Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda kwa Kristo wa Siku za Mwisho

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

30. Kwa nini Mungu hawaokoi wale wanaofanyiwa kazi na pepo wabaya na wale waliopagawa?

Maneno Husika ya Mungu:

Wale ambao walipagawa na roho wabaya hapo zamani (tangu kuzaliwa) watafichuliwa sasa. Nitakufukuza nje! Je, bado unakumbuka yale ambayo Nimeyasema? Mimi—Mungu mtakatifu na Asiye na waa—Siishi katika hekalu chafu na la kuchukiza. Wale ambao walikuwa wamepagawa na roho wabaya wanajua wenyewe, na Sihitaji kufafanua. Sijakujaalia! Wewe ni Shetani mkongwe, ilhali unataka kupenya katika ufalme Wangu! Hasha!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 81” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Kwa muda mrefu Nimeona waziwazi matendo mbalimbali ya pepo wabaya. Na watu wanaotumiwa na pepo wabaya (wale wenye nia mbaya, wale wanaotamani mwili au utajiri, wale wanaojikuza, wale wanaolivuruga kanisa, nk.) kila mmoja wao pia amebainika na Mimi. Usifikiri kwamba kila kitu kitakuwa sawa wakati ambapo pepo wabaya watatupwa nje. Hebu Nikwambie! Kuanzia sasa na kuendelea, Nitawaondoa watu hawa mmoja baada ya mwingine, nisiwatumie kamwe! Yaani, mtu yeyote aliyepotoshwa na pepo wabaya hatatumiwa na Mimi, na atafukuzwa! Usifikiri kuwa Sina hisia! Fahamu jambo hili! Mimi ndimi Mungu mtakatifu, na Sitakaa katika hekalu chafu! Mimi huwatumia tu watu waaminifu na wenye hekima ambao ni waaminifu kabisa Kwangu na wanaoweza kuudhukuru mzigo Wangu. Hii ni kwa sababu watu kama hao walijaaliwa na Mimi. Bila shaka hakuna pepo wabaya wanaowafanyia kazi hata kidogo. Hebu Nieleze wazi jambo moja: Kuanzia sasa na kuendelea, wale wote ambao hawana kazi ya Roho Mtakatifu wana kazi ya pepo wabaya. Hebu Nirudie: Simtaki hata mtu mmoja ambaye pepo wabaya humfanyia kazi. Wote watatupwa kuzimuni pamoja na miili yao!

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 76” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Mara nyingi watu hutaja kuzimu na jahanamu. Lakini maneno haya mawili yanarejelea nini, na tofauti kati yao ni ipi? Je, kweli yanarejelea pembe fulani ya baridi, ya giza? Akili ya binadamu daima inakatiza usimamizi Wangu, wakifikiria kwamba kutafakari kwao kusio na mpango maalumu ni kuzuri sana. Lakini haya yote ni mawazo yao wenyewe. Kuzimu na jahanamu zote zinarejelea hekalu la uchafu ambalo limeishiwa na Shetani awali au na roho wabaya. Hiyo ni kusema, yeyote ambaye amemilikiwa na Shetani au roho wabaya awali, ni wao ambao ni Kuzimu na wao ndio jahanamu—hakuna kosa kuhusu hilo! Hii ndiyo sababu Nimesisitiza kwa kurudia katika siku za nyuma kwamba Siishi katika hekalu la uchafu. Je, Mimi (Mungu Mwenyewe) Ninaweza kuishi Kuzimu, au jahanamu? Je, huo hauwezi kuwa upuuzi usio na maana? Nimesema hili mara kadhaa lakini ninyi bado hamwelewi Ninachomaanisha. Ikilinganishwa na jahanamu, Kuzimu imepotoshwa zaidi na Shetani. Wale ambao ni wa Kuzimu ndio walio katika hali mbaya sana, na Sijawaamulia kabla watu hawa kabisa; wale walio wa jahanamu ni wale Niliowaamulia kabla, lakini kisha wameondolewa. Kwa maneno rahisi, Sijamchagua hata mmoja wa watu hawa.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 90” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Wale walio na mashetani huishi kwa kudhihirisha asili yao mbaya mno, na asili hii mbaya mno huja kutoka roho waovu ambao wanakaa ndani yao. Asili ya roho waovu huwa asili ya ndani ya mtu aliye na mashetani. Asili husika ya mtu hutegemea roho husika ndani ya mtu huyo, na sifa bainifu ya asili ya mtu huyo huamua sifa bainifu ya tabia zao zilizopotoshwa—hii ni kweli kabisa. Wale walioteuliwa na kuchaguliwa na Mungu ni watu wote wenye roho ya binadamu. Wale wasio na roho za binadamu ni wale ambao ndani yao aina zote za roho waovu huishi. Kwa hivyo, watu hawa ni wale ambao ni wa mashetani waovu na roho waovu, na si walengwa wa wokovu wa Mungu. Walengwa wa wokovu wa Mungu ni wale wenye roho za binadamu. Ingawa watu hawa wamepotoshwa na Shetani, na wamesababisha asili ya kumpinga Mungu, wanaweza kusafishwa na kuokolewa kabisa. Hii ni kwa sababu ndani yao wana roho za binadamu, na sifa zao asili za binadamu na asili yao ni nzuri. Wale wasio na roho ya binadamu ni wanyama ama waovu, dubwana ndani ya vazi la binadamu, na hivyo Mungu hawaokoi; hii ni kwa sababu wao si wa wanadamu, na wanadamu, na hawajumuishwi katika binadamu ambao Mungu anazungumzia.

Umetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Iliyotangulia:Kupagawa ni nini? Kupagawa hudhihirishwaje?

Inayofuata:Wanawali wenye hekima ni nini? Wanawali wapumbavu ni nini?

Maudhui Yanayohusiana

 • Ujumbe ulioenezwa na Bwana Yesu Katika Enzi ya Neema ulikuwa tu njia ya toba

  Hapo mwanzo, Yesu Alieneza injili na kuhubiri njia ya kutubu, na Akaendelea mpaka kumbatiza mwanadamu, kuponya magonjwa, na kukemea mapepo. Mwishowe, Alimkomboa mwanadamu kutoka kwa dhambi na kukamilisha kazi Yake ya enzi yote.

 • Katika ulimwengu wa kidini, ni ukweli na Mungu wanaoshikilia uwezo, au ni wapinga Kristo na Shetani wanaoshikilia uwezo?

  Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?

 • Mtu anapaswaje kuitambua sauti ya Mungu? Je, mtu anawezaje kuthibitisha kwamba Mwenyezi Mungu kweli ni Bwana Yesu aliyerudi?

  Maneno ya Mungu mwenye mwili yanaanzisha enzi mpya, yanaongoza wanadamu wote, yanafichua mafumbo, na kumwonyesha mwanadamu mwelekeo mbele katika enzi mpya. Nuru anayoipata mwanadamu ni utendaji au elimu rahisi. Haiwezi kuelekeza binadamu wote kuingia enzi mpya au kufichua fumbo la Mungu Mwenyewe. Mungu, hata hivyo, ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu yuko na dutu ya Mungu, na mwanadamu yuko na dutu ya mwanadamu.

 • Kumfuata Mungu ni nini?

  Maneno Husika ya Mungu: Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafua…