamba “ni kwa kutenda ukweli tu ndipo unaweza kueleweka.”

Kimetoholewa kutoka katika “Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ikiwa mtu anaweza kumridhisha Mungu huku akitimiza wajibu wake, ni mwenye maadili katika maneno ya matendo yake, na anaweza kuingia katika uhalisi a vipengele vya ukweli, basi huyu ni mtu ambaye anakamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yamekuwa ya kufaa kabisa kwa watu kama hao, kwamba maneno ya Mungu yamekuwa maisha yao, wamepata ukweli, na wanaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili, asili ya mwili wao—yaani, msingi maalum wa uwepo wao wa kwanza—itatikisika na kuanguka. Baada ya watu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yao, watakuwa watu wapya. Maneno ya Mungu yakiwa maisha yao, maono ya kazi ya Mungu, matakwa Yake kwa wanadamu, ufunuo Wake kwa wanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anawahitaji watimize vikiwa maisha yao, wakiishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, basi wanakamilishwa na Mungu. Watu kama hawa wanazaliwa tena, na wamekuwa watu wapya kupitia maneno ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Kazi ya Mungu katika siku za mwishoni kuhukumu kupitia neno Lake. Kisha ikiwa tunataka tabia yetu potovuitakaswe na kufikia wokovu, tunapaswa kwanza kutia jitihadakwa neno la Mungu na kwa kwelikula na kunywa maneno ya Mungu, na kukubali hukumu na ufunuo wa Mungukatika neno Lake. Haijalishi jinsi neno la Mungu linauguza moyo,jinsi lilivyo kali, au ni kwa kiasi gani linatufanya kuteseka, kwanza kuwa na uhakika kwambaneno la Mungu lote ni ukweli, na uhalisi wa maishaambao tunapaswa kuuingia. Maneno yote ya neno la Munguni ya kututakasa na kutubadilisha, kutufanya kuacha tabia yetu potovuna kufikia wokovu, na hata zaidi kutufanya kuelewa ukweliili kufikia maarifa ya Mungu. Kwa hiyo tunapaswa kukubali hukumuna kuadibiwa,kupogolewa na kushughulikiwakwa neno la Mungu. Ikiwa tunataka kupokea ukwelikatika neno la Mungu, lazima tuweze kuteseka kwa kukubalina kutii neno la Mungu na ukweli. Tunapaswa kutafuta ukwelikatika neno la Mungu, kuhisi mapenzi ya Mungu,na kutafakari na kujijua wenyewe, kutafakari juu ya neno la Munguili kujua kiburi, udanganyifu, ubinafsi na kudharaulika kwetu, jinsi sisi hushiriki katika shughuli na Mungu,kumtumia Mungu vibaya,kumdanganya Mungu, kuchezea ukweli,na tabia zingine za kishetani, pamoja na uchafu mbalimbalikatika imani yetu kwa Mungu na nia za kupokea baraka. Kwa njia hii, tunaweza kujua hatua kwa hatua ukweli wa upotovu wetu na kiini cha asili yetu. Baada ya kuelewa ukweli zaidi,ujuzi wetu juu ya Mungu utakua zaidi hatua kwa hatua, na sisi kwa kawaida tutajua ni aina gani ya mtu ambaye Mungu anapenda au hapendi, ni aina gani ya mtu ambaye angeweza kuokoaau kuondosha, ni aina gani ya mtu ambaye angeweza kutumia, na ni aina gani ya mtu ambaye atakayebariki. Mara tu tunapoelewa mambo haya,tutaanza kuelewa tabia ya Mungu. Haya ndiyo matokeo yote ya kupata hukumuna kuadibiwa na neno la Mungu. Wote wanaotafuta ukwelihuzingatia kupata uzoefu wa hukumu na kuadibiwa kwa neno la Mungu, wanakuwa waangalifu kutafuta ukwelikatika kila kitu,na ni makini katika kutenda neno la Munguna kumtii Mungu. Watu kama hao wataweza kuelewahatua kwa hatua ukwelina kuingia katika ukwelikwa kupitia neno la Mungu, na kufanikisha wokovu na kufanywa kamili. Kwa wale ambao hawapendi ukweli, ingawa wanaweza kutambuakuonekana kwa Mungu na kazi kutoka kwa ukweliulioonyeshwa na Mungu, wanafikiri hakikawanaweza kufanikisha wokovu bora tuwaache kila kitu kwa ajili ya Munguna kutimiza wajibu wao. Mwishoni, bado hawawezi kupokea ukwelina uzima baada ya kumwamini Mungu kwa miaka mingi. Wanaelewa tu maneno machache, barua,na mafundisho,lakini wanafikiri wanajua ukwelina wamepata ukweli. Wanajidanganya wenyewena hakika wataondolewa na Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Tunaposoma maneno ya Mungu leo, jambo muhimu kabisa ni kwamba tukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu. Jambo la msingi ni kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, na hili ndilo jambo la muhimu kabisa. … Nyote mnasema kwamba mko tayari kuvumilia mateso ya hukumu na kuadibu. Kwa kuwa mko tayari kuvumilia mateso haya, mtatii vipi? Mtayakubali vipi? Ukiyaona maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu, je, utayakubali kama hukumu ya Mungu kwako? Au utashikilia kwamba maneno haya yanawahukumu wengine, kwamba hayahusiani na wewe, na hivyo kuepuka hukumu na kuadibu kwa Mungu? Utachukua njia ipi? Ikiwa uko tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu, basi hufai kuepuka mambo haya unaposoma neno la Mungu. Haijalishi maneno haya ni ya kuumiza au makali kiasi gani, unapaswa kuyakubali yote. Unamwomba Mungu: “Ee Mungu, niko tayari kukubali hukumu na kuadibu Kwako. Maneno Yako ya hukumu yanaelekezwa kwangu. Mimi ni aina hii ya mtu mpotovu, nina shida hizi za upotovu, kwa hiyo napaswa kukubali hukumu na kuadibu Kwako, kwani huu ni upendo Wako kwangu, ni Wewe kuniinua. Nayakubali na kuyatii kabisa, na nina shukrani kwa ajili ya upendo Wako.” Punde unapoomba kwa njia hii, utayakubali kwa urahisi, na hutaona ugumu. Kisha linganisha maneno ya Mungu na hali zako wenyewe ili kuzidisha ufahamu wako. Hivi ndivyo inavyoweza kufanywa. Hili ni onyesho la kutii hukumu na kuadibu kwa Mungu. Lakini ukiyaona maneno ya Mungu ambayo ni makali kiasi, na kusema: “Mungu, maneno haya si hukumu kwangu, ni hukumu ya wengine, ni hukumu ya Shetani. Hayahusiani na mimi, kwa hiyo sihitaji kuyasoma,” basi huku ni kuepuka hukumu na kuadibu kwa Mungu. Ndugu wengine wakikupogoa na kukushughulikia, unapaswa kufanya nini? Unapaswa kuomba haraka kwa Mungu: “Mungu, nakushukuru! Huu ni upendo Wako ukinijia. Umewagusa ndugu zangu wanipogoe na kunishughulikia kwa sababu ya upendo Wako kwangu. Natii.” Lazima uombe. Usipoomba itakuwa rahisi kwako kukataa, rahisi kwa mwili wako kuasi, rahisi kwa wewe kutokubaliana na wengine, rahisi kulalamika na hata itakuwa rahisi zaidi kwako kuwa hasi. Kwa hiyo, lazima uende haraka kuomba. Baada ya kuomba, akili yako itakuwa tulivu, na utaweza kutii. Punde unapoweza kutii kweli, utakuwa na roho moyoni mwako, na utasema: “Wakati huo sikukasirika bali kulikubali. Ilikuwa kwa sababu niliomba. Sasa hatimaye naweza kumtii Mungu.” Unaona dalili ya matumaini na unapata kimo kiasi; hivi ndivyo mtu anakua.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Iliyotangulia: 2. Kwa nini inamlazimu Mungu kuwahukumu na kuwaadibu watu?

Inayofuata: 4. Inamaanisha nini kuomba kwa kweli?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

8. Jinsi ambavyo Mungu anatamatisha enzi ya giza ya utawala wa Shetani katika siku za mwisho

Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa maelfu ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu, Atabadilisha namna wanavyomfahamu na mitazamo yao Kwake, ili kwamba maarifa yao juu ya Mungu, yaweze kuanza katika rekodi safi, na mioyo yao itakuwa imesafishwa upya na kubadilishwa.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki